Nini Hatma ya Upinzani Tanzania?

Nini Hatma ya Upinzani Tanzania?

Mie sielewi point yako ipo wapi?Unamaanisha wananchi wasiviunge mkono vyama vya upinzani kwa sababu vyote vipo kwenye system?Je njia mbadala ni ipi?Kwa nini usianzishe chama chako kisicho kwenye system ili utuonyeshe mfano?
SIKATAI WALA SIKUBALI KUWA SYSTEM NDIO ILIVIANZISHA KWA KUWA USHAHIDI NI WA MAREHEMU AMBAYE SIJUI KAMA ALIMPA KAMA SEHEMU YA WOSIA AU ALIMWAMBIA KAMA MWANDANI WAKE.LAKINI SIJAONA MAHALI WALIITWA VIONGOZI WENGI WA UPINZANI IKULU NA MZEE MAGUTO KUITWA KWAKE HAKUMAANISHI KUWA VIONGOZI WOTE WALIITWA NA WALA HAKUMAANISHI KUWA KUITWA NI ZOEZI ENDELEVU ATA WALIOZALIWA JUZIJUZI MRADI NI UPINZANI WATAITWA KUPEWA MAELEKEZO.NA WALA HAIMAANISHI KUWA KAMA WALIWAANZISHA BADO WANAWENZA KUWACONTROL MPAKA SASA,NI KAMA VILE WALIANZISHA JAMBO WASILOWEZA KULICONTROL ANYMORE......HOWEVER,TATIZO KUBWA LA VYAMA VYA UPINZANI NI KUONGOZWA NA REJECTED MATERIALS YA CCM,GANDA LA MUA LA JANA CHUNGU KAONA KIVUNO.
MATARAJIO YANGU NI KWA KIZAZI KIPYA CHA KINA ZITO,MNYIKA,AMBAO SEHEMU KUBWA YA MAISHA YAO YAMEKUWA NI NDANI YA UPINZANI NA PENGINE WATAZEEKA WAKIWA BADO NI UPINZANI.LAKINI SIYO KINA SLAA,MBOWE,SHARRIF,DK MASHA NA KINA CHEYO NA ATA WASOMI KAMA KINA DK CHEMPONDA
 
Kuna watu wana mawazo ya kizandiki kuliko SISIEMU yenyewe.Watu hawa ni hatari kuliko systemu tupambanayo kwa sababu ni watu wa kujikomba kwa kila hali, hata kama faida yao ni kuchakaza soli za viatu na kukausha sauti za makoo yao kwa kushangilia upuuzi wenye kuwadharirisha utu wao wenyewe.

Kingine kibaya zaidi ni ving'ang'anizi wa hoja zisizo weza simama kwa miguu yake mpaka ziwe juu ya hoja nyingine za kufikirika.
Kuthibitisha jambo kutokana na source moja tena ya mtu ambaye ndoto yake ilikufa kabla haijaotwa ni Uzandiki na Uhabithi mkubwa na pengine ni kujikana utu wako mwenyewe.
Kuna watu wanajipendekeza kwenye System kana kwamba mwisho wa Uhuni wao wa kisiasa uko sambamba na kiama.Katika maana kwamba maovu ya SISIEMU ni kama Natural Principle( Gravitation Force, Magnetism and Density) ambazo ni ujuha kutaka kwenda kinyume nazo.

Wakati ni kweli kwamba kuna maofisa kibao Usalama wa SISIEMU ndani ya vyama vya upinzani;pia kwamba SISIEMU wanatumia fedha walizo iba BOT kununua na wapinzani na kudhoofisha juhudi zao, si kweli kwamba vyama hivi vimeundwa na SISIEMU au serikali ya SISIEMU. Sisi wengine tulikuwapo toka enzi za akina James Mapalala wakieneza propaganda za mageuzi kinyume na sheria za serikali ya SISIEMU tunajua kianachoendelea.
Ukiona mtu ambaye kalelewa ndani ya Thermos( Uniform Tempeture and Pressure) anasimama na kudhihaki mapambano ya halisi ya kujikomboa Kiuchumi na kifikra ili tu joto la Thermos inamuhifadhi lisibadirike, ujue ni dalili moja kubwa kwamba ameng'amua kwamba joto la maji ndani ya Thermos linapungua na maji yameanza geuka barafu. Hakuna Shwari, sasa anatapatapa.

