CUF waende popote kushitaki na wataonekana wajinga na mahayawani wa kutupwa. Ni ukosefu wa mawazo kwa kuwa na ubongo ulioganda.
Waende watakapo kuishitaki CCM, na kama haitoshi huko Ulaya na America basi waende kwa waarabu pia.
 
Nimetafuta sana sehemu yoyote katika habari hii inayosema kuwa Seif kaenda kushitaki ulaya sijaiona. Kama kuna thread hapa zinabadilishwa vichwa vya habari hasa zile zinazomlenga Kikwete kwa vile zinaonekana kuwa za kichonganishi basi na hii nayo ni ya kichonganishi hivyo ibadilishwe kichwa cha habari ili kiwe kama vile habari yenyewe ilivyo
 
Mkuu ktk magazeti ya tz ndivyo walivyoandika ,hii nafikiri mleta maada kacopy tu
 
Nimetafuta sana sehemu yoyote katika habari hii inayosema kuwa Seif kaenda kushitaki ulaya sijaiona. Kama kuna thread hapa zinabadilishwa vichwa vya habari hasa zile zinazomlenga Kikwete kwa vile zinaonekana kuwa za kichonganishi basi na hii nayo ni ya kichonganishi hivyo ibadilishwe kichwa cha habari ili kiwe kama vile habari yenyewe ilivyo

babu, hakuna aliyebadirisha hicho kichwa cha habari, wewe hukusoma kwani hiyo habari ??
 
a9784 hauna habari kuwa Blair alishatoka madarakani.Hapa viko vitu viwili nahii tutake na tusitake.
1.Kwanza ni kuweza kupata support ya Wananchi na ni support ya sehemu gani ni visiwani ambako watapiga kura za maoni.Lakini tukumbuke kuwa alichofanya maalimu baada ya makubaliano alikwenda moja kwa moja ktk chama na wanachama akawaeleza nini walichoafikiana na ata Tamko nalo lilitolewa akiwa anaongea na baadhi ya wananchi wa Tanzania.

Pili ni kupata supprt ya nchi za nje na ni ukweli usiopingika kuwa bila ya msukumo wa Marekani Kenya wasingekuwa na muafaka na ndio maana maalimu anakwenda nje.

Wako Watanzania wanaishi nje na wenyewe wanahaki ya kujua kinachoendelea ndani ya nchi hii.

Chakufahamu ni kuwa historia ndiyo inamsuta Maalimu kwani Muafaka wa mara ya kwanza ni Jumuiya ya Madola walikuwa mstari wa mbele wakishinikiza lakini haukutekeezwa na huu hali kadhalika hivyo naona kama anatwanga maji kwenye kinu.

Rudi kwa wanacuf,jitoe kwenye Muafaka na Ingia msituni na jeshi lako kama suluhisho la Amani linakuwa gumu basi jaribu uhasi

Ni ukweli usiofichika kwamba tunataka Amani kwa gharama yeyote lakini isifikie kila siku ukawasherehesha watu kwa kupoteza muda wao huku unajua nini kinataka kufanyika.

Kam JK aliona umuhimu wa Wazanzibar kujadili Muafaka hakuwa na sababu ya kuwaita cuf peke yao,vyama vyote vya upinzani na chama tawala,NGOs,mashirika ya dini ili kwa pamoja waweze kujaribu.
Na cuf kwa urafi wao wa madaraka wakataka Muafaka ikiwa ndio wao tu washiriki kwa mategemeo kuwa serikali ya mseto itakuwa cuf na ccm.

Ushirikishwaji ulikuwa finyu sana.
 
