Mafanikio ya Rais Magufuli 2015 - 2020

babalao 2

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2012
Messages
4,816
Points
2,000

babalao 2

JF-Expert Member
Joined Apr 6, 2012
4,816 2,000


Wanajukwaa poleni na misukosuko ya kujibadili kutoka kuwa walaji wa Mwisho kuelekea nchi ya Viwanda.

Uwanja huu ni maalumu kama ule wa Safari za nje za Jakaya kikwete ila huu ni mahususi kukusanya mambo mazuri ya Awamu ya tano chini ya Rais Magufuli juu ya maendeleo yetu hasahasa kauli yake kuu Juu ya Nchi ya Viwanda na Elimu Bure nk.

Unaruhusiwa kugusia miundo mbinu, Afya, Usafiri, Maendeleo ya Majeshi Yetu, Uvuvi,Michezo, Habari, Siasa, Viwanda,Teknolojia, Pato la Taifa nk.
Ila tu iwe kwa tulipotoka na Alipofanikiwa na nini tufanye kumsaidia kujiongeza zaidi.

Mpaka sasa kafanya haya;

Hostel za Chuo cha UDSM.
Hostel za Askari Magereza.
Ununuzi wa Ndege 2 (Nyingine 3 ziko mbioni kuja).
Ujenzi wa Flyover Tazara na Ubungo
Upanuzi wa Airport Mwanza
Upanuzi barabara ya Moroco Dsm
Upanuzi wa Kisasa Airport Dar
Kukomesha Rushwa
Kurejesha nidhamu Makazini.
------------

Na haya ameanza tarehe 12/4/2017;

Uzinduzi ujenzi wa reli kwa ajili ya treni ya Umeme.
Ujenzi wa barabara ya Mtwara-Tandahimba

Kukomesha Watumishi Wenye Feki hivyo kuokoa Mabilioni ya Fedha.

Barabara ya kuunganisha Wilaya za Kibondo kigoma Kaliua huko Tabora.

Miradi Mikubwa ya Maji :

Uwezeshaji Ujenzi Bomba la Mafuta kutoka Hoima mpaka Tanga

============
emie emie posted: Kwa kweli Rais wetu kafanya makubwa sanaa..
Kila upitapo sasa hivi ni ujenzi unaendelea...Dar es Salaam kila kona Barabara ya Tandale-Sinza- Mawasiliano inajengwa
Madaraja yanajengwa

Upanuzi wa barabara kuu ya Ubungo hadi chalinze unafanywa

Daraja Kilombero miaka yote wapigaji walikuwa wanakula hela za wananchi kuwavusha ila sasa limejengwa

Flyovers zinajengwa

Miradi ya umeme inajengwa na miradi mingi ni kwa hela za watanzania wenyewe

Miaka yote maeneo ya Mbezi na kimara walikuwa hawapati maji japo yanapita njia hiyo hiyo lakini sasa maji yamefika mbezi, na bado wanaendelea kutandaza mabomba ili kupeleka maji. Awali waliokuwa wanakula hela za wananchi ni wenye miradi ya kuuza maji kwa magari. Ila sasa wananchi wamekombolewa.

Utendaji kazi umeimarika, sasa hivi kila mmoja anaona cheo akipewa ni kama kakalia kaa la moto..Yale mambo ya kupiga hela na kukaa ofisini kupiga usingizi yameisha watu ni kazi la sivyo unawajibishwa.

Madawa sasa yanapatikana hospitali, ile hali ya madawa ya hospitali yanapelekwa katika Pharmas binafsi imeisha.

Hospitali sasa za serikali ukienda mgonjwa anajaliwa sio kama ilivyokuwa awali.

Taasisi za serikali wafanyakazi wamekuwa wanawajibika ....hakika nidhamu imeimarika.
Kwa sasa taasisi za serikali zinajiendesha kibiasara bali si kihasara kama ilivyokuwa awali, ilikuwa ni ulaji tuu wa hela, upigaji dili, taasisi zinakufa, hakuna gawio kwa serikali, ila sasa zinatoa gawio...Hakika kila kitu ni usimamizi imara, ukicheka na kima utavuna mabua.

Awali watu walikuwa wanaulilia uongozi, hata wasio kuwa na elimu walikuwa wanagombea kupata uongozi, sasa uongozi umekuwa mgumu sababu kama wewe si muwajibikaji una ndoto za kupiga tuu, hupati nafasi, Uongozi umekuwa una hadhi kwa sasa.

Hakika Namsifu Rais wetu...
 

