Makamu wa Rais, Dkt. Emmanuel Nchimbi, ajiuzulu

Makamu wa Rais, Dkt. Emmanuel Nchimbi, ajiuzulu

Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk Emmanuel Nchimbi, amemwandikia Rais Samia Suluhu Hassan, barua ya kujiuzulu wadhifa huo, miezi michache baada ya kutoa kauli mbalimbali zenye utata.

Kabla ya taarifa hiyo, Dk Nchimbi kwa nyakati tofauti amekuwa akiibua kauli zinazoleta utata, ikiwemo ile aliyowataka Watanzania wapambane kuipata Katiba Mpya, ilhali ajenda hiyo tayari ilishawekewa utaratibu ndani ya chama chake cha CCM na hata kuwa katika Ilani ya chama hicho.

Kauli hiyo iliibua sintofahamu hata ndani ya CCM. Mwenyekiti wa Wazazi Taifa, Fadhili Maganya, aliijibu kwa kuhoji, anayewashinikiza Watanzania wapambane kupata Katiba Mpya, anataka wapambane na nani?

Sambamba na kauli ya Maganya, Mbunge kupitia Baraza la Wawakilishi, Mohamed Simai Said, aliwahi kusema ndani ya Serikali kuna kiongozi msaliti akimwita ‘Yuda’ kwa kile alichosisitiza, anakinzana na mwelekeo na dhamira ya Serikali.

Mienendo hiyo, ilimwibua Mwanasiasa mkongwe, John Shibuda ambaye Agosti 23, 2026 alizungumza na vyombo vya habari, akimsihi Dk Nchimbi ajiuzulu kutokana na mwenendo wake unaokwenda kinyume na mwelekeo wa Serikali

Dk Nchimbi ametoa taarifa ya kuandika barua ya kujiuzulu na kusambaza katika kurasa za mitandao yake ya kijamii leo, Agosti 25, 2026.

Katika barua yake, ameandika atajiuzulu wadhifa huo kuanzia Septemba 4, 2026 akimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan na wananchi kwa kipindi alichoongoza.
IMG-20260825-WA0005.jpg
 
Kwa lugha nyepesi ni Rais mwenza.
Exactly.

Kwa nini wabongo wengi hili jambo wanalidogosha sana?

Makamu wa Rais si sawa na Waziri Mkuu ambaye anateukiwa na Rais tu.

Makamu wa Rais anapata nafasi yaje kama running mate wa Rais kwwnye uchaguzi, on the same ticket.

Yani kuna watu wamechagua ticket ya Samia/Nchimbi kwq sababu ya Nchimbi, si kwa sababu ya Samia.

Na hakuna namna ya kujua hao ni wangapi.

Mbona watu wanalidogosha sana hili jambo?
 
Hii barua inamakosa mengi sana.
Wekeni audio/video kama ipo otherwise tusiamini.... kwasababu hii barua ilitakiwa iwe na ushahidi wa barua nyingne (attached document) kwa Mujibu wa maelezo ya barua ukiisoma.
Tusiende haraka tusubri kauli ya mdomo
Umekuwa Tomaso?

Dr Nchimbi anakabidhi ofisi tarehe 4 September.

Wewe endelea kuota tu.
 
Exactly.

Kwa nini wabongo wengi hili jambo wanalidogosha sana?

Makamu wa Rais si sawa na Waziri Mkuu ambaye anateukiwa na Rais tu.

Makamu wa Rais anapata nafasi yaje kama running mate wa Rais kwwnye uchaguzi, on the same ticket.

Yani kuna watu wamechagua ticket ya Samia/Nchimbi kwq sababu ya Nchimbi, si kwa sababu ya Samia.

Na hakuna namna ya kujua hao ni wangapi.

Mbona watu wanalidogosha sana hili jambo?
Mgombea mwenza siyo Rais Mwenza.
Someni katiba acheni mbwembwe.
 
Nchimbi na samia hawakugombea urais pamoja mana samia alipitishwa kihuni.

Sasa kama Nchimbi hajachaguliwa na wananchi kwa sababu ya uchaguzi kuharibika, inakuwaje samia awe amechaguliwa na rais?
Samia awe amechaguliwa na rais?

Let's make this simpke.

Achana na Nchimbi, achana na Samia, achana na CCM, achana na uhalali wa uchaguzi. Ondoa controversial subjects, tujadili mfumo wenyewe tu.

Tuuangakie mfumo wa uchaguzi wa Tanzania in the abstract.

Makamu wa Rais na Rais wote wanachaguliwa pamoja, kwenye tiketi moja, siku moja, kama wabia, na kuna watu wanaipigia kura tiketi hiyo kwa sababu ya mgombea u Makamu wa Rais, wala si kwa sababu ya mgombea u Rais.

This is packaged deal, huwezi kumoata mmoja bika mwingine.

Unakubali?
 
Japo Upo nje ya wakati, vp umefurai au na wewe chawa umetaharuki ?
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Emmanuel John Nchimbi, ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo na kustaafu siasa pamoja na utumishi wa umma.

Katika taarifa yake kwa umma iliyotolewa leo, Dkt. Nchimbi amesema amemuandikia barua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kumjulisha uamuzi wake wa kuachia nafasi hiyo.

Amesema uamuzi huo umefanywa kwa kuzingatia Ibara ya 50(2)(c) ikisomwa pamoja na Ibara ya 149(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kujiuzulu kwake kutaanza rasmi Septemba 4, 2026.

Dkt. Nchimbi ameeleza kuwa wakati alipomuahidi Rais Samia mwaka 2025 kuwa atamsaidia katika kutekeleza majukumu yake kwa uwezo na uaminifu wake wote, pia aliahidi kuwa angeachia nafasi hiyo siku ambayo Rais angeona anahitaji Makamu mwingine.

Amesema amefanya uamuzi huo pasipo shaka baada ya kubaini kuwa Rais anatarajia mabadiliko.

View attachment 3656524
Taarifa FEKI!!!!!!!
Barua gani hii yenye anuani za ajabu tu? Au ni UVCCM wanawinda kufanya kama ya Ndugai? NCHIMBI shikilia hapo hapoa!
 
Nadhani ni vizuri kujiuzulu kuliko kufukuzwa au kutenguliwa. Bado naamni kapiga hesabuu vizuri sababu yupo kwenye siasa muda mrefu. Sina shaka naye kuhusu siasa
Kama mtu anaamini katika principles zake, anaamini anapigania mambo fulani, na yuko tayari kuzilinda principles hizo at any cost, kwa nini ajiuzulu?

Na kama hayuko tayari kuzilinda principles hizo at any cost, kwa nini kaingia katika siasa za kitaifa Tanzania?
 
Back
Top Bottom