Makamu wa Rais, Dkt. Emmanuel Nchimbi, ajiuzulu

Makamu wa Rais, Dkt. Emmanuel Nchimbi, ajiuzulu

Hivi nafasi hiyo si huwa inapatikana kwenye sanduku la kura? Kwani Katiba inasemaje kuhusu hilo.
Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ibara ya 47 (2) inasema
Nanukuu.
Bila kuathiri masharti ya Ibara 37 (5).
Makamu wa rais atapatikana kwa kuchaguliwa katika uchaguzi ule ule kwa pamoja na rais, baada ya kupendekezwa na chama chake wakati ule ule anapopendekezwa mgombea wa kiti cha Rais na watapigiwa kura kwa pamoja.
Mgombea kiti cha Rais akichaguliwa basi na Makamu wa rais atakuwa amechaguliwa.

(3) Mtu atateuliwa kugombea kiti cha Makamu wa rais kwa kufuata kanuni kwamba endapo Rais wa Jamuhuri ya Muungano atatoka sehemu moja ya Muungano basi Makamu wa rais atakuwa ni mtu anayetoka sehemu ya pili ya Muungano.

50 (4)
Ikitokea kwamba kiti cha Makamu wa rais ki wazi kutokana na masharti yaliyomo katika ibara ndogo ya ( 3) kifo au kujiuzulu, basi mapema iwezekanavyo na kwa vyovyote ndani ya siku zisizozidi kumi na nne baada kushika madaraka yake, Rais atamteua mtu atakayekuwa Makamu wa rais na uteuzi huo utathibitishwa na bunge kwa kura za wabunge walio wengi.

Mwisho wa kunukuu.

Nadhani umetosheka mkuu Iyerdoy
 
Makamu wa Rais na Rais wote wanachaguliwa pamoja, kwenye tiketi moja, siku moja, kama wabia, na kuna watu wanaipigia kura tiketi hiyo kwa sababu ya mgombea u Makamu wa Rais, wala si kwa sababu ya mgombea u Rais.
Mkuu uko sahihi 💯, umetoa darasa kwa masaa kadhaa lakini watu hawataki kulewa.
Ni hawa hawa ambao mara nyingi wanabishana humu kutetea vyama vyao lakini Katiba tuliyonayo hawataki kuisoma.
Heri upumzike sasa ujadiri mambo mengine.
 
Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ibara ya 47 (2) inasema
Nanukuu.
Bila kuathiri masharti ya Ibara 37 (5).
Makamu wa rais atapatikana kwa kuchaguliwa katika uchaguzi ule ule kwa pamoja na rais, baada ya kupendekezwa na chama chake wakati ule ule anapopendekezwa mgombea wa kiti cha Rais na watapigiwa kura kwa pamoja.
Mgombea kiti cha Rais akichaguliwa basi na Makamu wa rais atakuwa amechaguliwa.

(3) Mtu atateuliwa kugombea kiti cha Makamu wa rais kwa kufuata kanuni kwamba endapo Rais wa Jamuhuri ya Muungano atatoka sehemu moja ya Muungano basi Makamu wa rais atakuwa ni mtu anayetoka sehemu ya pili ya Muungano.

50 (4)
Ikitokea kwamba kiti cha Makamu wa rais ki wazi kutokana na masharti yaliyomo katika ibara ndogo ya ( 3) kifo au kujiuzulu, basi mapema iwezekanavyo na kwa vyovyote ndani ya siku zisizozidi kumi na nne baada kushika madaraka yake, Rais atamteua mtu atakayekuwa Makamu wa rais na uteuzi huo utathibitishwa na bunge kwa kura za wabunge walio wengi.

Mwisho wa kunukuu.

Nadhani umetosheka mkuu Iyerdoy
Angalau sasa magazeti watapata habari za kuuza
 
Unajichanganya, kilichoshinda ni chama, ukijiuzuru umakamu bado chama chako kina haki ya kupeleka jina lingine kwa spika ili bunge likuidhi
Katiba haisemi kuwa Makamu wa rais akifariki au kujiuzulu kuwa chama chake ndicho kinachoteua na kupeleka jina kwa spika.
Katiba inasema rais ndiye anayeteua na kupeleka jina hilo ili liidhinishwe na wabunge walio wengi.
 
