Venus Star
JF-Expert Member
- Dec 6, 2018
- 19,674
- 59,774
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa mamlaka aliyopewa, alitoa maagizo kwa Msajili wa Vyama vya Siasa kuhusu kuandaa mkutano maalum wa Baraza la Vyama vya Siasa.
Lengo la maagizo hayo lilikuwa kutoa fursa kwa wadau wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa kutathmini utekelezaji wa mapendekezo yaliyotolewa na Kikosi Kazi kilichojikita katika kufanyia kazi masuala yanayohusiana na demokrasia ya vyama vingi vya siasa Nchini Tanzania.
View: https://www.youtube.com/live/gZteo95nx84?si=80sJfbMUI52t-UHX
Kwa maneno mengine sote kwa pamoja tuepuke kuugeuza Mkutano huu kuwa MUHURI wa kuhalalisha mawazo ya watu wachache au MSIMAMO wa kitaasisi.
Mheshimiwa Mwenyekiti na Waheshimiwa Viongozi, sote wakati tunaelekea katika Mjadala huu ni vyema tujikumbushe tulikotoka hadi kufikia hapa. Historia itatukumbusha Dhamira ya Miswada tutayoijadili na muelekeo tunaopaswa kuchukua ili kuakisi Dhamira yetu kama Taifa.
Tukumbuke kwamba Disemba 2021 Baraza la Vyama lilifanya Mkutano kule Dodoma uliopelekea kuundwa kwa Kikosi Kazi cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutazama hali yetu ya Demokrasia.
Aprili 2022 Kituo cha Demokrasia Tanzania kikafanya Mkutano wake Dodoma na kutoa mapendekezo mahususi kwa Kikosi Kazi kuhusu Sheria zetu za Uchaguzi na za Vyama. Septemba 2022 Kikosi Kazi kikakabidhi rasmi tarifa kwa Mheshimiwa Rais na Januari 2023 Mheshimiwa Rais akaondoa zuio dhidi ya Mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa na Tarehe 10 Novemba 2023, Mswada wa Sheria ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mswada wa Sheria ya Uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wabunge na Madiwani na Mswada wa Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa Sura ya 258 na Sheria ya Gharama za Uchaguzi Sura ya 278, ilisomwa kwa mara ya kwanza Bungeni.
Mheshimiwa Mwenyekiti na Waheshimiwa Wajumbe, Historia hiyo inatuonyesha kwamba Mchakato wa kutayarisha Miswada tunayotaka kuijadili haukuwa wa Serikali peke yake wala wa Chama kimoja peke yake.
Ni Mchakato uliokuwa shirikishi, uliosheheni mawazo na baraka za wadau wengi. Hivyo, katika mjadala wetu jambo hili la kuwa huu ni Mchakato shirikishi lazima tulipe kipaombele sana"
Lengo la maagizo hayo lilikuwa kutoa fursa kwa wadau wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa kutathmini utekelezaji wa mapendekezo yaliyotolewa na Kikosi Kazi kilichojikita katika kufanyia kazi masuala yanayohusiana na demokrasia ya vyama vingi vya siasa Nchini Tanzania.
View: https://www.youtube.com/live/gZteo95nx84?si=80sJfbMUI52t-UHX
OTHMAN MASOUD SHARIF, MAKAMU WA KWANZA WA RAIS-ZANZIBAR
Mkutano wa majadiliano hasa wa utajiri wa mawazo ya Washiriki na sio Mkutano wa mapambio na kutimiza tu utaratibu tunaoanza kuuzoea wa kusema “WADAU WALISHIRIKISHWA” japokuwa kiuhalisia HAWAKUSIKILIZWA. Kwa maneno mengine sote kwa pamoja tuepuke kuugeuza Mkutano huu kuwa MUHURI wa kuhalalisha mawazo ya watu wachache au MSIMAMO wa kitaasisi.