Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la Marekani Afrika afungua mazoezi ya kijeshi baina ya US na Tanzania

Kamanda wa Kamandi ya Afrika ya Jeshi la Marekani (AFRICOM) Jenerali Stephen Townsend, alikuwa na ziara ya siku mbili nchini Tanzania, tarehe 27 na 28 Julai, ambapo alikutana na maafisa waandamizi wa jeshi na kufungua mazoezi ya kwanza ya pamoja ya kijeshi ya nchi hizi mbili toka mwaka 2017.

“Tanzania imeendelea kuwa nchi kiongozi barani Afrika katika nyanja ya usalama na mbia muhimu sana wa Kamandi ya Afrika ya Jeshi la Marekani. Majeshi yetu ya ulinzi yana historia ndefu ya kufanya kazi bega kwa bega, na ziara hii ni kielelezo cha nia yetu ya kuimarisha zaidi ubia huo,” Alisema Jenerali Townsend.

Tarehe 28 Jenerali Townsend aliungana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo katika hafla ya ufunguzi ya mafunzo ya pamoja ya kijeshi (Joint Combined Exchange Training – JCET) kati ya askari wa Vikosi Maalumu vya Jeshi la Marekani na askari wa Jeshi la Wanamaji la Tanzania katika Chuo cha Ulinzi wa Amani kilichopo Kunduchi.

Mazoezi hayo ya kijeshi ya wiki sita ni ya kwanza ya aina yake kwa majeshi ya Tanzania na Marekani toka mwaka 2017.

Askari wa Kimarekani na wa Kitanzania watakuwa bega kwa bega wakishiriki mafunzo haya ili kuimarisha ujuzi wao katika mbinu za medani kwa kikosi kidogo, ulengaji shabaha, utoaji matibabu, mbinu za kimapambano za kikosi kulingana na maeneo tofauti tofauti(unit maneuver), mafunzo kuhusu sheria za kivita au migogoro ya kivita (Law of Armed Conflict) na jinsi ya kulinda haki za binadamu wakati wa mapambano.

“Kamandi ya Afrika ya Jeshi la Marekani inadhamira ya dhati kufanya kazi na Jeshi la Tanzania katika kutanzua changamoto za kikanda. Tunaimarisha ushirikiano baina ya majeshi yetu kupitia program mbalimbali za mafunzo na mazoezi ya pamoja,” alisema Jenerali Townsend. Aliongeza kuwa “Ni muhimu kukuza ushirikiano wetu na Tanzania ili kuendeleza malengo ya pamoja ya kiulinzi.”

Ziara Jenerali Townsend ilijumuisha pia kutembelea makao makuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Upanga, Jijini Dar es Salaam, ambapo alikagua gwaride rasmi na kukutana na viongozi waandamizi wa jeshi hilo.

Aidha, alitembelea Ubalozi wa Marekani alipokutana na Balozi wa Marekani nchini Tanzania Donald Wright na wafanyakazi wengine wa Ubalozi.

Kwa mujibu wa Balozi Wright, mazoezi haya ya kimafunzo na ziara ya Jenerali Townsend ni ishara ya umuhimu ambao Marekani inauweka katika ushirikiano imara kati yake na Tanzania katika nyanja ya usalama.

“Ziara ya Jenerali Townsend inathibitisha ubia mpana na wa muda mrefu wa kiusalama kati ya Marekani na Tanzania. Tunaadhimisha miaka 60 ya ushirikiano rasmi kati ya Marekani na Tanzania na ziara hii inasisitizia umuhimu wa ushirikiano wa kiusalama katika uhusiano huo uliojengwa katika kuheshimiana na maadili ya pamoja.

CHANZO: Ubalozi wa Marekani Tanzania

Itakavyokuwa hawa viumbe sio watu wema kabisa kabisa! lazima wanalo wanalolitafuta! Lazima!!!! ....
 
So what! Cha ajabu ni nini? Kwani ndiyo mara ya kwanza? Mbona nchi nyingine kama Kenya haya ni mambo ya kawaida?
 
