Nimeichungulia ratiba yetu ya mechi zijazo imenibidi nikubaliane na unachokisema kwa njia ya maandishi, lakini kuna jambo moja laziba tuliweke vichwani mwetu.

Ole wa sasa ana kundi kubwa sana la wachezaji wenye uwezo wa kumpa huduma ya magoli pengine kuliko kocha mwengine yeyote pale England, na hii ndio silaha yake kubwa itakayoendelea kumweka mjini kama ataendelea kuchanga karata zake vyema.

Ukitaka kupima ubora wa Ole kiufundishaji na si kimatokeo basi subiria mechi atakayofanya mabadiliko ya kikosi kwa kuwaweka nje key players hususani bruno fernandez, kwa mfano nimeona mechi ya leo akizungumzia mpango wake wa kufanya mabadiliko ndani ya kikosi kwa kuwapa nafasi wachezaji wengine kama lingard, mata, telles, elanga n.k

tukumbuke kuna timu hazibadiliki kiuchezaji hata kama zitatumia wachezaji wa kikosi cha pili, timu ni hizo ni man city, liverpool, leeds, chelsea, brighton.

je pattern ya kiuchezaji itabaki vile vile au itaathiriwa na mabadiliko ya wachezaji?
bila ya shaka jibu tutalipata usiku wa leo na hapo ndipo tutakapofahamu rasmi Ole ni kocha wa aina gani.
katika makocha ambao wakifikiria tu kubadili mfumo wanapigwa ni pep, jamaa ana plan A tu, ukitaka ushahidi nitakutafutia mkuu.
 
Back
Top Bottom