Huyu jamaa kaenda ulaya ,sasa CCM wameanza kuona yale yaliyotokea miaka ya iliyopita yatarudi upya na safari hii sio Zanzibar tu bali hata upande wa pili ,huyu anapokwenda huko na kuonyesha kuwa haki imeborongwa basi hata zile funguo za misaada hupewa yeye ,yaani kuna watu wana bahati ya kusikilizwa na wazungu na Seif ni mmoja wao ,na vile kumezuka uzushi wa Ufisadi basi ndio kabisa CCM wajitayarishe kutumia rasilimali za mifukoni mwao au watu watazidi kufa na njaa,Sefu Sharif mwisho kwa hatua za kuzuia misaada ,nafikiri Wazanzibari bado hawajamsahau.
Ikiwa tunakumbuka sababu ya kuanguka kwa uchumi wa Nchi ya Zimbabwe ambayo kimaendeleo ilikuwa mbele kuliko Tz kwa masafa na kumfanya Rasi Mugabe aone hata misaada ikizuiwa basi hawatababaika ,tusijidanganye na kusema misaada ya wazungu si lolote si chochote tunaiona leo majigambo ya Mugabe yalipofikia ,ukibadili dola 40 unapata milioni 400 za kizimbabwe ,maana wazungu hawana haraka mambo yao ni mahesabu tu wanajua tulichowapa kitawachukua kama miaka mitano au sita lazima maji wataita mee...!! Na hapa Tz CCM wasione kama wazungu wanawapenda na watawawacha wafanye wanachotaka,hilo ni jambo la kujidanganya na kujipa moyo ,kwamba hawatoachiwa kufa njaa kwa sababu za kisiasa ,wazungu hawana huruma na mtu wapo tayari kuona watu wanakufa na kuuwana lakini usawa wanaoutaka wao unapatikana,mnajua hadi hii leo bado wanawashangaa WaTanzania kwa nini hawawachangamkii mafisadi au hawaichangamkii hii serikali ya mafisadi ,hii ni serikali ambayo inatakiwa ijiuzulu mara moja si ya kuachiwa muda hata dakika.
Serikali iliyooza kwa rushwa na utapeli haina nafasi katika kuongoza nchi inahesabiwa kuwa ni serikali ya kidikteta ,inawaburuza wananchi vile wanavyotaka wao wezi wa mali ya uma wanatamba na kutembea kifua mbele ,hii si serikali ya kuongoza wananchi bali ni serikali ya wachache wanaohifadhiana kwa kutafutiana njia mbali mbali za huyu ni mwenetu au mwenzetu.
Majaribu mangapi serikali ya Kikwete imepata..Ukianza na yule kiongozi alieua dereva wateksi kama sikosei akiitwa Ditopile ,kesi yake inazunguushwa huku na kule.Ukifuata yule Mkuu wa Polisi alietia mimba mfanyakazi wa nyumba kesi yake ipo wapi ? Wizi wa fedha za Umma zimefikia wapi mabilion kwa mabilion
,raisi kufanya mradi akiwa Ikulu ,na wakuu na mawaziri karibuni wote kujihusisha na ubadhirifu wa mali ya umma ,kila kukichwea kunabadilishwa tu huyu anapelekwa huku yule anahamishiwa kule utafikiri wanacheza CHESS ole wao wakumbuke tu kuwa kuna CHECKMATE,huu ni usanii na uhuni dhidi ya wananchi kwa kuwa tu wanainchi wamekaa kimya hawana ubavu na hawana wa kumshitakia hivyo Raisi hawezi kuwatia hatiani eti ni marafiki zake wa karibu kwa habari zinazoandikwa kila siku.Na hili ndilo linalowaangusha viongozi wengi wanaweka urafiki na kazi wanasahau kuwa katika biashara hakuna cha rafiki wala ndugu ,waswahili tunasema cheza na mwenyemali usicheze na mali. Viongozi wa CCM ambao ndio wapo serikalini wanacheza na mali ya Watanzania ipo siku wenye mali wataweka uswahiba pembeni kama Raisi hakuwajibika katika kuwatia hatiani wale wote wanaocheza na mali ya Taifa hili.Maalim Seifu endelea na msimamo wako huo huo na choma utambi kwa baruti kwa upande wako na Wazanzibari na wao watachoma kwa upande wao.Halali mtu.
 
Nilishawahi kusema Maalimu Seif ni miongoni kwa Threats za Muafaka Zanzibar.

Kwa kuwa anatamani ashike madaraka hata kwa siku mbili!!! That is ngangari bwana.

Huko Nyuma nilishawahi kumlinganisha na Marehemu. Jonas Savimbi... ambaye alivyoondoka tu... it took hardly less than 10 days... vita ya miaka zaidi ya 25 ya Angola ikaisha...Ingawa siku zote tuliambia tatizo ilikuwa la chama chake cha UNITA, kumbe ilikuwa yeye mwenyewe Savimbi.

Na leo hii Maalimu Seif akisema siasa basi, au hagombei tena, au uongozi wa siasa basi... Muafaka Zanzibar utapatikana same day/week/month or maximum same year. Kwani Tatizo sio CUF, tatizo ni Maalim Seif mwenyewe.

Kumbukeni munkari wake ulivyopungua alivyoanza kupewa mafao ya Waziri Kiongozi mstaafu...
 
JK alichukua Nchi akaanza kuzunguka Dunia nzima kujitangaza kwamba ndiye Rais baada ya Mkapa je hatukusema maneno haya hapa mkawa mnabisha ?

Nimejiunga mwaka jana mwishoni sasa ningekubishia wapi?
 
Mhhhh!!!!!!!!!!!!
Nashauri wakristo woooote hii kazi ya kupindua wawaachie waislamu kwani hata serikali yenyewe imejaa waislamu au siyo wakulu?