Sishangai, utamaduni wa kusema uongo na kujidanganya ni hulka ya SISIEMU na wanachama wake wengi. Ndani ya miezi 12 iliyo pita SISIEMU na Vikaragosi wake wamejidanganya zaidi ya mara 1000 katika masuala kibao ambayo sasa hivi wanajaribu kujitoa kimaso maso kwa kupaka rangi Upumbavu wa makanusho yao kwa mafanikio haba au bila mafanikio kabisa.

Madai haya kwamba Upinzani Tanzania ni uongo mtupu yanaweza tolewa na mtu ambaye yuko kwenye kada ya juu ya SISIEMU, ni mtoto wa kiongozi wa SISIEMU, ni mke wa kiongozi wa SISIEMU au Kimada ambaye anafaidika moja kwa moja na Uharamia wa $133 Bill.
Lakini maneno haya kama yanasemwa na mwanachama mtiifu wa SISIEMU ambaye anaiona SISIEMU kwenye Fremu ya 1977, mwanachama huyu inabidi azinduliwe kutoka kwenye usingizi ulo mzito mithili ya ule wa pono na kuambiwa:

" Hi Mr Pono mkia wako umeshika moto unateketea, tena unateketezwa kwa moto wa hila za pono wenzako."
Wewe unachoongea ni utumbo mtupu, soma hoja vizuri. Au unaogopa ukweli? au unaona doooh, "kupigia debe kote kule upinzani lakini leo naambiwa ni system, haiwezekani!".

Aliyasema m/mungu amrehemu, ndio hayupo, lakini mimi niliyoyatowa hapa nipo hai na hao viongozi wa upinzani niliowataja hapo juu, wapo hai.

watu kama wewe ndio daima mnaficha mafisadi na ufisadi kwa mambo ya kusadikika tuu, ukweli hamuutaki. Nina uhakika kilichokuuma sio kutajwa hao viongozi wa upinzani ambao woote ni ex sisiem na mpaka leo ni system. Unalo lililo-kukera, weka wazi.

Na kama unauhakika hao sio system haya tuambie una ushahidi gani kuwa wao sio sisiem ooopsss system? Jee, huijui system ni nini?
 
Nakumbuka Mwalimu aliwahi kusema kuwa upinzani wa kweli utatokea ndani ya CCM, sasa sijui ndio alikuwa anatuandaa tukiona watu wanatoka CCM kuanzisha chama kingine tuone huo ndio upinzani wenyewe haswa na wale ambao hawakuwa CCM(ila enzi za chama kimoja sidhani kama kuna watu ambao hawakuwa CCM) wakianzisha vyama tuwaone si wapinzani wa kweli bali wababaishaji tu.

Sasa kama hiyo ni kweli je nitakosea kuhitimisha kuwa Mwalimu alikusudia CCM iendelee kuongoza nchi daima dumu?
 
Mheshimiwa Ndugu Zomba, Nimesoma wakala wako si chini ya mara moja. Pia nimesoma mawazo ya wengine katika mada hii, Kadhalika nimepata kiasi cha muda wa kutafakari yote katika pande mbili za mjadala yaani upande wako na ule unaopingana nawe. Yangu ni machache tu kwako.

Siwezi kuyakubali wala kuyakataa yako kwa kuwa sina ushahidi. Na katika uliyoyazungumza sioni popote unapoyatolea ushahidi. Hali kadhalika siuoni ushahidi unaotoka kwao pia. Ili mradi, mtaniwia,
mnabishana kama wototo wadogo.

