Hao watakuwa mashujaa wa wana Chadema sio mashujaa wa Watanzania maana tunatafuta chama na rais wa kuongoza nchi. Kushinda uchaguzi sio Ushujaa wa nchi hata kidogo mnataka kupunguza thamani ya ushujaa kwa maneno ya mtungo.Mzee ngoja nikwambie leo chadema ikishinda shujaa atakuwa Mbowe na Slaa maana chini ya uongozi wao wameeneza Chadema nchi yote sawa alivyofanya Mwl.Nyerere wakati wa uhuru.
Nyerere alikuwa rais wa kwanza wa TANU na rais wa Tanganyika na kisha Tanzania. hakuna Ushujaa pale unasubiri kura za wananchi kukuchagua na wala TANU haikuongoza nchi ili kuupata Uhuru bali ilijijenga kichama ili washinde uchaguzi hivyo historia ni yao kama chama sio ya Watanganyika. Mashujaa wetu ni wale wa Maji maji walopigania uhuru japo wakashindwa. Shujaa sii lazima ashinde mapambano!
Sasa kama mzee wangu alikuwa chama cha Fundikira, Marealle au Mtenvu na wakashidwa uchaguzi mkuu wao hawakuwa mashujaa. Hivi kweli unaweza sema Hizbu ndio mashujaa wa Uhuru wa Zanzibar kwa sababu tu walishinda uchaguzi na mbona wakaja ondolewa na Mapinduzi kama walistahili sifa na leo hii viongozi wake wamesahaulika! Huo Ushujaa wao upi haswa!