Nini Hatma ya Upinzani Tanzania?

Nini Hatma ya Upinzani Tanzania?

Mtu wa Pwani,
Kweli na kusikitikia sana, sijui kama wewe unaona Makamba ni mtyu makini, na sijui kama kwako kipi kiko mbele, maslahi ya viongozi watu wachache wa CCM au maslahi ya taifa. Unadhani hizo tuhuma za mabilioni yaliyochotwa ni sifa kwa CCM? Sasa hivi uchunguzi unaendelea yeye Makamba ambaye nina hakika hajui loop holes za grand corruption, anasema mbele za watu tena bila hata aibu waongo, je ikijathibitishwa nani atakuwa mwongo.
Labda utueleze kama wewe pia ni beneficiary wa hiyo mipesa, au ni shabiki tu wa kama yangu na Simba. Nasikitika kuona kuwa wewe unaona maslahi ya watu wachache ndani ya CCM yana maana zaidi kuliko maslahi ya taifa. Lakini unatakiwa ujue kuwa kuna watu wa maana nadni ya chama chako ambao wanaupinga uchafu huu kwa nguvu zote.

Bongolander,

Upinzani wakishinda ni kwa manufaa ya taifa, CCM wakishinda ni kwa manufaa ya viongozi wa CCM binafsi. Nafikiri hayo ni maneno yako binafsi na hayawakilishi Watanzania walio wengi.

Kwa mimi vyama vyote vya siasa karibu vinafanana tu, vyote vinashirikiana kutumia mapesa yetu adimu kununua mashangingi, , kupeana posho nene nene, kuchukua pesa kama ruzuku za chama badala ya kupeleka mashuleni ambako hakuna walimu, au hospitalini ambako hakuna madawa.

Kote kote kuna mafisadi ambao tunawajua wazi wanaibia taifa letu. Kinachotofautiana ni ukubwa wa mnofu ambao kila mtu anakata
kwenye maliasili Tanzania. Wengine tunachoangalia ni intention, so longer wanaanza kunyofoa kabla hata hawajawa na kisu kikali, je wakikabidhiwa panga, watakata kipande kikubwa kiasi gani?

Kwenye vyama vyote kuna watu wachache ambao ni waaminifu na wanataka kumsaidia Mtanzania lakini bahati mbaya wale waovu walio wengi wanafanya hata hawa wazuri wasionekane. Hawa ndio wa kutumia njia zote kuwa promote kwa faida ya taifa letu.

Hawa wengine wanaoficha nyumba zao London, au ambao hata hawezi
kuelezea mali zao wamezitoa wapi, wanafanana tu na mafisadi wa CCM, wanapinga sasa kwasababu wako nje, siku wakipata hawatakuwa tofauti na hao CCM. Mifano tunayo, Kenya, Malawi, Zambia nk.

Tunataka mabadiliko ya kweli na sio kuondoa fisadi mmoja na kumbandika mwingine.
 
Acheni Makamba apige kelele za mwisho-mwisho.Radio-mbao zinadai kuwa "wenye chama chao" wameshaamua kumuondoa katika wadhifa huo (ukatibu mkuu) mara baada ya uchaguzi mkuu wa chama cha mafisadi.
 
Sasa nyie mlitegemea Bwana Yusufu Makamba asemeje, he's the Katibu Mkuu for crying out loud, inabidi awe mpiga debe tu. Angeongea independent observer basi maneno hayo yangekuwa na uzito wa kuweza kujadiliwa.
 
Wakati umefika kwa NEC kumtema Makamba, tayari ana Ubunge lakini kwa upande wa Ukatibu amekuwa hafai kabisa. Nadhani ule ukuu wa mkoa unaendana zaidi na character yake kuliko Ukatibu Mkuu.
 
•
CCM yatamba kwenye udiwani



*CHADEMA yafurukuta Songea, TLP Arusha

Na John Daniel, Dodoma

KATIBU Mkuu wa CCM Bw. Yusuph Makamba, ameubeza Muungano wa vyama vinne vya Upinzani, akisema ni sawa na wagonjwa dhidi yakwani utasambaratika wakati wa Uchaguzi Mkuu mwaka 2010.

Amesema Muungano huo pia ni sawa na paka watatu ambao wakiwekewa panya mbele kila mmoja atataka kumla bila kujali kuwa ni kitu kimoja hivyo kuishia kugombana wao kwa wao.
Bw. Makamba alisema hayo jana mjini hapa wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu matokeo ya uchaguzi wa udiwani katika kata 14 ambazo alitamba kuwa CCM imeuaibisha muungano huo kwa kunyakua kata 11.

"Kuna Muungano wa Vyama vinne vya Upinzani vya CUF, CHADEMA, TLP na NCCR-Mageuzi, lengo la Muungano huo ni kuing'oa CCM madarakani na juzi wamefanya majaribio ya kuachiana kata katika uchaguzi wa kata 14, lakini awali katika kata 16 walikuwa na viti sita lakini sasa wameambulia viti vitatu tu kati ya kata 14, tumewashinda sana," alitamba.
Katibu huyo ambaye aliainisha kata zote 11 ambazo CCM imeshinda na zile tatu zilizochukuliwa na wapinzani alisema Watanzania bado wanakipenda chama chake tawala na kwamba kama mtu ana matatizo ni mtu na wala si chama na kutamba kuwa kitaendelea kutawala kwa kuwa kina sera zinazotekelezeka. Kuhusu tuhuma zinazotolewa na wapinzani dhidi ya viongozi mbalimbali wa Serikali na chama chake, alikebehi akisema hayo ni maneno yanayotokana na kukosa sera baada ya kuona kuwa za CCM zinatekelezeka na kugusa mahitaji muhimu ya Watanzania na kuwataka kwanza wao wajisafishe kabla ya kukinyooshea kidole chama chake.

"Wapinzani walisema sera za CCM hazitekelezi, sasa shule tunajenga, walimu wanajifunza, barabara tunatengeneza na mwakani tunaanza kila kijiji kuwa na zahanati, wamekosa cha kusema sasa wamebaki na kusema uongo na kashfa dhidi ya viongozi wa Serikali na CCM, rushwa, mara mafisadi. "Hata mwongo uwe na akiba ya uwongo wa kusema kesho, usimalize uwongo wote kwa siku moja, nawatahadharisha wapinzani, kuwa wamewachosha Watanzania kwa uongo, hata siku watakaposema ukweli hawataeleweka," alisema Bw. Makamba na kuongeza:

"Wanasema CCM inachota fedha za Serikali wakati wao wanaiba fedha za ruzuku zinazotolewa na Serikali na kununua majumba yao binafsi, wanapokuwa jukwaani hawasemi hayo, wanasema tu mawaziri wa CCM, kila chama kinapata ruzuku ya Serikali, CCM inatumia vizuri kwa kazi za chama si kununua nyumba za watu binafsi kwa sh. milioni 40," alisema Bw. Makamba.
Kuhusu Uchaguzi Mkuu wa CCM alisema maandalizi yote yamekamilika na kwamba kinachosubiriwa sasa ni wajumbe kuwasili na kwamba jumla ya wajumbe 1,969 (sasa ni 1,968 baada ya Bibi Salome Mbatia, kufariki dunia hivi karibuni) wa mkutano pamoja wageni waalikwa 550 wamealikwa wakiwamo 60 kutoka nje ya nchi, viongozi wa vyama vyote vya siasa, waasisi wa CCM, viongozi waastafu na wageni wengine.

"Mwaka huu tumejiandaa vya kutosha, kila mjumbe atapata mashati mawili sawa na muda wa kikao cha siku mbili, hoteli zote tulishalipia tangu mwezi wa nane, nyumba tatu mpya zimejengwa kwa ajili ya viongozi wakuu, wastaafu na waasisi na viongozi waalikwa, hata wajumbe wakifika leo, mkutano unafanyika," alitamba Bw. Makamba.