Mimi nafikiri, ungetoa maelezo yako, kisha ukayatolea ushahidi na kuyapa uzito maelezo hayo na mwisho ungetueleza nini cha kufanya ili tuweze kuupata huo upinzani/ushindani wa kisiasa. Labda cha ziada, kama itawezekana utueleze jinsi ya kuuendesha upinzani huo na labda utupe majina ya akina nani wanastahili kuwa viongozi wa upinzani huo.

Sisi wengine, pengine hatujui system ni nini na watu gani wamo au hawamo katika system yenyewe.
Ahsante kwa wazo lako zuri, ushahidi wa mwanzo:

1) sina sababu ya kutia maneno yangu mdomoni mwa maiti (Mzee Kassim Maguto)(yaani sina sababu ya kumzulia uwongo) aliyekuwa rafiki yangu aliyeweza kunieleza hayo na mengine mengi tuu, ambayo yakifika wakati wake nitayaanika, sio mahala pake hapa.

2) sina sababu ya kuvichukia vyama vya upinzani ambavyo ndani yake kuna wanachama ambao kwa dhati kabisa wanataka mabadiliko ya kweli na wana-upinzani wa kweli, lakini wanarudishwa nyuma na hao viongozi niliowataja.

3) Ninayatowa haya kwa kuhofia yasitufike kama ya Kenya, kwani ni wengi walipomchaguwa Kibaki walijuwa kuwa ni mpinzani wa kweli, lakini masikini roho zao, damu inamwagika huko Kenya, simply kwa sababu Kibaki alikuwa kwenye system ya Kanu na aliweza kuwahadaa "wapinzani" na kupokeya nchi kwa urahisi uchaguzi wa mwanzo, nikimaanisha kuwa bila damu kumwagika. Sasa hivi baada ya wengi kujuwa, nini kilijiri, Kanu wapo nyuma yake wanamsaidia na watu wasio na hatia wanakufa bila sababu ya maana, hawataki system ibadilike, ndio sababu ya kuuwana sasa hivi. Hapo mwanzo ingawa ilionyesha kuwa ni mpinzani mkuu wa kanu, lakini kwa kifupi haikuwa hivyo na ndio maana haikumwagika damu na kanu wakaachiya madaraka kwa urahisi wakijuwa kuwa system inaendelea (of course si wana Kanu wote walijuwa hilo, ni wale viongozi tuu).

4) Jamani hamuoni, jinsi sefu sharifu anvyowadanganya wanachama wake? anawafanya kama vifaranga vya kuku, mtanyonya kesho, mtanyonya kesho, mpaka wanazeeka. Huo tuu, ni ushahidi tosha kuwa huyu muheshimiwa ni system.

5) Hamkuona ya viongozi wengi walioachia ngazi vyama vya upinzani, wengi wanarudi sisiem na wanaula kama kawaida.

6) Hamkuyaona ya Mrema, kila chama anachohamia anakidhoofisha mpaka kinakuwa hakina nguvu ya kupinga chochote, kama mrema si system ni nini?

7)Hamuyaoni ya lipumba, mara tuu baada ya uchaguzi, wakati alitowa ahadi kibao za kubainisha "siri za wizi wa kura", kachoropoka pyuu na kwa sasa yupo majuuuu, habari za upinzani anazitazama kwenye JF tuu, anangoja uchaguzi ujao ufike, aje kufanya kazi yake anayoijuwa vizuri. Kwa nini asikae nchini akakiimarisha chama chake? au CUF hawawezi kumlipa? au nchi hii hawezi kutowa mchango wa taaluma yake hata akiwa nje ya chama tawala? utakuta no, si hivyo bali ni system ndio anayoifanyia kazi na ndio inayomruhusu nini afanye na nini asifanye.

Kwa sasa naona hayo machache yanatosha na nina uhakika kuna watakaonisaidia kwa mengine nisoyajuwa, kwani haiwezekani binadamu nikajuwa kila kitu. Kama vile wengi wetu humu hatujuwi system ni nini, Jee unaijuwa system ni nini?
 
