Kisa cha Adam; Utangulizi 2
Salaamoun Alaikoum.
Ni nini mbu?
Licha ya Tafsil na Lisan, mbinu muhimu sana iliotumika ndani ya Qutr’an ni ‘dhikr”, dhikra kwa tafsiri za wengi ni ukumbusho, hapa tunalitumia neno ‘dhkr’ kumaanisha visa na hadithi za ndani ya Qur’an, kama tulivyoeleza kwa uchache juu huko, kua asilimia zaidi ya 60 ya Qur’an ni visa na hadithi mbali mbali, visa na hadith hizo ndizo dhikr zenyewe. Hili la dhikr ni somo la kipekee ambalo kila tunavooendelea na hiki kisa cha Adam tutaliona umuhimu wake.
Kwa hio mpaka sasa tuna mbinu tatu za kuifahamu Qur’an, “Tafsil, Lisan na Dhikr. Mbinu zote hizo sio za kubuni wala za kutoa kwingine kokote ni za ndani ya Qur’an. Tutaendelea kuzionesha kila zinapotumika kwa Ushahidi wa ndani ya Qur’an.
Kama kuna yeyote katika mada hii hajaelewa kitu au hajaelewa kuhusu hizo mbinu, anaruhusiwa kuuliza swali.
Hapo juu, tumeweka aya Q2:26 inayojulikana kama aya ya mbu, tarjama iliotumiwa hapo na Sheikh Muhsin Barwani haikuzingatia mbinu za ndani ya Qur’an tulizozitaja hapo juu. Yaani, Tafsil, Lisan na Dhikr. Nalo hilo limejitokea kwa wanazuoni wengi wa tarjama.
Ukizisoma tarjama maarifu za Kiswahili, ile ya zamani ya Sheikh Abdallah Farsy, utaona ina maneno kadhaa ambayo ni tofauti na alioyatumia Sheikh Muhsin Barwani. Hivyo hivyo kwa tarjama za Qur’an za Kingereza, kila alietarajama kutumia baadhi ya maneno tofauti na mwengine, hilo lnajionesha wazi kwenye hizo tarjama. Ambazi zipo nyingi zaidi ya za Kiswahili.
Katika kuzipitia hizo tarjama nilizozitaja hapo juu, nimegundua kua watarajama wengi, kama si wote, wamefata wa tafsiri wa Qur’an ambao hawajazingatia mbinu za ndnai ya Qur’an. Kwani kila mtafsiri kaleta maana zingine zinatofautiana na mgtafsiri mwengine japo kwa uchavche kama si wingi. Hio inamaanisha ujumbe kusidiwa wa Qur’an hatufikii kama ulivyo kwa lugha ya Kiarabu, kwa kusudio la kua mwongozo ambao kila mmoja anatakiwa aufikishe kama ulivyo kwa lugha yake ya asili iliotumika au ukaribiane kabisa ki maana na kusudio la kufikishwa kwetu mwongozo huo na Allah.
...