Marekani yakubali kuwaondoa wanajeshi wake nchini Niger

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,045
1,058
VCG111447385707.jpg


Vyombo vya habari vya Marekani vimeripoti kuwa Marekani imekubali kuwaondoa wanajeshi wake zaidi ya elfu moja nchini Niger kufuatia agizo la serikali ya mpito ya nchi hiyo. Mjumbe maalum wa zamani wa Marekani katika eneo la Sahel J. Peter Pham alisema, "Marekani na washirika wake wamepoteza mali ya kijeshi ya kimkakati ambayo nafasi yake haiwezi kuchukuliwa. Wakati huo huo, habari zinasema serikali ya Chad pia imeitaka Marekani iondoe jeshi lake nchini humo.

Niger kwa muda mrefu imekuwa nguzo kuu ya kimkakati kwa Marekani na Ufaransa katika mapambano yao dhidi ya wapiganaji wa "jihadi" huko Afrika Magharibi. Mwaka 2015, Oktoba, nchi hizo mbili zilisaini makubaliano ya ushirikiano wa kijeshi, ambapo Marekani inaweza kutumia vituo vya kijeshi nchini Niger "kutoa msaada katika vita dhidi ya ugaidi." Marekani kwa sasa ina kambi mbili za kijeshi nchini Niger, ambapo kati ya hizo kituo cha droni cha jeshi la angani cha 201 kiko karibu na Agadez, mji wa kati wa Niger na ujenzi wake uligharimu zaidi ya dola za kimarekani milioni 100. Je, kwa nini Marekani iliagizwa kuondoa kambi hizo muhimu na ghali za kijeshi barani Afrika?

Kwanza kabisa, Marekani imeweka jeshi lake barani Afrika kwa muda wa miaka kumi ili kupambana na ugaidi, lakini matokeo yake kumekuwa na uasi na machafuko zaidi barani humo. Katika miaka ya hivi karibuni, mapinduzi ya kijeshi yametokea mara kwa mara katikati na magharibi mwa Afrika, ambapo Niger ni mojawapo ya nchi sita za Afrika zilizo Kusini mwa Sahara kuwa na mapinduzi ya kijeshi tangu 2021, pamoja na Chad. Tovuti ya habari ya Marekani isiyo ya faida ya Truthout iliwahi kuchapisha makala iliyokosoa "vita dhidi ya ugaidi" vya Marekani kwa kuwaweka Waafrika chini ya shinikizo kubwa. Makala hiyo imeeleza kuwa katika miongo kadhaa iliyopita, operesheni za Marekani za kupambana na ugaidi barani Afrika hazijapunguza vitendo vya kigaidi barani Afrika, bali zimeharibu utulivu katika bara hilo. Ripoti iliyotolewa na Kituo cha Afrika cha Utafiti wa Mkakati (ACSS) mwaka 2019 ilionyesha kuwa shughuli za kigaidi barani Afrika ziliongezeka maradufu kutoka 2012 hadi 2018, na idadi ya nchi zilizoshambuliwa ikiongezeka kwa 960% katika kipindi hiki. Isitoshe, matukio ya kimabavu pia yaliongezeka mara kumi.

Wakati huo huo, watu pia wametambua kwamba madhumuni ya Marekani kuweka jeshi lake Niger na nchi nyingine za Afrika si tu kwa ajili ya "kupambana na ugaidi", lakini pia kudhoofisha ushawishi wa China na Russia katika Afrika, na hata igeuze Afrika kuwa medani ya vita. Hali halisi ni kuwa Kamandi ya Afrika ya Jeshi la Marekani (USAFRICOM) ambayo ilianzishwa chini ya kivuli cha "kutoa misaada ya kibinadamu na kusaidia amani na utulivu barani Afrika," ilipingwa na viongozi wa nchi za Afrika ilipoanzishwa, wakiamini kuwa hili ni jaribio la Marekani la kuanzisha vituo vingi vya kijeshi barani Afrika. Kama ilivyotarajiwa, Kamandi hiyo sio tu ilishindwa kuchangia usalama na utulivu wa Afrika, lakini badala yake ilipanua nyayo za jeshi la Marekani ili kudumisha umwamba wake kimataifa kupitia nguvu za kijeshi. Kamanda wa USAFRICOM Stephen Townsend alisema moja kwa moja kwamba kwa Marekani, China na Russia ni vitisho vikubwa barani Afrika, hivyo jeshi la Marekani linahitaji kuongeza uwepo wa kijeshi barani Afrika ili kukabiliana na China na Russia, na kuhakikisha maslahi, usalama na ushawihi wa Marekani barani Afrika.

Aidha, Marekani mara nyingi hutumia "nafasi ya juu" kufanya ushirikiano usio sawa na nchi na serikali za Afrika, ikiwa ni pamoja na kutamani na kudhibiti maliasili kwa njia za kijeshi, au kuingilia masuala ya ndani na diplomasia ya nchi za Afrika, kwa hivyo watu wa Afrika hawawezi kuona tumaini la usalama na maendeleo, jambo ambalo linasababisha kuongezeka kwa hisia za kuipinga Marekani.

Kwa hiyo, Marekani kuagizwa kuondoa jeshi lake Niger, Chad na nchi nyingine ni jambo lisiloepukika, na kuashiria kwamba nchi za Afrika zinachukua uhuru na ukombozi halisi kutoka kwenye mikono ya nchi za Magharibi, na kuwa pamoja na nchi nyingine za “dunia ya kusini” kupinga siasa za nguvu na uingiliaji wa nje, na kuhimiza kujenga utaratibu wa kimataifa ulio wa haki zaidi.
 
Wazungu wapo Afrika Ili kuhakikisha wanatunyonya na kulididimiza bara la Afrika, hakuna wazungu wanao hitaji Afrika tuendelee wakati bado wanahitaji Mali zetu.
Si mmebeba debe la kupepetea midomo hapo juu ya kichwa? Acha wawanyonye tangu kuumbwa ulimwengu mwenye akili ndo humtawala ndondocha
 
Back
Top Bottom