Mazishi ya Mh. Regia Mtema huko Ifakara (updates)

Mazishi ya Mh. Regia Mtema huko Ifakara (updates)

Ewe Mungu mwenye rehema, utujalie na sisi ujasiri wa kufanya yale ambayo Regia ameyafanya katika kipindi kifupi cha maisha yake.
 
Regia siwezi siwezi mama kuendelea kuona watu wako wakibubujikwa machozi.
Nasikia mengi wanayokusema.
Sasa tunakuona uso wako kwa mara ya mwisho,imebaki historia.
Watu wanajipanga kutoa salamu za mwisho,mvua inanyesha kidogo.
Please open you eyes just foa minute Regia.

Nakulilia mama,niliumia hivi siku baba yangu mzazi aliponitoka.
Noooooo!
Pole sana Dada!
Lila Josephine lia! Kilio kinapunguza maumivu kuliko kugugumia.
Maandiko ya Mungu yametimia. "Sote tumetoka kwake na kwake tutarejea".
Dada yetu Regia ametangulia nasi tuko nyuma yake.
Inauma lakini ndio ukweli, kuwa kifo chake kimetuunganisha zaidi na kutufanya tulio hai bado tutafakari thamani ya maisha na wajibu wetu katika maisha. Marehemu Regia aliyatimiza yote mawili na ametuwachia mafundisho makubwa kwa anayetaka kujifunza, kuwa "Mtu hathaminiwi kwa alichonacho bali kwa alivyo".
Mungu Amlaze Mahali Pema - Amen!
 
Picha hiyo ya 3 imeniweka kwenye hali mbaya kwa muda fulani!
RIP REGIA!
 
LEO

attachment.php

Naibu spika Ndugai anatafakari, anasikitika ama ameuchapa?
 
Jamani wanaJF,
Josephine anaelekea kuziba pengo la marehemu Regia angalau katika shughuli hii nzito na ya huzuni kubwa. Namwomba aendelee na moyo huu mkuu.

Hv First lady na dada Regia walikua close friends sana??hii kitu nime sense,japo siko that sure!Ifakara imejaa,shughuli zimesimama,siku ya leo ni ya kipekee kwa moro,hata hali ya hewa imejua ilo,na mbingu zimepoa kwa ajili ya kumkaribisha kamanda,kiongozi,mzalendo,mtu wa watu dada Regia E Mtema!tangulia dada,nasi tunakuja
 
Pole sana Dada!
Lila Josephine lia! Kilio kinapunguza maumivu kuliko kugugumia.
Maandiko ya Mungu yametimia. "Sote tumetoka kwake na kwake tutarejea".
Dada yetu Regia ametangulia nasi tuko nyuma yake.
Inauma lakini ndio ukweli, kuwa kifo chake kimetuunganisha zaidi na kutufanya tulio hai bado tutafakari thamani ya maisha na wajibu wetu katika maisha. Marehemu Regia aliyatimiza yote mawili na ametuwachia mafundisho makubwa kwa anayetaka kujifunza, kuwa "Mtu hathaminiwi kwa alichonacho bali kwa alivyo".
Mungu Amlaze Mahali Pema - Amen!

Uko sahihi kabisa mkuu
 
Dah sasa itabaki historia.
Mama Josephine unakila dalili za kuliziba pengo hili la Regia umejitahidi sana kutupa updates
Tunashukuru sana umeshindwa kujizua na kutupa sisi wa TZ tulio mbali nini kinacho jili Ifakara.
Ahsante sana Josephine
 
Vipi mwakilishi wa Papa Balozi wa Vatican yupo huko?
Na vipi salam toka kwa mwakilishi wa CDU ?

Mwakilishi wa papa si askofu ila sijasikia mwakilishia wa BAKWATA sijui Sheikh ametuma nani mwakilishi
 
JK tayari yuko makaburini anasubiri kuupokea mwili na kuwaongoza umati wa Watanzania katika maziko!.

Pasco,

Mkuu wa kaya hakwenda uwanjani ameamua kutangulia makaburini? ama shughuli zimeshakwisha uwanjani na safari ya makaburini ndiyo imeanza?
 
Regia siwezi siwezi mama kuendelea kuona watu wako wakibubujikwa machozi.

Nasikia mengi wanayokusema.

Sasa tunakuona uso wako kwa mara ya mwisho,imebaki historia.

Watu wanajipanga kutoa salamu za mwisho,mvua inanyesha kidogo.

Please open you eyes just foa minute Regia.

Nakulilia mama,niliumia hivi siku baba yangu mzazi aliponitoka.

Noooooo!

Mama yetu umeonyesha uchungu wa moyoni na kudhihirsha kuwa women have two brains-can handle multi duties than men. Unasononeka but still unatujuza kile kinachoendelea hapo sehemu ya tukio. Inadhihirisha Dr.hakufanya makosa kwa kukuchagua kuwa mwenzi ili muweke bongo zenu pamoja kwa ajili ya Tanzania ya kesho. Dada Regia amekuwa ana unabii.

Musa alikufa kabla hajaingia nchi ya ahadi mbali na kuongoza Taifa la Mungu. Papa Yohana wa XXII aliyeongoza Mtaguso wa Pili ulioleta mabadiliko katika Kanisa Katholiki naye alikufa akiwa anaelekea kuhitimisha mkutano. Mchago wa Regia ndani ya CDM na Taifa kwa ujumla ni mbegu ilipondwa kwenye udongo mzuri. Tutaipalili na kuimwagilia ili matunda tuvune sisi, watoto , wajukuu na vijukuu.

Mungu Ibariki CDM.

Raha ya milele umpe ee Bwana na mwanga wa milele umwangazie Regia. Apumzike kwa amani.Amina
 
Rest in piace our sister! We will rember you forever.
 
Kwli JF tumepata pigo, naona inakuwa ngumu kupata picha hapa, ingekuwa enzi zaRegia hapa, kungekuwa sambamba kabisa na matukio muhimu.
Jitahidini wanaharakati mliobaki, inameni okoteni silaha ya regia, mojawapo ni media/JF, endeleeni na mapambano, jeshi kubwa liko nyuma yenu.

Okoteni silaha kabla adui hajaiwahi
 
Umati wa waombolezaji unapita kwenye heshima za mwisho.
Jamani Wakristo wenzangu, lazima tufike mahali tukubali tukatae, wenzetu Waislamu wametuzidi kidogo katika ustaarabu wa taratibu za heshima za mwisho kwa kuaga bila kuangalia mwili!.

Just imagine Ile Jumatatu ameagwa kwa kuangaliwa pale nyumbani Tabata. Baadae ameagwa kwa kuangaliwa pale kanisani kwenye misa!. Jana tumemuaga kwa kumwangalia pale Karimjee!. Leo pia ameagwa tena kwa kuangaliwa hapa Ifakara!.

My own opinion, its more than enough, baada ya kuagwa na familia kwa kumwangalia, the rest wangepita tuu mbele ya jeneza kwa heshima na mwisho huku wakiangalia ile picha ya smiling innocent baby face yake ndio ikabaki kama kumbukumbu yetu ya mwisho ya Regia!.

Sasa imetosha na kupitiliza, tumpumzishe shujaa wetu apumzike kwa amani!.

Pumzika Regia!.
 
Back
Top Bottom