Magu alikimbia mabeberu akadhani atafaidi kwa wachina kwa kuwa hawaingilii migogoro ya kisaisa ya watu. Kule akakuta karuka mkojo kadondokea mavi. Karudi pyaa!
Wachina ndo mabeberu hatari Wana exploit rasilimali za Africa bila huruma angalia mikataba ya kishenzi inayoingia na nchi za Africa huko Zambia hadi na babdari na mbaya zaidi wachina hawaheshimu Haki za binadamu, na mazingira jumla
 
KQUOTE="Evarist Chahali, post: 39775379, member: 8563"]
Kamanda wa Kamandi ya Afrika ya Jeshi la Marekani (AFRICOM) Jenerali Stephen Townsend, alikuwa na ziara ya siku mbili nchini Tanzania, tarehe 27 na 28 Julai, ambapo alikutana na maafisa waandamizi wa jeshi na kufungua mazoezi ya kwanza ya pamoja ya kijeshi ya nchi hizi mbili toka mwaka 2017.

“Tanzania imeendelea kuwa nchi kiongozi barani Afrika katika nyanja ya usalama na mbia muhimu sana wa Kamandi ya Afrika ya Jeshi la Marekani. Majeshi yetu ya ulinzi yana historia ndefu ya kufanya kazi bega kwa bega, na ziara hii ni kielelezo cha nia yetu ya kuimarisha zaidi ubia huo,” Alisema Jenerali Townsend.

Tarehe 28 Jenerali Townsend aliungana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo katika hafla ya ufunguzi ya mafunzo ya pamoja ya kijeshi (Joint Combined Exchange Training – JCET) kati ya askari wa Vikosi Maalumu vya Jeshi la Marekani na askari wa Jeshi la Wanamaji la Tanzania katika Chuo cha Ulinzi wa Amani kilichopo Kunduchi.

Mazoezi hayo ya kijeshi ya wiki sita ni ya kwanza ya aina yake kwa majeshi ya Tanzania na Marekani toka mwaka 2017.

Askari wa Kimarekani na wa Kitanzania watakuwa bega kwa bega wakishiriki mafunzo haya ili kuimarisha ujuzi wao katika mbinu za medani kwa kikosi kidogo, ulengaji shabaha, utoaji matibabu, mbinu za kimapambano za kikosi kulingana na maeneo tofauti tofauti(unit maneuver), mafunzo kuhusu sheria za kivita au migogoro ya kivita (Law of Armed Conflict) na jinsi ya kulinda haki za binadamu wakati wa mapambano.

“Kamandi ya Afrika ya Jeshi la Marekani inadhamira ya dhati kufanya kazi na Jeshi la Tanzania katika kutanzua changamoto za kikanda. Tunaimarisha ushirikiano baina ya majeshi yetu kupitia program mbalimbali za mafunzo na mazoezi ya pamoja,” alisema Jenerali Townsend. Aliongeza kuwa “Ni muhimu kukuza ushirikiano wetu na Tanzania ili kuendeleza malengo ya pamoja ya kiulinzi.”

Ziara Jenerali Townsend ilijumuisha pia kutembelea makao makuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Upanga, Jijini Dar es Salaam, ambapo alikagua gwaride rasmi na kukutana na viongozi waandamizi wa jeshi hilo.

Aidha, alitembelea Ubalozi wa Marekani alipokutana na Balozi wa Marekani nchini Tanzania Donald Wright na wafanyakazi wengine wa Ubalozi.

Kwa mujibu wa Balozi Wright, mazoezi haya ya kimafunzo na ziara ya Jenerali Townsend ni ishara ya umuhimu ambao Marekani inauweka katika ushirikiano imara kati yake na Tanzania katika nyanja ya usalama.