Mie sielewi point yako ipo wapi?Unamaanisha wananchi wasiviunge mkono vyama vya upinzani kwa sababu vyote vipo kwenye system?Je njia mbadala ni ipi?Kwa nini usianzishe chama chako kisicho kwenye system ili utuonyeshe mfano?
Ahsante kwa maswali yako.

La hasha sina maana wanachama wasiwe wapinzani, lakini ni vizuri wakachaguwa vijana wapya, badala ya hao niliotajiwa na mwenzao.

mbona sikusema kina zito kabwe ni system? kwa kuwa silijuwi hilo, na kwa uwono wangu naona ni kijana mpinzani mahiri na anahamasa. tuwachaguwe vijana wadogo amabao hawajawahi kuifanyia kazi serikali hii iliyopo madarakani wala hawajawahi kuwa wan sisiem. Hapo tunaweza kuanza kupata damu mpya isiyokuwa na virusi vya system.

kuhusu, mimi kuanzisha chama, kusema kweli wazo hilo sina . Na sina sababu ya kuanzisha chama kipya kuzidi kugawa upinzani kwani kugawanyika sana hakuna faida, kinachotakiwa ni kuutambuwa uozo uliomo kwenye vyama na kuukatilia mbali, kwa kuanzia mimi nasema hao niliyowataja majina yao hapo juu ni uwozo, tuwakate tuwatupe na tuimarishe upinzani kwa damu mpya.
 
Hebu tujadili mambo yenye mantiki na tuachane na huyu anayetutaka tuanze kujadili hisia bila kuwepo na ushahidi wa mazingira ama wa moja kwa moja.

Ukiangalia ushahidi wake utaona kuwa amejaribu kusema vibaya CUF na TLP ila vyama vingine hajavisema sasa asitufanye watoto wadogo.

Wako tayari kuutetea ufisadi kwani ndio unawafanya waishi........
 
3) Ninayatowa haya kwa kuhofia yasitufike kama ya Kenya, kwani ni wengi walipomchaguwa Kibaki walijuwa kuwa ni mpinzani wa kweli, lakini masikini roho zao, damu inamwagika huko Kenya, simply kwa sababu Kibaki alikuwa kwenye system

Mkuu Zomba,

Heshima mbele, some of your points ni very convincing I am not sure in general kama the conclusion ni balanced au fair, lakini binafsi I kind of think about it kwa sababu ninawajua wanachi wengi ambao wanafiki ndani ya hii fourm, ambao mchana wanajidai ni upinzani, usiku ni Chadema, na ninajua for a fact kuwa they are not part of any CCM's scheme, isipokuwa ni tabia yaop tu kujikomba komba kwa kiongozi yoyote wa CCM,

Ninalijua Ri-jamaa hapa JF ambaye yuko radhi kuwanunulia viongozi wa CCM anything, lakini sio ndugu zake wala wazazi wake, Ri-jamaa litawanunulia hata watoto wao mizawadi isiyokuwa na mfano, litajipendekeza weee, mpaka kuwafuata viongozi kwenye majimbo yao ya uchaguzi na kujifanya lina NGO huko majuu, kumbe ni Ri-ongo likubwa na viongozi walishalishitukia, lakini hata uliambie nini ni kazi bure,

Sasa nimesema mara nyingi sana hapa kuwa viongozi wetu ni reflection yetu wenyewe wananchi, nikiangalia points zako Zomba, ninataka kuzikataa, lakini nikiliangalia hili Ri-jamaa ambalo viongozi wa CCM hawalipi hata senti moja lakini liko tayari kufa kuwafanyia wasio liomba, na kuja hapa JF kujifanya Ri-pinzani nambari moja, then ninataka kuamini kuwa kuna wanaoweza kukubali kulipwa kuwa wasaliti,

My take, kuna viongozi safi wa upinzani, na kuna mazezeta, sasa mkuu zomba, tafuta dataz zaidi ku-support your argument so far hazitoshi, lakini you have a big point ila sio viongozi wote walionunuliwa na CCM, wengine hufanya kwa hiari yao tu kama hili Ri-jamaaa hapa JF.