Sasa akiwa nje ya huo mfumo ndo hatari zaidi aisee japo naona kesi yake ni kama ilivyokua kwa Job Ndugai ...yule Mbunge wa Znz aliyemuita yuda ndo maana alikua na iiburi aisee.
Nchimbi aliwaambia wananchi kuwa anaekwamisha kupatikana kwa Katiba ni Samia; mdaini Katiba kwa nguvu. Hii inaitwa usaliti (insubordination). Ni nguvu kiasi gani wananchi watumie ili Samia aiandike Katiba? Yaani unamsagia kunguni usoni boss wako ili anuke.

Jambo kama hilo bila shaka ni kinyume cha collective responsibility. Vance JD, Makamu wa Rais wa Marekani ana vitu vingi hakubaliani na Rais Trump, lakini hajawahi kutoka hadharani kuwaambia wananchi wampinge Rais kwenye jambo lolote hata yale ya hovyo anayofanya Trump.
 
Makamu wa Rais hateuliwi anachaguliwa..

Ki ufupi UCHAGUZI nataka Kujua Upo au HAupo?

Na ni wa Makamu Peke ake au kwa wote? ILA TANZANIA nchi 1 ambayo kama unahela zako...unaenda tafuta Pori uko unaenda unakaa na masilaha yako unaishi unatulia.

Nchi gani inahangaika hangaika kama inataka ingia Period....
Soma Katiba kijana
 
Unafikiri utaoneshwa wewe? Na huyo aliyeandikiwa anajali hata kujibu?
Hata asipoonesha kwa Umma, akiteua tu mtu mwingine tutajua kuwa AMEKUBALI kujiuzulu kwa VP. Asipoteua mwingine ndani ya muda uliowekwa tutajua kuwa AMEKATAA.
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Emmanuel John Nchimbi, ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo na kustaafu siasa pamoja na utumishi wa umma.

Katika taarifa yake kwa umma iliyotolewa leo, Dkt. Nchimbi amesema amemuandikia barua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kumjulisha uamuzi wake wa kuachia nafasi hiyo.

Amesema uamuzi huo umefanywa kwa kuzingatia Ibara ya 50(2)(c) ikisomwa pamoja na Ibara ya 149(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kujiuzulu kwake kutaanza rasmi Septemba 4, 2026.

Dkt. Nchimbi ameeleza kuwa wakati alipomuahidi Rais Samia mwaka 2025 kuwa atamsaidia katika kutekeleza majukumu yake kwa uwezo na uaminifu wake wote, pia aliahidi kuwa angeachia nafasi hiyo siku ambayo Rais angeona anahitaji Makamu mwingine.

Amesema amefanya uamuzi huo pasipo shaka baada ya kubaini kuwa Rais anatarajia mabadiliko.

View attachment 3656524
Nchi hii ukiwa Rais kutoka zanzibar halafu hauko stable lazima makundi haya matatu yakutoe kwenye focus au falsafa yako. Kwanza ni ccm yenyewe (wale wanaojiona wanakijua chama na nchi hii), pili ni watu wa usalama ( wazee wa kunusanusa) na tatu wazanzibari (wanaojiona ni ndugu zako). Wote hao watakupa ushauri ambao utaonekana ni muhimu na unakulinda wewe lakini utakuyumbisha sana kwenye maamuzi na utulivu wa kiuongozi, mwisho utajikuta unamalizi muhula wako bila kujua ulishindwaje kudemonstrate falsafa yako ulipokuwa Rais.
 
Utaratibu. Kumbuka huyo Mama alishawahi kusema kuwa "Katiba ni kakijitabu tu" Unaweza kupima uwezo wake wa akili kwa maneno anayotamka hadharani.
Kwa hiyo mtu aliyesema katiba ni kijitabu tu ndiye barua yake itakuwa muhimu?

Sijaelewa point ya umuhimu wa barua bado.

Na hiyo point ya katiba ni kijitabu tu inazidi kuonesha barua haina umuhimu kabisaa.

Na kiukweli katiba ni kijitabu tu, ndiyo maana hata sasa hamuitekelezi, kwa sababu hamna utamaduni wa ukatiba.
 
Back
Top Bottom