Alipoulizwa kama Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wamealikwa kushughulikia tatizo hilo katika Mkutano huo alisema "wewe (Mwandishi) kazi yako nini...na wale kazi yao ni kushughulikia rushwa popote wanapohisi kuna rushwa wanakwenda si lazima waalikwe".

Kuhusu malalamiko yaliotolewa na baadhi ya wana CCM ya kuwapa vyeo wanaohamia chama hicho kutoka kambi ya upinzani alisema hilo si tatizo na kwamba hata Mwislamu akiokoka na kuingia Ukristo, anaweza kuwa Mzee wa Kanisa ili mradi awe na uwezo.

Naye Cresensia Kapinga anaripoti kutoka Songea, kuwa mgombea udiwani katika Kata ya Majengo mjini hapa kwa tiketi ya CCM, Bw. Alfani Kigwenembe, amebwagwa na mgombea wa CHADEMA, Bw. Iddi Ibrahim Abdalah, aliyeibuka kidedea kwenye uchaguzi mdogo.

Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo juzi saa 5 usiku huku mamia ya wakazi wa manispaa ya Songea wakiwa wamelizunguka jengo la SACCOS ya wafanyakazi wa halmashauri ya manispaa ya Songea ambamo shughuli za kuhesabu kura, zilikuwa zikifanyika, msimamizi wa uchaguzi, Bw. Edgar Belege, alisema wapiga kura waliotarajiwa walikuwa 3,754 kati yao wanawake wakiwa 1,948 na vituo vilivyopangwa kupigia kura vikiwa 10.

Bw. Belege ambaye pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea, alisema katika uchaguzi ambao ulianza saa 12 asubuhi, ulifanyika vizuri na kwamba matokeo ni Kwamba Bw. Kigwenembe alipata kura 554 na Bw. Abdalah kura 1,015 na hivyo kutangazwa kuwa mshindi.

Alisema pamoja na ushindi huo, Bw. Abdalah hatua ya kwanza atakula kiapo cha kuingia kwenye Baraza la Madiwani ambalo linatalajiwa kufanyika hivi karibuni na kuwa mpaka mchakato wa uchaguzi unamalizika hakukuwa pingamizi kutoka kwa mgombea aliyeshindwa.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutangazwa mshindi, Bw. alisema ushindi alioupata ni matokeo ya udhaifu wa CCM kwani awali aliomba kugombea udiwani kwa tiketi ya CCM kwenye kura za maoni, wakambwaga na kudai kwamba yeye ni 'bata' asiyeuzika lakini CHADEMA wakaridhika naye na kumteua kugombea.

Alieleza kukubali kuwa mwakilishi wa wananchi wa Majengo kwenye Baraza ambako atakuwa mtetezi katika kuchochea maendeleo ya kata hiyo na si kukimbilia kutafuta maslahi binafsi ambayo hayanufaishi wananchi ambao ni wapiga kura wa kata ya Majengo.

Mwenyekiti wa CHADEMA, Bw. Joseph Fuime, alisema ushindi wa udiwani wa kata ya Majengo, ni mvua za rasharasha na kwamba kwa sasa CHADEMA inajipanga kuchukua nafasi nyingine za udiwani wa kata zingine ikiwa ni pamoja na ubunge wa jimbo la Songea Mjini.

Aidha, matokeo ya awali ya uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata za Muwesi na Malumba wilayani Tunduru, CCM iliibuka kidedea, ambapo katika kata ya Muwesi, Bw. Nurdini Nolela alipata kura 1,140 na kata ya Malumba Bw. Msenga Saidi alipata kura 1,557.

Naye Glory Mhiliwa, anaripoti kutoka Arusha, kwamba CCM katika manispaa ya Arusha kimebwagwa na Tanzania Labour Party (TLP), katika uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata ya Sombetini uliofanyika juzi.

