Mkutano maalum wa Baraza la Vyama vya Siasa na Wadau wa Demokrasia tarehe 03 Januari 3, 2024 (kipindi cha pili)

Venus Star

JF-Expert Member
Dec 6, 2018
19,695
59,850
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa mamlaka aliyopewa, alitoa maagizo kwa Msajili wa Vyama vya Siasa kuhusu kuandaa mkutano maalum wa Baraza la Vyama vya Siasa.

Lengo la maagizo hayo lilikuwa kutoa fursa kwa wadau wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa kutathmini utekelezaji wa mapendekezo yaliyotolewa na Kikosi Kazi kilichojikita katika kufanyia kazi masuala yanayohusiana na demokrasia ya vyama vingi vya siasa Nchini tanzania.


View: https://youtu.be/OcbTrJeOa5s
 
Ajari Msafa Nguwahambi,
Tuanzie waliochangia kuhusu falsafa ya 4R. Hii imebeba utashi wa kile kilitotukutanisha.
Kuhusu Sheria ya vyama vya siasa na gharama za uchaguzi.

Nitachambua kwa jicho la kijinsia.
1. Vyama kuvifanya sura ya kitaifa maana yake wanawake na wanaume.
2. Kurekebisha ushiriki
3. Kurekebisha gharama za uchaguzi.

Mapendekezo ni kubadili au kurekebisha sheria zenye malengo ya ubaguzi.

Katika jicho la sayansi ya siasa Dr. Semakafu ameongelea kuhusu siasa zinazozungmzia watu wote. Lazima kuzungumza aina ioi ya wawakilishi tunawahitaji.

Katika mada yake inahusu wanawake.

Kwenye Sheria kuna mambo yaliyopendekezwa. Lengo la andiko lake ni kuongeza wigo wa wanawake na makundi maalum.
Tuwapongeze Uringo na Mtandao. Zinaonekana ni hoja za muda mrefu. Kuna wadau wapo wanapiga kelele ukiwaita wanashindwa kuongea.

Hoja zao zitachambuliwa.
 
Mchaniaji Mwingine: Mussa Kombo
Mtumishi wa Serikali ya mapinduzi zanzibar tume ya kurekebisha sheria

Tusijikite sana katika mada ya jinsia pekee yake.
Niliupitia mswada wenye sheria mbili.
Nipongeze Serikali kwa kuwasilisha hiki na kusomwa mara ya kwanza katika bunge la jamhuri ya muungano Tanzania.

Asubuhi kuna mmoja aliniuliza kwanini tunazungumzia 4R wakati tunaongelea mswada wa sheria.
Nilimjibu kuwa tunaangalia msalah ya taifa kwanza.

Nitazungumza nukta 6 lakini nitaongea nukta 4 za ujumla.
Zanzibar tumeshiriki kwa kina. Na baadhi ya maoni yamezingatiwa

1. Suala la uzingatiwaji wa gharama za uchaguzi vyama vyote.
Katika utafiti niliofanya ni moja ya chanzo cha kuimarisha demokrasia. Kila chama kina falsafa zake. Lakini kwa kukosa fedha vyama vingine vinaweza kushindwa kuwafikia wananchi. Hili siyo jambo geni, limeandikwa kwenye nyaraka mbalimbali. Nimepitia sheria za nchi mbalimbali, wanajaribu kuwezesha vyama vya siasa. Nchi kama Afrika kusini wameweka asilimia kiasi fulani kwaajili ya kugharamia vyama vya siasa. Hiyo ni moja ya kujenga demokrasia. Ujenzi wa demokrasia ni gharama.

