Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
2,061
991

Mbunge Vuma Holle: Rais Samia Suluhu Hassan Atakumbukwa Kigoma

Mbunge wa Kasulu Vijijini mkoani Kigoma, Augustine Vuma amesema kazi kubwa ya kumtua mama ndoo kichwani inayofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan kupitia Wizara ya Maji imeleta mabadiliko makubwa ya upatikanaji wa huduma ya maji mkoani Kigoma kupitia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maji.

Amesema jambo hilo litawafanya wakazi wa Kasulu Vijijini na Mkoa wa Kigoma kuendelea kumkumbuka Rais Samia Suluhu Hassan.

Akichangia bajeti ya Wizara ya Maji kwa mwaka wa fedha wa 2024/2025, mbunge huyo ameiomba Serikali kukamilisha mradi wa maji wa Ziwa Tanganyika ili wananchi waendelee kunufaika na miradi ya kumtua mama ndoo kichwani.
 

Attachments

  • maxresdefaultmnbvcfg.jpg
    maxresdefaultmnbvcfg.jpg
    92.2 KB · Views: 1
Back
Top Bottom