Maulidi Kitenge aacha kazi ITV/Radio one

Maulidi Kitenge aacha kazi ITV/Radio one

du, hivi utangazaji nao unajiuzulu? du naona anawaza siasa, au amepata na yeye post serikalini ya upande wa habari nini? angeandika yah: kuacha kazi basi.
Kwenye ajira unaacha kazi lakini sio kuijiuzulu.Waliomshauri walikosea.
Pia when you read between the lines unaona ana ulalamishi fulani ambao amekuwa mwoga kuutaja nayo ni kuhusu kipato.
Tatu amefanya makosa makubwa kuweka barua yake ya kuacha kazi mtandaoni nani atakayemwamini kuwa hawezi kuweka nyaraka zingine mtandaoni?
Kwa ujumla tunamtakia kila la khei na ni vizuri kwani kuna mwingine ataingia naye kuonyesha kipaji chake.
 
E fm homa ya jiji.... Wamchukue Geof Leah pale Azam....michezo itabamba sana
 
Utashangaa anaenda Azam tv au clouds. itv kila siku inapewa bichwa humu jf alafu mshahara mdogo kwa wafanyakazi wake.wawe makini sasa bado alfred masako na marato kusepa
 
10523320_10152325499543479_7980446177339854228_n.jpg

Niliiona hii kwa jamaa mmoja thn ikawa ameandika Efm.
 
hivi ishawahi kutokea mtangazaji mkali katoka labda clous au chten kaenda ipp?
 
Azam Tv inaweza kuhusika.

Hapana mkuu, AZAM kakaa mbaliii anacheki muvi, jamaa kaenda kuungana na kina SSEBO ndani ya Efm.
MTANGAZAJI mahiri wa habari za michezo wa siku nyingi Maulidi Baraka Kitenge amejiunga na kituo cha radio kiitwacho EFM 93.7 kilichopo Kawe jijini Dar es salaam leo.

Kutokana na tafiti ya Ipsos ya mwaka 2013, inasemekana kuwa mtangazaji huyo wa zamani wa kituo cha Radio One, ndiye mtangazaji bora wa michezo nchini Tanzania.

Mkurugenzi wa vipindi wa Radio EFM, Dickson Ponela, ameeleza kufurahishwa kwake kwa mtangazaji huyo kinara kuhamia katika kituo hicho.

“Mpaka sasa Kitenge ameisha saini mkataba na kituo chetu na anatarajiwa kusikika hivi karibuni katika kipindi cha michezo hapa EFM”, alisema mkuregenzi huyo.

Kitenge au jezi nambari tisa mgongoni, amejiunga na magwiji waliobobea katika fani hiyo akiwemo Dizo One, Dennis Sebo, Sos B, Kanky Mwaigomole na Dj Majay.
 
Miaka 14, amepata mashavu mengi ya kwenda nje, nafasi hio hio imempatia cv, nafasi hiyo hiyo imempa mshahara, nafasi hio hio imemfanya akawa Maulid kitenge. Eti leo unataka kuondoka unamkejeli mwajiri? Kama mshahara ulikuwa mdogo kwanini hakuondoka mapema? Ndiyo maana waajiri wengi wanapenda wageni
 
Kimeota vp wakati mtu karesign na wewe

Hakija ota mkuu, jamaa kala shavu la kutakata toka kwa EFM 93.7 ,
Mcheki hapa kitenge akisaini mkataba na Mkurugenzi wa vipindi wa EFM Bw.Dickson Ponela
 

Attachments

  • KITENGE1.JPG
    KITENGE1.JPG
    38.5 KB · Views: 259
  • KITENGE2.JPG
    KITENGE2.JPG
    37.6 KB · Views: 249
Atakuwa amepata kazi sehemu nyingine ama ashajipanga maana kulisha wake watatu mjini Dar es Salaam halafu kuacha kazi bila kujipanga unaweza ukashangaa kesho kajitundika

N i kweli kapata kazi kwingine na si mbali sana ni pale kawe ndani ya EFM. Nadhani jamaa saa hizi anakwambia Life goes on as usual..
 
Kwa hiyo!

Mtu B.W.A.B.W.A utamjua tu kwa kauli zake... coz nakuona umebana na pua kabisa ukisema "KWAHIYO".
hebu tizama jinsi ulivyo hapa chini ...
 

Attachments

  • images.jpg
    images.jpg
    6.7 KB · Views: 385
  • imagesQ.jpg
    imagesQ.jpg
    5 KB · Views: 407
ntamkumbuka akimchokoa WAMBURA...na makocha wengine....?

akisomea SHERIA atakuwa mchokonoaji mzuri zaidi...huenda kapata shavu mahali

Aahahaaa...... kweli mkuu, tena nikikumbuka alivyo zenguana siku moja na Alhaji Muhidin Ndolanga , baaa ya kuitwa Ndolanga Na kitenge, jamaa akamtolea uvivu na kumwambia "usiniite ndolanga sema Alhaji Muhidin Ndolanga kwani mimi ni sawa na baba yako" haa ilikuwa burudani sana kwa anayekumbuka hii scene.
 
Wenzake walitangaza kwa hali ngumu iliyokuwepo na wakafanikiwa now wako bbc, voa, na kungineko,, kikeke, chaz hilari, nk. Yeye alioa wake kadhaa, angetoka kweli utaendaje ulaya na wake wote hao?

Duh umenichekesha kwelikweli!you have made my day!!!!
 
Back
Top Bottom