Bandari ya Dar es Salaam yajivunia kuvuka lengo

FbUser

JF-Expert Member
Oct 22, 2014
430
623
MAMLAKA ya Usimamizi wa Bandari Tanzania TPA imetoa taarifa inayoonyesha mafanikio makubwa yaliyofikiwa na Bandari ya Dar es Salaam kwa mwaka jana.

Akiongea mbele ya Waandishi wa habari Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania Plasduce Mkeli Mbossa amesema katika kipindi cha Julai hadi Disemba mwaka jana TPA imeweza kuvuka malengo yake kwa kuhudumia meli 979 ambalo ni ongezeko la meli zaidi ya 200 kutoka lengo la awali la meli 792.

Mbossa amesema katika kipindi hcho lengo jingine liliwekwa kuhudumia takriban makasha 500 lakini lengo lilivukwa na kufikia makasha 900 huku tani za mizigo milioni 17.2 kutoka tani milioni 15.6 zilizokusudiwa awali.

Amesema hayo ni mafanikio makubwa ambayo mamlaka imeyafikia hatua hiyo ikiwa imechangiwa na mpango mkubwa wa TPA kuboresha huduma kwenye bandari zote nchini.

Mkurugenzi huyo pia amefafanua kuwa mpango huo ndio umechangia hatua za maboresho ya bandari ya Dar es Salaam na kuweza kuleta mafanikio na sasa meli hadi 12 zinahudumiwa kwa wakati mmoja na kuongeza wastani wa meli 100 kuhudumiwa kwa mwezi mmoja kutoka meli 70 kwa mwezi hapo awali.

Kuhusu kampuni ya Dubai, DP WORLD Mbossa amesema Kampuni hiyo itaanza shughuli zake kwenye Bandari ya Dar es Salaam robo ya kwanza ya mwaka ya mwaka huu pale itakapokamilisha taratibu za kisheria.

Mkurugenzi amesema kuna taratibu ambazo hazijakamilika kama vile ukataji wa leseni ya kuendesha Bandari, pamoja na uundwaji wa kampuni ya pamoja kati yake na serikali kama makubaliano yanavyoelekeza.

"Kwahiyo mategemeo yetu ni kwamba tutaanza katika nusu ya mwaka huu wa kifedha taratibu zikikamilika, tutatoa taarifa rasmi ya tarehe ambayo wataanza kazi" Amesema Mbossa

Sent from my Infinix X669 using JamiiForums mobile app
 
Hongera sana TPA.
Ongezeni juhudi ili mfike mbali zaidi ya hapo.
 
Hawa DP WORLD WANASHUSHA MA CRANES KUANZIA LINI?
 
Kusema ukweli watanzania tukiamua tunaweza. Mambo machache yanayotukwamisha ni pamoja na Ujinga, Ubabaishaji, Rushwa/Ufisadi, na Kufanyakazi kwa mazoea/bila ufanisi. Tukiyaondoa hayo tunaweza kuipaisha nchi yetu kimaendeleo ndani ya miaka 20 hadi 30 tu.
 
MAMLAKA ya Usimamizi wa Bandari Tanzania TPA imetoa taarifa inayoonyesha mafanikio makubwa yaliyofikiwa na Bandari ya Dar es Salaam kwa mwaka jana.

Akiongea mbele ya Waandishi wa habari Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania Plasduce Mkeli Mbossa amesema katika kipindi cha Julai hadi Disemba mwaka jana TPA imeweza kuvuka malengo yake kwa kuhudumia meli 979 ambalo ni ongezeko la meli zaidi ya 200 kutoka lengo la awali la meli 792.

Mbossa amesema katika kipindi hcho lengo jingine liliwekwa kuhudumia takriban makasha 500 lakini lengo lilivukwa na kufikia makasha 900 huku tani za mizigo milioni 17.2 kutoka tani milioni 15.6 zilizokusudiwa awali.

Amesema hayo ni mafanikio makubwa ambayo mamlaka imeyafikia hatua hiyo ikiwa imechangiwa na mpango mkubwa wa TPA kuboresha huduma kwenye bandari zote nchini.

Mkurugenzi huyo pia amefafanua kuwa mpango huo ndio umechangia hatua za maboresho ya bandari ya Dar es Salaam na kuweza kuleta mafanikio na sasa meli hadi 12 zinahudumiwa kwa wakati mmoja na kuongeza wastani wa meli 100 kuhudumiwa kwa mwezi mmoja kutoka meli 70 kwa mwezi hapo awali.

