Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,912
- 30,253
Jioni hii imenifikia taarifa kutoka Lindi kuwa Hassan Mohamed Said Kinyozi mmoja katika vijana waliowasha moto wa kupigania uhuru wa Tanganyika Southern Province, yaani Jimbo la Kusini amefariki dunia akiwa na umri wa kiasi cha miaka 90.
Nakumbuka kama jana siku nilipofika Lindi kwa basi dogo nikitokea Mtwara.
Barabara ya Lindi Mtwara ilikuwa mbovu sana miaka ile basi likiendeshwa kwa tahadhari kubwa.
Nakumbuka tulipoingia Lindi tunaelekea stendi natazama yale mandhari ya mji nageuza shingo huku na huku zile nyumba naziona mfano wa nyumba za Mtaa wa Swahili Dar es Salaam miaka ya 1950.
Nami nimo katika basi la Dar es Salaam Motor Transport (DMT) natokea Moshi shule nakuja likizo Dar es Salaam.
Nakumbuka nilikuwa nakabidhiwa kwa dereva Kapesa Johari kijana wa Gerezani kwani nilikuwa bado mdogo niko shule ya msingi hata uhuru bado.
Niko Lindi ndani ya basi naangalia minazi na nyumba zilizoezekwa kwa makuti.
Hii Lindi machoni kwangu ilikuwa sawasawa na Dar es Salaam ya udogoni kwangu.
Nilikuwa katika utafiti wa kitabu cha Abdul Sykes na mwaka ulikuwa wa 1993.
Hassan Mohamed Said Kinyozi amefariki.
Nimemtaja shujaa mzalendo huyu Maalim Hassan Mohamed Kinyozi, mtoto wa Sheikh Kinyozi aliyekuwa anaendesha moja ya madrasa maarufu mjini Lindi iliyofahamika kama Madrasa ya Sheikh Kinyozi.
Madrasa hii bado ipo hadi leo na baada ya kifo cha baba yake marehemu Hassan Kinyozi alisimamia chuo hiki na kuendelea kusomesha hadi kifo kilipomchukua hii leo.
Kuna mtu alinikumbuka wakati nilipokwenda Lindi kufanya utafiti na mahojiano na Rashid Salum Mpunga na Yusuf Mohamed Chembera.
Huyu ndiye aliyenitafuta na kunipa taarifa ingawa hatukupata kuonana tena toka mwaka ule wa 1993.
Ukisoma kitabu cha Abdul Sykes nikieleza historia ya TANU ni nani walioasisi chama cha TANU hapo Lindi utasoma maneno haya:
''...hawa wawili Ahmed Seif na Hassan Mohamed Kinyozi walikuwa ndiyo wafanyakazi wa kwanza wa TANU waliokuwa wakilipwa mshahara Southern Province.
Kwa ajili hii wakawa miongoni mwa wafanyakazi wachache sana walioajiriwa na TANU kwa wakati ule.
Suleiman Masudi Mnonji alitoa nyumba yake katika mtaa wa Makonde kuwa ofisi ya kwanza ya TANU kusini yote.
Baada tu ya kuanzishwa kwa TANU, Athumani Mussa Lukundu, kiongozi wa Lindi Dockworker's Union, aliunganisha chama chake na TANU.
Jambo hili kwa TANU lilikuwa la kuitia moyo sana kwa sababu Dockworker's Union ilikuwa na wanachama wengi na hatua ile iliongezea TANU nguvu.''
Bahati mbaya sana kuwa majina haya niliyoyataja hapo juu hayamo katika historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika.
Naamini si wengi hata hapo Lindi kwenyewe wanaifahamu historia hii ya mzee wetu Hassan Mohamed Said Kinyozi.
Waasisi wakuu wa TANU ukimtoa Suleiman Masudi Mnonji walikuwa vijana wawili - Rashid Salum Mpunga na Yusuf Mohamed Chembera.
Baada ya kupokea taarifa ya msiba huu nikaanza kupiga simu huku na huku kutafuta picha ya marehemu.
Mmoja katika marafiki zangu wazawa wa Lindi akanitumia picha ya marehemu ya mwaka wa 1954 wakati huo akiwa kijana mdogo sana aliyopiga na wazee wa mjini wengi wao walikuja si muda mrefu kuwa mstari wa mbele katika TANU na harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika.
Angalia picha ya pili hapo chini:
1.Aliyeketi chini mbele kushoto ni Hassan Mohamed Saidi Kinyozi
2. Aliyekaa kwenye kiti nyuma ya Hassan Kinyozi ni Rashid Salum Mpunga.
3. Aliyefunga tai ameketi ni Yusuf Mohamed Chembera.
4 Picha ilipigwa Ghana Restaurant 1954 na hii ilikuwa vilevile ni ofisi ya Lindi Seamens Club mahali walipokuwa wanakutana wanamji kwa mazungumzo na kituo cha harakati za TANU.
Picha ya tatu ni Hassan Mohamed Said Kinyozi katika ujana wake.
Sheikh Hassan Kinyozi ni mtu maarufu hata kwa wale ambao leo hawaijui historia yake kama mpigania uhuru.
Mtoto wa dada yake Bi. Salma bint Rashid ni mke wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete.
Marehemu anategemewa kuzikwa leo Jumatano hapo Lindi.
Tunamwomba Allah amsamehe makosa yake na amweke Pepo ya Fidaus.
Amin.