- Thread starter
- #2,521
Unasubiri nini, mwaga elimu na wewe.Ngoja tusubiri kashaanza kuelezea.
Simba.
Unasubiri nini, mwaga elimu na wewe.Ngoja tusubiri kashaanza kuelezea.
Huko ndiko walikotoa tulio, Lidafo, Etugrul Bey Nourhan na mashehe zao, labda kuelewa au kuto kuelewa.Mwanzo 2:21-23
[21]BWANA Mungu akamletea Adamu usingizi mzito, naye akalala; kisha akatwaa ubavu wake mmoja, akafunika nyama mahali pake,
And the LORD God caused a deep sleep to fall upon Adam, and he slept: and he took one of his ribs, and closed up the flesh instead thereof;
[22]na ule ubavu alioutwaa katika Adamu BWANA Mungu akaufanya mwanamke, akamleta kwa Adamu.
And the rib, which the LORD God had taken from man, made he a woman, and brought her unto the man.
[23]Adamu akasema, Sasa huyu ni mfupa katika mifupa yangu, na nyama katika nyama yangu, basi ataitwa mwanamke, kwa maana ametwaliwa katika mwanamume.
And Adam said, This is now bone of my bones, and flesh of my flesh: she shall be called Woman, because she was taken out of Man.
Wewe mwaga elimu ya upande uujuao.Kwanini hii elimu imeegamia upande mmoja wa dini?
Huko ndiko walikotoa tulio, Lidafo, Etugrul Bey na mashehe zao.Mwanzo 2:21-23
[21]BWANA Mungu akamletea Adamu usingizi mzito, naye akalala; kisha akatwaa ubavu wake mmoja, akafunika nyama mahali pake,
And the LORD God caused a deep sleep to fall upon Adam, and he slept: and he took one of his ribs, and closed up the flesh instead thereof;
[22]na ule ubavu alioutwaa katika Adamu BWANA Mungu akaufanya mwanamke, akamleta kwa Adamu.
And the rib, which the LORD God had taken from man, made he a woman, and brought her unto the man.
[23]Adamu akasema, Sasa huyu ni mfupa katika mifupa yangu, na nyama katika nyama yangu, basi ataitwa mwanamke, kwa maana ametwaliwa katika mwanamume.
And Adam said, This is now bone of my bones, and flesh of my flesh: she shall be called Woman, because she was taken out of Man.
Hicho kisa cha "adamu" kiko wapi, ulichonipa? Qur'an au Biblia?Kama hazina sawa, Mimi nishakupa zenye kisa cha adamu.
Muite Arsis ajibu maswali yamekuwa mengi
Nimefurahi unaanza kupata elimu na kukiri kama hivi "... Ndio quran haijasema kuwa Adam Ni binadamu."Hoja yako hapo ni nini sasa?
Rudia kunisoma hujaelewa.
Fikra zako hazipo sawa, sisi tunasema Adam hajatajwa kwenye Qur'an kua ni mtu wa kwanza, mmeyatoa hayo kwenye biblia.Ko huenda kwamawazo yangu kunafikra inapenyezwa kuonyesha kwamba Adam sio binadamu wa mwanzo na hao majini watataka kuja na hoja kwamba ndio maana waligoma kumsujudia
Tuwe makini Kuna mengi yajayoooo. Tuwe macho nakutumia fikra zetu kutafakari hizo fikra na ajenda atakazo kuja nazo.
Waislam wengi ni wakristo wa zamani, au wao au wazazi wao. Naamini Mkristo wa kweli ni Muislam.Wewe ni muislam mie mkristu halafu unajua dua zako mie sio kama wewe wewe ni mganga mie naona tu vitu kwa mtu mwenye hitaji nakumwelekeza akatibiwe mahali basi. Sasa nikikuambia jambo maana mie bado nasaidiwa mambo na watu ambao nao ni wanao yao huoni majini yako yataniandama nikikuelekeza ukawa na nguvu zaidi ya hapo kama msaada maana kuna vyakutoa nanaogopa kusema nisirudiwe nalo .
