Mazishi ya Mh. Regia Mtema huko Ifakara (updates)

Mazishi ya Mh. Regia Mtema huko Ifakara (updates)

R.I.P. Regia.
Hakika ametutoka kipenzi chetu na kamanda kijana kabisa, ila wa Jf nawaomba ktk kipindi hiki kigum tuzidi kuiombea roho yake ipumzike kwa amani kwani alichomwagiza Mola wake kukifanya chini ya jua tayari amekimaliza na kwa ushindi mkubwa ndio maana utaona ktk mazishi yake amesindikizwa na kila aina ya watu masikini kwa matajiri, na hivyo ndivyo Mungu anapenda tuishi.
La mwisho wana Jf wenzangu tuombe na tutafakuri vizuri na Mungu atuongoze ili tupate kamanda mwingine atakaeweza kuvaa viatu vya Regia......... R.I.P. Regia
 
Mkuu Barubaru.

Asante nimekupata barabara.


Ngongo.

Wakti nipo Tanganyika hususan Dar na mwanza, bukoba . Kulikuwa na kitu kinachoitwa utani wa makabila. Na utani huu unashamiri sana pale watu wanapokuwa msibani au kwenye matanga. Utashangaa mnaweza mkawa mnalia na wengine wanakuja na ngoma na kuanza kucheza. (Sina hakika kama siku hizi kuna watani)

mara ya mwisho niliona pale Upanga mtaa wa mazengo kwa jirani yangu Ditopile. watani walikuja juu sana wakti wa mazishi yake mpaka wakapewa pesa. Nakumbuka pesa za utani wa wasukuma alichukua Endrew Chenge na ilikuwa ni shilingi 200 za tanzania.

Hayo yote ni matani. Lakin yakiwa na nia ya kuboresha. haiwezekani watu wate muwe serious lazima pawe na mas'khara kidogo kupunguza tension.

Samahani kama nilikuwa nimekukwaza. Lakin kwangu ilikuwa ni joke tu.

Tusimame pamoja kumuombea Regia apokewe kwa amani huko Kwa Muumba.

Pole sana.

 
Kwa heshima na kumbukumbu ya kudumu kwa Regia, CDM wafikirie kuanzisha kitu kwa jina lake.
Napendekeza ianzishwe Taasisi ya Uongozi ya Vijana ya Regia Mtema (Regia Mtema Youth Leadership Institute) au Wakfu wa Maendeleo ya Regia Mtema (Regia Mtema Development Foundation). Supporters and Wellwishers wa CDM wachangie hata elfu moja kila mwaka.
Hilo ni wazo zuri saana Mkuu italeta changa moto na kumbu kumbu nzuri kwa wapambanaji!!!!!!!!!! R.I.P. dada Regia!!!!!!!!!!

 
Hapa namuona Arfi hana suti Nyeusi, naamini hata Abdalla safari kaja na Kanzu. ZItto yeye jina tu, kapata elimu yake CDU , hajui nini atendalo
Kumbe hata Ghalib Bilal nae hajui atendalo!! kazi kweli kweli kweli, umaamuma ni mzigo mzito mzito.
JANA%2B3.jpg
 
R.I.P. Regia.
Hakika ametutoka kipenzi chetu na kamanda kijana kabisa, ila wa Jf nawaomba ktk kipindi hiki kigum tuzidi kuiombea roho yake ipumzike kwa amani kwani alichomwagiza Mola wake kukifanya chini ya jua tayari amekimaliza na kwa ushindi mkubwa ndio maana utaona ktk mazishi yake amesindikizwa na kila aina ya watu masikini kwa matajiri, na hivyo ndivyo Mungu anapenda tuishi.
La mwisho wana Jf wenzangu tuombe na tutafakuri vizuri na Mungu atuongoze ili tupate kamanda mwingine atakaeweza kuvaa viatu vya Regia......... R.I.P. Regia

sent by: Mchuma SM
 
Buriani Regia.

