Mazishi ya Mh. Regia Mtema huko Ifakara (updates)

I can imagine what your going through my dear.
Binafsi sikuwahi kumuona Rejia uso kwa uso ila uwepo wake hapa Jf ulinifanya nijione kama ni ndugu tunayefahamiana kwa karibu. Kila nikifungua Jf najikuta nalia uncontrollably! Sasa wewe uliyekuwa naye karibu naweza kupata picha how hard it is! Mungu akupe nguvu yakuendelea mbele mama.
RIP - Regia!
Regia tunakusindikiza kwa mara ya mwisho leo,
moyoni nabubujikwa machozi,kumbuka mama yale tuliyozungumza na kuyawekea mikakati.

Regia nani atanisaidia kuyasimamia yale tuliyoyaongea,nisaidie mama,nitafanya,lakini wewe ndiye yalikuwa maono yako,nisaidie huko uliko.

Dr anakulilia,watoto wangu nyumbani wanakulilia,hata dada aliyekuwa anakuhudumia anakulilia.

Tulikupenda.
 
Wewe ndiye unayejua Regia alishindwa lakini mimi najua Regia alishinda na ITV na Radio One zilimtangaza mshindi lakini kwa msaada wa tume wa ya kishetani alishindwa!!!!

Kuhusu kalifanyia nini taifa naomba umuulize boss wako JK kilichomtoa ara mbili Magogoni na kwenda Tabata na hatimaye Ifakara ni nini? Huyo ndiyo atakupa mchango wake.

Yani kama kazi yake hujaiyona hata ukiambiwa ni bure.
 
This is so hard for me. Especially with the pictures. A picture is more than a thousand words, and these photos speak volumes of the love people had for Regia.

Yaani nilikuwa na shauku sana ya kuona Regia ataendeleaje. Ingawa tulikuwa marafiki wa JF (kati ya watu wachache walio katika kurasa yangu ya JF kama marafiki) sitaki kuwa mnafiki na kusema nilikuwa rafiki yake mkubwa, sikuwa. Lakini nilifikiri, kwa dhati ya moyo wangu wote uliojaa ubishi na maswali ya kila aina, nikifikiri kwamba, kwa ubishi na maswali yangu, nilikuwa nachangia sio tu kumjenga yeye, bali kujijenga mie mwenyewe kimawazo kwa kuhoji umakini wa uongozi wa kisiasa wa Tanzania. Hata kama ilikuwa ni kwa malumbano ya hoja nzito yaliyopelekea saa nyingine kuonekana kama twajenga uhasimu, hususan kwa wale ambao hawakuelewa kwamba "you can't make an omelette without breaking an egg".

"Gender Sensitive" alipotangaza nia ya kugombea ubunge, wakati karibu wote hapa walipofurahia na kushangilia, wengi bila hata kujua huyu "Gender Sensitive" ni nani, mie nikakataa kuunga tela la kushangilia. Nikalazimisha tumjue huyu anayetaka kugombea ubunge jina lake ni nani na anagombea jimbo gani. Maaana kuna wengine wangetaka kuchangia michango ya hali na mali, lakini wasingejua wachangie wapi. Wengine wangeweza kuona huyu "mtoto" anatutania tu.

Akakubaliana na maoni yangu. Akajitangaza rasmi. Kuanzia hapo ukaanza uhusiano kama wa mtu anayeona kila kinachofanywa sawa kuwa ni "wajibu wake" na "ana wafuasi wa kumsifu wa kutosha". Lakini kila alipokosea - au nilipofikiri alikosea- asingeweza kusema tumemdekeza hata siku moja.

Nafikiri hatujawa na mbunge ambaye ameonyesha ushirikiano wa kutoa mawasiliano, hususan hapa bodini, kama Regia. Hilo tu latosha. Lakini sishangai sana, kwani alikuwa mwanachama wa JF kabla hajawa mbunge, na kama nilivyosema hapo juu, hata sehemu ya kampeni mwanzo kaanzia hapa. Kwa hiyo ningeshangaa kama asingerudi kutoa ripoti hapa.

Nashukuru kumjua, kujua kwamba alikuwa anajifunza mengi.