Thanks for this very interesting thread, please do us a favour, compile all episodes into thread starter.Ilikuwa ni siku chache kabla sijatimiza miaka 18. Nilipelekwa Tanga, kijiji kimoja kipo karibu sana na mpaka wa kwenda Kenya. Kabla ya kuingia huko kijijini ndani kuna ki mji kinaitwa Duga. Ilikua sio mara yangu ya kwanza kupelekwa huko kwa mambo ya kimila na jadi.
Limka za muendelezo zipo chini hapo.
Hayo utajaza wewe kondoo wa bwana.Faiza, uliandika nyuma hapo "tunapangwa" how come 'unaumwa' ?
Nimefurahi kwa bingwa na gwiji wa uandishi kama wewe kuliona hilo.Thanks for this very interesting thread, please do us a favour, compile all episodes into thread starter.
Nimesoma page one nikavutiwa sana, nilipokuta kuna pages 128!, nikaishiwa nguvu!.
Please do the needful. Hii story ukiiweka kwenye kitabu kitakuwa best seller!.
P
nzaghamba naona na wewe umepigwa na mshangao.Nimefurahi kwa bingwa na gwiji wa uandishi kama wewe kuliona hilo.
Nitawapata wapi publishers, kisa cha kufunguliwa macho ni kirefu sana, ninaishi katika hali hiyo kwa zaidi ya miaka 30 sasa.
Nimekusoma kuhusu Karma mpaka nilipokuona umeandika hapa, nimemuuliza Arsis, ni nini maana ya Karma? Amecheka sana, jibu alilonipa bado nimepigwa na mshangao, kama ilivyo kawaida yake, elimu yake ina mitazamo tofauti kabisa na majibu yake ni tofauti na matarajio yetu.
Simba.
Hio hadithi unayosema "mtume amefasiri na kusema ndio binaadam wa mwanzo" iko wapi? hujatuonesha.Mtume amefasiri hadithi nakusema Adam ndio binadamu wamwanzo
Sema kama unapinga Hilo na wakati dini yote imefasiriwa kupitia hadithi Kila kitu kimefundishwa kupitia hadithi za mtume
Wewe unaswali umejifunzia wap kuswali? Quran imesema watu wasimamishe swala je imekufundisha namna ya kuswali? Quran imekuelezea adhuhuri utaswalije na magharib utaswalije? Quran imekufundisha namna ya kuswalia maiti? Quran imekuambia ukahiji makka je imekufundisha namna yakuhiji? Quran inasema watu waoane na ww umeoa je unajua ndoa ili iwe ndoa bila ya mafundisho ya mtume na hadithi?
Kwahiyo kama hayo yote unayaamini na kufanyia kazi ww mwenyew elimu ndogo yaani hadithi imekufundisha jinsi yakuswMtume amefasiri hadithi nakusema Adam ndio binadamu wamwanzoali? Hadithi zimekufundisha namna ya kuhiji? Hadithi zimekufundisha namna yakumswalia maiti na mambo mengine mengi,,,,hvo hvo kupitia hadithi amesema na kufafanua Quran kuwa Adam ndio binadamu wa mwanzo,,,,,,kupitia hadithi mtume Muhammad amemtaja kwamajina dhahiri mke wa Adam alikuwa akiitwa Mtume amefasiri hadithi nakusema Adam ndio binadamu wamwanzoHawa,,,,,,ko usiwe jitahidi kuwa mwelewa na usikaze ubongo
AKIJIBU HII HOJA KWA HOJA MNIITE NMMtume amefasiri hadithi nakusema Adam ndio binadamu wamwanzoEKAA PALE HII MESEJI ATAIPITA KAMA ANAAGA MAITI
Vionjo vya Arsis 5 - 1"theology"
Vionjo vya Arsis 4 Kumwokoa Msukule Unguja 8.
Inatokea post namba 2358.
Sheha; wachawi wenzenu wengine wa hapa mtaani ni kina nani?
Afisa; Hio ni siri ambayo hatuwezi kuisema hadi kifo. Mmeshatushika sisi na wote waliohusika na hii kazi, ambao hawajahusika hata kanuni za kikawaida zinakatzaa kuhusishwa.