Kabla ya kutangazwa matokeo ya jumla ya uchaguzi huo, TLP tayari ilishabaini kuwa mgombea wao amenyakua kiti cha udiwani wa kata hiyo, hivyo kuanza shamrashamra kushangilia kuibwaga CCM.

Shamrashamra hizo zilisababisha vurugu kubwa baada ya aliyekuwa mgombea ubunge wa TLP, Arusha, Bw. Godbless Lema kupigwa na Polisi.

Pia wafuasi wa TLP katika vurugu hizo, walipigwa na mabomu ya machozi na Polisi kwenye kituo cha kupigia kura cha shule ya msingi Sombetini, ambako kulikuwa na vurugu.

Vurugu hizo zilianza saa 12 jioni, kutokana na wafuasi wa TLP na CCM kuanza kurushiana maneno ya kejeli na polisi kufika katika kituo hicho na kutumia mabomu ya kutoa machozi kutuliza vurugu.

Hata hivyo, licha ya tambo na shamrashamra za wana CCM kujihakikishia kuchukua kata hiyo kwa madai kuwa ni chama tawala kisicho na upinzani,TLP iliibuka kidedea kwa kura 42.

Akitangaza matokeo hayo jana jijini hapa, Msimamizi wa Uchaguzi wa manispaa ya Arusha, Dkt. Job Laizer, alisema Bw. Chemu Mawazo wa TLP aliibuka mshindi baada ya kupata kura 1,515 na mpinzani wake kutoka CCM Bw. Fabian Muhindi kupata kura 1,473.

Dkt. Laizer alisema katika uchaguzi huo, kura 2,988 zilipigwa sawa na asilimia 13 ya watu waliojiandikisha ambao walikuwa ni 22,149.

Alieleza kuwa katika uchaguzi huo, kura 49 zilikataliwa na wapiga kura waliojitokeza.

Upinzani katika kampeni zake ulitumia silaha za kashfa kuhusiana na mkataba wa Buzwagi na tuhuma za ufisadi dhidi ya viongozi wa Serikali.

Hata hivyo, baadhi wa wana CCM wa wilaya ya Arusha, waliwatupia lawama viongozi wa CCM ngazi ya wilaya, kwa kukaidi maoni yao ambao tangu awali waliutaka uongozi huo kuwa makini katika uteuzi wa wagombea.

http://www.majira.co.tz/kurasa.php?soma=tanzania&habariNamba=4371


sasa hili la kuiba pesa za ruzuku si ufisadi eeh?

haya tuchambue ripoti ya mkuuu makamba.

mwaka huu utaisha kwa kilio kwa ndugu zetu hawa.

Mtanzania yeyote anayependa kuona maendeleo ya kweli ya Watanzania hawezi kufurahia kuona CCM wanatamba katika chaguzi za madiwani? Kwa kipi hasa walichokifanya mpaka watambe kwenye chaguzi hizo? Chama kimegubikwa na tuhuma nzito za ufisadi unaofanywa na viongozi wa ngazi za juu kabisa wa chama hicho, wala rushwa, wasaini mikataba ambayo haina maslahi kwa Watanzania, viongozi wanaotumia madaraka yao kujilimbikizia mali. Mtanzania yeyote anayefurahia hali hii basi ana kasoro ya aina moja au nyingine. Kwa maoni yangu Tanzania itachukua kipaumbele siku yeyote ile mbele ya chama chochote kile cha siasa. Hivyo kufurahia ushindi wa CCM wakati tunajua hali halisi ya jinsi CCM inavyoboronga mambo mbali mbali ndani ya Tanzania ni sawa na hayawani amuone mmoja wa wazazi wake akiwa mgonjwa taabani lakini yeye hali hiyo aione haina kasoro yoyote na anaendelea na starehe kama vile hakuna baya lolote linalomuhusu.

Tanzania iko taabani na hili linamuhusu kila Mtanzania awe ni mwanachama wa CCM au la. Wale wanaojifanya kuona kila kitu kiko shwari ndani ya Tanzania basi wanakasoro kubwa vichwani mwao.
 
Wakuu wa JF

OMBI : Nadhani hii thread ingefaa ikae wazi. Nimepitia zinazosemekana zinafanana ila focus is very different be it similar.

http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=1633

ifunguliwe kwani naona iko closed ingawa ina debate nzuri tuu kwa maoni yangu.

In the meantime, napenda kurejea kwenye comment ya JMnyika, ikitokea kwenye hiyo thread hapo juu - inga muda umekuwa mrefu ila mjadala bado muhimu:

"Huu ni mtazamo finyu sana. Ni mtazamo ambao unaashiria kutokujua dhana ya vyama vya siasa na dhima yake kwa jamii. Watetezi wa hoja hii watupe mifano ya vyama duniani katika nchi ambazo zimekomaa kidemokrasia ambapo kila kukicha chama kinatoa huduma za namna hiyo kwa wananchi." JMnyika

Nadhani dhana imepotoshwa hapa au Mnyika hajaelewa hoja. Hatujasema lazima chama kama Chadema au CUF au chochote cha Upinzani au Mbadala sasa kazi yake tupu ibakie ni kujenga mashule etc.

La maana, ni kuangalia kule ambapo wameshinda kwa kuchaguliwa na pia kule ambapo hawajashinda ila wanaamini wamepata kura au support ipo. Kule wafacilitate kwa karibu kabisa, harakati ambazo zitakuwa na kuleta maendelea moja kwa moja kwa wananchi. Hiyo mifano anayoulizia tena nasikitika lugha anayotumia kusema eti akili finyu kwa watu wa hoja hii! Kwa kweli bila kuingia kuchambua hiyo lugha, kwangu binafsi ni dhahiri ukosefu wa upeo wa mbali, ukosefu wa ukomavu wa kisiasa na vilevile mambo ya maendeleo. Hiyo mifano ipo mbona mingi tuu, angalia HAMAS - ingawa sikubaliani nao kwenye nyanja kadhaa zao ila approach yao ya kuwa karibu na communities zao ndio iliowawezesha kuchaguliwa kwani PLO siku zote walilaumiwa kwa rushwa. Leo hii, Conservative Party in the UK, iko upinzani na sasa guess what, Ian Duncan Smith is leading a wing on social justice agenda (unusual for Tories) ila ni NGOs equivalent za TZ, and they influence policy in Tory party and at the same time wananchi benefit from the services provided by these NGOs which are supported by Tory party.

Pia, mimi naamini Chadema kuna nafasi nzuri zaidi kukomaa na kuondokana na hulka za CCM za Ulafi wa Madaraka, kama akina Mnyika watachukua mwelekeo tofauti. Hatushauri eti leo mutoa kila kitu hapa at to what in detail mtafanya, ila position mnayodebate nayo, shows where you guys are heading and it is not much different from CCM kwani mkiingiliwa tuu na walafi mkiwa katika position ya leo ya kusema la muhumu ni kushika dola, basi sio ajabu eti mturudishe kulekule CCM ilotoka manake emphasis ni kutawala na sio kumtoa mwananchi kwenye Umaskini.

Nasema hivyo kwani, sio tatizo eti leo CCM au any other party ajikute amemuiga CHADEMA katika sera X and mwananchi amenufaika. Kuna Ubaya gani? Kama owner wa policy, mtakuwa mmeifanyia uchuzi wkina na mnajua what is next and it will get to a point, watu wanaona mnachokifanya and you get the credit and people benefit from that. Mfano Mzuri ni pressure to get the answers za corruption. Zitto kapigwa chini Bungeni and stood on his principle from what we see and the dividends seemingly paying off (kudos kwake na strategists wake), kibano kikifanikiwa hopefully kuna pesa zitaongeza idadi ya shule mpya etc. That is benfit to a nation.

