darcity

JF-Expert Member
Jul 20, 2009
8,700
16,851
Nashauri serikali imfungulie mashtaka Wakili Msomi Tundu LISSU kwa kutoa taarifa za uongo na kusababisha taharuki kuwa Rais ametekwa/amewekwa mateka na Waziri Mkuu ndiye anaongoza nchi.

Hata Kama yupo nje ya nchi anapaswa kuheshimu uhuru wa maoni.

Mara nyingi akihojiwa na vyombo vya habari amekuwa akipotosha taarifa.

Na hii si mara ya kwanza kutoa taarifa hizi. Hata wakati alipohojiwa na BBC alisema hili.
 
Akiongea katika kipindi cha Maria Sarungi Space Jana akijibu maswali mbalimbali ya washiriki wa mjadala huo, Tundu Lissu ametoa taarifa serious kidogo kuhusu Rais na nchi yetu...

Kwamba, taarifa walizonazo kwa sasa ni kuwa "....Madam President Samia Suluhu Hassan is held hostage..." , kwamba si yeye anayeongoza nchi kwa sasa. Ameshauriwa yeye akae pembeni na swala la usalama wa nchi awaachie PM Majaliwa na waziri wa usalama, Mchengelewa washughulike nalo...


MAONI YANGU:

Kama hii ni kweli, kikatiba imekaaje? Kama Rais huyu mama kakubali ushauri huu, atakuwa anajua kweli jukumu na wajibu wake kama Rais wa nchi...? Kwanini washauri wake wakuu wamefanya hivi..? Ni kama vile amefanywa mdoli na wajanja kuuchezea kwa kutumia "udhaifu wa mwanamke" ili wafanye mambo yao..!!

Kuna possibility kubwa hili linaweza kuwa la kweli kwa kuangalia viashiria fulani fulani...

Hebu chunguzeni ziara na matukio ambayo Rais Samia Suluhu anapangiwa kushiriki kwa takribani miezi miwili iliyopita....

Ni yale ya utoto utoto tu ambayo siyo level yake kuyafanya kwani yangeweza kufanywa na wasaidizi wake kama waziri wa sekta husika, RC au DC...

Inashangaza kuwa anajihusisha ktk mambo madogo madogo mno huku akiacha kuumiza akili kushughulika na maswala serious kama vile hali ngumu ya uchumi, tozo kandamizi, hali tete na mbaya ya kisiasa na mengine mengi yanayohusu nchi na wananchi ambayo kwa sasa yanaelea elea hewani tu bila mwongozo thabiti toka kwa Rais kiongozi makini wa nchi...

Angalia matukio anayoshiriki Rais; mfano Royal Tour, kushiriki tamasha la ngoma za kienyeji Magu Mwanza nk nk ni ya kupumbaza tu, yasiyo na positive impact yoyote katika maisha ya watu kwa ujumla. Nyuma ya matukio haya lipo lengo fulani baya nyuma ya pazia. THE TIME WILL TELL...

Naweza kuamini hili la Tundu Lissu kwa 99%...
 
Eti halafu nyinyi ndio mpewe nchi muongoze? Badala ya kushughulika na vitu vya maana mnaendekeza umbea tu.

Nyinyi endeleeni kupiga soga huku CCM inajipanga na mikutano ya mpaka kwenye matawi huko. Mkija mkishtuka ni July 2025, mnachezea kichapo tena ikifika October 2025 mnaanza kujazana ujinga wa muandamane.

Ama kweli CCM itaendelea kutawala for more years to come.

Viva CCM viva Mama Samia Suluhu Hassan.
 
Mswahili hawezi kuendesha nchi maana hana lugha ya moja kwa moja tofauti ni kubwa mno toka kwa Jpm kwenda kwa mama samia,Tulizoea kufanya kazi kwa lugha moja iwe nzuri au mbaya msimamo ulikuwepo ila kwa sasa kauli zina mashaka haziko wazi
 
E-12KwcWQAMlVv8.jpg
 
LISSU anatakiwa mambo mengine akae Kimya yanamshushia credibility, nchi inajulikana anayeongoza ni nani hata Majaliwa hana ubavu huo! Na take over ilifanyika tokea mwezi March 13 ,2021 … LISSU ajichunge sana na Rwehumbiza atamuingiza Chaka kwa baadhi ya Taarifa
 
Back
Top Bottom