2. Tunayo sheria ndani ya Zanzibar inayohusu Gharama za uchaguzi. Inaonekana kama vile sheria hii inalenga kusaidia uchaguzi wa rais na wabunge wa muungana. Kwa mawazo yangu jambo la vyama vya siasa ni la muungano. Nadhani Sheria yetu ingetazama kwa ujumla wake. Nadhani hakukuwa na haja ya sheria ya uchaguzi inayohusu zanzibar pekee yake

3. Uwajibikaji. Mswada huu umegusa baddhi ya maeneo. Kila chama cha siasa kinakuwa na nyraka muhimu kuhusu masuala ya kijinsia. Tunaweza kila chama kikatengeneza nyaraka nzuri. Lakini sasa baada ya kutengeneza nyaraka hizo ikiwamo genda policy uwajibikaji wake ni upi. Tuwe na kifungu cha uwajibikaji

4. Kudhibiti kwa kiwango kikubwa rushwa ya ngono. Nimewahi kufanya utafiti sehemu moja. Kuwa kwanini wanawake hawashiriki kwa wingi. Jambo kubwa ni rushwa ya ngono.


Tofauti na mambo ya kisheria:-
1. Sheria hizi ni muhimu sana kwa wananchi. Wananchi hawana uelewa wa sheria. Nimuhimu sheria hizi zikaandikwa kwa lugha nyepesi. Ili kila mwananchi aweze kuzifahamu kwa wapesi. Popula version iweke kwa lugha nyepesi.

2. Huu mchakato ni mzuri umeshirikisha makundi yote. Napendekeza pia ufanyike Zanzibar

3. Kifungu cha 132 cha katiba ya Zanzibar. Kwa sasa kifungu hiki kipo. Ili kifungu kiweze kutumika zanzibar lazima ipelekwe baraza la wawakilishi. Baada ya kutiwa saini ipelekwe baraza la wawakilishi.
 
Nafasi kwa wajumbe wa mkutano kuzungumza na kutoa mapendekezo. Naanza na viongozi wetu.
 
Mwenyekiti UWT Taifa. Mary Chatanda baadae Zitto Kabwe. Kisha nitachukuwa mikono mitano
 
Mary Chatanda:
Mwenyekiti umoja wa wanawake CCM Taifa.
Sisi kama UWT tumeona hali kwa nyuma zilikuwepo. Wenye viti wa vijiji ni wachache sana.
Sasa basi katika mswada huu tumeona ili msajiri wa vyama siasa ili awe na meno.
Atamke wazi kuwa agharau chama kipendekeze 20% ya wanawake. Pia itamke kuwa kiasi fulani cha wanawake kutoka kwenye ruzuku ziende kwa wanawake.

Uteuzi wa mwenyekiti na makamu. Kitamke kuwa kama mwenyekiti ni jinsia fulani awe jinsia fulani basi awe jinisa tofauti.
Kesho nitaoa hii
 
Zitto Kabwe:
Nina maoni kwenye sheria ya vyama vya siasa. Serikali imeleta mswada mmoja wenye sheria mbili.
Maoni yangu kwenye sheria ya vyama vya siasa. Malalamiko mengi yaliyotolewa na wadau ilikuwa ni kuhusu amendment zilizofanywa 2019. Zilizofanya kuwepo na ujinai. Natulisema ujinai uondolewe. Katika mswada huu mapendekezo haya hayajatekelezwa.

Eneo la pili. Jinsia. Taarifa ya kikosi kazi ni maelezo mahususi. Kwamba isipungue 30% kwenye sheria inayopendekezwa na serikali halipo kabisa. Limeondolewa kabisa. Tunawaomba wale wanaodraft wakaangalie tena

Jambo jingine. Ruzuku ya vyama vya siasa. Mfumo wa ruzuku kwa sasa vyama vinaenda kwenye uchaguzi kutokana na idadi ya wale waliochaguliwa ndio ruzuku yako. Bases ya uchaguzi mkuu isiwe uchaguzi mkuu. iwe na chaguzi ndogo.
Hakuna kitu hicho duniani kote. Hii haiwezekani maana mtu akihama chama anahama na ruzuku yake.

Pendekezo ni kubadilisha ruzuku na kuvifanya viwe taasisi. Yaani 10% ya bajeti ipelekwe kwa na kugawanywa kwa usawa.
Kinachotakiwa ni kuvijenga vyama kitaasisi. Mfumo tunaoutumia ni wa zamani umepitwa na wakati.
Issue ilikuwa vyama kupewa ruzuku pesa itatoka wapi. Ni pesa hii hii ya ruzuku 10% inagawiwa kwa vyama vyote.
Naomba kupendekeza ofsi ya wanasheria mkuu wa serikali achukue mambo yenye mwafaka.
 