“Ziara ya Jenerali Townsend inathibitisha ubia mpana na wa muda mrefu wa kiusalama kati ya Marekani na Tanzania. Tunaadhimisha miaka 60 ya ushirikiano rasmi kati ya Marekani na Tanzania na ziara hii inasisitizia umuhimu wa ushirikiano wa kiusalama katika uhusiano huo uliojengwa katika kuheshimiana na maadili ya pamoja.

CHANZO: Ubalozi wa Marekani Tanzania

[/QUOTE]
Kwani hapo lipi la ajabu. Ushirikiano mbona upo tu na mataifa mengine makubwa kama china na urusi.
 
Wachina ndo mabeberu hatari Wana exploit rasilimali za Africa bila huruma angalia mikataba ya kishenzi inayoingia na nchi za Africa huko Zambia hadi na babdari na mbaya zaidi wachina hawaheshimu Haki za binadamu, na mazingira jumla
Yaani huelewi kitu kuhusu ubeberu. Wachina wametoa sana msaada afrika kabla ya kuanza kukopesha kibiashara. Mfano reli ya tazara kama tulijengewa bure tu. Mkopo ulikua na masharti laini sana. Usisahau pia msaada wa mafunzo na silaha kwa ukombozi wa bara la afrika. Ukikopeshwa na china kibiashara halafu hulipi siku hizi usitegemee kusamehewa. Hili halipo. Sasa ujue mabeberu ni wale waliyotunyonya kwa kutuweka kwenye ukoloni na hadi leo wanatunyonya kwenye masharti ya biashara.
 
B
Africom ni iliwekwa ili kupambana na ughaidi ambao unatishia maslahi ya Wamarekani. Ukiona wanashirikiana na majeshi ya nchi za Afrika, nia yao ni hiyo hiyo. Kuwafundisha jinsi ya kupambana na hao ambao Amerika inawaita maghaidi. Kwa hiyo JWTZ watapewa mafunzo, vifaa vya kivita ili wawe tayari kupigana na Al Shabaab, Al Qaeda, ISIS, na wengineo.
Mbona umesahau Chadema?
 
Wanakuja kujua udhaifu wa jwtz watachunguza kila kitu na kupandikiza wapelelezi wao humo baadae wakija kuanza chokochoko wanajua pa kupenyea
Babu toka enzi ya nyerere wachina wamejaa kwenye macamp yetu,nenda navy kigamboni uwaone,na kota za jeshi pale keko ndio wamejaa kibao miaka na miaka na mpaka leo atuoni athari zozote,hao wagermany waliokabidhi mradi jana kwa mama samia pale lugalo wana miaka wapo lugalo,mataifa kama hayo yakitaka kukuchunguza wala hawaji kitoto namna hii
 
Unakumbuka vitangulizi vitatu vya ukoloni afrika?

1. Wafanyabiashara
2. Wamisionari
3. Wapelelezi.

jifunze kubashiri yajayo usiwe na uoni wa karibu.

Kule Somalia na Ethiopia na hata Yemeni na Saudi Arabia mambo yalianza hivi hivi.
Unrelated facts/events lead to unrelated conclusion.
 
Tukijadili hili swala kwa maslahi ya taifa tufikirie kuhusu kesho yetu. Tusidhani tuko salama sana.

Nachokiona ni kutaka kuuza nchi kwa maslahi y na tamaa za madaraka.
Marekani wakiamua mtawala wa nchi fulani atawale milele bila vurugu inawezekana. Aliweza kuigeuza Saudu Arabia kuwa ya kifalme wakati ilikuwa na utaratibu mwingine wa kiutawala.

Kwa tabia za hawa marais wa nchi zetu pale wanapoona tishio ktk uongozi wao wako tayari kuweka nchi rehani ili wasaidiwe ulinzi na mataifa yenye nguvu. hilo kwa nchi ya USA, Ufaransa na Urusi wako vizuri sana.

Ktk nchi zote duniani ambako Marekani kwa visingizio vya udumavu au tishio la usalama waliingiza vikosi vyao vya kijeshi( US miltary bases) nchi hizo hazikubaki salama hadi leo hazijatengamaa.