Bakora: Mimi namuunga mkono kwa hilo. Tuendelee na mengine.
Sheha; Tueleze waliohusika.
Afisa; Wameshikwa wote na sikjii kama wapo hai mpaka sasa, maana hukumu ya hili ni kifo tu, haina mjadala kichawi. Hata chama chetu tukikamata waliongilia himaya yetu bila kukubaliana kabla tukiwakamata ni kifo tu. Labda tusiwakamate.
Bakora; Huyu analeta mambi ya kichawi ili apoteze muda. Mimi nashauri kwa kua ewotw wamekiri wahukumiwe.
Sheha, wapelekwe mahakamani?
Bakora; ndio, hilo moja na sisi tutapitisha hukumu yeytu kwanza na nyinyi, hususan wewe, upo hapa Kiserikali huo utakua uamuzi wako. Sisi hukumu yetu, hatuwezi kuisema hapa mbele za watu, tunajua tuwajulisha vipi, hatutaki kesi.
Sheha; Nimeelewa. Mimi wacha nipige simu polisi, mkubwa wa kitiuo cha hapa jirani namfahamu.
Bakora: hautompata huyo leo, wala kesho. Labda umpigie msaidizi wake.
Sheha, aah kasafiri?
Bakora; Ndio.
Sheha, wewe ngeni Sheikh, unajuaje?
Sheha: Mimi tunafahamiana nae, najua kua kasafiri alfajiri ya leo. Uliza hata ofisini kwao waytakueleza.
Sheha; Sasa tunafanyaje?
Bakora; Wazo la kuwashitaki hawa ni zuri, ushahoidi woite upo na wao lazima watakiri hawatoisumbua mahakama, kwa kua binti yupo hai, sijui hukumu yao itakuaje kiserikali.
Sheha: Wacha nipige simu hapo nje,. jamani akam kuna hawa leteni ytunywe. Haya si mabo madogo, maana naanza vbipi kuwael;eza polisi?
Bakora: Waeleze ukweli kama ulivyouona na kuusikia kuanzia alfajiri. Watuhumiwa si hawa hapa mnao?
DSheha; Sawa wacxha niende nje nikapige simu.
Kijana: Na mimi wacha niende nje, kweli kama kuna kahawa uje jamani.
Kuna wanawake wakainuka, waksema kule ipo nyingi wacha tukalete na vikombe.
Mimi, Kijana, Balora tukatoka nje. na wengine wote wakatufata kasoro watuhumiwa tu. EWakabaki wamekaa, kama wamepigiliwa misumari.
Kutoka nje mimi na kija n na Bakora yukaenda kukaa pembeni, tukawacha pale Waunguja na Sheha wao.
Bakra: sasa hapa kaszi imeisha, hawa sisi tutatimiza hukumu kama ya wale, hawatiweza kufanya kazi kabisa, lak9ini cha kwanza inatakiwa mali za yule bwana lazima huyu binti na mamake walipwe kwa machungu waliopitia. Na huyu mumewe, ndio hana chake tena. Mtito yule asafiroshwe kabisa asibaki Unguja, maana hii hadithi tayari ipo mitaani saa hizi inazagaa kama moto wa makumbi.
Kahaw aikaja tukanywa pale.
Sheha; Polisi wanakuja kikosi cha maana.
Bakora twendeni ndani tukamalize sisi tuna safari jamani, hapalkaliki.
Tukaingia ndani wote, mimi nikaitwa ndani na kina mama huko, nikakuta kumbe mipango yao ya kumsafirish binti kwenda bara ytayari lakini hakuna alieambiwa, na ataondoka na mama yeke mdogo, kimyakimya. Nikaone heri. Ikaja sauti ya Arsis kichwani ikinambia, usiwe na wasiwasi, yupo chini ya ulinzi wetytu, wewe uytawaona Datr hao. Nyyie mnawsza kusafiri wakija polisi anagalia msisema lenu mkafanywa mashahidi, itakua ngumu kwenu nenda rudi. Nikamuelewa.
