Drifter
JF-Expert Member
- Jan 4, 2010
- 5,444
- 5,646
Mnabishana buree juu ya UHURU wakati ukweli ni kwamba UHURU wetu tulipewa kwenye silver plate. Haya yoote yanakuja kwa sababu TANU ndio ilishinda uchaguzi lakini kama chama kingine kingeshinda uchaguzi mkuu msingefikia hapa wala huyo Nyerere na hao wazee wasingekuwa historia mnayoitaka. Historia ya chama ndio mnataka kuifanya Historia ya Nchi?
Pengine mngeweka nguvu kubwa kujadili TANU iliwezaje kushinda uchaguzi wa mwaka 1960 mikoa yote, na kina nani waloshughulika na maandalizi ya ushindi maana hatukuupata Uhuru wetu kupitia mtutu wa bunduki tukawajua mashiujaa wetu walo risk maisha yao ili tuwe huru. Uhuru wetu ulipangwa na Jumuiya ya madola kupewa tukiwa kuwa tayari. Ni Utayari gani? na nini mchango wao.
Mtu yeyote ambaye angekuwa kiongozi wa TANU wakati huo angeweza kushinda uchaguzi na kuwa shujaa wa leo maana penye ukweli tuuseme. Pasipo Malkia kupitisha na kukubali kutupa Uhuru tusingekuwa HURU. Huu ushujaa mnaolilia haswa ni upi, hao wazee walifanya nini kama sio kujiunga na chama kama mavyojiunga na CCM leo na Chadema! Mnataka nanyi mhesabiwe ktk historia kama mkishinda 2015. Kwa nini sifa zote msiwape wananchi walokusanyika kwa wingi kupiga kura hadi idadi na asasi ilotakiwa ikapatikana?
Mtanisamehe kwa kuwapeleka nje ya mada yenu! Bofya
Mkuu, shukrani nyingi zikuendee kwa ukweli huu ambao wengi hawataki kuutazama kwa vile hauvutii. Hujatoka nje ya mada. Ni kweli kwamba "waasisi" walikuwa na nafasi yao katika "kupigania" uhuru; lakini ukweli mkubwa zaidi ni kuwa wakoloni hatimaye waligundua, kulingana na mazingira, kuwa ni mkakati mzuri zaidi "kuachia baada ya kubania muda mrefu" na kurudi kwa gia mpya ya uhisani na blabla za aina hiyo na kutuchuma kirahisi kama inavyozidi kudhihirika hivi leo. Hii imewawezesha kula kwa kuletewa (on a silver pater) bila bugdha ya kuwajibika na maslahi ya hayo makoloni na wala kuletewa fujo zisizo na maana.
Nilishawahi kuwaambia rafiki zangu wa Afrika ya Kusini kwamba mwisho hasa wa Apartheid uliharakishwa na vikao vya wanamikakati wa South African based multinationals waliokuwa wakikutana na uongozi wa ANC huko Conakry, Guinea na kwingineko kutafuta kuirejesha Afrika ya Kusini kwenye jumuia ya kimataifa baada ya kugundua wanapoteza fursa kibao za kibiashara na uwekezaji nchini na barani Afrika kwa ujinga wa kufurahisha wazungu (boers) wasio na shule.
Hawa wanaohangaika na historia ya "mashujaa" wao katika kupigania uhuru hawana dhamira njema na Tanzania zaidi ya kutafuta mada za kichonganishi zisizo na mantiki wala mashiko leo hii. This is a non-issue.