Mazishi ya Mh. Regia Mtema huko Ifakara (updates)

Mazishi ya Mh. Regia Mtema huko Ifakara (updates)

Kwa sababu wafu hawajui lolote hivyo hawezi kona wala kusikia kwa maana kuwa file la maisha yake hapa duniani limeisha fungwa. La msing siye wafu watarajiwa tutengeneze njia zetu na kusafisha mapito ya Bwana.

Ulishakua mfu mkuu?
 
......Kweli tuliumbwa na udongo na mavumbini tutarudi, hii ni safari ya kila mmoja wetu. Kila nafsi itaonja umauti......Regia hatimaye umepumzishwa kwenye nyumba yako ya milele. Maisha haya ni mafupi na inabidi tutumie muda wetu uliobaki vizuri.
 
R.I.P ndugu yangu Regia...........Mungu akutangulie. Mama yetu Josephine (Omukama akubele) i mean Mungu akubariki.......kwa njia moja au nyingine nimeshiriki mazishi.
 
Hakika tumemaliza.

Salamu za shukrani kutoka kwa familia.

Nawashukuru nyote mlionipa ushirikiano nilipokuwa na post kwa uchache sana.Asanteni kwa kunisahihisha pale nilipokosea.

Tutaendelea kuwa pamoja.

Regia alisema,JF ni shule na pia ni numbani,ni kweli haijawahi kupita siku bila kungulia JF.

ASANTENI SANA.

Aksante sana Josephine.
Tunashukuru kwa kazi nzuri uliyofanya ya kutushirikisha sisi katika shughuli nzima ya kumuaga kipenzi chetu lady RM.
Tunawaombea wote safari njema ya kurudi katika maeneo yenu.
Mwenyezi Mungu awalinde na azidi kuwapa nguvu hasa katika kipindi hiki kigumu.

Regia ametutoka. Ama kwa hakika amepumzika katika usingizi wa amani.
Tunachotakiwa ni kuyaenzi yale yote ambayo Regia aliyasimamia na kuyasisitiza ambayo pengine leo ndio tunagundua hasa umuhimu wake.

Pamoja na sifa zake zote, bado ninaamini kuwa Regia alikuwa na KITU KINGINE cha ziada ambacho pengine Mwenyezi Mungu pekee ndiye anayejua.
Hii imedhihirishwa na jinsi mamilioni ya watanzania kutoka maeneo tofauti, rika tofauti, dini tofauti na itikadi tofauti walivyoguswa kwa dhati na kuondokewa na huyu mpendwa wetu.

Tunaomba Mwenyezi Mungu ailaze mahala pema roho ya marehemu mpendwa wetu Regia Doto Estelatus Mtemanyange. AMINA.

:hand:
 
Hakika imekwisha, safari yake hapa duniani imefika mwisho, pamoja na udogo wa umri wake lkn amefanya makubwa
kwa taifa letu, imedhihirika kutokana na jinsi watu walivyo guswa na habari za kifo chake,je sisi tumefanya nini kwa
taifa letu? tuamke sasa, tuache usingizi tupambane kwa manufaa ya nchi yetu. dunia yote mabadiriko huletwa na
vijana,tupiganie nchi yetu bila woga! tumuenzi mpendwa wetu kwa kuendeleza mapambano aloanzisha.
R.I.P Regia.
Tutakukumbuka daima.
 
Pole sana Mkuu Aspirin. Mungu akujalie upone haraka.
Kwa nini usitafute Avatar nyingine ya kutumia? nadhani sio busara kuanza kuitumia picha ya Regia sasa hivi kama Avatar yako, wacha muda upite kidogo then it will fine to use it.
 
Dada Josephine,

..asante kwa kazi kubwa uliyoifanya.

..kama alivyopendekeza mchangiaji mmoja CDM mkiangalie hiki kitengo chenu cha habari.

..kitengo cha habari kinashindwa kwenda na wakati ukizingatia kwamba wanachama na wapenzi wenu wengi ni vijana wa kileo.
 
Unamtaniaje mtu ambaye hayupo duniani?
Ningekushauri unapotaka kufanya Argument na mimi hakikisha unajiandaa kwa hoja zenye mashiko, kila msiba kuna wanaolia na kuna wanaoliwaza na kuna watani kupunguza stress na tension ya msiba, kama umeguswa sana nilitegemea uwe Morogoro kwenye mazishi.
 