Tunaweza kutofautiana itikadi na misimamo mbalimbali ila nilimpenda Regia kwa sababu
- alikuwa jasiri
- alikuwa hodari
- alikuwa honest
- alikuwa mchapakazi
- alikuwa na upendo.

Ameonyesha wanawake na mabinti kuwa unaweza kufanya lolote kama ukiamua. Sina uhakika ni nani wa umri wake waliweza kuthubutu kugombea ubunge jimboni kama yeye. Hata wazee wengi kinamama hawathubutu.

Msilie. Regia hawasikii. Ukifariki kitabu chako kinafungwa unaenda unapostahili - Mbinguni kama ulikufa ukiwa hauna dhambi au jehanamu kama ni tofauti. Ndiyo maana misiba inatukumbusha kuweka sawa maisha yetu.

Its so so so sad.

Poleni wote.
 
ndugu umezoea kudharau na kukejeli ? kwa mawazo yangu sijaona dharau bali ni katika kukumbushana kibinadamu. Ajali zinaepukika.

Pumzika kwa amani Rejia. Pumzika Dotto. Ulotumwa kuyafanya pengine ulishayakamilisha. Kazi kwetu tuliobaki

Mwana FA,

Bahati mbaya sana umedandia treni kwa mbele, ungefuatilia kwa makini ungefahamu alichoandika Ngongo na kujua tumetoka wapi na huyu barubaru.
 
Pole sana kiongozi wangu, unajua wakati mwingine tunajikuta tunataja vitu hivyo bila kutarajia.

mkuu hata kuandika nako unatumia sihasa? hahahaha, bandiko lile ulikusudia kabisa kuyaandika yale maneno, siwezi kuyarudia manake dah! aaaaagh! siku hizi mshahara unaisha kwa matumizi kabla ya kuchukua, loh! haya bana, kidogo nimefarijika baada ya mwili wa dada yetu regia ulioharibika kurudi mavumbini ili ukavae ule wakutokuharibika. sasa tugange yajayo, kesho natuma hela kijijini dogo akalipe ada ya NECTA 4m 4, hivi imerudishwa kimya kimya? loh! sorry kwakuingia nje ya mada.
 
Nakulilia mdogo wangu na rafiki yangu Regia. Niko kitandani hapa nakabiliana na maradhi (kama ulivyokuwa unajua). Nimefuatilia yaliyokuwa yanajiri tangu kifo chako kwa majonzi sana. Nimesikitika sana lakini nimefarijika kwa kuwa moyo wangu umeniambia umelala mahali pema. Nauamini moyo wangu ndio maana naamini iko siku moja tutaonana tena. Kwaheri mjukuu wangu, kwaheri rafiki yangu kwaheri Regia wangu. Upumzike kwa amani mama.
 
Nashukuru kwa wote waliotuletea updates na kufanya kujua yale yaliyotokea arusi ya mwisho ya mpendwa wetu. Mungu wabariki sana.
 
Kwako shujaa wetu Regia, ulipigana kwa nguvu zote dhidi ya dhuluma, ulishinda kwa kishindo, pokea sasa tuzo lako Mbinguni!! Leo tunakuaga, leo tunakulilia mara ya mwisho, lakini mawazo na matendo yako yatadumu daima mioyoni mwetu! Mbele ya maelfu haya ya watu wanaohudhuria mazishi yako, leo umetuinua sana Chadema Kilombero, Chadema Ulanga, Chadema Morogoro na Chadema taifa. Safari yako ya mbinguni imeacha faraja sana kwetu kwani leo Chadema inatajwa na kila mtu hapa Ifakara kupitia jina lako. Tunaamini kuwa utaendelea kuwa nasi katika mapambano ya ukombozi wa wananchi maskini mpAka ushindi upatikane. Zidumu fikra zako!Basi enenda kwa amani shujaa wetu, enenda kwa amani mpiganaji wetu, enenda kwa amani binti yetu Regia Mtema.Mungu akujalia maisha mema mbinguni! AMINA!
 
Jamani Wakristo wenzangu, lazima tufike mahali tukubali tukatae, wenzetu Waislamu wametuzidi kidogo katika ustaarabu wa taratibu za heshima za mwisho kwa kuaga bila kuangalia mwili!.

Just imagine Ile Jumatatu ameagwa kwa kuangaliwa pale nyumbani Tabata. Baadae ameagwa kwa kuangaliwa pale kanisani kwenye misa!. Jana tumemuaga kwa kumwangalia pale Karimjee!. Leo pia ameagwa tena kwa kuangaliwa hapa Ifakara!.

My own opinion, its more than enough, baada ya kuagwa na familia kwa kumwangalia, the rest wangepita tuu mbele ya jeneza kwa heshima na mwisho huku wakiangalia ile picha ya smiling innocent baby face yake ndio ikabaki kama kumbukumbu yetu ya mwisho ya Regia!.

Sasa imetosha na kupitiliza, tumpumzishe shujaa wetu apumzike kwa amani!.

Pumzika Regia!.
Kwa taarifa yako Ifakara ndiyo wana haki ya kumuaga kuliko wewe ni wapiga kura wake....
 
Shukrani sana mama Josephine kwa kazi nzito uliyo ifanya
 
Mkuu Josephine,

Hakika nikiwa ofisini nilisitisha shughuli zangu zote na kufatilia maziko ya mpendwa wetu Regia Mtema. Umeonyesha ni kwa kiasi gani unavyojitolea katika jamii na kujishusha kwa kutupatia updates ambazo mnacho kitengo ndani ya Chadema cha kufanya uliyoyafanya.

Btw, nakushukuru, nakupongeza na udumu katika kuwa karibu na wananchi kama hivi. Pole sana kwa machungu ya kufiwa kwa ukaribu uliokuwa nao na marehemu. Sisi waislamu hunena 'INNALILLAHI WAINAILAIH RAJIUN'.
You deserve to be WHO you are !!!
 
HATIMAYE HATUNA REGIA TENA! Mungu utupe nguvu maana watu wako tumekata tamaa. RIP my beloved sister!
 
mkuu hata kuandika nako unatumia sihasa? hahahaha, bandiko lile ulikusudia kabisa kuyaandika yale maneno, siwezi kuyarudia manake dah! aaaaagh! siku hizi mshahara unaisha kwa matumizi kabla ya kuchukua, loh! haya bana, kidogo nimefarijika baada ya mwili wa dada yetu regia ulioharibika kurudi mavumbini ili ukavae ule wakutokuharibika. sasa tugange yajayo, kesho natuma hela kijijini dogo akalipe ada ya NECTA 4m 4, hivi imerudishwa kimya kimya? loh! sorry kwakuingia nje ya mada.

Nimekusoma Zumbe wa Muheza,

Kama unavyojua jukwaa lenyewe la siasa full stress, mpendwa wetu tunayemuaga naye alikuwa mwanasiasa kwahiyo utaona mgongano wa mawazo unapoanzia, ningekuwa MMU ningekuruhusu kunishangaa, nadhani unanielewa.

Hilo la ada ya mitihani ya NECTA inawezekana wameirudisha, kama wamerudisha mitihani ya kidato cha pili na kutangaza ada yake ambayo walezi na wazazi tutalazimika kuilipia, sitoshangaa kusikia kwamba hata hiyo ya form four wameirudisha.
 
Umenikumbusha mbali sana - Gender Sensitive!

Yeah, alikuwa shupavu sana kwenye kujenga hoja hata baadhi wa JF members wakataka kujua jinsia yake, wengi walidhani ni mwanaume. Enzi hizo majority ya JF members walikuwa wanaume, basi mwanamke hodari ataambiwa ni mwanaume au ni pseudonym ya Mwanafrika wa Kike.

Rest in Peace Gender Sensitive.
 
Back
Top Bottom