Ile tunatusi ndani hatujjakaa polisi wamegonga nje, akatoka Sheha akaanza kuomngea nao, nje, na sisi tukaaga,m hakauna aliesema chochote. Tukatoka mimi, Bakora na kijana, mama ndani huko washasuka kuondoka na binti na mamake mdohgo. Tukaondoka.
WWale mbwa wawili wakachukuliwa wakapelkwa polisi, wakaelezea kama walivyoelezea, wkawekawa ndani bila dhamana, mahakamni siku ilipofika kwa kua wanakiri makosa, wakahukumiwa jela. Walipokua jela ndio hukumu ya majini walioifanya hio kazi ikapitishwa.
Tutaendelea na kionjo kingine tutaporusi, hiki cha Unguja tukimalizie hapa.
Simba.
Itaendelea
Simba
Nyingi hapo ni fikra zako au za kujikusanyia kwa wengine wasioamini Mungu.Hadithi za Biblia, Quran na Torah; ni myth and legends tu za Middle East.
Theory of ‘legend and myth’ (over time they evolve).
Kwenye evolution ya hizo stories zikaja variation luluki.
Kabla ya dini rasmi kwanza watu wakachagua mtindo wao wa kufanya ibada na version zao za story ambazo zi kubadilika over time (given the theory of undocumented stories).
Japo watu walikuwa na imani ya ‘monotheistic god’ lakini baada ya muda kukawa na mitindo kibao ya kufanya ibada given the version of story ilivyobadilishwa kwenye eneo.
Jews wakawa wa kwanza kurasimisha kitabu maandishi yepi (version ipi inakubalika) kikaundwa kitabu cha Torah.
Wapili nani jibu lake mtihani (but factually most likely were Muslims, given the logic). Kwanini kwasababu hizi dini mbili zinafanana sana taratibu zake na wahusika wengi walikuwa Middle East, hata forms of Christianity za maeneo hayo zinafanana na hizo dini mbili.
Tofauti ya Jews na Islam ni New Testament (kwenye biblia). Jews wanaishia kwenye Old Testament.
Tofauti Islam na Muslims na Christians (Japo wote wanatambua, Old Testament) Iła vitabu vyao vina nyongeza ya New Testament (sehemu ya hadithi zao zinapishana) na waislamu wana nyongeza ya Muhammad.
Kwanini Christianity aiwezi kuwa dini ya pili, promoter wake ni foreigner wa eneo wa msingi wa hizo ‘myth and legends’. Na historia inasema Constantine kabla ya kuamuru kuandika biblia alikuta wenyeji hawajielewi (isipokuwa Jews walikuwa tayari washachagua version ya kitabu) Ila mtindo wa kufanya ilikuwa bado.
Kwa hivyo ilikuwa bado vurugu machi kwenye kufanya ibada na kuchagua version sahihi. Constantine akaamuru mtindo wake wa kufanya ibada na kuchagua version yake ndio ikaundwa biblia na utaratibu rasmi wa kufanya ibada (sasa shughuli ya kulazimisha wengine wafuate huo utaratibu sikia tu).
Halikadhalika wenyeji nao wakaunda kitabu kingine chenye variation ya myth wanazotaka ndio Quran.
Ndio maana utaratibu wa Quran na Turah culturally unafanana sana, it resembles wenyeji, whereas Christianity ina tofauti kubwa sana nao culturally kwa sababu Constantine aliingiza mambo yao ya paganism ya masanamu. Na Ukristo uliokuwa unafanana na Jews na uislamu culturally cha moto walikiona wasiotaka kuelewa kitabu cha Constantine na masanamu yao.
Je hawa ndio sahihi kwenye dini kuliko Buddhist, Hindus na kadhalika (personally I don’t think so) to me those are myth just as Greek Gods, Norse Gods and those of other culture (shida ni kwamba hazikuwa monotheism).
View attachment 3084685
Uhalisia ni kwamba sisi tunaishi kwenye hako kajiwe kadogo sana kwa picha iliyopigwa na rover from mars. Hako kajiwe chetu kina watu kila pembe (kila mtu ana mbingu yake tofauti) ukikakinganisha na Jupiter ni kubwa mara mia. Ukikafananisha na jua kadogo mara million moja. Yaani tunaishi kwenye kajiwe kadogo sana kwenye solar system. Achilia milkway gallaxy (yenye nyota kati billion 1 mpaka mbili na luluki zina solar systems na pengine life). Let alone the universe which is estimated to have trillion galaxies. We are so insignificant in this universe.