Hakuna haja ya mkristo kushiriki hapo.tutahamia bara woooote wakati wakipindua pindu.

pindua pindu pindu pinduuuuuuuuuuuuuuuuuuuu

POLE MBAGUZI WA KIDINI NA USHINDWE NA ULEGEEE

MZEE KARUME ALIPOSEMA MAPINDUZI DAIMA, HAMAANISHI WATU WAPINDUANE KWA SILAHA.

BALI MAPINDUZI YA KIFIKRA NA KULETA MAENDELEO MSIPOTESHE MAANA HALISI YA MAPINDUZI DAIMA
 
CUF waende popote kushitaki na wataonekana wajinga na mahayawani wa kutupwa. Ni ukosefu wa mawazo kwa kuwa na ubongo ulioganda.
Waende watakapo kuishitaki CCM, na kama haitoshi huko Ulaya na America basi waende kwa waarabu pia.
Kimsingi nakubaliana na wewe. Na hii siyo kama ni mshabiki au mpenzi wa CCM. Nina mawazo pia kuwa CCM sio wanaotufaa. Mimi nafikiri Znz sasa wanahitaji alternative political forces. Chama mbadala ambacho kitapambana na vimbwanga vya CCM, na udhaifu wa CUF, Chama kitakachoongoza mapambano ya kweli ya kizazi cha leo katika kuwakomboa kweli wa-zanzibari na kuwaletea umoja wao. sio mashairi ya CUF na CCM, wote wana fikra na mawazo mgando.
 
mkuu nnaona kama vile kiko chama kule kinaitwa JAHAZI ASILIA hakiwezi kuwa alternative ?

nnamkumbuka kulikuwa nakijana anaitea kitole aligombea urais miaka ya nyuma kijana smart sana
 
Niliongea suala hili katika thread moja na watu wameshafuta kama kawaida yao.Vyama hivi ninanipa shaka kubwa sansa kama wakipewa waongoze nchi sababu watatuletea mambo ya Neo colonoalism.kuna chama kimoja cha kikabila huwa wanapata pesa toka Ujerumani ili waongoze shughuli zao.CUF sijui zinatoka wapi.CUF-Zanzibar kuwa watu makini ila kwa hapa Bara,Upinzani Bado sana labda wajipange kwa miaka kama 50 huku wakisaidiwa na waandishi wa habari ila kama siyo hivyo bado sana..sana sana CHADEMA,hakina viongozi na kimejaa watu wabinafsi tu(Mawazo Binafsi)
Mataifa ya Nje tumeyachoka na tunahitajki kufanya maamuzi sie wenyewe.Matokeo ya kuzikaribisha nci za magharibi ni kuchochea uharibifu wa Amani.

Gembe wewe ni mmoja wa wachache sana nina penda kusoma michango yao .Leo naona unajishusha hadhi kwa kusema kuna chama cha Kikabila na uongo wa kupata pesa Ujerumani .Kama ni misaada kwa Chadema basi huwa wanapata sana UK na si Ujerumani .Kama unaona Zitto kwenda huko mara kwa mara basi huwa na mambo yake binafsi na si kwa Chadema .Kwanza chama cha kikabila kwa kivipi ?CCM yenu ni Chama kweli cha watu wote wa Tanzania na hasa baada ya Mwalimu ?
 
Kimsingi nakubaliana na wewe. Na hii siyo kama ni mshabiki au mpenzi wa CCM. Nina mawazo pia kuwa CCM sio wanaotufaa. Mimi nafikiri Znz sasa wanahitaji alternative political forces. Chama mbadala ambacho kitapambana na vimbwanga vya CCM, na udhaifu wa CUF, Chama kitakachoongoza mapambano ya kweli ya kizazi cha leo katika kuwakomboa kweli wa-zanzibari na kuwaletea umoja wao. sio mashairi ya CUF na CCM, wote wana fikra na mawazo mgando.

Ndivyo unaweza kuutaja udhaifu wa CUF ?
 
Mtu wa Pwani:
Nakuuliza tena una uhakika mimi ni mbaguzi wa kidini?
Hivi kwanini viongozi wa vyama na serikali ya hapa zanzibar wooote ni waislamu?Hili limefanyika na waislamu,then unaacha kukemea ushenzi huu,na kuniita mimi mbaguzi wa kidini.
Hivi huwa unakaa na kufikiria kabla ya kukosoa watu?hivi ni kwanini mnapinga politics za BUSH zidi ya waislamu wenzenu huko uarabuni?so mnataka na sisi tuwaachie wakristo wenzetu waingie ktk gharama zisizo na maslahi kwao?embu nikuulize wewe mnafiki,wakristo watafaidika vipi na kuisaidia serikali ya zanzibar?wakati hata mjumbe wa shina mkristo hapa zenj hakuna.
Naomba ujicheck kwanza,usitake tufunue na yasiyofunuliwa hapa.
 