Mifano iko mingi michachi ni kama Somalia, Afighanistan, Uganda na Ethiopia.

Maeneo mengi waliingia kwa sababu za kupambana na ugaidi. Hadi leo nchi hizo hazitawaliki, hazina amani, ugaidi na uharifu wa kibinadamu na rasilimali umeongezeka mara dufu.

Tangu habari za Mboww kukamatwa kwa movie ya Ugaidi tunaona Mabeberu wakimiminika nchini. Kibachonishtua ni hawa makamanda wa AFCOM.

Je mama anataka kuweka rehani nchi ili wale maadui wa ndani wasimzingue? je tutasalimika??
Mkuu umesema vizuri sana!! Kingine tukikumbuke, Marekani akitia mguu mahali fulani anapoona kuna maslahi hung'ang'a ia hapo na hawezi kutoka!! Mifano ni mingi; Japan, Ujerumani, Korea ya kusini, Syria, Iraq nk Wanakaa nchi hizo kwa lazima na n hi hizo hutozwa gharama za kuhudumia wanajeshi wa marekani kwenye nchi zao!
Wamarekani tukiwalegezea wakaweka askari wao nchini kwetu kwa kisingizio cha mazoezi ya pamoja hawatatoka!! Watazidi kuongezeka taratibu!! Tushtuke sasa kungali mapema!
 
Kamanda wa Kamandi ya Afrika ya Jeshi la Marekani (AFRICOM) Jenerali Stephen Townsend, alikuwa na ziara ya siku mbili nchini Tanzania, tarehe 27 na 28 Julai, ambapo alikutana na maafisa waandamizi wa jeshi na kufungua mazoezi ya kwanza ya pamoja ya kijeshi ya nchi hizi mbili toka mwaka 2017.

“Tanzania imeendelea kuwa nchi kiongozi barani Afrika katika nyanja ya usalama na mbia muhimu sana wa Kamandi ya Afrika ya Jeshi la Marekani. Majeshi yetu ya ulinzi yana historia ndefu ya kufanya kazi bega kwa bega, na ziara hii ni kielelezo cha nia yetu ya kuimarisha zaidi ubia huo,” Alisema Jenerali Townsend.

Tarehe 28 Jenerali Townsend aliungana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo katika hafla ya ufunguzi ya mafunzo ya pamoja ya kijeshi (Joint Combined Exchange Training – JCET) kati ya askari wa Vikosi Maalumu vya Jeshi la Marekani na askari wa Jeshi la Wanamaji la Tanzania katika Chuo cha Ulinzi wa Amani kilichopo Kunduchi.

Mazoezi hayo ya kijeshi ya wiki sita ni ya kwanza ya aina yake kwa majeshi ya Tanzania na Marekani toka mwaka 2017.

Askari wa Kimarekani na wa Kitanzania watakuwa bega kwa bega wakishiriki mafunzo haya ili kuimarisha ujuzi wao katika mbinu za medani kwa kikosi kidogo, ulengaji shabaha, utoaji matibabu, mbinu za kimapambano za kikosi kulingana na maeneo tofauti tofauti(unit maneuver), mafunzo kuhusu sheria za kivita au migogoro ya kivita (Law of Armed Conflict) na jinsi ya kulinda haki za binadamu wakati wa mapambano.

“Kamandi ya Afrika ya Jeshi la Marekani inadhamira ya dhati kufanya kazi na Jeshi la Tanzania katika kutanzua changamoto za kikanda. Tunaimarisha ushirikiano baina ya majeshi yetu kupitia program mbalimbali za mafunzo na mazoezi ya pamoja,” alisema Jenerali Townsend. Aliongeza kuwa “Ni muhimu kukuza ushirikiano wetu na Tanzania ili kuendeleza malengo ya pamoja ya kiulinzi.”

Ziara Jenerali Townsend ilijumuisha pia kutembelea makao makuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Upanga, Jijini Dar es Salaam, ambapo alikagua gwaride rasmi na kukutana na viongozi waandamizi wa jeshi hilo.

