Venus Star
JF-Expert Member
- Dec 6, 2018
- 21,336
- 64,724
- Thread starter
- #81
Naamini kabla ya wabunge kwenda kujadiliana. Naamini Waziri atayachukua na kuyafanyia kazi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa mamlaka aliyopewa, alitoa maagizo kwa Msajili wa Vyama vya Siasa kuhusu kuandaa mkutano maalum wa Baraza la Vyama vya Siasa.
Lengo la maagizo hayo lilikuwa kutoa fursa kwa wadau wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa kutathmini utekelezaji wa mapendekezo yaliyotolewa na kikosi kazi kilichojikita katika kufanyia kazi masuala yanayohusiana na demokrasia ya vyama vingi vya siasa Nchini Tanzania
View: https://www.youtube.com/live/x3LQPRi8598?si=Um8CK-rCUseVWIEw
View attachment 2861467
Hatari snKweni huwajui chawa walivyo?
Mgeni rasmi ni nani?Naomba niwashukuru wote waliotoa maoni yao.
Nimeelezwa kuwa mmejadiliana kwa uungwana. Hata aliyejadili nje ya mada amevumiliwa. Tunaudhaifu mkubwa katika zama hizi badala ya kujadili mada tunajadili watu. Na mwisho tunakuwa hatuna suluhu.
Lakini mkutano huu haukuwa wa namna hiyo. Kwamba wa chama fulani anamawazo mazuri ya mtu mwingine.
Imani yangu kwa yale mliyojadiliana itakuwa maridhiano
Mgeni RasimMgeni rasmi ni nani?
Sema kazi yenu ni kuongeza idadi ya Wanawake kwenye ngazi za juu ili mtawale nchi vizuri kama ilivyo Rwanda na Uganda.Wachangiaji
Dr. Idda
Mwasilishaji ameweza kutoa maelezo yote. Nina mshukuru na naipongeza Serikali inayoongozwa na Rais Samia. Kwa kutuletea mswada huu. Tunaamini utaenda kuongza kiwango cha demokrasia.
Naenda haraka kwenye kifungu cha nane.
8(f) na 9(d) Kifungu kinaeleza kuongeza kwa jinsia. Tafiti zinaonesha kadiri tunapokuwa na usawa wa kijinsia tunapata mawazo kutoka kwenye makundi yote. Kifungu hiki nakipongeza. Hatuangalii tu idadi bali tuweke watu wenye uwezo.
Nimefanya utafiti kwenye upande wa madiwani. Kweli kuna wanawake lakini mazingira wanayofanyia kazi wanakuwa hawawezi. Ni muhimu tuweke watu wenye uwezo.
Kifungu cha 9 sehemu ya tano.
Nafikiri Tangazo liweze kuwafikiwa watanzania wote wenye uono hafifu na wale wenyematatizo ya usikivu.
Tangazo hili tunaamini litaongeza idadi ya watu kuwemo kwenye hizi kamati.
Kifungu 21, 22. Inatakiwa kuwa na watendaji na rasilmali fedha. Tume hii itakapokuwa na watenda na kuwa na raslmali fedha itakuwa inaweze kutenda kazi kwa uhuru.
Wajumbe watano kutafanyika usaili. Naomba kuwe na usawa na kijinsia. Ikitokea watu wote wanafanana basi waangalie jinsia. Siyo kuongeza tu mwanamke kwa sababu ya jinsia.
Kifungu 13. Hili pendekezo linaweza kuwekwa kwenye kanuni na siyo kwenye sheria. Mapema kwa muda gani siku masaa au nini.
Sheria hii tunayoenda kuitunga ya tume ya uchanguzi. Hatjawahi kuwa na sheria hii. Ikitumika vizuri itakuza demokrasia.
Bwana Hashim endelea ili tupate mwafaka sahihi.Hashimu Juma MWenyekiti wa wazee Chadema
Mjumbe mmoja alisema kwenye 4R kuwa tuwe wajasili katika kusikiliza.
Mambo yote tunayoyafanya katika nchi hii hatupo serious. Kama hapa tupo katika kutafuta katiba. Katiba ya warioba ipo. Mtoa mada anamwelekeza tujielekeze kwenye mada.
Taarifa kutoka kwa Maganya kwenda kwa mchangiaji. Seriousness ya Rais ni pamoja na huu mchakato huu tulionao.
Mwongozaji anaeleza kuwa hata kuwepo hapa ni seriousness ya Rais.
Hashim Juma anaendelea.
Kwakuwa hakuna sheria. Namtaka mwenyekiti mtungi atuoneshe barua ya wale wanawake 19 wa CHADEMA.
Maelewano yanapotea kwenye mkutano.
Mwangozaji anasema mchangiaji hakuwa anaongelea mada alikuwa anaongelea mambo mengine.
Anaeleza mawazo hayo tunayaheshimu sana. Anaombwa bwana Hashimu atulie.