Sasa mkiwa na sera za kusupport NGOs au maeneo yenu mlioshinda kwa idadi fulani ya kura au hata kama hamjashinda kuna idadi ya kujengea, basi fikirieni kwa makini kuweka mikakati itakayoleta DIRECT BENEFITS TO THE PEOPLE OF THAT AREA. Sio zile hongo za parties etc, noo... hapa naongelea maendeleo ya Jamii diectly. Kuna Ubaya gani Chadema kufacilitate soe funding from any donors kujenga mashule kupitia NGOs Z au Y katika eneo fulani?? Nendenni kwenye strong holds zenu, nendeni kule you need to make progress. Hiyo sio hongo ndio kazi mtategemewa kufacilitate in full swing mkiwa serikalini mekamata dola. Kwa sasa, CCM watazidi kupiga debe kuwa hakuna opposition ya maana, na majority watabakia confused what is going on, in the end, ikija kura they vote what they think they know - better the devil you know! Hivyo, I strongly suggest, and honestly hope Chadema will one day get to see uzuri wa hii policy. Policy hii, ikiambatana na mikakati dhabiti ya kuwa na zero tolerance kwenye ufujaji wa pesa, na kuhakikisha planning za projects zinaweka mishahara decent, and people are getting DIRECT benefits and Chadema is registered and recognized by the people - ordinary people, I can assure you, hata vote rigging haitatosha kufanya hiyo kazi. How can CCM ay any other party rig votes to take a ward which is Chadema kila mahali? Kuanzia makansellas na huduma kadhaa nyeti? Sisemi hawawezi kabisa, ila it will burn on their faces very soon after.

Kama hamsikilizi, au mmesikilza ila hamkubaliani, ni sawa. Ni choice. Ila, kama kuna watu wengine kwenye vyama vingine, wakiwa smart, they will take note.

Huu mlolongo wa kuweka la mbele ndugu zangu, ni worldwide ila effect mbaya zaidi Afrika kwa ajili ya Umasikini wa fikra ya jinsi ya kutumia resources zetu. We need to think out of the BOX. Hakuna mtu atakaeuja kutufanyia hiyo kazi. Ni sisi Watanzania wenyewe!

Nawasilisha in 2008!
 
Vyama vyoooote vya upinzani Tanzania "vilianzishwa na system", na hii niliambiwa na rafiki yangu aliyekuwa mwenyekiti wa NCCR kabla ya mrema, mzee Kassim Maguto (M/Mungu amsamehe dhambi zake na amuweke pema peponi, Amin.).

Vyama ambavyo havikuwa kwenye system vilishindwishwa kuanza, havikusajiliwa mpaka leo hii.

kwa kifupi, upinzani kwa sasa hakuna kabisa Tanzania, kuna kina sisi huku nje tunaeshangilia siasa kama mpira tuu, tukijuwa nini kinachoendelea na kuna wengi sana wenye kupandisha hasira na ghadhabu, wasiojuwa nini kinaendelea.

Narudia, upinzani kwa sasa hakuna Tanzania. Si CUF, si Chadema, Si NCCR wala si kingine chochote chenye usajili ambacho hakina viongozi ambao wapo kwenye system.

kwa kifupi, si mbowe, si lipumba, si sharif, si mrema, wote hao ni system (according to Marehem Kassim Maguto) ambae na yeye mwenyewe alikiri kuwa ni system wa miaka mingi na alinipa siri kuwa aliitwa Ikulu kuelekezwa waanzishe vyama vya upinzani na wakawa wanafundishwa kila kukicha ni nini cha kufanya na funds zote zikatoka huko, kwa vyama vyote vilivyosajiliwa.

kuna baadhi ya wanachama (wengi tuu) ambao masikini hawalijuwi hili, wapo kwa nia moja ya upinzani na wapo tayari kufa lakini masikini roho zao, laiti wangelijuwa hili nadhani wasingekuwa na hamu hata ya siasa.

Enyi kina Lipumba, Sharifu, Mbowe na Mrema wacheni dhulma hii, haya mnayajuwa lakini mtasababisha watu wauwane bure wakati nyinyi mnajuwa nini mnakifanya. Hebu rudini kwa mola wenu kabla ya watu wasiyoyajuwa haya hawajaanza kughadhibika na kumwaga damu.