Mchangiaji wa tatu: Mzee Kificho
Naomba nitoe chango nikiwa nimekaa.
Jambo moja ninataka nichangie. Kutengenza sheria kisha ikapigwa saini kisha ikapitishwa baraza la wawakilishi. Nadhani mswada uje kabla ya raisi kitiwa saini.

Ushiriki wa wanawake. Nilikuwa uingereza nikauliza sabau za ushiriki mdogo wa wanawake. Mambo ya wanawake ni mengi. Ikiwemo kulea, kuzaa nk. Wanawake kuzaa ni wajibu wao.
 
Mchangiaji mwingine: Dominata Ruchungura TLP
Sisi ndio waddau wa mswaada huu. Nampongeza Avemaria Dokta. Nimekuwa kwenye siasa nikiwa kijana. Mpaka leo nimekuwa mzee sijawahi kuwa mwenyekiti au katibu. Tatizo ni sheria. Sheria itamke Mwenyekiti akiwa Mwanaume Katibu awe mwanamke.

Gharama ya uchaguzi. Leo tukosalama kesho tutakuwa salama? Anaweza mwarabu, mhisnid mzungu akanunua chama. Serikali igharamie vyama vya siasa vyote.
 
Bwana Msafiri Mwajuma Mariam
Natokea upande wa kwanza wa Tanganyika.
Mimi natokea mtandao wa wanawake na Katiba. Nembo ya taifa yenye nembo ya bibi na bwana. Nitaifa la kwanza ku saporti genda.

Nilikuwa naangazia 50/50. Anasema wanataka 50/50. Anataka viti maalum vifutwe. Wanawake wasimame maana viti maalum ni kuwazalilisha.

Tunatakiwa tuwe na sera ya taifa. Atakaechaguliwa atekeleze sera ya Taifa siyo Ilani ya Chama.
 
Mwingine:
Neema Lugangila Mbunge wa CCM
Kwenye mada ya kwanza ya 4R. Napendekeza katika sheria ya vyama vya siasa kuwa lazima kuwe na wajumbe wanawake. Liwe jambo la kisheria kwenye baraza la vyama vya siasa kuwe na wanawake. Ili kuongeza wigo wa wanawake.
 
Doyo:
Mimi lishachangia na hoja yangu ulishaijibu. Kuwa vyama vya siasa viandae kanuni.
 
Wamealika watu waliowaandalia cha kuchangia na account zao zimewekwa kitita danganyeni wajinga.

Mkitaka maoni halisi muwafuate watu level ya mtaani mbona sensa mlikua mnazunguka ?

Hayo ni maoni ya wachache ambao ni "sell outs" tu, na ni rahisi kupika data.

State sponsored decoy to hoodwink the majority will.
 
Mng'ong'o:
Nilikuwa mjumbe wa kikosi kazi. Baraza la vyam vya siasa lazima litengewe ruzuku. Sheria lazima iseme kuwa ni muhimu baraza liweze kutengewa ruzuku.
Tuwe makini katika kutoa ruzuku. Lazima vyama vyenyesifa viweze kukdhi vyama. Mbunge akfariki inakuwaje.
Kuna vitengo mbalimbali. Mfano jumuiya na nk. Walemavu wataweza kuhudumiwa vipi kama hakuna ruzuku.
 
Mzee Duni
Mengi yamesemwa. Kunahoja moja nzito haijazungumzwa. Matatizo tunayopata na polis. Vurugu tunazokuwa tukizipata kutoka kwa polis. Sheria inaonekana kama wanatumilki katika kuendesha sheria. Lazima tuweke sehemu kuhusu hawa polisi wasiweze kututhibiti. Ukifika wakati tunaweza kupata taabu sana.
 
Back
Top Bottom