Kila mtu akiangalia alipo anaona nyota na galaxy. Hakuna mbingu labda tuamue kwa pamoja mbingu yetu ni jua lilipo.
Sasa aina maana hiki kijiwe chętu hakina maajabu ya kujiuliza binadamu tumetokea wapi. Personally I don’t buy the evolution theory na naamini kwenye spiritual world. Shida zaidi ni kusikiliza huu upuuzi wa dini na kulumbana based on ‘myth and legends’ za M.E now that’s just stupid us.
Dini ni hadithi tupu, aina maana hakuna spiritual world.
Hayo maneno.Vionjo vya Arsis 5 - 1
nilivyokutanishwa na majini ya Kingazija (Comoros) na Kipemba Kojani.
Baada ya kurudi kisa cha Unguja mengi sna yaliendelea lakini kw aufupi nilirudi kwenye maisha yangu kawaida ya kwenda kutengeza magarei na kushughulika na kiduka changa kidogo, kwa siku hizo, cha spare za umeme wa magari.
Tulipoondoka unguja, yule binti na mamake walikuja Dar na mamangu, ilifanywa siri kubwa kuondoka kwao na wakaja kwa ndege ya kukodisha na ndugu wengine ili waweze kujifich kuondoka kwao, kuepusha kujulikana kwani Unguja minong'ono ya kisa ilikua mingi.
Kwa ufupi yule mama nilikuata nae Dar na binti yake lakini hawajakaa sana Dar wakaondoka nchi za nje, walikua hawana kabisa hamu na Tanzania, bara wa Unguja. Mambo yaliwakumba si madogo.
Katika kua nao Dar, yule mama akanihadithia kua mwanamke aliemstua, alikua ni mke wa yule DSheikh wa Unguja tulikua nae siku ya kikao na wahalifu. Akanambia yule Shehe ndio tuna w))wasiliana na kamuomba namba zangiu za simu, nikampa. Tukawa na mimi tuna mawasiliano ya hapa na pale na yule Sheikh.
Siku moja akanambia kwenye simu, Simba, nafahamu ulikua kimya sana kwenye kikao cha siku ile ya hukumu pale nyumbani lakini mimi naelewa wewe ndio ulikua kiongozi wa yote yale ingawa u kijana mdogo sana. Nafahamu kwa pete yako ulioivaa, hio pete sio ya kawaida kabisa na wenyewe waliokipa hio pete wana nguvu kubwa sana. Natamani niwaelewe. Nimeshindwa mbinu zangu zote kuwafahamu.
Mimi; Unafikiria tu hivyo.
Sheikh, mimi nafahamu babu yako na namfahamu yule Sheikh wa Tanga mlikja nae tulikutana nae kwa babu yako tanga miaka si mingi sana nyuma. babu yako ndio mwenye hio pete, naona kakuachia mikoba.
Mimi; hapana, ana yake.
Sheikh: mimi nimeongea na babu yako juzi, kuna tatizo jingine kabisa limetukabili, akanambia niongee na wewe. Toka siku zile mnaondoka mimi nawasiliana na babu yako. Nilifikiri kakujulisha kua tunafahamiana.
Mimi: Nafahamu mnafahamiana, toka nilipokua Unguja.
Sheikh; Sikiliza Simba, kuna dada mmoja niDaktari wa binadam, huyu dada ni mgazija, na yupo huko huko Dar. lakini ana matatizo makubwa sana ya mambo yao ya majini ya Kingazija sijui ya hapa Unguja, maana huyo ameshaolewa mara mbili, zote na madaktari hukohuko dar, lakini zote kaachika, mmoja kazaa nae, mmoj hajawahi kuzaa nae. Wazeew wake walinifata hapa Unguja, ni watu maarufu sana, wakamleta hapa Unguja, tuamshugulikia sna, lakini hayo majini yanatulia anafanya mamboi yake vizuri sema ayataki kabisa awe na mahusina na mwnamme, binti wa Kiislam ana kisomo chake, ana mtoto wa kike mmoja, lakini kawa mlevi, hatoki ma klabu ya starehe huko na hata akija hapa. Wazee na ndugu zake sio watu wa hivyo kabisa, anawaibisha sana. Simba tunamsaidia vipi huyu ndugu yetu?