Kitwa-Mulomoni

JF-Expert Member
Joined
Oct 25, 2016
Messages
832
Points
1,000

Kitwa-Mulomoni

JF-Expert Member
Joined Oct 25, 2016
832 1,000
Uko sahihi sana, tatizo pekee la wananchi wa nchi hii ni barabara pekee yake, ajira kwako sio jambo muhimu?
Ajira inakuja hivi.: kwanza kutengeneza barabara kunleta ajira kuanzia mkandarasi, vibarua mpaka mama ntilie. Pili barabara zikiwa tayari usafiri unakuwa wa uhakika kutokana na hilo ukijiongeza unaweza kuona wingi wa ajira kutokana na kuwepo barabara (miundo mbinu kwa ujumla).
 

tindo

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2011
Messages
23,049
Points
2,000

tindo

JF-Expert Member
Joined Sep 28, 2011
23,049 2,000
Ajira inakuja hivi.: kwanza kutengeneza barabara kunleta ajira kuanzia mkandarasi, vibarua mpaka mama ntilie. Pili barabara zikiwa tayari usafiri unakuwa wa uhakika kutokana na hilo ukijiongeza unaweza kuona wingi wa ajira kutokana na kuwepo barabara (miundo mbinu kwa ujumla).
Wakati wa ujenzi wa miradi hizo sio ajira bali ni vibarua, maana baada ya mradi kukamilika ajira hukoma. Hizo ajira za kwenye miradi ya ujenzi sio endelevu.

Kama barabara ndio huondoa tatizo la ajira, huko Afrika kusini kuna barabara mpaka chumbani, ni kipi kinafanya raia wake wavamie wageni kuhusu suala la ajira?
 

Kitwa-Mulomoni

JF-Expert Member
Joined
Oct 25, 2016
Messages
832
Points
1,000

Kitwa-Mulomoni

JF-Expert Member
Joined Oct 25, 2016
832 1,000
Wakati wa ujenzi wa miradi hizo sio ajira bali ni vibarua, maana baada ya mradi kukamilika ajira hukoma. Hizo ajira za kwenye miradi ya ujenzi sio endelevu.

Kama barabara ndio huondoa tatizo la ajira, huko Afrika kusini kuna barabara mpaka chumbani, ni kipi kinafanya raia wake wavamie wageni kuhusu suala la ajira?
Swala la Afrika ya kusini liko complex siyo rahisi hivyo kwamba ni Ajira. Nimekaa huko zaidi ya miaka 26. Ajiri inachangia kitu kidogo sana kama 1%!
 

HIVENY

New Member
Joined
Sep 23, 2019
Messages
1
Points
20

HIVENY

New Member
Joined Sep 23, 2019
1 20
Miaka ya nyuma ilikua baba anaenda kazn au shamban alaf yey anaenda kucheza pool..shukuran ziende kwa serekari ya awamu ya5 police wamejitahid saana kudhibit vijiwe vya kamali magenge ya kupiga story..hakika taifa hili tukiendelea hiv tutalijenga na mpaka G7 tutaingia 2050 Amin vijana ndio nguzo za kesho tuwaache wazee wapumzike kwa maana wamefanya Kaz kubwa
 

wa stendi

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2016
Messages
12,366
Points
2,000

wa stendi

JF-Expert Member
Joined Jul 7, 2016
12,366 2,000
Pole sana wee ukitaka kujua hali mbaya nenda kwenye prium bet (kule wanakobet mambo ha mpira)ndo utajua kuwa kuna kundi kubwa sana hawana la kufanya na pa kwenda ndo wanakoshinda wanafanya hadi dada zetu au wadogo zetu wanaogopa hata kwenda dukani wakigumwa
 

NYEKUNDU YA BIBI

JF-Expert Member
Joined
Oct 27, 2017
Messages
1,791
Points
2,000

NYEKUNDU YA BIBI

JF-Expert Member
Joined Oct 27, 2017
1,791 2,000
Habarini wakuu!

Mabadiriko huanza na mimi nakua na uongozi sahihi wenye tija kwa taifa,

Ninaomba kwa heshima na taadhima ya hali ya juu, kuijua miradi mikubwa iliyotekelezwa tangu Mheshima Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndugu JOHN POMBE MAGUFULI alivyokuwa ameanza harakati zake za kisiasa,
Akiwa kama mbunge wa chato na akiwa kama waziri wa ujenzi

Natanguliza shukrani za dhati kwa watendaji wote wa serikali hii ni kutokana na shughuri nzito mnayoifanya kuhakikisha tunakwenda kule tunakopaswa kufika

Pia niwape pole za dhati kabisa ndugu zangu wote mnaopitia changamoto za kisiasa maana ni lazima zile kuti chakavu zibadirishwe na kuwekwa mpya
 

Boniphace Kichonge

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2017
Messages
1,324
Points
2,000

Boniphace Kichonge

JF-Expert Member
Joined Jul 31, 2017
1,324 2,000
Wadau wa JF.

Unaweza kusema kuwa Historia Sasa imeandikwa na Serikali ya Awamu ya 5 chini ya Mzalendo Nambari 1 na Mtetezi wa Wanyonge Dkt John Pombe Magufuli.

Hospitali ya kisasa ya Rufaa inajengwa Mpanda Mkoani Katavi kwa Kutumia fedha za ndani.

Wakazi wa Katavi hawatakuwa na haja ya kwenda Mbeya kufuata huduma mbalimbali za kisasa kama CT Scan au MRI.

Tunatekeleza
 

Forum statistics

Threads 1,343,343
Members 515,022
Posts 32,781,535
Top