Na hayo yote yalipangwa na kuanzishwa na nyerere, ndio maana ufisadi haufi Tanzania na aliyeuanzisha huo ufisadi ni nyerere.

Naapa kuwa hayo yote niliyoyasema ni kweli tupu.



Jee, hamjuwi system ni nini?
 
Vyama vyoooote vya upinzani Tanzania "vilianzishwa na system", na hii niliambiwa na rafiki yangu aliyekuwa mwenyekiti wa NCCR kabla ya mrema, mzee Kassim Maguto (M/Mungu amsamehe dhambi zake na amuweke pema peponi, Amin.).

Vyama ambavyo havikuwa kwenye system vilishindwishwa kuanza, havikusajiliwa mpaka leo hii.

kwa kifupi, upinzani kwa sasa hakuna kabisa Tanzania, kuna kina sisi huku nje tunaeshangilia siasa kama mpira tuu, tukijuwa nini kinachoendelea na kuna wengi sana wenye kupandisha hasira na ghadhabu, wasiojuwa nini kinaendelea.

Narudia, upinzani kwa sasa hakuna Tanzania. Si CUF, si Chadema, Si NCCR wala si kingine chochote chenye usajili ambacho hakina viongozi ambao wapo kwenye system.

kwa kifupi, si mbowe, si lipumba, si sharif, si mrema, wote hao ni system (according to Marehem Kassim Maguto) ambae na yeye mwenyewe alikiri kuwa ni system wa miaka mingi na alinipa siri kuwa aliitwa Ikulu kuelekezwa waanzishe vyama vya upinzani na wakawa wanafundishwa kila kukicha ni nini cha kufanya na funds zote zikatoka huko, kwa vyama vyote vilivyosajiliwa.

kuna baadhi ya wanachama (wengi tuu) ambao masikini hawalijuwi hili, wapo kwa nia moja ya upinzani na wapo tayari kufa lakini masikini roho zao, laiti wangelijuwa hili nadhani wasingekuwa na hamu hata ya siasa.

Enyi kina Lipumba, Sharifu, Mbowe na Mrema wacheni dhulma hii, haya mnayajuwa lakini mtasababisha watu wauwane bure wakati nyinyi mnajuwa nini mnakifanya. Hebu rudini kwa mola wenu kabla ya watu wasiyoyajuwa haya hawajaanza kughadhibika na kumwaga damu.

Na hayo yote yalipangwa na kuanzishwa na nyerere, ndio maana ufisadi haufi Tanzania na aliyeuanzisha huo ufisadi ni nyerere.

Naapa kuwa hayo yote niliyoyasema ni kweli tupu.



Jee, hamjuwi system ni nini?

Watu wengine kusukumizia wenzao, wewe nini kinakuzuia kuanzisha chama nje ya system? Au kwa nini usianzishe system yako? Dunia yote ingekuwa na watu wanaomaintain status quo au kuogopa vile visivyoonekana tungekuwa bado kwenye ice age or sumt'n like that
 
sasa kama hakuna upinzani, wale walioibua kashfa ya Benki Kuu kina nani? Wakati mwingine mjifunzage mantiki kabla ya kuja na kauli za jumla namna hiyo. Jifunze pia kuqualify things kuliko kutoa kauli za namna hiyo halafu tukiuliza chanzo tunaambiwa ni mtu mmoja ambaye naye ni marehemu, kwa maneno mengine tuamini maneno yako.

Sasa tukifanya hivyo, nini kitatuzuia kusema kuwa CCM wote ni mafisadi kama alivyosema Marehemu Malima (mungu ailaze pema roho yake)..!
 
Watu wengine kusukumizia wenzao, wewe nini kinakuzuia kuanzisha chama nje ya system? Au kwa nini usianzishe system yako? Dunia yote ingekuwa na watu wanaomaintain status quo au kuogopa vile visivyoonekana tungekuwa bado kwenye ice age or sumt'n like that
Mwafrika wa kike, ukipenda usipende huo ndio ukweli, au huijuwi system ni nini?
 
