Mkurugenzi Mkuu (TPA): Mkataba hauna miaka 100, muda bado haujaamuliwa. Tumemchagua DP World kwakuwa tuna uhakika tutakwenda kutatua changamoto zetu

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,817
4,566
1686214149162.png

Plasduce Mkeli Mbossa, Mkurugenzi Mkuu TPA

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Plasduce Mkeli Mbossa akiwa katika Clubhouse ya Msemaji Mkuu wa Serikali Juni 7, 2023. Ametoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali kuhusu Mkataba wa Bandari ambao umezua mijadala mingi.

Akioa ufafanuzi wa jabo hili Plasduce Mkeli Mbossa alisema:

Mkataba huo hauna Miaka 100, muda bado haujaamuliwa ila unasema tutashirikiana katika masuala ya uendeshaji wa bandari na mafunzo na si mkataba wa utekelezaji wa shughuli yoyote ila ukiridhiwa unatengeneza mkataba mwingine wa utekelezaji.

Serikali inafanya juhudi kubwa lakini juhudi kubwa zaidi zinahitajika. Ndiyo maana tuliona kuna haja ya kushirikiana na wenzetu. Kama nchi tumehakikisha tunamchagua mbia tunayeona tunaweza kufaya naye kazi na tumekuwa na maongezi na makampuni mbalimbali ikiwamo Dubai Port na DP World

Baada ya kuondoka kwa Kampuni ya TICTS Mamlaka ya Bandari imekuwa ikifanya juhudi mbalimbali kulingana na sheria ili kuwa na ufanisi wa hali ya juu kama kuhudumia meli.

Tumekuwa tukionea na nchi nyingi na kampuni tofauti tofauti za kuendesha bandari kama Singapore, APM Terminals na DP World lakini unaangalia ni yupi anakupa manufaa makubwa zaidi. DP World anaendesha bandari nyingi na hivyo anafanya vizuri na tuna sababu nyingi za kumchagua DP World kwakuwa tuna uhakika tutakwenda kutatua changamoto zetu.

Tuliona upo umuhimu wa kushirikiana na DP World ambao wanaendesha bandari kubwa Kigali hivyo tuliona bandari hiyo ya Kigali inabeba mzigo mkubwa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo tunaweza kushirikiana nao.

Katika mikataba tunayoingia masuala yote ya ulinzi yanabaki kuwa ya nchi yetu. Mipaka yote inalindwa na nchi yetu na Vyombo vya Ulinzi na Usalama vitaendelea kuwapo miaka yote. Vifungu vyote vya kataba vinatakiwa kuzingatia masuala ya ulinzi kuwa ni suala la nchi husika.

Hati ya makubaliano tuliyoingia na DP World ni makubaliano lakini si mkataba, tunaongea na Makampuni mengi na baada ya kufanya hivyo tutaangalia utaratibu wa kisheria kuweza kuingia mkataba. Matarajio yetu kwamba Wafanyakazi wote wa TPA watabaki na ajira zao na hilo tutaliweka katika mikataba ya makubaliano.

TPA itaendela kuendesha maeneo mengne kulingana na makubaliano tutakayokuwa tumeweka. Lengo ni kuhakikisha kuwa kunakuwepona ufanisi na kukuwa kwa shughuli nyingine za kiuchumi.

Mwaka ujao wa fedha serikali itaanza kujenga Bandari ya Bagamoyo, Ziwa Nyasa na Mtwara. Katika Bandari ya Tanga tutaongeza geti moja. Mwanza North na South zote hizi zinajengwa na Serikali lakini mahitaji ni makubwa. Katika masuala ya uendeshaji bandari kuwa na geti peke yake haizuii kuhusisha Sekta Binafsi.
 
Bwana Mkurugenzi mkuu acha kujibu na kutoa ufafanuzi wa hivi viishu vidogo vifogo. Jibu tuhuma hizi nzito kwa mfano watu wanasema kuliko kuendelea na uwizi, ubadhirifu, rushwa na hujuma za aina hiyo zinazoendelea sasa bandarini ni bora apewe mwarabu. Utendaji wa kizembe bandarini ni moja ya sababu kuu inayotumiwa kuhalalidha huu ubinafisishaji. Wewe unasemaje mheshimiwa sana???
 
Ni spika tu huyo tunataka kuona redio
 
Duh.......!
 
