Uchaguzi 2020 Kwanini Vyama vya Upinzani nchini Tanzania vimeanguka vibaya sana katika Uchaguzi Mkuu wa Rais, wabunge na madiwani

Kwanini upinzani umeanguka vibaya:

1) Hakuna Mtanzania yeyote anayeweza kuchagua mbunge ambaye anashauri mashirika ya fedha na wadau wa maendeleo wasiipe fedha Tanzania kwa ajili ya ujenzi wa nchi yetu, hili liwe funzo watu wabishane kwa hoja lakini si kuchoma nyumba tunayoishi sote.

2) Hakuna Mtanzania anayeweza kuchagua mbunge ambaye hadi leo anaamini Corona ipo na akili zake ni kufanya lockdown, nasema Watanzania hawako tayari kwa hilo kabisa.

3) Hakuna Mtanzania anayeweza kukipigia kura chama kilichojipambanua wazi kwamba kitaweka rehani rasilimari za nchi yetu kama mafuta, madini, gesi na mbuga ili kuweza kukopa fedha nje kwa ajili ya kuleta maendeleo hapa nchini, watu wanaogopa kuweka rehani nyumba zao sembuse mali za nchi, hii ni sera mbovu sana kuwahi kutokea.

4) Hakuna Mtanzania ambaye anaweza kukubali kukipigia chama kinachopanga kubinafsisha miradi ya kimkakati kama Bwawa la Umeme, SGR inayoendelea kujengwa na kuwapa watu binafsi ambao ni wao wenyewe, tumeshatoka huko na hatutaki kurudi tena kwenye ujinga huo. Being there done that no turning back.

5) Hakuna Mtanzania ambaye anaweza kuchagua chama kinachotaka kuzidi kufukarisha maskini kwa kurasimisha madalali kama kangomba, chama cha ACT kiliifanya hii kuwa sera yao kuu kwenye uchaguzi huu, na wananchi wameweza kuwajibu vizuri.

6) Wananchi wanapenda viongozi wenye hofu ya Mungu sio wale viongozi wanaobeza kumtegemea Mungu kama Tundu Lissu alivyokuwa anajidai kutumia science ya kuiga kuthibiti Corona huku akikejeri wito wa maombi uliotolewa na Mheshimiwa Rais Magufuli, akidai Mungu yuko busy hawezi dili na upuuzi huo. Bado aliacha kuvaa barakoa pamoja na matusi yake yote na kukusanya watu bila kujali taratibu za kujikinga na Corona.

7) Hakuna Mtanzania anayeweza kumchagua mbunge ambae anapinga na hana wazo la kuwajengea Wananchi Hospitali, Bandari, Meli, Barabara, Umeme, Maji, Kilimo, Shule bure, na mengine kama hayo, hakuna kabisa. Hivi wao wanaviita ni vitu na si maendeleo ya watu kwahiyo kwao havina maana wakati wananchi wanavitaka.

8) Wananchi wanapenda vitu vinavyowatatiza viongelewe na vipewe suluhu, sasa wapinzani wanapoongelea kuwapa wananchi uhuru, sera ngumu sana kueleweka kwasababu watu wako huru unawezaje kuwaahidi uhuru, uhuru upi wa kutukana matusi ama upi, kwahiyo hapa upinzani hawakuwa na agenda ya msingi na walipoteza muda mwingi kulihubiri hili kumbe ni tatizo lililopo vichwani mwao tu na wananchi wameshindwa kuwaelewa.

9) Kulikuwa kuna tofauti kubwa sana ya kuhubiri ilani, mgombea wa CCM alikuwa akifika sehemu anakuwa anayajua matatizo halisi ya eneo husika, kama ni maji, hospitali, uhitaji wa mji, mambo ya ardhi n.k na amekuwa akiyaongelea hayo matatizo halisi wakati Tundu Lissu ataanza kuongelea uhuru wakati wananchi wa eneo husika wanahitaji Hospital ama shule ama maji, ni ngumu kuchagulika ni ngumu sana. Tunawachagua wanaoyajua matatizo yetu halisi kabisa si matatizo yao kuyafanya ni ya kwetu.

