Ufunguzi wa mkutano maalum wa baraza la vyama vya siasa

Venus Star

JF-Expert Member
Dec 6, 2018
19,675
59,775
UFUNGUZI WA MKUTANO MAALUM WA BARAZA LA VYAMA VYA SIASA

Mkutano huu kushirikisha Wadau wa Demokrasia ya Vyama vingi vya Siasa.

Lengo ni kujadili Miswaada ya Sheria za Uchaguzi na Sheria za Vyama vya Siasa iliyosomwa kwa mara ya kwanza Bungeni Novemba 10, 2023.

Kauli Mbiu;
" TOA MAONI YAKO KUIMARISHA DEMOKRASIA "

MGENI RASMI;
Mhe. Othman Masoud Othman
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar

🗓️ Mkutano huu utafanyika Tarehe 3 na 4 Januari, 2024
📍Ukumbi wa Julius Nyerere International Convetion Centre - Dar es salaam

#ImarishaDemokrasia
#TunzaAmani
#KatibaYaWatu
#KatibaNiMaridhiano
#UchaguziNiMashindano
#MatokeoChanya
##SisiNiTanzania
 
1703997946620.png
 

Baraza la Vyama vya Siasa​



Baraza la Vyama vya Siasa limeundwa ndani ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa. Wajumbe wa Baraza hili hujumuisha viongozi wa kitaifa wawili wa kila chama cha siasa chenye usajili wa kudumu. Ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa ndio yenye jukumu la kisheria ya kuratibu shughuli za Baraza la Vyama vya Siasa.

Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa na Makamu Mwenyekiti huchaguliwa kwa kupigiwa kura na wajumbe wa Baraza.

Majukumu ya Baraza la Vyama vya Siasa

1. Kumshauri Msajili wa Vyama vya Siasa juu ya mgogoro inayotokea kwenye vyama vya siasa;
2. Kumsahuri Msajili wa Vyama vya Siasa juu ya masuala yenye maslahi kwa Taifa kuhusiana na vyama vya siasa au kuhusiana na hali ya kisiasa nchini;
3. Kuishauri Serikali kupitia kwa Msajili wa Vyama vya Siasa juu ya kupitishwa kwa marekebisho na utekelezaji wa Sheria ya Vyama vya Siasa na sheria zingine zinazohusu masuala ya vyama vya siasa;
4. Kushauri juu ya kanuni zinazosimamia masuala yanayohusu vyama vya siasa;
5. Kutoa taarifa kwa Msajili wa Vyama vya Siasa juu ya uendeshaji wa chama chochote cha siasa.
 
Hujanijibu swali langu mdogo wangu. Au umeshindwa?
Kwani Tanzania hakuna ukabila?

Ulivyo tutusa unadhani CCM haina ukabila 😂😂

Unadhani ACT haina Udini

Unadhani Chadema siyo Wakabila!

Bure kabisa na Baraza lako la Mchongo Mtungini!
 
Back
Top Bottom