Mimi; Kewa jinsi unavyonieleza, huyu mkamate koo babu. Mimi siyajui kabisa mambi haya jamani. Mimi ni kama bendera, nasukumwa na upepo tu, unakovuma ndio hukohguko.
Sheikh: sasa huo upepeo umevumia kwa huyo binti wacha ukupeleke utakavyo. babu yako kasema tuongee na wewe, anakojua hiki kisa chote.
Mimi: Sheikh mimi na nakushauri huyo mchukueni tu mumpeleke kwa babu, mkimfikisha pale babu hachomoi, itabidi amshughulikie tu. Lakini mimi binagsi siyajui yote hayo.
Sheikh; Nimekuelewa sana Simba, wacha tuone tunafanya nini maana huyo binti ukimuona wala huwezi kujua mambo yake, anaishi vizuri tu anapoata kazi nzuri nuri tu, lakini atishi maisha ya kihuni mpaka lini? Aliekua mumewe ni Daktari mkubwa sana na mwenye heshima sana Tanzania.
Tutaongea tena Simba ikiwezekana, waha niendelee kumrai babu yako atusaidie. Kumwedea ghafla itakua si vizuri, na hatujui hata kama huyo binti atakubali kwenda, babu yako kasema Dar hawei kuja kwa sasa tuongee na wewe.
Mimi; Ongeeni nae tu, babu mtaalamu, mimi sina nilijualo.
Tukaagana kwenye simu. Siku kama tatu kupita babu yangu akanipigia siimu. Tukasalimiana, kama kawaida yetu tukataniana kidogo, mtu na wajina wake. Akalianzisha...
Babu; Simba, vipi unakataa kusaidia watu?
Mimi; Vipi tena babu? (Ingawa nilijua anamaanisha nini).
Babu; Sheikh... wa Unguja kanipigia simu, kanambai aameongea na wewe, lakini anachokwambia unamsukumia kwangu, usifanye hivyo Dimba, huyo binti yupo Dar, itakua wepesi sana wewe kumuona, tena Sheikh anasema kuna bwna mmoja wa Kipemba yupo hapo Buguruni si mbali na kwenu, anajaribu kumsaidia hiyo binti kimatibabu, lakini Sheikha ansema anasema hata huyoi binti atakata tamaa maana muda unazidi kwenda, haioni ile tija anaoitarajia.
Mimi: Buguruni ya wapoi hio, babu usifikiri kila buguruni ni karibu ya ketu, buguruni kubwa.
Babu: Cha msingi sio hicho Simba, hata iwe mbali vipi, nyie mna magari huko, hamtembei kwa miguu, halafu buguruni si ndio njia ya kwenda na kurudi kazini kwako Tabata?
Mimi; Babu, ukitaka lako unajidai profesa. Niache nipambane na magari huku, wewe pamna na binadamu. Hizo kazi zako zinatisha, kashesje la Unguja halikua dogo.
Babu: Simba, kwani wewe unafanya nini zaidi, wewe wawachie wenye kazi zao, mimi nataka wewe ujifunze ya dunia, ujionee mwenyewe ndio kuna siku utaona ni heri usaidie watu kuliko kusaidia magari.
Babu; Wewe arrange siku tu na huyo Sheikh wa Buguruni ukamjue, ni vizuri, utajionea wanavyofanya tiba zao, ni elimu hio. hakikisha tu siku unayokwenda na huyo Dada awepo anashughulikiwa, wewe uwepo kama mtazamaji tu, tuanzie hapo Simba.
Mimi; babu mbona unanipa kazi ngumu?
Babu: nenda, unaweza kukuta toto la Kingazija jisomi hilo, limenona, ukajipaytia mke wa Kunguja. Muhimu wewe nenda, yule Shjheikh hatojua umeenda kufanya nini, mimi nimemwabia huyu Sheikh wa Unguja rafiki yake, asimwambia kabisa unaenda kufanya nini, yeye amwambie, wewe unaenda kwa mabo yakohuyoi Sheikh, lakini yeye mwenyewe Sheikh atanuelea, hatomueleza chochote kuhusu kazi zetu, maana hawa waganga wengi waoo wachawi tu, hatopenda kuingiliwa himaya yake.
Mimi: babu mimi sitaki, kwanza umeshanitisha hapo, yamalizeni wenyewe.
Babu; Usiwe hivyo, usikatae mwito kataa uliloitiwa.
Mimi: Si nimeshajua ninaloitiwa babu?
Babu; Simba wacha niende, tutaongea kesho, naona leo hatuelewani lugha.
Nikacheka, babu na yeye akacheka, akanichomekea, huyo mtoto ukimuona na sifa zake nilizopewa natamani nije huko Dar, toto, toto kweli, si mchezo. Unamuogopa sana mkeo?
Mimi; Njoo wewe babu.
Babu; Natamani kuja, lakini umri ushakimbia tena.
Mimi: babu kawahi kusali, wacha na mimi nikawahi. Kwa heri
Tukaagana pale. Nikaendelea na mambo yangu.
Simba.
... 5.2
Soma vizuri post yangu uone msingi wa Torah, Bible na Quran.Nyingi hapo ni fikra zako au za kujikusanyia kwa wengine wasioamini Mungu.
Umeshaisoma Qur'an?
Simple question: Umeshaisoma Qur'an?Soma vizuri post yangu uone msingi wa Torah, Bible na Quran.
Ukipata msingi wa foundation zake ndio utaelewa source ya tofauti zake kutokana na watu walioamua ku-accumalate information wanazotaka.
Au wewe kweli unaamini Quran ilishushwa kutoka mbinguni kitabu kizima?
Before I answer that who wrote the Quran and its source.Simple question: Umeshaisoma Qur'an?
Sasa sikila jini hapo ulionalo safiWaislam wengi ni wakristo wa zamani, au wao au wazazi wao. Naamini Mkristo wa kweli ni Muislam.
Sihitaji msaada, haya aliniochia babu yangu soiyatumii. Ukiusoma vizuri huu mjadala utaona hata waliposaidia kutoa matatizo ya watu, mimi nilikuepo tu kwa kua ni marafi zangu. Lakini sijawahi kufanya kazi ya uganga, isipokua nikikutana na mtu ana matatizo na naweza kuyatatua namtatulia. Mwiko kukataa, hata nikikataa wanakuja wao wanasaidia.
Majini wanaotaka uwafanyie na wao vitu vyao, hao sio wema ni wachawi kwa mujibu wa Arsis.
Kama unakumbuka kisa cha Unguja? Baba yule alianza kwa kutoa jogoo ikaenda akaanza mbuzi, ikaenda ikawa ng'ombe, ikaenda ikawa ng'omba, ikaenda ikawa ngamia, ikaenda ikawa nyama na damu za watu, mwisho kamba ikakatia kwa binti yake.
Simba.
Mkuu anzia mwanzo 2:7Mwanzo 2:21-23
[21]BWANA Mungu akamletea Adamu usingizi mzito, naye akalala; kisha akatwaa ubavu wake mmoja, akafunika nyama mahali pake,
And the LORD God caused a deep sleep to fall upon Adam, and he slept: and he took one of his ribs, and closed up the flesh instead thereof;
[22]na ule ubavu alioutwaa katika Adamu BWANA Mungu akaufanya mwanamke, akamleta kwa Adamu.
And the rib, which the LORD God had taken from man, made he a woman, and brought her unto the man.
[23]Adamu akasema, Sasa huyu ni mfupa katika mifupa yangu, na nyama katika nyama yangu, basi ataitwa mwanamke, kwa maana ametwaliwa katika mwanamume.
And Adam said, This is now bone of my bones, and flesh of my flesh: she shall be called Woman, because she was taken out of Man.