Kiu yangu ya kujua Regia angeenda kukua vipi bungeni imekatazwa kunyweshwa maji ya kujua. Imekuwa kama ndoto iliyokatizwa na kuamka kabla ya kumalizika.

Ndoto nzuri iliyokatizwa na ukweli kwamba hatuna uhakika kama kesho tutaiona.

Kwa hili wote tunajifunza kutoka kwa Regia hususan katika waraka wake wa kuukaribisha mwaka mpya, kuwa wapole, kuishi na watu vizuri, kujiombea udhuru kwa wale tunaowakosea, kuheshimu tulipotoka, kutoogopa kusemwa vibaya, kutoogopa kusema tunachosimamia, kutoogopa kukubali tunapokosea, kusikiliza wengine wanasemaje na mengine mengi kama hayo.

Sintojua maendelezo ya waraka ule wa mwaka mpya tena. Ukatili wa kifo, kisicho huruma kama alivyosema Remmy Ongala, umehakikisha hilo.

Lakini nafarijika kuona maisha yake hayajaisha bila maana, kwani kasimama kidete kueleza alichoamini hata pale tulipoona kakosea, tulijua yuko wapi. Na katika wabunge walioweza kugusa wengi katika muda mfupi kabisa itakuwa vigumu kumpata wakumfananisha.

Sote tunakongoroka. Kumbuka hilo kila siku. Litakusaidia kuishi vyema zaidi na watu.

Kiranga.
 
Bado mnaendeleza porojo zisizo na mashiko!Tuambieni mchango wa Regia kitaifa ni upi? Wewe unasema jimbo lake wanajua, kwanza nataka ujue Regia alikuwa hawakilushi jimbo lolote, aligombea akashindwa jimbo la Kilombero, akapata ubunge wa viti maalum, no wonder alijokomba sana kwa Mbowe! Yale aliyoyaorodhesha hapa Mteketa mbunge wa sasa anasema ni kazi yake yeye kama mbunge wa Kirombero!
Ungefanya ufuatiliaji kidogo wa wazungumzaji kwenye msiba wa mpendwa wetu Regia ungeelewa kwa nafasi yake amefanya mengi tu katika taifa hili kwa muda mfupi sana wa UHAI wake:
-WM Pinda: Mh Mbowe mtaliziba pengo la Regia lakini sijui kama mtapata mtu kama yeye;
-Spika Makinda: Regia alikuwa mwelewa hata anapokuwa amekosea hakusita kuomba radhi;
-Rejea thread ya Zitto iko humu. Ina mengi tu kumhusu Regia.
-Mbowe: Tulimlea Regia awe KIONGOZI katika TAIFA hili.
Wamekufa WABUNGE wengi miaka ya hivi karibuni. Niambie msiba uliokaribia huu wa Regia kwa mvuto kuanzia VIONGOZI WAKUU wa NCHI hii hadi RAIA wa kawaida kabisa hapa Dar na kule Ifakara. Watu wote hawa kuna kitu walikiona na kukikubali kwa huyu binti mdogo kwa umri.
 
Usiandikie mate wakati wino upo, kuna yule mbunge wa Arumeru anaitwa Sumari amefariki usiku wa kuamkia leo ngoja uone kama atalihudhunisha Taifa zaidi ya mke wake na familia yake tu.
Regia ameligusa Taifa zima hakuna mwenye uwezo wa kubadili ukweli huu.
 
Wednesday, 18 January 2012 21:08
SLAA AMPIGA CHENGA JK MSIBANI IFAKARA

bye-regia.jpg
Askari wa Bunge wakiuingiza kaburini mwili wa aliyekuwa mbunge wa viti maalum (Chadema) Regia Mtema wakati wa mazishi yaliyofanyika kwenye makaburi ya Ipangalala Ifakara mkoani Morogoro jana.Picha na Juma Mtanda

AKWEPA KUKAA JUKWAA KUU, WENGI WAMZIKA REGIA
Juma Mtanda na Shakila Nyerere, Ifakara
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willbrod Slaa, jana alimkwepa tena Rais Jakaya Kikwete safari hii ikiwa katika mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu kwa tiketi ya chama hicho, Regia Mtema yaliyofanyika katika Kijiji cha Lipangalala.Tangu kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu wa 2010, ambao Dk Slaa alishika nafasi ya pili kwa kupata kura 2,271,941 sawa na asilimia 26.34 akiwa nyuma ya Rais Kikwete aliyepata kura 5,276,827 sawa na asilimia 61.17, Dk Slaa hakuwahi kukutana na mkuu huyo wa nchi ana kwa ana.