Aidha, alitembelea Ubalozi wa Marekani alipokutana na Balozi wa Marekani nchini Tanzania Donald Wright na wafanyakazi wengine wa Ubalozi.

Kwa mujibu wa Balozi Wright, mazoezi haya ya kimafunzo na ziara ya Jenerali Townsend ni ishara ya umuhimu ambao Marekani inauweka katika ushirikiano imara kati yake na Tanzania katika nyanja ya usalama.

“Ziara ya Jenerali Townsend inathibitisha ubia mpana na wa muda mrefu wa kiusalama kati ya Marekani na Tanzania. Tunaadhimisha miaka 60 ya ushirikiano rasmi kati ya Marekani na Tanzania na ziara hii inasisitizia umuhimu wa ushirikiano wa kiusalama katika uhusiano huo uliojengwa katika kuheshimiana na maadili ya pamoja.

CHANZO: Ubalozi wa Marekani Tanzania

Nawaheshimu sana hawa watu.Waite majina yote lakini watabaki kuwa walivyo.
 
Kama unajua kwanini kigamboni iliuzwa kwa america hadi Obama na Bushi wakaja utajua kigamboni itakuwa military Base ya america!!!Tujiulize kwanini kigamboni???wanaiona future ijayo ambayo sisi hatuioni!!!KAMUULIZE KIKWETE YEYE AMEWAHI KUA MJEDA NA ANAJUA ALIONGEA NINI NA BUSHI PIA OBAMA KUHUSU KIGAMBONI!!!!
Story za vijiweni hizi, kigamboni imeuzwa wapi, lini na bei kiasi gani. Kama huna proof endelea na dabokick zako uache story za vijiweni kwenye hili jikwaa
 
Mkuu umesema vizuri sana!! Kingine tukikumbuke, Marekani akitia mguu mahali fulani anapoona kuna maslahi hung'ang'a ia hapo na hawezi kutoka!! Mifano ni mingi; Japan, Ujerumani, Korea ya kusini, Syria, Iraq nk Wanakaa nchi hizo kwa lazima na n hi hizo hutozwa gharama za kuhudumia wanajeshi wa marekani kwenye nchi zao!
Wamarekani tukiwalegezea wakaweka askari wao nchini kwetu kwa kisingizio cha mazoezi ya pamoja hawatatoka!! Watazidi kuongezeka taratibu!! Tushtuke sasa kungali mapema!
Umenielewa vizuri. Wameanza taratibu kujichomeka.
 
..wewe labda umri wako ni mdogo.

..kwa taarifa yako Tanzania iliwahi kutimua maofisa wa ubalozi wa Marekani hapa nchini.

..Tanzania pia ilishawahi kuvunja mahusiano ya kidiplomasia na kuufunga ubalozi wa Ujerumani Magharibi.

..Sasa hivi tumekuwa watu wa kupiga domo tu na kudanganya-danganya wananchi kwa propaganda lakini hatuna msimamo wowote.

..Mwaka jana Tundu Lissu alisindikizwa na balozi wa Ujerumani mpaka uwanja wa ndege alipotokomea.

..Lissu ana kesi na alikuwa akihitajika mahakamani, lakini serikali na polisi wakaacha aondoshwe nchini na balozi wa Ujerumani.

..Jambo hilo lisingeweza kutokea wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere kwani wakati ule serikali na viongozi wetu walikuwa na misimamo na kamwe hawakuruhusu mabeberu watupande kichwani.
Huo msimamo ndo ulisababisha
Bidhaa kupungua nchini
Sukari kuadimika
Watu kupanga foleni kununua sukari, sabuni na dawa ya meno
Mafuta kuadimika
Na uchumi kudidimia kabisa
Mpaka nchi ilipomshinda nyerere akaona ajiuzulu.
Kama ndo hiyo misimamo unaizungumzia tuambie ilitufikisha wapi !?
 
Back
Top Bottom