Huyo mkurugenzi atoe sababu za nini kimepelekea wao wenyewe kushindwa kama mamlaka kuendesha bandari mpk wahitaji msaada

Mojawapo ya faida ya uwekezaji ni pamoja na kupata teknolojia pamoja na skills kutoka kwa muwekezaji Ticts alikuwepo hapo ina maana hawakugain chochote ili kuwasaidia wakiondoka wao watakeover kama hawakupata chochote then wana matatizo ndiyo maana wanaona waingie mkataba mwingine lini watakua hao TPA?
 
Bwana Mkurugenzi mkuu acha kujibu na kutoa ufafanuzi wa hivi viishu vidogo vifogo. Jibu tuhuma hizi nzito kwa mfano watu wanasema kuliko kuendelea na uwizi, ubadhirifu, rushwa na hujuma za aina hiyo zinazoendelea sasa bandarini ni bora apewe mwarabu. Utendaji wa kizembe bandarini ni moja ya sababu kuu inayotumiwa kuhalalidha huu ubinafisishaji. Wewe unasemaje mheshimiwa sana???
Ukijibiwa hapa niite "nyau" nimekaa pale 👉
 
View attachment 2649919
Plasduce Mkeli Mbossa, Mkurugenzi Mkuu TPA

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Plasduce Mkeli Mbossa akiwa katika Clubhouse ya Msemaji Mkuu wa Serikali Juni 7, 2023. Ametoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali kuhusu Mkataba wa Bandari ambao umezua mijadala mingi.

Akioa ufafanuzi wa jabo hili Plasduce Mkeli Mbossa alisema:

Mkataba huo hauna Miaka 100, muda bado haujaamuliwa ila unasema tutashirikiana katika masuala ya uendeshaji wa bandari na mafunzo na si mkataba wa utekelezaji wa shughuli yoyote ila ukiridhiwa unatengeneza mkataba mwingine wa utekelezaji.

Serikali inafanya juhudi kubwa lakini juhudi kubwa zaidi zinahitajika. Ndiyo maana tuliona kuna haja ya kushirikiana na wenzetu. Kama nchi tumehakikisha tunamchagua mbia tunayeona tunaweza kufaya naye kazi na tumekuwa na maongezi na makampuni mbalimbali ikiwamo Dubai Port na DP World

Baada ya kuondoka kwa Kampuni ya TICTS Mamlaka ya Bandari imekuwa ikifanya juhudi mbalimbali kulingana na sheria ili kuwa na ufanisi wa hali ya juu kama kuhudumia meli.

Tumekuwa tukionea na nchi nyingi na kampuni tofauti tofauti za kuendesha bandari kama Singapore, APM Terminals na DP World lakini unaangalia ni yupi anakupa manufaa makubwa zaidi. DP World anaendesha bandari nyingi na hivyo anafanya vizuri na tuna sababu nyingi za kumchagua DP World kwakuwa tuna uhakika tutakwenda kutatua changamoto zetu.

Tuliona upo umuhimu wa kushirikiana na DP World ambao wanaendesha bandari kubwa Kigali hivyo tuliona bandari hiyo ya Kigali inabeba mzigo mkubwa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo tunaweza kushirikiana nao.

Katika mikataba tunayoingia masuala yote ya ulinzi yanabaki kuwa ya nchi yetu. Mipaka yote inalindwa na nchi yetu na Vyombo vya Ulinzi na Usalama vitaendelea kuwapo miaka yote. Vifungu vyote vya kataba vinatakiwa kuzingatia masuala ya ulinzi kuwa ni suala la nchi husika.

Hati ya makubaliano tuliyoingia na DP World ni makubaliano lakini si mkataba, tunaongea na Makampuni mengi na baada ya kufanya hivyo tutaangalia utaratibu wa kisheria kuweza kuingia mkataba. Matarajio yetu kwamba Wafanyakazi wote wa TPA watabaki na ajira zao na hilo tutaliweka katika mikataba ya makubaliano.

TPA itaendela kuendesha maeneo mengne kulingana na makubaliano tutakayokuwa tumeweka. Lengo ni kuhakikisha kuwa kunakuwepona ufanisi na kukuwa kwa shughuli nyingine za kiuchumi.

Mwaka ujao wa fedha serikali itaanza kujenga Bandari ya Bagamoyo, Ziwa Nyasa na Mtwara. Katika Bandari ya Tanga tutaongeza geti moja. Mwanza North na South zote hizi zinajengwa na Serikali lakini mahitaji ni makubwa. Katika masuala ya uendeshaji bandari kuwa na geti peke yake haizuii kuhusisha Sekta Binafsi.
Naunga mkono hoja.
P
 
Back
Top Bottom