10) Mimi kutomchagua Lissu, Mbowe, Sugu, Msigwa ama Lema hakunisumbui chochote kwa sababu kwanza hawana mahusiano mazuri na serikali, hawawezi kuongea na Rais kwa maana hiyo hawawezi lobby matatizo ya jimbo letu yatatuliwe, kwahiyo ntajisikia vizuri nikiwa na mbunge ambaye ana access na waziri husika na hata Rais inapobidi si mtu ambaye anapayuka na kubwabwaja bila mpango wowote, so napenda nipate mbunge mwenye mahusiano mazuri na viongozi wa serikali ili matatizo yetu yatatuliwe haraka.

Wenu katika ujenzi wa nchi.

Mwanakijiji Mpenda Nchi.

Excellent. Sina la ziada.
 
Ila wa tz wengne Bado hawajatambua thamani ya Uhuru wa0 nA utawAla wa kisheria
NB:-siku zinakuja watalpa thamani ya ujinga wa0 na kuwakumbuka ata kwakusema kitu

Mungu ni weTu sote(Mungu ibark Tz)
 
What a joke! Hata kushangilia unyang'anyi roho zenu zinawasuta. Mko kimya kama mmefiwa:

View attachment 1616743

UKIWAONA HAWA KATIKA MAANDAMANO, ANDAMANA!!
---------------------------------

1. Ukimuona Dudley, mtoto wa kwanza na Freeman Mbowe na wadogo zake wakiongoza maandamano nawe andamana. Freeman Mbowe pekee hatoshi, yeye hawezi kupigwa risasi hata moja. Nafasi yake ya Uenyekiti wa Chama kikuu cha Upinzani nchini inamlinda, ni jicho la Dunia anatazamwa, hakuna risasi inayoweza kuelekezwa kwake hata moja. Pale Mkwajuni Kinondoni risasi ilimkwepa Mbowe ikamuua Akwiline Akwelina. Wazazi wake wanalia hadi sasa, hakuna kitu. Usipowaona watoto wa Freeman Mbowe usiandamane!!

2. Ukimuona Alicia Magabe na watoto wake wa damu andamana. Alicia ni mke wa Tundu Lissu ambae Urais wa Lissu unamhusu zaidi kuliko mimi na wewe. Ukimuona Tundu Lissu peke yake usidanganyike kuandamana. Lissu ndie aliegombea Urais kwa Chama kikuu cha upinzani akiungwa mkono na ACT Wazalendo, huyu ni icon ya uchaguzi, ndie mwanamkakati ktk maandano hayo. Dunia yote ipo kwake, akifa hakuna cha kujificha, mission INATIKI.

Hakuna Askari mpumbavu anaweza kulenga shabaha ktk mwili wa Lissu, risasi zitaelekezwa kwako. Utakufa na si ajabu usifahamike, taarifa zako hazitofika popote, utakufa kama Mbwa, utazikwa siku inayofuata ktk kabuli la futi mbili au usizikwe kabisa. Usipomuona Alicia na wanawe, usiandamane!!

3. Ukimuona Bi Fourtuna Salehe na Bi Aweina Sinani na watoto wao katika maandamano andamana. Hii ni familia ya Maalim Seif ambayo inasemwa kuwa imepelekwa Oman mafichoni tayari. Wanasema watu wameuawa Zanzibar lkn hakuna jina la mtoto wa Maalim Seif wala wa mtoto wa Jussa hata moja. Usiwe mjinga, hukuzaliwa kuwa chambo, hukuzaliwa kwa ajili ya Urais wa Maalim au Lissu. Wakiwa Marais wewe haitokusaidia chochote. Usipomuona mtoto wa Maalim Seif, wake zake na familia yake jilalie zako nyumbani hauna cha kupoteza.