Katika hafla ya kutangazwa matokeo ya urais iliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), kwenye Ukumbi wa Karimjee, Dar es Salaam, Dk Slaa hakuhudhuria tofauti na ilivyokuwa kwa waliokuwa wagombea wenzake wote.

Jana, Dk Slaa tofauti na viongozi wenzake wa Chadema akiwemo Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, hakutaka kujiweka katika mazingira ambayo yangemkutanisha na Rais Kikwete katika mazishi hayo.
Nyumba kulikofanyika shughuli za awali za mazishi, waandalizi waliandaa majukwaa mawili, moja maalum kwa ajili ya wabunge huku jingine likiwa ni maalumu kwa ajili ya viongozi wakuu ambalo alikaa Mbowe, Spika wa Bunge, Anne Makinda, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe.

Mbali ya kukaa viongozi hao, kulikuwa na nafasi ambayo ilikuwa imetengwa maalumu kwa ajili ya Rais. Mbali ya nafasi hiyo, pia kulikuwa na kiti ambacho ilitegemewa kwamba Dk Slaa angekalia.
Hata hivyo, Katibu Mkuu huyo wa Chadema alikikwepa na kwenda kujichanganya katika jukwaa la wabunge na kiti hicho kubaki bila ya kuwa na mtu.

Hata hivyo, Rais Kikwete hakuweza kufika nyumbani hadi mwili wa marehemu Regia ulipopelekwa katika Viwanya vya Viungani ambako uliagwa na mamia ya waombolezaji.

Uwanjani hapo nako kulikuwa na majukwaa mawili. Kama ilivyokuwa nyumbani, jukwaa moja lilikuwa la wabunge na jingine la viongozi wa ngazi za juu lakini bado, Dk Slaa alilikwepa jukwaa hilo ambalo Rais alitarajiwa kuwa angefikia. Rais hakuweza kufika Viungani pia.

jk-udongo.jpg
Rais Jakaya Kikwete akiweka udongo kwenye kaburi la aliyekuwa mbunge wa viti maalum (Chadema) Regia Mtema wakati wa mazishi yaliyofanyika kwenye makaburi ya Ipangalala Ifakara mkoani Morogoro jana.Picha na Juma Mtanda

Baadaye wakiwa eneo la mazishi, Rais Kikwete alifika na kushiriki tukio hilo na kisha kusalimiana na wabunge mbalimbali na viongozi waliokuwa wamefika akiwemo Mbowe, Mbunge wa Rombo Joseph Selasini, Zitto na viongozi wengine lakini Dk Slaa hakuonekana.

Ilitegemewa kuwa tukio hilo la msiba lingewaleta wanasiasa hao lakini hadi Rais Kikwete alipoondoka hakuna mahali ambako walisalimiana.
Mbali ya tukio hilo, hata katika hafla mbalimbali ambazo viongozi wa Chadema wamekuwa wakialikwa ikiwemo Ikulu, Dk Slaa hakuwahi kuhudhuria.

Novemba mwaka jana viongozi wa Chadema wakiongozwa na Mbowe, walifanya mazungumzo na Rais Kikwete, Ikulu ya Dar es Salaam kujadili suala la Katiba Mpya, lakini Dk Slaa hakuhudhuria.

Chadema wahaha
Wakati viongozi wa Chadema wakihaha kumaliza mgogoro ndani ya chama hicho wilayani Kilombero, Pacha wa marehemu Regia, Remigia Mtema amesema ndugu yake Regia alikuwa akipeleka malalamiko kwa Dk Slaa mara kadhaa kuomba asuluhishe bila mafanikio.

Hata hivyo, Remigia alisema marehemu Regia alikuwa amepanga kuonana tena na Dk Slaa katika siku za hivi karibuni kumweleza kinachoendelea.

