Ufunguzi wa Mkutano maalumu wa baraza la Vyama vya Siasa 03 Januari 2024

Venus Star

JF-Expert Member
Dec 6, 2018
19,695
59,848
UFUNGUZI WA MKUTANO MAALUM WA BARAZA LA VYAMA VYA SIASA

Mkutano huu kushirikisha Wadau wa Demokrasia ya Vyama vingi vya Siasa.

Lengo ni kujadili Miswaada ya Sheria za Uchaguzi na Sheria za Vyama vya Siasa iliyosomwa kwa mara ya kwanza Bungeni Novemba 10, 2023.

Kauli Mbiu;
" TOA MAONI YAKO KUIMARISHA DEMOKRASIA "

MGENI RASMI;
Mhe. Othman Masoud Othman
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar

🗓️ Mkutano huu utafanyika Tarehe 3 na 4 Januari, 2024
📍Ukumbi wa Julius Nyerere International Convetion Centre - Dar es salaam

#ImarishaDemokrasia
#TunzaAmani
#KatibaYaWatu
#KatibaNiMaridhiano
#UchaguziNiMashindano
#MatokeoChanya
##SisiNiTanzania

247e69a4-ca3f-491a-8891-21f4e82351bb.jpg
 
Kama vikao hivi huwa na posho ya vikao basi ndiyo huwa inawavutia wajumbe kuhudhuria! Vinginevyo havina manufaa yo yote na wajumbe wanalifahamu hilo!

Ni heri Baraza livunjiliwe mbali kuliko kuendelea kuwepo kwa manufaa ya CCM!
 
Unahasira sana kijana mwenzangu kwanini?
 
Sijawahi kusikia kama serikali ya CCM hutilia maanani maoni yo yote ya vikao hivi zaidi ya CCM kuvifanya kama propaganda ya kuonyesha Tanzania kuna vyama vingi vya siasa!
Kwa sasa ndio mwafaka maana ndio kipindi sahihi cha Serikali kuchukua maoni ya watu. Karibu ujionee.
Mwaka Mpya na Mambo Mapya. Forget the past.
 
Kama vikao hivi huwa na posho ya vikao basi ndiyo huwa inawavutia wajumbe kuhudhuria! Vinginevyo havina manufaa yo yote na wajumbe wanalifahamu hilo!

Ni heri Baraza livunjiliwe mbali kuliko kuendelea kuwepo kwa manufaa ya CCM!
Posho ya kikao ni 200,000 kwa kila mjumbe siku 2= 400,000 kama ametoka nje na Dar perdiem 250,000 x 3 = 750,000 na nauli ya ndege inategemea anatoka wapi = 1,150,000 nje na nauli ila kama ni Dar ni 125,000 x 3 = 375,000 + 400,000= 775,000 si haba na hii January na jamaa waliweka January makusudi wakijua hapo akili za wengi zitakuwa kwenye posho badala ya mada yenyewe.
 
Jina la Netanyahu linanikumbusha Mbali sana. Unamfahamu?
 
Baraza la Vyama vya Siasa limeundwa ndani ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa. Wajumbe wa Baraza hili hujumuisha viongozi wa kitaifa wawili wa kila chama cha siasa chenye usajili wa kudumu. Ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa ndio yenye jukumu la kisheria ya kuratibu shughuli za Baraza la Vyama vya Siasa.

Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa na Makamu Mwenyekiti huchaguliwa kwa kupigiwa kura na wajumbe wa Baraza.

Majukumu ya Baraza la Vyama vya Siasa

1. Kumshauri Msajili wa Vyama vya Siasa juu ya mgogoro inayotokea kwenye vyama vya siasa;
2. Kumsahuri Msajili wa Vyama vya Siasa juu ya masuala yenye maslahi kwa Taifa kuhusiana na vyama vya siasa au kuhusiana na hali ya kisiasa nchini;
3. Kuishauri Serikali kupitia kwa Msajili wa Vyama vya Siasa juu ya kupitishwa kwa marekebisho na utekelezaji wa Sheria ya Vyama vya Siasa na sheria zingine zinazohusu masuala ya vyama vya siasa;
4. Kushauri juu ya kanuni zinazosimamia masuala yanayohusu vyama vya siasa;
5. Kutoa taarifa kwa Msajili wa Vyama vya Siasa juu ya uendeshaji wa chama chochote cha siasa.
 
Wenyenia nzuri na nchi hii wanatoa maoni yao. Je wewe upo upande gani?
 
Hekima, Umoja na Amani
Hizi ni ngao zetu.
Maneno haya ukiyatafakari kwa kina utajua sisi ni nchi ya kipekee sana hapa duniani.
 
Back
Top Bottom