R.I.P Mpendwa wetu Regia
Huu msiba umetoa mafundisho mengi hasa kwa wale watu wenye kupenda kuwabeza wenzao hata pasina sababu.
Tujifunze kuwathamini wenzetu hasa wakiwa hai.

Wana JF, TUAZIMIE KUWA MORE APPRECIATIVE FROM NOW ON!
" Kind words shouldn't be saved for funerals."
BR
 
Rais wa Wabeba Mabox Nyani Ngabu, yuko wapi Raia wako anaeitwa Kiranga? sijaona condolence yake kwenye msiba huu!!
 
Nakulilia mdogo wangu na rafiki yangu Regia. Niko kitandani hapa nakabiliana na maradhi (kama ulivyokuwa unajua). Nimefuatilia yaliyokuwa yanajiri tangu kifo chako kwa majonzi sana. Nimesikitika sana lakini nimefarijika kwa kuwa moyo wangu umeniambia umelala mahali pema. Nauamini moyo wangu ndio maana naamini iko siku moja tutaonana tena. Kwaheri mjukuu wangu, kwaheri rafiki yangu kwaheri Regia wangu. Upumzike kwa amani mama.

Pole rafiki. Bwana akutie nguvu, na nakutakia afya njema rafiki. Bwana akuponye, nimekumiss rafiki!
 
Mkuu Pasco.

Hivi Gaddaf aliangwa kwa siku ngapi vile ?.Tuache watu watoe heshima za mwisho bila kuingiza Itikadi za dini.

Hlafu ikizingatiwa wale walioga Dar es salaam sio wana ifakara.Nadhani ungewanyima haki yao watu wake wa nyumbani.wewe pasco ndo hukupaswa kuaga tena ungewaachia wengine kwani huwa kuaga hakulazimishwi.
 
Rais wa Wabeba Mabox Nyani Ngabu, yuko wapi Raia wako anaeitwa Kiranga? sijaona condolence yake kwenye msiba huu!!

Matola,

..katika ile thread ya kwanza ya taarifa ya msiba huu Kiranga alitoa rambirambi zake.

..kwa mtizamo wangu Kiranga always expected the best frm Regia[r.i.p] na ndiyo maana mkaona mara kwa mara alikuwa akimbebea bango.
 
Tunashukuru sana mama yetu Josephine kwa updates zote,umetufanya tujisikie kama nasi tumehudhuria msiba.tunamuombea dada regia apumzike kwa amani!
 
Hatimaye yametimia! Huzuni zetu zisitufanye kusahau kumshukuru na kumsifu Mungu kwa kutuletea Regia duniani! Kupitia dada Regia Mungu ameonyesha upendo wake na jinsi tunavyopaswa kuishi kwa kujitoa kwaajili ya wengine! Mungu ni mwema sana na daima anatuletea mifano hai ili tujifunze kuwa inawezekana! Turudishe sifa kwa Mungu kwa upendo wake kupitia dada yetu Regia Mtema! Hakika Acha Mungu aitwe Mungu! Asante dada Regia kwa kuitii dhamira njema ya Mungu kujitoa kwaajili ya wengine na hakika safari yako ya Wokovu imetimia!!

AMEN, kweli kupitia maisha ya Regia tumeuona upendo wa Mungu kwa mema yote aliyotenda kwa wengine,ujasiri wa kimungu na nguvu ya Mungu. Tumejifunza mengi kutoka kwake na tunamshukuru Mungu kwa maisha yake pamoja nasi.

Nuru yako ing'ae katika maisha yetu Regia,tuchukue yaliyo mema kutoka kwako na kutii dhamira njema ya Mungu katika maisha!!
 
everything that God does, do for a reason.... we loved our hero Regia Mtema but Our God the All-Mighty has a reason to take her off at her age... He Who created hasa just harvested at his planned time... M ay Regia's Soul Rest In Eternal Peace 4 ever... Aaaamen.
 
Vimvua vya furaha kuonyesha kua hata mbingu imefurahia kurejea kwa dada yetu Regia Mtema huko mbinguni,baada ya wajibu wake na mazuri yete aliyoifanyia Tanzania!Morogoro ilikupenda sana dada,Tanzania ilikupenda pia,kapumzike kwa amani Reggy
 
Back
Top Bottom