Akizungumzia suala hilo, Dk Slaa alisema alishaanza kushughulikia mgogoro huo lakini msiba huo ndiyo uliomkwamisha.

“Ni kweli nimekuwa nikielezwa tatizo hilo na tayari nilishaanza kulifanyika kazi ila sasa siwezi kusema suala hilo limefikia wapi kwani wote tuko kwenye mazishi,” alisema.

Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa wabunge wa Chadema waliotangulia kufika katika msiba huo, Mchungaji Peter Msigwa, Ezekia Wenje na Lucy Owenya, walikutana na uongozi wa kata wa Chadema ili kumaliza mgogoro huo.

Katibu mwenezi wa Chadema kata ya Ifakara, Antony Kamonalelo alisema viongozi hao walikaa na wanachama hao na kuwataka wapunguze munkari ili kumruhusu Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Kilombero, Salum Ngozi na Mbunge wa Viti Maalumu, Susan Kiwanga kuhudhuria mazishi.

Hata hivyo, inadaiwa kwamba wanachama hao waliukubalia uongozi huo kumruhusu Susan peke yake kuhudhuria mazishi hayo.

Juzi, wanachama hao walimtimua msibani Ngozi kiasi cha kuwalazimu polisi waliokuwa eneo hilo kuingilia kati kwa kumchukua mwenyekiti huyo na kumpeleka katika Kituo cha Polisi Wilaya.

Hiyo ilikuwa mara ya pili kwa Ngozi kutimuliwa katika msiba huo. Mara ya kwanza ilikuwa siku moja iliyotangulia ambayo ilimlazimu Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Francis Miti kuingilia kati.

Ngozi amekuwa akidai kwamba anafanyiwa fujo na kikundi cha watu aliowaita wahuni na kwamba amefungua kesi ya kufanyiwa vurugu katika Kituo cha Polisi Wilaya ya Kilombero na kwamba baada ya kumalizika kwa mazishi atasimamia suala hilo ili haki itendeke.
 
Usiandikie mate wakati wino upo, kuna yule mbunge wa Arumeru anaitwa Sumari amefariki usiku wa kuamkia leo ngoja uone kama atalihudhunisha Taifa zaidi ya mke wake na familia yake tu.
Regia ameligusa Taifa zima hakuna mwenye uwezo wa kubadili ukweli huu.
Tena Mkuu Matola huyo alikuwa waziri ndogo wa fedha, nina uhakika jibu atalipata!!!!!!!!!!!!

This is so hard for me. Especially with the pictures. A picture is more than a thousand words, and these photos speak volumes of the love people had for Regia.

Yaani nilikuwa na shauku sana ya kuona Regia ataendeleaje. Ingawa tulikuwa marafiki wa JF (kati ya watu wachache walio katika kurasa yangu ya JF kama marafiki) sitaki kuwa mnafiki na kusema nilikuwa rafiki yake mkubwa, sikuwa. Lakini nilifikiri, kwa dhati ya moyo wangu wote uliojaa ubishi na maswali ya kila aina, nikifikiri kwamba, kwa ubishi na maswali yangu, nilikuwa nachangia sio tu kumjenga yeye, bali kujijenga mie mwenyewe kimawazo kwa kuhoji umakini wa uongozi wa kisiasa wa Tanzania. Hata kama ilikuwa ni kwa malumbano ya hoja nzito yaliyopelekea saa nyingine kuonekana kama twajenga uhasimu, hususan kwa wale ambao hawakuelewa kwamba "you can't make an omelette without breaking an egg".

"Gender Sensitive" alipotangaza nia ya kugombea ubunge, wakati karibu wote hapa walipofurahia na kushangilia, wengi bila hata kujua huyu "Gender Sensitive" ni nani, mie nikakataa kuunga tela la kushangilia. Nikalazimisha tumjue huyu anayetaka kugombea ubunge jina lake ni nani na anagombea jimbo gani. Maaana kuna wengine wangetaka kuchangia michango ya hali na mali, lakini wasingejua wachangie wapi. Wengine wangeweza kuona huyu "mtoto" anatutania tu.