Kuhusu kampuni ya Dubai, DP WORLD Mbossa amesema Kampuni hiyo itaanza shughuli zake kwenye Bandari ya Dar es Salaam robo ya kwanza ya mwaka ya mwaka huu pale itakapokamilisha taratibu za kisheria.

Mkurugenzi amesema kuna taratibu ambazo hazijakamilika kama vile ukataji wa leseni ya kuendesha Bandari, pamoja na uundwaji wa kampuni ya pamoja kati yake na serikali kama makubaliano yanavyoelekeza.

"Kwahiyo mategemeo yetu ni kwamba tutaanza katika nusu ya mwaka huu wa kifedha taratibu zikikamilika, tutatoa taarifa rasmi ya tarehe ambayo wataanza kazi" Amesema Mbossa

Sent from my Infinix X669 using JamiiForums mobile app
Hongera kwa Menejiment na Wafanyakazi wa Mamlaka ya Bandari (TPA) kwa kuvuka lengo. Waedelee kuongeza ufanisi na kuboresha huduma kwa wateja.

Kwa huduma bora ya Clearing & Forwarding (Local & Transit) kwa mizigo aina yote, karibu Ruaha Freight Ltd,
Wasiliana nasi;

Ruaha Freight Ltd,
Umati building 3rd Floor, Room No 18 Samora Avenue / zanaki street Dar es Salaam. P.O.Box 62442
Dar es Salaam
.
Email: info@ruahafreight.com
Website: www.ruahafreight.com
Tel: +255222128447

Mob: +255718 866 651 (call or whatsapp).
 
Hofu ya DP World hiyo. Wameanza kujirekebisha na akili kuwakaa sawa. Na bado mna uwezo wa kufanya zaidi ya hapo x2.
 
MAMLAKA ya Usimamizi wa Bandari Tanzania TPA imetoa taarifa inayoonyesha mafanikio makubwa yaliyofikiwa na Bandari ya Dar es Salaam kwa mwaka jana.

Akiongea mbele ya Waandishi wa habari Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania Plasduce Mkeli Mbossa amesema katika kipindi cha Julai hadi Disemba mwaka jana TPA imeweza kuvuka malengo yake kwa kuhudumia meli 979 ambalo ni ongezeko la meli zaidi ya 200 kutoka lengo la awali la meli 792.

Mbossa amesema katika kipindi hcho lengo jingine liliwekwa kuhudumia takriban makasha 500 lakini lengo lilivukwa na kufikia makasha 900 huku tani za mizigo milioni 17.2 kutoka tani milioni 15.6 zilizokusudiwa awali.

Amesema hayo ni mafanikio makubwa ambayo mamlaka imeyafikia hatua hiyo ikiwa imechangiwa na mpango mkubwa wa TPA kuboresha huduma kwenye bandari zote nchini.

Mkurugenzi huyo pia amefafanua kuwa mpango huo ndio umechangia hatua za maboresho ya bandari ya Dar es Salaam na kuweza kuleta mafanikio na sasa meli hadi 12 zinahudumiwa kwa wakati mmoja na kuongeza wastani wa meli 100 kuhudumiwa kwa mwezi mmoja kutoka meli 70 kwa mwezi hapo awali.

Kuhusu kampuni ya Dubai, DP WORLD Mbossa amesema Kampuni hiyo itaanza shughuli zake kwenye Bandari ya Dar es Salaam robo ya kwanza ya mwaka ya mwaka huu pale itakapokamilisha taratibu za kisheria.

Mkurugenzi amesema kuna taratibu ambazo hazijakamilika kama vile ukataji wa leseni ya kuendesha Bandari, pamoja na uundwaji wa kampuni ya pamoja kati yake na serikali kama makubaliano yanavyoelekeza.

"Kwahiyo mategemeo yetu ni kwamba tutaanza katika nusu ya mwaka huu wa kifedha taratibu zikikamilika, tutatoa taarifa rasmi ya tarehe ambayo wataanza kazi" Amesema Mbossa

Sent from my Infinix X669 using JamiiForums mobile app
hongera yao kwa kweli. kwa data wanazomwaga sasa hivi. wanastahili pongezi
 
Back
Top Bottom