Kuna mkenya mmoja ameniuliza swali gumu, nikashindwa kujibu na akanipa jibu lililo nisisimua sana, naomba kama kuna mtu mwenye jibu zuri zaidi anisaidie. Nimeulizwa, Regia alikuwa nani? Mbona ameziteka sana nyoyo za watanzania? Nilimjibu alikuwa mbunge wa watu. Akaniambia wapo wengi na pia tangia amekaa Tz hajawahi kuona mazishi makubwa hivi ukiachilia nyerere. Akasema hata kawawa hakupata mazishi makubwa hivi. Hapo nilikosa jibu. Akaniambia Mandela alishawahi kusema "Mtu shujaa atazikwa kwa heshima na historia yake inaanza kuandikwa siku ya kifo chake na siku zote watu watasema, hapa amelala mtu shujaa, lakini mtu mwoga mwisho wa historia yake ni pale udongo wa mwisho utakapowekwa kwenye kaburi lake. Kwa hiyo akasema Regia amewavuta sana Watanzania na ameweza kupasua pazia la vyama, ukabila , udini nk kwa kuwa alikuwa shujaa na daima watu watalitembelea kaburi lake na kusema hapa amelala shujaa.
Maneno haya yamenigusa sana. Ni kweli Regia hakuwa na pesa, wala hakuwa na uzoefu wa kisiasa,wala hakuwa na elimu kubwa, tena alikuwa na ulemavu ila alikuwa jasiri shujaa. kuna mabilionea na maprofesa wamezikwa, leo wala hakuna anayewakumbuka. Hawakuwa mashujaa, walikuwa waoga na kujali maslahi binafsi ambayo mwisho wake ulikuwa ziku za kuzikwa kwao.
Tujifunze kwa Regia, Nyerere at el, fanya kazi ya umma, kuwa mtu wa watu, kuwa mkweli, shujaa na usiwe mwoga, wala usiweke maslahi ya familia yako mbele, utazikwa kama shujaa. Una nafasi ya kuchagua kuwa shujaa ufe masikini ila uzikwe kwa heshima na ukumbukwe milele au uwe mwoga, uwe tajiri wa rushwa ila uzikwe kama mbwa! Mwana JF ni wakati wa kuchagua!