Akakubaliana na maoni yangu. Akajitangaza rasmi. Kuanzia hapo ukaanza uhusiano kama wa mtu anayeona kila kinachofanywa sawa kuwa ni "wajibu wake" na "ana wafuasi wa kumsifu wa kutosha". Lakini kila alipokosea - au nilipofikiri alikosea- asingeweza kusema tumemdekeza hata siku moja.

Nafikiri hatujawa na mbunge ambaye ameonyesha ushirikiano wa kutoa mawasiliano, hususan hapa bodini, kama Regia. Hilo tu latosha. Lakini sishangai sana, kwani alikuwa mwanachama wa JF kabla hajawa mbunge, na kama nilivyosema hapo juu, hata sehemu ya kampeni mwanzo kaanzia hapa. Kwa hiyo ningeshangaa kama asingerudi kutoa ripoti hapa.

Nashukuru kumjua, kujua kwamba alikuwa anajifunza mengi.

Kiu yangu ya kujua Regia angeenda kukua vipi bungeni imekatazwa kunyweshwa maji ya kujua. Imekuwa kama ndoto iliyokatizwa na kuamka kabla ya kumalizika.

Ndoto nzuri iliyokatizwa na ukweli kwamba hatuna uhakika kama kesho tutaiona.

Kwa hili wote tunajifunza kutoka kwa Regia hususan katika waraka wake wa kuukaribisha mwaka mpya, kuwa wapole, kuishi na watu vizuri, kujiombea udhuru kwa wale tunaowakosea, kuheshimu tulipotoka, kutoogopa kusemwa vibaya, kutoogopa kusema tunachosimamia, kutoogopa kukubali tunapokosea, kusikiliza wengine wanasemaje na mengine mengi kama hayo.

Sintojua maendelezo ya waraka ule wa mwaka mpya tena. Ukatili wa kifo, kisicho huruma kama alivyosema Remmy Ongala, umehakikisha hilo.

Lakini nafarijika kuona maisha yake hayajaisha bila maana, kwani kasimama kidete kueleza alichoamini hata pale tulipoona kakosea, tulijua yuko wapi. Na katika wabunge walioweza kugusa wengi katika muda mfupi kabisa itakuwa vigumu kumpata wakumfananisha.

Sote tunakongoroka. Kumbuka hilo kila siku. Litakusaidia kuishi vyema zaidi na watu.

Kiranga.
Kiranga,
A very concentrated message!
Huwa binaadam tunachelewa sana kung'amua mantiki za mambo, aidha tunakuja kuzinduka muda ushapita!

Wengi tulikulaumu sana kuwa ulikuwa una agenda ya wivu au kumkwamisha Regia katika mission zake, lakini , of late tunajifunza kwamba you had something deep into your heart of which u wanted to instil into her!

Na bahati nzuri, yeye aligundua hilo, na akasema kuwa hapa JF anapitia kwenye Tanuru la moto, lakini anjua kuwa hatimaye atatoka akiwa imara!
Finally, thank you Kiranga!
 
Nakulilia mdogo wangu na rafiki yangu Regia. Niko kitandani hapa nakabiliana na maradhi (kama ulivyokuwa unajua). Nimefuatilia yaliyokuwa yanajiri tangu kifo chako kwa majonzi sana. Nimesikitika sana lakini nimefarijika kwa kuwa moyo wangu umeniambia umelala mahali pema. Nauamini moyo wangu ndio maana naamini iko siku moja tutaonana tena. Kwaheri mjukuu wangu, kwaheri rafiki yangu kwaheri Regia wangu. Upumzike kwa amani mama.
Pole sana....Pona haraka
 
Poleni sana wafiwa wote, wazazi, ndugu, jamaa, marafiki na wana JF wote kwa ujumla.
Naamini safari ya kumsindikiza dada yetu kwenye nyumba yake ya milele imeenda vizuri na nawaombea wote watakorudi majumbani kwao toka Ifakara, Mungu wetu awatangulie.
Ee Mungu mpokee mwanao Regia, msamehe makosa yake kama binadamu, sisi tuliobaki tunakumbushwa kujiandaa kwani siku moja tutatwaliwa kama mdogo wetu na dada yetu Regia.
 
Back
Top Bottom