Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la Marekani Afrika afungua mazoezi ya kijeshi baina ya US na Tanzania

Evarist Chahali

JF-Expert Member
Dec 12, 2007
994
1,000
Kamanda wa Kamandi ya Afrika ya Jeshi la Marekani (AFRICOM) Jenerali Stephen Townsend, alikuwa na ziara ya siku mbili nchini Tanzania, tarehe 27 na 28 Julai, ambapo alikutana na maafisa waandamizi wa jeshi na kufungua mazoezi ya kwanza ya pamoja ya kijeshi ya nchi hizi mbili toka mwaka 2017.

“Tanzania imeendelea kuwa nchi kiongozi barani Afrika katika nyanja ya usalama na mbia muhimu sana wa Kamandi ya Afrika ya Jeshi la Marekani. Majeshi yetu ya ulinzi yana historia ndefu ya kufanya kazi bega kwa bega, na ziara hii ni kielelezo cha nia yetu ya kuimarisha zaidi ubia huo,” Alisema Jenerali Townsend.

Tarehe 28 Jenerali Townsend aliungana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo katika hafla ya ufunguzi ya mafunzo ya pamoja ya kijeshi (Joint Combined Exchange Training – JCET) kati ya askari wa Vikosi Maalumu vya Jeshi la Marekani na askari wa Jeshi la Wanamaji la Tanzania katika Chuo cha Ulinzi wa Amani kilichopo Kunduchi.

Mazoezi hayo ya kijeshi ya wiki sita ni ya kwanza ya aina yake kwa majeshi ya Tanzania na Marekani toka mwaka 2017.

Askari wa Kimarekani na wa Kitanzania watakuwa bega kwa bega wakishiriki mafunzo haya ili kuimarisha ujuzi wao katika mbinu za medani kwa kikosi kidogo, ulengaji shabaha, utoaji matibabu, mbinu za kimapambano za kikosi kulingana na maeneo tofauti tofauti(unit maneuver), mafunzo kuhusu sheria za kivita au migogoro ya kivita (Law of Armed Conflict) na jinsi ya kulinda haki za binadamu wakati wa mapambano.

“Kamandi ya Afrika ya Jeshi la Marekani inadhamira ya dhati kufanya kazi na Jeshi la Tanzania katika kutanzua changamoto za kikanda. Tunaimarisha ushirikiano baina ya majeshi yetu kupitia program mbalimbali za mafunzo na mazoezi ya pamoja,” alisema Jenerali Townsend. Aliongeza kuwa “Ni muhimu kukuza ushirikiano wetu na Tanzania ili kuendeleza malengo ya pamoja ya kiulinzi.”

Ziara Jenerali Townsend ilijumuisha pia kutembelea makao makuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Upanga, Jijini Dar es Salaam, ambapo alikagua gwaride rasmi na kukutana na viongozi waandamizi wa jeshi hilo.

Aidha, alitembelea Ubalozi wa Marekani alipokutana na Balozi wa Marekani nchini Tanzania Donald Wright na wafanyakazi wengine wa Ubalozi.

Kwa mujibu wa Balozi Wright, mazoezi haya ya kimafunzo na ziara ya Jenerali Townsend ni ishara ya umuhimu ambao Marekani inauweka katika ushirikiano imara kati yake na Tanzania katika nyanja ya usalama.

“Ziara ya Jenerali Townsend inathibitisha ubia mpana na wa muda mrefu wa kiusalama kati ya Marekani na Tanzania. Tunaadhimisha miaka 60 ya ushirikiano rasmi kati ya Marekani na Tanzania na ziara hii inasisitizia umuhimu wa ushirikiano wa kiusalama katika uhusiano huo uliojengwa katika kuheshimiana na maadili ya pamoja.

CHANZO: Ubalozi wa Marekani TanzaniaWebsite-images-750x450-11-1.png
 

beny jr

JF-Expert Member
Jul 15, 2018
685
1,000
Ilianza kuonekana ndege imekaa tuu pale uwanja wa ndege taarifa ikatoka inaleta vifaa vya ubalozi wiki chache baadae tunaskia Tanzania imepokea msaada wa chanjo kutoka marekani chanjo imefika tuu ghafla marekani anafanya mazoezi ya pamoja na. Majeshi yetu naweza nikawa na akili fupi kwa mitazamo ya wengi lakini kwa akili ndogo tuu naiona shida kubwa sana mbeleni ninahofu na dunia ya wakati ujao zile movie za ma vampire nadhani ni wakati wa mabadiriko ya mwanadamu
 

VAPS

JF-Expert Member
Jul 10, 2012
5,123
2,000
Leo pia Mama kazindua hospitali ya kisasa ya utafiti Lugalo na miradi kadhaa kwa hisani ya Wajerumani, na ahadi miradi Dodoma military hisp 20B... Mwakani akazindue... Natumai Mama Balozi kamdokeza Mama mwenzie, aachane na Mambo za ugaidi fake kwa Mbowe.
 

wa kupuliza

JF-Expert Member
Jun 15, 2012
6,397
2,000
Ilianza kuonekana ndege imekaa tuu pale uwanja wa ndege taarifa ikatoka inaleta vifaa vya ubalozi wiki chache baadae tunaskia Tanzania imepokea msaada wa chanjo kutoka marekani chanjo imefika tuu ghafla marekani anafanya mazoezi ya pamoja na. Majeshi yetu naweza nikawa na akili fupi kwa mitazamo ya wengi lakini kwa akili ndogo tuu naiona shida kubwa sana mbeleni ninahofu na dunia ya wakati ujao zile movie za ma vampire nadhani ni wakati wa mabadiriko ya mwanadamu

No wonder mnaamini Gwajima anafufuaga misukule.

Ujinga ni kipaji cha kuzaliwa nacho.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom