Mbunge Mchafu: Wanaume Tanzania wanajadili zaidi Simba na Yanga kuliko afya zao

Kichuchunge

JF-Expert Member
Dec 2, 2020
338
891
Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Hawa Mchafu amedai baadhi ya wanaume wa Tanzania wanatumia nguvu kubwa kujadili habari za timu za Simba na Yanga zinazoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara, kuliko hata kujadili afya zao.

Hawa amesema kama nguvu hiyo ingetumika kujadili masuala ya afya ikiwemo kupima Ukimwi, huenda vita dhidi ya ugonjwa huo ingekuwa nyepesi.

Mbunge huyo ametoa kauli hiyo leo Jumanne Mei 11, 2021 bungeni mjini Dodoma wakati akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Afya mwaka 2021/22.

Amesema wanaume wakikutana maeneo yote wanazungumzia timu hizo zenye upinzani wa jadi nchini badala ya kujadili masuala mengine ya msingi zikiwemo afya zao.

"Wanaume wa Tanzania wanatumia muda mwingi kujadili Usimba na Uyanga, hawapimi virusi vya Ukimwi na hawataki kupima, hivi ingetumika muda huo kuzungumza masuala ya kupima afya zao si tungeshinda," amehoji Mchafu.

Mei 8, 2021 mchezo kati ya miamba hiyo ya soka nchini uliahirishwa baada ya kutokea mkanganyiko uliosababishwa na ratiba kubadilishwa kutoka saa 11 jioni na kusogezwa mbele hadi saa 1 usiku jambo lililozua sintofahamu huku kila shabiki wa soka nchini akizungumza lake.

Akieleza zaidi kuhusu maambukizi ya Ukimwi, Hawa amesema tatizo lipo kwa wanaume waliooa ambao hutegea wake zao wapime afya ndio nao wapate majibu na kujipa matumaini wakati hawajui kuwa kinga za mwili zinatofautiana.

Kuhusu ukeketaji, amesema wanaume wanatakiwa kutangaza hadharani kwamba hawawezi kuwaoa wanawake waliokeketwa lakini kukaa kwao kimya bado ukatili huo utaendelea.

Kwa mujibu wa Hawa, wanaume wakisema ladha ya waliokeketwa in tofauti na wasiokeketwa, jambo hilo litakwisha mara moja na kubaki historia.

Chanzo: Mwananchi
 
Hawa ndo wale wapenda mademu soka liliwapita kushoto, akikuta mada za mademu anavuta kiti anakaa na kua mchangiaji mkuu.
 
Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Hawa Mchafu amedai baadhi ya wanaume wa Tanzania wanatumia nguvu kubwa kujadili habari za timu za Simba na Yanga zinazoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara, kuliko hata kujadili afya zao.

Hawa amesema kama nguvu hiyo ingetumika kujadili masuala ya afya ikiwemo kupima Ukimwi, huenda vita dhidi ya ugonjwa huo ingekuwa nyepesi. Mbunge huyo ametoa kauli hiyo leo Jumanne Mei 11, 2021 bungeni mjini Dodoma wakati akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Afya mwaka 2021/22.

Amesema wanaume wakikutana maeneo yote wanazungumzia timu hizo zenye upinzani wa jadi nchini badala ya kujadili masuala mengine ya msingi zikiwemo afya zao.

"Wanaume wa Tanzania wanatumia muda mwingi kujadili Usimba na Uyanga, hawapimi virusi vya Ukimwi na hawataki kupima, hivi ingetumika muda huo kuzungumza masuala ya kupima afya zao si tungeshinda," amehoji Mchafu.

Mei 8, 2021 mchezo kati ya miamba hiyo ya soka nchini uliahirishwa baada ya kutokea mkanganyiko uliosababishwa na ratiba kubadilishwa kutoka saa 11 jioni na kusogezwa mbele hadi saa 1 usiku jambo lililozua sintofahamu huku kila shabiki wa soka nchini akizungumza lake.

Akieleza zaidi kuhusu maambukizi ya Ukimwi, Hawa amesema tatizo lipo kwa wanaume waliooa ambao hutegea wake zao wapime afya ndio nao wapate majibu na kujipa matumaini wakati hawajui kuwa kinga za mwili zinatofautiana.

Kuhusu ukeketaji, amesema wanaume wanatakiwa kutangaza hadharani kwamba hawawezi kuwaoa wanawake waliokeketwa lakini kukaa kwao kimya bado ukatili huo utaendelea.

Kwa mujibu wa Hawa, wanaume wakisema ladha ya waliokeketwa in tofauti na wasiokeketwa, jambo hilo litakwisha mara moja na kubaki historia.

Chanzo: Mwananchi
 
Jina lake tu majanga. Hawa Mchafu usiku huu uchafu wake wa tabia ndio unaosababisha magonjwa ya UKIMWI aanze yeye kwanza awe msafi ili UKIMWI uishe kabisa.
 
Afya ni Issue binafsi ya mtu na sio Issue ya kujadiliwa mitandaoni. Mpira unajadiliwa mitandoni publicly sababu ni burudani na Inaleta afya pia.

Tunajadili sana afya zetu tukiwa chumbani na wapendwa wetu.

Au anataka tuanze kujadili afya zetu mitandaoni ndio ajue tupo makini!

Pathetic.
 
Back
Top Bottom