Mwanakijiji, ukipenda usipende huo ndio ukweli, au huijuwi system ni nini?

Ha ha ha ha haha,

Naona kuna tafsiri nyingi na matumizi mengi sana ya neno ukweli hasa kutoka kwa mchangiaji ambaye anasisitiza kuwa kuna tafsiri moja tu ya neno system!
 
Mzee Mwanakijiji - busara safi hiyo.

Tuchukulie basi ndio walianzisha, they might have wanted to manage the change then. Ila things move on and wenye kuamini will get in and do what they have to do.

Hakuna kuuwana, hao hao wenye kuuwa wataua uwe CCM au uwe Chadema . Wakitaka kuuwa kwa jina la "usalama" they will do it irrespective.

Hatukuunga mkono kuondolewa Ubeberu wa Mwingereza ili tuweke Ubeberu wa Mtanzania against fellow Tanzanians
 
Ha ha ha ha haha,

Naona kuna tafsiri nyingi na matumizi mengi sana ya neno ukweli hasa kutoka kwa mchangiaji ambaye anasisitiza kuwa kuna tafsiri moja tu ya neno system!
hakuna mahali hata pamoja nilipotafsiri neno system, kinachokuchekesha ni nini? onyesha wapi nimetafsiri neno sytem!
au huijuwi system ni nini?
 
hakuna mahali hata pamoja nilipotafsiri neno system, kinachokuchekesha ni nini? onyesha wapi nimetafsiri neno sytem!
au huijuwi system ni nini?

Hujatafsiri system kwa sababu huna hiyo tafsiri yake no wonder kila mtu unamuuliza kama anajua maana ya system!
 
sasa kama hakuna upinzani, wale walioibua kashfa ya Benki Kuu kina nani? Wakati mwingine mjifunzage mantiki kabla ya kuja na kauli za jumla namna hiyo. Jifunze pia kuqualify things kuliko kutoa kauli za namna hiyo halafu tukiuliza chanzo tunaambiwa ni mtu mmoja ambaye naye ni marehemu, kwa maneno mengine tuamini maneno yako.

Sasa tukifanya hivyo, nini kitatuzuia kusema kuwa CCM wote ni mafisadi kama alivyosema Marehemu Malima (mungu ailaze pema roho yake)..!
Tafadhali soma vizuri niliyoyaandika, usikurupuke tuu. nimesema vyama "vimeanzishwa na system" na sikusema kuwa wanachama wote ni system!

ikiwa hoja ni kutaja mafisadi, hiyo pia inaweza ikawa ni kazi ya system, kwani zilizofisadiwa ni hizo pesa za account moja tuu? au BoT imebadhiriwa wakati wa mkapa tuu? inawezekana kabisa kuwa balali na wengine kidogo ni kafara tuu.

The point is hao viongozi wote wa upinzani na wao ni system na aliyesema hayo ni mwenzao M/Mungu amlaze pema. au huijuwi system ni nini?
 
Hujatafsiri system kwa sababu huna hiyo tafsiri yake no wonder kila mtu unamuuliza kama anajua maana ya system!
sasa kipi kilichokufanya utake kuzuwa kuwa nimetafsiri maana ya system? na ilhali unajuwa kuwa mimi sina hiyo tafsiri? jee, unaijuwa system ni nini?
 
Mimi niko hapa duniani kutokana na system ya maisha ya viumbe hai iliyotokana na system ya ndani ya maumbile ya mwanadamu anayepumua kutokana na system ya viungo vyake ambavyo vinafanyakazi kutokana na system ya chembe hai zake zilizowezeshwa kutokana na system ya maumbile ya viini hai ambavyo hutokea na kutoweka kutokana na system ya uhai na mauti ambazo hutokana na system za ulimwengu mzima x 10,000,000,000,000
 
Back
Top Bottom