Na kwa wle mnaompinga, jaribuni kuwa wastaarabu kwa kuweka points badala ya hoja za nguvu, wengine tunajifunza hapa elimu ya bure!

Ahsante Wakuu!
 
Hebu tujadili mambo yenye mantiki na tuachane na huyu anayetutaka tuanze kujadili hisia bila kuwepo na ushahidi wa mazingira ama wa moja kwa moja.

Ukiangalia ushahidi wake utaona kuwa amejaribu kusema vibaya CUF na TLP ila vyama vingine hajavisema sasa asitufanye watoto wadogo.

Wako tayari kuutetea ufisadi kwani ndio unawafanya waishi........
Ama kweli asiyejuwa maana haambiwi maana, sijakisema vibaya chama chochote cha upinzani, usitie mameno yako katika mdomo wangu. Koma!

Nimesema viongozi wa upinzani na majina nimeyataja, soma vizuri kabla hujapayuka.

halafu mara sina ushahidi mara ushahidi wake, ndio tukuelewe vipi? au ni lazima useme tuu, hata kama hujuwi ukisemacho ni nini? au huijuwi system ni nini?
 
Umesema kuwa LIPUMBA NA MREMA ,ni watu wa system ,na ukatolea mfano mwingine wa mazungumzo ya muafaka kuwa hayaendi na kumalizika kwa sababu seif ni system,ama hukusema hayo?

N a je kitendo cha Lipumba kwenda kufanya kazi ya consultancy WTO huo ndio ushahidi kuwa alikuwa system?

Ama huijui historia ya Lipumba? jaribu kusema mambo yenye mantiki na pia huna data huna haki ya kuzungumza hovyo hovyo.....

Tuwekee ushahidi kuwa waliwahi kufanya kitengo gani cha hiyo system unayoisema , kwa mzee Mrema naweza kujaribu kukubali ila ninachokijua ni kuwa system ilimfukuza na kumtema kazi kama inavyofanya kwa wengine wengi ambao sina sababu za kuwataja hapa.

Weka ushahidi hapa acha kubwabwaja .....
 
Ninalijua Ri-jamaa hapa JF ambaye yuko radhi kuwanunulia viongozi wa CCM anything, lakini sio ndugu zake wala wazazi wake, Ri-jamaa litawanunulia hata watoto wao mizawadi isiyokuwa na mfano, litajipendekeza weee, mpaka kuwafuata viongozi kwenye majimbo yao ya uchaguzi na kujifanya lina NGO huko majuu, kumbe ni Ri-ongo likubwa na viongozi walishalishitukia, lakini hata uliambie nini ni kazi bure,

Ahsante Wakuu!

Mzee hiyo unayosema ni kweli kabisa. Inasikitisha sana kuona hali hii ipo na inaendelea kuwepo, simply put ni unafiki. Hao watu wanakuwa wanafanya hivyo kwa kulinda maslahi yao fulani. Mimi mwenyewe nimewasikia baadhi ya waheshimiwa wakiongea sense kwenye mambo mengi yanayohusu maslahi ya umma, lakini hao hao wakiongea kuhusu msimamo wa chama au vitendo vyao vinavyohusu msimamo wa chama vinakuwa tofauti kabisa na dhamira zao.
Unashangaa sana hapa ni nini kinaendelea, at least sasa tunaona wengine, ndi hata wanajaribu kusaidia kuonesha hizi issue za BOT na nyingine. Mimi hata ninapoambwa na wazungu your country is doomed, nainamisha kichwa tu naona sio tusi, kwa sababu naambiwa ukweli unaouma.
 
Kama tungejivunza kujenga hoja zetu kimantiki na kutumia evidence kidogo ingetusaidia sana. Tatizo moja kubwa tulilonalo kama taifa ni kwamba watanzania mara nyingi tumekuwa wepesi sana kukubali propaganda. Sasa kwa mfano kwa kuwa huyu ndugu yetu aliambiwa na mzee Kassim Maguto, basi imekuwa kweli as if huyu mzee alikuwa na uwezo wa kusoma yaliyomo nyoyoni mwa hao viongozi wa upinzani bila hata kutafakari kidogo lengo la Maguto kusema hivyo lilikuwa ni nini. Hivi, kwa mfano, leo ukienda kuongea na Tambwe kuhusu CUF au upinzani kwa ujumla unategemea kusikia nini zaidi ya kashfa na matusi lukuki dhidi ya upinzani?

