Waziri Mkuu wa Ethiopia, Dkt. Abiy Ahmed Ali kuwasili nchini kwa ziara ya siku tatu

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
WhatsApp Image 2024-02-27 at 17.18.59_3c39e02c.jpg

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Shirikisho la Ethiopia Mheshimiwa Dkt. Abiy Ahmed Ali anatarajiwa kuwasili nchini kwa ziara ya kitaifa ya siku tatu kuanzia tarehe 29 Februari hadi 02 Machi, 2024 kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Mhe. Dkt. Abiy atapokelewa rasmi Ikulu, Dar es Salaam tarehe 01 Machi, 2024 na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Akiongelea ziara hiyo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.), alisema lengo la ziara hii mbali na kukuza na kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizi mbili, inalenga pia kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na Ethiopia ambazo zimekuwa zikishirikiana katika maeneo ya biashara na uwekezaji, elimu, utamaduni, usafirishaji wa anga, kilimo, mifugo, udhibiti wa uhamiaji holela, ulinzi na usalama.

“Tanzania na Ethiopia zina uhusiano wa kidiplomasia wa muda mrefu na wa kihistoria ambao ulioasisiwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Mtawala wa Ethiopia, Hayati Haile Selassie. Viongozi hawa walishirikiana bega kwa bega katika harakati za ukombozi wa Bara la Afrika na ni miongoni mwa Viongozi Waanzilishi 32 wa Umoja wa Afrika wakati huo OAU mwaka 1963,” alisema Waziri Makamba.

Waziri Makamba aliongeza kuwa, mbali na ushirikiano wa kidiplomasia, Tanzania na Ethiopia zinashirikiana katika sekta ya anga ambapo mwaka 2016 hadi 2023 jumla ya marubani 75 na wahandisi 25 kutoka Tanzania wamepokea mafunzo katika ngazi tofauti nchini Ethiopia. Hivyo ni wazi kuwa, ziara hii itafungua milango zaidi ya ushirikiano kati ya Shirika la Ndege la Ethiopia na Shirika la Ndege la Tanzania – ATCL katika kujiendesha kibiashara.

Hali kadhalika, Tanzania na Ethiopia zinashirikiana katika sekta ya mifugo na kilimo. Nchi hizi zinaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya mifugo na uzalishaji mkubwa wa mazao ya kilimo kama kahawa, chai, asali, mbogamboga na matunda barani Afrika. Kupitia ziara hii Tanzania na Ethiopia zitaimarisha ushirikiano katika masuala ya umwagiliaji, matumizi ya teknolojia katika kilimo na matumizi ya mbegu zenye ubora na uhakika wa mavuno sambamba na tafiti katika sekta hizo mbili.

“Kuhusu sekta ya nishati, ziara hii itaziwezesha Tanzania na Ethiopia kujengeana uwezo na kubalishana uzoefu katika uzalishaji wa umeme unaotosheleza mahitaji ya nchi pamoja na kuzalisha umeme wa kibiashara utakaoiwezesha Tanzania kuuza katika nchi mbalimbali kupitia uanachama wake katika Jumuiya ya kuuziana umeme ya Afrika Mashariki (East African Power Pool), alisema Waziri Makamba.

Aidha, katika sekta ya elimu ziara hii itaziwezesha nchi hizi mbili kubadilishana wanafunzi na kujenga uwezo katika uuandaji wa mitaala na Tanzania kupata fursa ya kufundisha Kiswahili nchini Ethiopia.

Mhe. Waziri Mkuu Abiy na ujumbe wake wataondoka nchini kurejea Ethiopia tarehe 02 Machi 2024.
 
Mumtaje Haile sellasie kwa status yake
Emperor Haile Sellasie aka Ras Tafari Makonen
 
Back
Top Bottom