Kimsingi nakubaliana na wewe. Na hii siyo kama ni mshabiki au mpenzi wa CCM. Nina mawazo pia kuwa CCM sio wanaotufaa. Mimi nafikiri Znz sasa wanahitaji alternative political forces. Chama mbadala ambacho kitapambana na vimbwanga vya CCM, na udhaifu wa CUF, Chama kitakachoongoza mapambano ya kweli ya kizazi cha leo katika kuwakomboa kweli wa-zanzibari na kuwaletea umoja wao. sio mashairi ya CUF na CCM, wote wana fikra na mawazo mgando.

Ndivyo unaweza kuutaja udhaifu wa CUF ?

Ndugu yetu huyo muachie tu kama ukisoma post zake zote zinazohusu mgogoro wa Znz utajua yuko upande gani ingawa katika hii alianza kwa kujishuku na kujipapatua kuwa si mshabiki Chi Chi Emu - tufanyeje ndio demokrasia na moja katika vigezo vyake ni kuvumiliana.

Tusubiri pengine atakupa huo udhaifu kama si kushambulia viongozi binafsi.
 
Watu wanafanya unazi kabisa .Nashangaa wanaishindwa kuona kwamba Seif had a trip planned prior NEC ya Butiama .Lakini pia mnalaumu sana kwamba Arudi kwa wananchi kuishitako CCM .Wamesha fanya tayari na kusema wanajitoa mlitaka ashitaki mara ngapi ? CCM wanasema shauri lirudi kwa wananchi mbona wakati wanaiba kura nan kutangaza matokeo kwa nguvu hawawashirikishi wananchi ?
 
Maneno yako swadakta kabisa lakini wengine ndio ni mashabiki hata uwambie nini hawasikii - ama mimi CCM hata wanambie Mungu mmoja siwaamini lazima niwaulize Mungu yupi isijeikawa Lata.
 
Nilishawahi kusema Maalimu Seif ni miongoni kwa Threats za Muafaka Zanzibar.

Kwa kuwa anatamani ashike madaraka hata kwa siku mbili!!! That is ngangari bwana.

Huko Nyuma nilishawahi kumlinganisha na Marehemu. Jonas Savimbi... ambaye alivyoondoka tu... it took hardly less than 10 days... vita ya miaka zaidi ya 25 ya Angola ikaisha...Ingawa siku zote tuliambia tatizo ilikuwa la chama chake cha UNITA, kumbe ilikuwa yeye mwenyewe Savimbi.

Na leo hii Maalimu Seif akisema siasa basi, au hagombei tena, au uongozi wa siasa basi... Muafaka Zanzibar utapatikana same day/week/month or maximum same year. Kwani Tatizo sio CUF, tatizo ni Maalim Seif mwenyewe.

Kumbukeni munkari wake ulivyopungua alivyoanza kupewa mafao ya Waziri Kiongozi mstaafu...

na mimi nilishasema kuwa Maalim sio kitu. ni kama sadamu Hussein. watu wengi walimuonya Marekani kuwa ukimuondoa Sadam na watoto wake wawili, sio jibu la matatizo. jibu lake ni kuangalia mzizi mzima. ila marekani alikataa. sasa ona yanayotokea Iraq.
 
Hakuna haja ya kuandika sana na kumsema ovyo mpiganiaji haki wa WaZanzibari ,huyu ni sawa na mpiganiaji wa ukombozi wa Wananchi wake ambao wamewahi kutokea hapa duniani ,kuna aina nyingi za mapambano wako wanaoona maneno ya mezani hayafai ni bora msituni na wako wanaoona maneno yote yawepo mezani.Seif ameamua kuwepo mezani na kutumia njia na mbinu za mapambano ya mezani.Hivyo juhudi zake anazochukua ni kuepusha mambo ya mapambano na madikiteta ,inajulikana madikiteta ni wagumu kuondoka kwa mazungumzo ya mezani lakini kutokana na hali ya Zanzibar na msimamo wa dunia hivi sasa mambo ya kutumia mtutu hayatakiwi na nafikiri kuna sheria kuwa serikali inayoingia madarakani kwa mtutu haitambuliwi,na ukitazama kwa mbali utaona Zanzibar ni visiwa vidogo sana na vimekaliwa kimabavu na serikali ya Muungano nguvu zozote zikifanywa na CUF za kulazimisha mtutu watakaopata tabu ni wananchi labda wakiamua kufa na mtu kitu ambacho kimeanza kuvuma chini kwa chini ,wanasema wapelestina wanakufa na watu kwa nini na wao hawaigi mfumo huo ,kuna sehemu nimesoma wanasema hakuna kisichowezekana Zanzibar ulinzi uliokuwepo hauwakoseshi nafasi ya kufa na mtu ikiwa wataamua.Sasa wanasema kuvumilia kuna mwisho na dalili zinaonyesha wamefikia kikomo.
 
Back
Top Bottom