Edo Kumwembe: Simba na Yanga, peponi hazipo motoni hazipo

Oldmantz

JF-Expert Member
Jan 24, 2023
430
998
HAKUNA kundi jepesi wala gumu kwa Simba na Yanga baada ya Ijumaa jioni kushuhudia wakipangwa na timu mbalimbali katika makundi yao ya Ligi ya Mabingwa. Waswahili tumeanza kupiga ramli. Inachekesha sana lakini ndio hali halisi. Fikiria kama wangepangwa wenyewe kwa wenyewe ingekuwaje?

Rafiki zangu Yanga wapo na Al Ahly ndugu zangu wa damu Simba wapo na Waydad Casablanca. Unakohoa kidogo kabla ya kufikiria ukweli ambao watu hawataki kuusema. Hawa wawili ndio viongozi wa kundi. Wazungu wanasema wapo katika Poti A.

Halafu huku chini kwa Simba kuna wadogo wawili ambao ni ASEC MIMOSAS na Jwaneng Galaxy. Kwa Yanga kuna mkubwa mwingine mmoja juu yake, CR Belouzidad halafu kuna mdogo wake Medeama. Tunajaribu kutafakari namna makundi yalivyo. Katika hali halisi hakuna kundi gumu wala jepesi.

Tatizo letu la msingi ni kuziangalia timu katika historia zao katika michuano hii, halafu tunatazama mataifa waliyotokea. Baada ya hapo tunaamua mambo mawili. Ama kujipeleka juu au kujishusha. Tunapaswa kuwa makini wakati tunafakari makundi ya mapacha hawa wa Kariakoo. Umakini unapaswa kuwa mkubwa kidogo.

Kwa mfano, kundi la Simba kuna ulazima gani Wydad Casablanca kuongoza kundi kama watu wanavyojipangia katika akili zao? Wydad walioitoa Simba katika hatua robo fainali walikuwa hoi. Labda warudi kivingine ndio tunaweza kuwapa uhalali wa kuwatoa Simba. Kwa Wydad wale basi kundi linaweza kuwa wazi tu.

Simba alikosa mabao kibao akiwa pale Temeke halafu akaenda kufungwa kizembe ugenini. Shukrani kwa bao la kizembe la kipa Ally Salim. Baadaye Clatous Chama na Shomari Kapombe wakakosa penalti zao kizembe tu wakati muda wa mpira ulipokwenda katika matuta. Naruhusu kukosolewa.

Kundi la Mnyama pia lina ASEC Mimosas na Jwaneng Galaxy. Hapa ndipo mpira wa Afrika haueleweki. Simba waliwahi kutolewa na Jwaneng katika michuano ya Shirikisho. Aibu iliyoje? Walishinda 2-0 pale Gaborone halafu wakafungwa 3-1 kwenye Uwanja wa Taifa. Hapa ndipo ambapo naamini kundi la Simba wala sio la kudharau wadogo na pia kuogopa wakubwa.

ASEC Mimosas ni timu ya kihistoria. Kwa sasa jina ni kubwa kuliko hali halisi. Kama zilivyo timu nyingi za Afrika Magharibi na wao hawana uwekezaji mkubwa katika michuano hii. Katika dirisha kubwa la uhamisho lililopita la uhamisho Rais wao alimpigia simu Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said akimpa ofa ya kuchukua wachezaji wanne klabuni kwake.

Yanga walifanikiwa kuwapata Pacome Zouzoua na Yao Kouassi. Simba wakaondoka na Aubin Kramo. Tatizo la soka la Afrika Magharibi hatujui ASEC imeziba mapengo hayo kwa kuwachukua wachezaji gani. Kama watarudi vizuri basi bado watafanya kazi chafu nitakayoielezea hapo baadaye.

Yanga? Kundi lao linaacha maswali ya msingi. Mbabe wao anatajwa kuwa Al Ahly. Nimekumbuka mambo mawili. Kwanza ni namna ambavyo kuna nyakati Simba walipangwa katika kundi lenye klabu za Al Ahly na AS Vita. Mwisho wa mechi zote Simba akaibuka kinara wa kundi akiwa na pointi 13. Al Ahly alikuwa akipigana kwa machozi, jasho na damu kufuzu kutokea kwenye kundi hilo.

Lakini hapo hapo nakumbuka namna ambavyo Al Ahly wanakuwa wateke kidogo wakicheza Dar es Salaam. Ushindi wao wa mwisho kwenye Uwanja wa Taifa pale Temeke ulikuja mwaka 2009 wakati Flavio Amado alipoitungua Yanga mwaka huo. Kuanzia hapo wamekuwa wakipata matokeo ya kushangaza Kwa Mkapa.

