Mshahara wa Januari vipi mbona unachelewa?

Mshahara wa Januari vipi mbona unachelewa?

Samahani kwa kutumia lugha ngumu ,ukitumia lugha ngumu yenye ukweli na inayokera huwa inaeleweka na kukaa akilini vizuri.

Mwananchi mwenzangu hata mimi nilipitia hiyo hali ya kutegemea salary ila nikajiongeza kupata kipato nje ya mshahara ikanisaidia sana ,sasa hawa WEHU ukiwaambia kwamba watafute other source wanaanza kuleta MATUSI.
Mi nimekuelewa sana tu Mkuu. 🤝

Usione napita huku nacheka kuna muda nashangaa comments za wanazengo inakuwaje mtu anakosa hadi nauli kuna saa najisemea huenda wanachangamsha genge.

Mfano kama mimi siko kwenye hatua ya kukaa hadi kukosa mpaka nauli sababu nina Plan B. Kama hapa nilishalitumikia Taifa kwa sasa nipo sehemu natafuta mia mbili.

Hivyo uko sahihi kabisa sababu asikwambie mtu kiuhalisia Mshahara pekee hautoshi na ukisema kuutegemea basi ujiandae kuwa mkopaji kila uchwao sababu ni ngumu sana mshahara wenyewe kama wenyewe kukutana.

Na ukitaka iwe hivyo inabidi uishi kujibana bana kweli kweli.
 
Huyu jamaa atakuwa Dalali si unajua madalali kwa kuomba beer

Akisikia mshahara umetoka anakuja bar kuomba beer
 
Ndo kusema Watumishi tukikosa Mshahara tunakuwa wakali hivyo. Lol.

Siku zote ushauri huwa unapokelewa halafu kufanyiwa au kutofanyiwa kazi ni maamuzi ya wewe mpokeaji.

#Mnisamehe jamani msinitukane.
 
Ndo kusema Watumishi tukikosa Mshahara tunakuwa wakali hivyo. Lol.

#Mnisamehe jamani msinitukane.
Hakuna ukali haina haja ya kuchekea ******* wanatudhiaki thread ziko nyingi sana sasa wao wanakujaje kutukejeli ilahali tukiwa tunatoa huduma wanakuwa wasumbufu sana wao inawauma nini sisi kuulizana mshahara
 
TEMESA kuna pesa sana zaidi ya ujuavyo. Pesa za TEMESA TBA na TANROADS ni za upepo. Ukikaa kwenye mfumo hata uambiwe wakupeleke BOT huwezi kukubali huo upumbavu.
Hizo taasisi ni za uza nunua. Pesa tu inaongea mda wote.
Ila ukiwekwa nje ya mfumo lazima upagawe
Nimegoma kwenda TAMESA, Kuna Taasisi naitaka pale Dodoma.
Ndio napambana, NIOMBEEE.

Ombi la uhamisho lipo Utumishi

#YNWA
#YANGA_BINGWA
 
Back
Top Bottom