Sasa mkuu, ungekuja na argument strong kidogo, lakini hii ya kuanzisha thread nzima on such a big topic kwa kutumia maneno uliyoyasikia kwa mzee Maguto kidogo ni below the standard of this forum.

Tufike mahala pia tuache kuwaweka wapinzani wote katika kapu moja. Tusiwe kama wazungu wanaofikiri Afrika yote ni moja, wakiona wanyarwanda wanauana basi wanajua ndio wafrika wote walivyo. Sasa vyama vya upinzani vipo zaidi ya 15 so far na inawezekana kesho kikazaliwa kingine. Tuwe very specific, ni chama gani tunaongelea. Tuachane na hii tabia ya kusema jumlajumla wapinzani, hii haitusaidii sana kwa sababu hata CHAUSITA, NLD, pia ni vyama vya upinzani.
 
Kitila thanks kwa kumwelimisha huyu jamaa kwani hajitambui na pia hajijui bila shaka ........
 
Ahsante, siwezi kujenga hoja kwa nisolo lijuwa, nimebainisha na kuweka wazi niliyoambiwa na mmoja wa hao watu aliyekuwa kwenye system.

Kitu kinachowatatiza wengi hapa ni kuwa mnakimbilia kuvitaja vyama, vyama si tatizo, tatizo ni viongozi, na kwa hili ni baadhi ya viongozi si wote, ni hao niliotajiwa kuwa ni system.

Kuna ubaya gani gani tukianzia kwa kuwa-chomowa hao kwenye vyama na kuhakikisha kuwa tunapata damu mpya, wapo kina Zitto na wengine wengi tuu ambao hawajakuwepo kwenye serikali ya ssiem wala sisiem yenyewe wala hawajakuwepo kwenye vyama vikianzishwa (labda walikuwa darasani bado).

Siongelei vyama vya vya upinzani hapa, naomba nieleweke kwa hili, naongelea viongozi ambao wametajwa na mwenzao kuwa wapo kwenye system kama alivyokuwa yeye. Na kama ni hivyo basi, hawana faida katika upinzani wa kweli.

Wala kuwa na vyama vingi vya upinzani si tija, bali ni kujivunja zaidi nguvu (devide and rule), cha muhimu ni kuubaini uozo uliopo na kuutowa kwa kutumia damu mpya.
 
Nakumbuka Mwalimu aliwahi kusema kuwa upinzani wa kweli utatokea ndani ya CCM, sasa sijui ndio alikuwa anatuandaa tukiona watu wanatoka CCM kuanzisha chama kingine tuone huo ndio upinzani wenyewe haswa na wale ambao hawakuwa CCM(ila enzi za chama kimoja sidhani kama kuna watu ambao hawakuwa CCM) wakianzisha vyama tuwaone si wapinzani wa kweli bali wababaishaji tu.

Sasa kama hiyo ni kweli je nitakosea kuhitimisha kuwa Mwalimu alikusudia CCM iendelee kuongoza nchi daima dumu?

Mtazamo wangu: Kwa sasa upinzani bado ni mchanga mno. Upinzani wa kweli utatokea pale chama tawala kitapomeguka na baada ya hapo itachukua miaka kama kumi ya kupata upinzani wa kweli.
Kinachoondelea sasa hivi ni kwamba walio wengi ni wapinzani kwa maslahi binafsi.
 
Kitila thanks kwa kumwelimisha huyu jamaa kwani hajitambui na pia hajijui bila shaka ........
Mie nadhani nyie ndio hamjitambuwi na wala hamuelewi mambo yanakwendaje, mnayatazama kijujuu tuu. Kama nyinyi ndio wapinzani wenyewe, basi kazi ipo kweli kweli, si leo wala si kesho, kwa sababu hata ninachokisema hamkijuwi wala hakiwaingii hata kidogo, lakini kwa kuwa tupo kwenye gari moja, haya twendeni tutafika tuu, iwe leo iwe kesho, Je huijuwi system ni nini?
 
