COMRADE CHRIS HANI
Member
- Sep 25, 2012
- 63
- 15
Kaka! nashinda nikijiuliza, kwa nini pamoja na utajiri wetu mkubwa wa maliasili(nikijumuisha na nguvukazi ya takribani watu milioni 20) hatujapiga hatua tunayostahili kuwa...kwa nini? nilikuwa rwanda wiki ya juzi, nilichokiona kilithibitisha taarifa za kusifia (hususan za kitakwimu) maendeleo ya kiuchumi na kijamii, ambayo rwanda imeyapata ktk kipindi kisichozidi miongo miwili...rwanda kirasilimali kuilinganisha na jamhuri ya muungano, ni kuionea!...lkn kimaendeleo, ukitazama walivyokuwa miaka 18 iliyopita, na tulivyokuwa sisi ktk miaka hiyo 18....aaah! ni nini siri ya wenzetu wa rwanda...NIDHAMU....!sisi hatuna nidhamu inayotakiwa, ambayo ikichanganywa na rasilimali tulizonazo itatuwezesha kupata maendeleo yanayolingana na utajiri wa raslimali tulizonazo...hatuna nidhamu ya kuendeleza demokrasia ya kweli na ya dhati ktk taifa letu na ndani ya vyama vyetu vya siasa...! hatuna nidhamu ya kutii sheria..mambo yetu ya kukosa nidhamu kiujumla unaweza kuyalinganisha na vitimbi vya madereva wa dalala...!tujirekebishe, sisi sote...wapiga kura, na wapigiwa kura, tuwe na nidhamu inayostahili..kisha tupate maendeleo tunayolingana nayo...HATUNA MAENDELEO TUNAYOSTAHILI SABABU HATUNA NIDHAMU INAYOTAKIWA KITAIFA , KUPATA MAENDELEO YANAYOLINGANA NA UTAJIRI NA RASLIMALI TULIZONAZO...HATA AJE NANI KIUONGOZI, BILA KUWA NA NIDHAMU....BURE!!!!....lord almight....guide and guards all the inhabitants of this part of "mama africa" towards nothing short than deserved displine needed for our political, economical, and social progress and development...