Mara mbili, Nadir Haroub Cannavaro na Jose Luis Miquissone wamewahi kuitungua Al Ahly kwa mabao ya ushindi kwenye Uwanja wa Taifa na mashabiki wa timu hizi pacha za Kariakoo wakaondoka mashujaa nje ya mageti ya Uwanja wa Taifa. Nini huwa kinawatokea Dar es Salaam? Huwa hatujui.

Lakini wakati Yanga akimfikiria zaidi Al Ahly bado anakabiliwa kucheza na bingwa wa Algeria, CR Belouzidad. Hatujui itakuwaje lakini majuzi tu Yanga walikuwa Algers wakishangaza mashabiki wa Algeria kwa kushinda pambano la marudiano dhidi ya USM Alger ugenini. Walikosea kwa kufungwa katika pambano la kwanza.

Sidhani kama CR Belouzidad watajiona salama wakicheza na Yanga. Nilipokuwa Algeria na timu ya taifa hivi karibuni, rafiki zangu fulani Waalgeria ambao wapo katika uongozi wa klabu za soka nchini humo waliniambia kwamba zamani viongozi hao walikuwa wanatamani kupangiwa kucheza dhidi ya timu za Tanzania lakini kwa sasa hawataki.

Kwanini hawataki? Kwa sababu ya kile ambacho Simba imekifanya katika miaka ya karibuni katika michuano ya soka barani Afrika lakini pia ni pale waliposhuhudia USM wakifungwa bao moja na Yanga katika pambano la fainali katika ardhi yao ya Waarabu. Hapa kazi bado ipo.

Yanga pia imeshinda mechi sita mfululizo ugenini katika michuano ya Afrika. Hakuna timu ya Tanzania iliyowahi kufanya hivi. Unapofikiria kwamba Yanga inaweza kufungwa ugenini kiurahisi tu na timu hizi inabidi uweke mguu katika breki.

Halafu kuna hii timu ya mwisho katika kundi. Medeama. Hawa ni kama ilivyo kwa ASEC. Timu kutoka Afrika Magharibi ambazo haziwekezi sana katika kununua wachezaji wakubwa wa ndani barani Afrika. Kazi yao kubwa ni kutibua tu matokeo ya kundi. Mara ya mwisho kwa timu ya Afrika Magharibi kuchukua taji la Afrika ilikuwa Enyimba mwaka 2003.

Watu wa Afrika Magharibi hawapo ‘serious’ na hilo taji lakini naamini kwamba kwa sasa katika makundi haya wataungana na Jwaneng Galaxy kuharibu matokeo ya vigogo. Simba na Yanga wawe makini na watu hawa. Wakati mwingine unaweza kuwa makini hasa na Wydad Casablanca na Al Ahly halafu ukaharibiwa na wengine.

Ukiangalia mienendo ya wakubwa wa Afrika kama Al Ahly na Wydad Casablanca ukweli ni kwamba bado hawatoi mwanga halisi wa namna makundi yatakavyokwenda. Ni kama ambavyo wadogo pia hawatoi hali halisi ya namna makundi yatakavyokwenda. Hii inasababisha nisiwaone Simba na Yanga popote pale baada ya makundi haya. Peponi hawapo na motoni hawapo.

Inabidi wapambane hasa. Hakuna hofu dhidi ya wakubwa lakini hakuna dharau dhidi ya wadogo. Mpira wa Afrika umekuwa na mawimbi makubwa yasiyoeleweka. Dharau inabidi iwekwe kando na mpira uchezwe uwanjani. Sioni sababu ya kuwa na dharau wala sioni sababu ya kuwa na hofu.

Matokeo ya Simba kuongoza kundi la Al Ahly na AS Vita kisha ikatolewa na Jwaneng Galaxy yanatupa picha ya namna mpira wa Afrika usivyoeleweka. Na ndio maana mpaka sasa naamini Mnyama na Mwananchi hadi sasa peponi hawapo na wala motoni hawapo!

Credit: Mwanaspoti
 
Edo ANAANDIKA vizuri mno ni muandishi mzuri sana WA Michezo na makala za kisiasa.

Huko kwenye Utangazaji, UCHAMBUZI amevamia fani ya JEMEDARI na Ambangile.

Nimshauri abaki na Uandishi wake tu.
Kure KUROPOKA kunamshusha thamani yake.
 
Yuko vizuri sana kuandika kuliko kuongea,zamani alikuwa anaweka sana uandishi Facebook ,ukisoma unamkubali,lakini akija kuongea ni tofauti.
Ndo Ile kauli hakuna mkamilifu...jamaa n mwandishi mzur kina Ali kamwe ..Farhan wote wanamuiga yeye Ila ukija kwenye speaking skills n average sana
 
Sio Simba & Yanga tu. Na yeye PEPONI HATOINGIA. Narudia HATOINGIA
 
Edo kumwembe ni legend. Huyu jamaa alinifanya niwe nanunua gazeti la mwananchi kila wiki mara mbili kuanzia 2010-2013. Mara chache sana nilikosa kununua
 
Back
Top Bottom