Kitila mimi na wewe ni Wapinzani na hatuna connection na system anasemaje jamaa ?.

Nyie mnao ngojea maneno ya Mwalimu yatimie fikeni mahali mbadilike si kila nabii alitabiri yaliyo tokea. Tumemuona Nabii mmoja muongo hapa JF na kalala mbele naye tuamini na tungoje ?
 
Mtazamo wangu: Kwa sasa upinzani bado ni mchanga mno. Upinzani wa kweli utatokea pale chama tawala kitapomeguka na baada ya hapo itachukua miaka kama kumi ya kupata upinzani wa kweli.
Kinachoondelea sasa hivi ni kwamba walio wengi ni wapinzani kwa maslahi binafsi.
Dotori, hiyo unayosema inaweza ikawa ni kweli kabisa na pia inawezekana kuwa viongozi wengine wapo kwa kuwa wamekula kiapo cha system, mpaka waondoke hao na waje ambao hawajalishwa kiapo, ndipo tutakapoona upinzani wa kweli. Jee huijuwi sysytem ni nini?
 
Kitila MKumbo unanikumbusha enzi za Nkurumah na Rev square.
Unachosema ni kweli kabisa, hatuwezi kuviweka vyama vyote kwenye kapu moja, na hatuwezi kusema vyama vyote ni trick ya serikali kuwa-fool international community kuwa Tanzania ni nchi ya vyama vingi, wakati wengine mapaka leo tunaona kuwa de facto ni bado ni chama kimoja, tena ni kimoja worse kuliko tulivyokuwa chama kimoja de jure. Nasema hivyo kwa sababu opposition bado haijaweza kutupatia alternative tunayoitaka, itakayotupa chama tunachoweza kusema hiki kinaweza kushika dola. The opposition have been very disappointing, in most part wamekuwa wana act kama observer wanaosubiri kuingia bungeni na kusema Serikali imefanya hivi au vile. Lakini bado hatujaona juhudi za kujenga chama na ku-reach out the grass root na kujifahamisha, kwa sera na strategies zinazotekelezeka zitakazoondoa umaskini na unyonge kwa wabongo. Sasa hivi unaona kabisa kuwa CCM inatumika kisawasawa na mafisadi. Kile chama cha wakulima na wafanyakazi, au kile chama cha kutetea wanyonge hakipo tena, kilichopo sasa ni chama cha kutetea watu kama kina Dito, Patel na watu wa design hiyo, wengine wanatumiwa tu. Kwanini nyie chadema msijio-rganise na ku-capitalize kwenye hilo mkatupa tunachotaka. Mmeonesha mwanzo mzuri, lakini that is only a tiny part of what we want here.
Vyama vingine unaweza kuzungumza mwenyewe, vingine vimeanza na vimekufa vingine vimekufa, na kingine umesema kinaweza kuanzishwa kesho, lakini ukiangalia tofauti yao ni nini? vimeanzishwa kwa nini? sera zao zinatofauti gani na CCM, hupati jibu ndio maana unaona ni bora hata kuishughulikia hii CCM ili iwe nzuri, isuwe ya wezi na mafisadi. Hayo ni maoni yangu, i might be wrong!
 
Zomba unajichanganya sana kwani unasema huvisemi vyama bali unawasema viongozi wao ile hali kichwa cha mada yako kimesema naomba kunukuu....UPINZANI HAKUNA TANZANIA NI UONGO MTUPU......

kama ulimaanisha viongozi kwa nini hukusema viongozi wa u[pinzani ni system na sio kuweka general kama ulivyofanya .

'watakuwa tayari kuwatetea mafisadi kwa sababu hawawezi kuishi bila kuwasujudu mafisadi>
 
Back
Top Bottom