Dah!......
Hakika wema hawaishi maisha marefu....
Yaani kila nikitaka kuandika nazidi kuumia tu.....
Upumzike kwa amani mpendwa wetu Regia Dotto Mtema...
Watanzania tunakulilia,wana Morogoro wanakulilia,wana Kilombero wanakulilia,CHADEMA wanakulilia, CCM wanakulilia, CUF wanakulilia, NCCR-Mageuzi wanakulilia, UDP wanakulilia, Vijana watakulilia,wazee watakulilia, JF inakulilia............Nami daima nitakulilia Regia.......Upumzike kwa amani Regia.....
Daraja liliounganisha watanzania,wana Morogoro, wana Kilombero.....Daraja liliounganisha CHADEMA na vyama vingine,daraja liliounganisha vijana,daraja liliounganisha JF na Bunge,JF na siasa nk limevunjika wakati bado likiendelea kuhitajika kuwa kiunganishi katika safari ya Tanzania.......Upumzike kwa amani Regia....
Daima nitakulilia Regia........Upumzike kwa amani Regia....
Raha ya milele umpe mpendwa wetu Regia ee bwana na Mwanga wa milele umuangazie apumzike kwa amani......Amina...
Inauma sana yaani......