Mazishi ya Mh. Regia Mtema huko Ifakara (updates)

Mazishi ya Mh. Regia Mtema huko Ifakara (updates)

WanaJF
nimesikia concern zenuzenu. Tunaomba radhi kwa usumbufu. Nimekwenda mwenyewe kwa wenye mitambo na nimekuta wakihangaika na network. Tunatambua umuhimu wa kuwajuza kinachojiri. Tutaendelea kuboresha mitambo. Nashukuru baada ya picha zimeanza ku postiwa. Tunawashukuru wana JF na wapenzi wote wa Regia kwa ushiriki wa kina kumsindikiza mpendwa wetu.

.
Ee bana ee, kumbe rais wa mioyo ya watanzania yupo mitaa hii? Saafi sana.
RIP bint Abraham, Regie!
.
 
Huyu binti kweli ana nyota, viongozi wengine hebu jifunzeni kupitia huu msiba, Jiulizeni hivi mkiondoka kama alivyoondoka Regia mtafanyiwa haya kama yanavyofanyika kwa Regia?

Josephine, Pasco, Edson na wengine hongereni kwa kutujulisha kila kinachoendelea huko, kila la heri nyote!
 
Thats life na hiyo iko kila mahali!. Ila kwa sisi tuliokuja kuzika, ukiondoa wale ambao ilibidi waje ama kwa nyadhifa zao au kwa kuwajibika sehemu zao, wengi wa tuliokuja huku Ifakara, tumekuja kwa mapenzi yetu kwa Regia!. Wengine kama mimi sio CCM sio Chadema, sio ndugu, sio rafiki wala hatuna uhusiano wowote na Regia ila tumekuja kwa sababu Regia ni mwanachama mwenzetu wa jf! tumekuja tuu kwa sababu tumeguswa!.

Safi sana kaka, we really appreciate kwa moyo wenu wa upendo kutuwakilisha. Mungu awabariki sana, hata kushinda kwenu njaa pia ni sadaka njema, inshallah mwenyezi Mungu atawazidishia mema yake.
 
Poleni sana. Tuko pamoja in spirit. Asante kwa kutuwakilisha First Lady wangu.
 
Tunashukuru kwa kutujuza, yaani sipati picha mpo katika hali gani. Mimi leo nimeona nisiende kabisa kwa ofisi maana najua hali ingekuwa mbaya sana........................
 
Huyu binti kweli ana nyota, viongozi wengine hebu jifunzeni kupitia huu msiba, Jiulizeni hivi mkiondoka kama alivyoondoka Regia mtafanyiwa haya kama yanavyofanyika kwa Regia?

Josephine, Pasco, Edson na wengine hongereni kwa kutujulisha kila kinachoendelea huko, kila la heri nyote!

The ordinary people loved her.
She seemed to understand and liked them.
She was simply a woman of the people
 
Naoana haitambui nafasi yake kama First lady kivuli (according to ritz). Huwezi kuwa msibani ukawa muda wote unabrowse! kwa nafasi yake anatakiwa awaachie vijakazi kama wewe ufanye kazi ya kutuhabarisha!
Tatizo ni nini hasa. Kaweza. Hutaki kumsoma unaacha.
 
WanaJF
nimesikia concern zenuzenu. Tunaomba radhi kwa usumbufu. Nimekwenda mwenyewe kwa wenye mitambo na nimekuta wakihangaika na network. Tunatambua umuhimu wa kuwajuza kinachojiri. Tutaendelea kuboresha mitambo. Nashukuru baada ya picha zimeanza ku postiwa. Tunawashukuru wana JF na wapenzi wote wa Regia kwa ushiriki wa kina kumsindikiza mpendwa wetu.

asante sana Dr, kwa kujali na kuwa msikivu. Mambo haya wala hayahitaji kutembea na warehouse, ni laptop tu yenye uwezo mzuri na kamera, bila kusahau mtu makini na mwenye mapenzi na kazi ya habari. Hu umekuwa wimbo kama si kilio cha muda mrefu kuhusu idara ya hbr ya CDM. Mbona ni kitu kdg tu, hata mimi niliyesoma shahada ya wanyamapori nafanya.
 
Bila shaka kamanda Regia ameonyesha na kufungua njia kwa wanamorogoro, hasa kwa huo ukanda wa kusini Kilombero-Ulanga.

Natarajia huko mbele ya safari mkoa wa morogoro utakuwa mbele katika kuchagua mabadiliko ya kweli na ya kujiletea maendeleo.

Kamanda Regia ama kwa hakika amewaunganisha wana moro na watanzania wote katika kipindi hiki kifupi.

Nakubaliana nanyi kabisa,Moja ya appreciation ya dada Reggy ni kua alikua chachu ya kuwaamsha WaTz juu ya haki zao na fursa zilizowazunguka,na kwa kweli kwa kiasi kikubwa amefanikiwa ilo,kilombero imeamka sasa!sehemu nyingine za Moro zinafuata!mkuu Mkeshaji ile ilikua joke,najua wewe ni mwana Kilombero damu,ndio maana ume react faster!tupambane kuwaamsha wana Moro wote
 
attachment.php
Asanteni kwa kuja. Mrisho Mpoto - Ahsanteni Kwa Kuja RIP dada Regia.
 
Vipi maziko bado mpaka saa hizi huko Tanzania. 1517 Hrs
 
Eee mungu tunakuomba umpumzishe mja wako,mpendwa wetu,dada yetu Regia kwa aman,AMINA.
 
Niko hapa wami tumekwama, nafuatilia matukio ya msiba! Magari yamepangana foleni karb inafika chalinze. Du!
 
Back
Top Bottom