Mitandaoni kuna mambo mengi na serikali ijikite kuchukuwa mazuri kama ushauri na wakati mwingine hata rushwa tunajua kutokana na mitandao. Lakini Vilevile msipoteze muda kuwa tafuta watu ambao ni wapoyoshaji maana kwenye mitandao kuna mpaka watoto wa miaka 20 na 21 huku ambao mitandao kwao ni michezo tu ya kutumia wakati hawana la kufanya. Hivyo msipoteze pesa zetu kutafuta watu au kuzuia mitandao. Pesa za kuzui mitandao ni maana yake ni kuzuia hata mawazo mazuri maana ni sehemu hizohizo kuna mazuri na mabaya. Lakini hatuna uwezo wa China na kuwa na youtube zao na vitu kama hivyo maana wenzetu wana lugha tofauti ni rahisi. Lakini kama ni kijana wa kitanzania katukana yupo uingereza ana miaka 20 na ni raia wa uingereza mtamfanya nini? Hata kama mkimjua?!!!. Hivyo chukuweni mazuri. Mfano wa mazuri ni jinsi wasanii wetu vijana wanavyopata pesa za youtube au kufungua chanel tofauti siku tukisema tuzuie youtube kwasababu ya wale wanaosema vibaya ni kuzuia kazi, kodi, na maendeleo ya vijana wetu. Kuna channels ngapi za youtube za Watanzania!. Pesa kiasi gani vijana wamepata, show kwa wasanii kwasababu ya youtube. Tanzania imejulikana kwasababu ya youtube mfano nilikuwa simfahamu dogo janja au rosa ree mpaka youtube sikuhizi nawaangalia kila siku na wenyewe wanalipwa.
Sasa mkitoa hotuba kwamba mtawatafuta hao watu hata hawasikilizi hizo habari na haziwafikii maana sio waelewa ki hivyo!.
 
kwani yeye mwenyewe siyo ccm? siyo mataga?
Wewe ndiyo MATAGA, Hiyo lugha ya "ni kitu kimoja" ni lugha ya siasa tu. Yeye hayuko huko. Anaongea kisiasa hamuwezi kumuelewa. Angalia matendo yake upate majibu. Jipange tu umkubali maisha yaendelee. The late is gone, and will never be back.
 
Nilijua wapiga makofi watashangilia kuwa huru kwa sababu yupo Madame ikulu now burn inaendelea kwa walopokaji 😁!!
 
Wabunge wa CCM wamepiga makofi leo mpaka mikono yao imebakia na malengelenge kwa ajili ya unafiki wao. Roho zimewashuka Rais SSH aliposema atakuwa akikutana na viongozi wa vyama vya kwa ajili ya mazungumzo juu ya mustakabali wa amani ya nchi yetu.View attachment 1760640
Video hii hapa
 

Attachments

  • VID-20210422-WA0069.mp4
    117.6 KB
Mpe muda jaribu kujiconect na nini unataka serikali hii ikutendee na wewe ukiahidi kuwa mwaminifu katika kufuata taratibu za nchi!
bado anahitaji muda kuweni wavumilivu
 
Kwa nchi za kiafrika, mwanamke kukiongoza kiti cha uraisi kwa weledi inakuwa ngumu. Kwa sababu zifuatazo,
1: Sheria za utawala ni mbovu, katiba ni duni.
2: Vitengo vya ki-usalama na nyeti vya serikali na taifa kwa asilimia kubwa vimeshikiliwa na wanaume (Jeshi, Polisi, taasisi za intelligentsia, taasisi za ujasusi, taasisi za ushushu).
3: Mihimili ya serikali (Bunge na mahakama) vimeshikiliwa na wanaume.
4: Mitazamo dume kwa wanaume (Kuwa hatuwezi kutawaliwa na mwanamke).
5: Maamuzi ya wanawake (Mfano: Mama Banda kule Malawi, ndani ya miaka miwili kaanza kusema Ziwa nyasa ni lake).

Mwisho wa siku, unakuta mwanamke kiti Cha uraisi amekalia kama pambo nchi inaongozwa na wanaume vile vile.
Pole sana. JPM is gone for ever.
 
Kuwa na chuki binafsi na mtu hata kama hajakukosea chochote ni mwanzo wa mtu kuwa mchawi. Stage zake ni chuki, kijicho, husda na hatimae uchawi.

Kwavile tayari umeamua kumchukia tu bila sababu huwezi muelewa.

Ila ukiwauliza waandishi wa habari ambao vyombo vyao vimefunguliwa baada ya kufungiwa kiuonevu, ukiwauliza Taasisi za kiraia ambazo account zao zimefunguliwa baada ya miezi kadhaa ya kuzuiliwa wao wanamuelewa analolifanya.

Angalizo: Chuki binafsi ni moja ya magonjwa makubwa sana ya nafsi jiepushe na ujikinge na gonjwa hilo
 
Sijui Kama namchukia au nimeadhirika na muziki wa mzee baba Magufuli.

Huyu mama sijui afanye nini ili nimuelewe.


Ila poa tu ngoja tuone.

Niko njiapanda kwa kweli.

Sent from my Infinix X5515 using JamiiForums mobile app
Huta shawishika kwa kuwa maslahi yako umeona yako mashakani kwani huamini katika yale anayoamini. Ili ushauri tu,neema inakuja mtazamo wako haukuwa sahihi.
 
Back
Top Bottom