4. Ukimuona Anna Bwana, Wiza na Josina ktk maandamano yaliyoitishwa na wewe ungana nao, andamana kwa moyo mkunjufu kabisa. Hii ni familia ya Zitto Kabwe, akiwa peke yake muache aendelee na kazi yake. Zitto Kabwe ni Kiongozi wa Chama cha upinzani (KC), ni jicho la Dunia hawezi kupigwa risasi taratibu za kuzuia maandamano zinamtambua na kumlinda. Usipomuona mke wake, watoto na ndugu zake wengine achana na kazi hiyo haina faida itakupeleka kuzimu bure.

5. Ukimuona Askofu Bagonza na mkewe, na watoto wake wote ktk maandamano andamana. Akiwa peke yake muombee kwa Mungu, usijiunge nae. Ukimuona Lema na watoto wake, Sugu na mke wake na watoto zake, Msigwa na wadogo zake kutoka Iringa, Heche na mkewe na watoto wake andamana.
Ukiwaona wao peke yao usiandamane, Ubunge na Urais wao hauna maana yoyote kwako. Maisha yako ni ya kwako peke yako, pambana!!
#USIANDAMANE!!
 
Hili tanga
Tangazo la hii poster ni la kubumba tu, chanzo chake siyo sahihi maana CHANNEL 10 walishalikataa kuwa siyo la kwao. Nimeona hata ma activists wengi wa mtandaoni kama akina Kigogo, Karume, Sarungi na wapinzani wengi wameruka nalo sana na kudai ni la kweli. Ila ukweli ni kwamba hata wewe unaweza kutengeneza poster kama hii na ikaenda sana VIRAL kwenye social medias.

Acheni kudanganya umma.
 
Anayekulipa kufanya propaganda za kumtetea shetani mwambie wamekataa. Amri za Mungu na sheria za nchi zinakataza wizi. Wewe unakuja hapa unatetea unyang'anyi na wizi na kutisha watu. Kama siyo shetani wewe ni nani. Hata pale busitanini Hawa hakujua kuwa naongea na shetani. Alifikiri anaongea na nyoka. Lo and behold! The rest is history. CCM haina legitimacy tena. Mmebaki na matumizi ya nguvu na vitisho na mauaji tu.
UKIWAONA HAWA KATIKA MAANDAMANO, ANDAMANA!!
---------------------------------

1. Ukimuona Dudley, mtoto wa kwanza na Freeman Mbowe na wadogo zake wakiongoza maandamano nawe andamana. Freeman Mbowe pekee hatoshi, yeye hawezi kupigwa risasi hata moja. Nafasi yake ya Uenyekiti wa Chama kikuu cha Upinzani nchini inamlinda, ni jicho la Dunia anatazamwa, hakuna risasi inayoweza kuelekezwa kwake hata moja. Pale Mkwajuni Kinondoni risasi ilimkwepa Mbowe ikamuua Akwiline Akwelina. Wazazi wake wanalia hadi sasa, hakuna kitu. Usipowaona watoto wa Freeman Mbowe usiandamane!!

2. Ukimuona Alicia Magabe na watoto wake wa damu andamana. Alicia ni mke wa Tundu Lissu ambae Urais wa Lissu unamhusu zaidi kuliko mimi na wewe. Ukimuona Tundu Lissu peke yake usidanganyike kuandamana. Lissu ndie aliegombea Urais kwa Chama kikuu cha upinzani akiungwa mkono na ACT Wazalendo, huyu ni icon ya uchaguzi, ndie mwanamkakati ktk maandano hayo. Dunia yote ipo kwake, akifa hakuna cha kujificha, mission INATIKI.

Hakuna Askari mpumbavu anaweza kulenga shabaha ktk mwili wa Lissu, risasi zitaelekezwa kwako. Utakufa na si ajabu usifahamike, taarifa zako hazitofika popote, utakufa kama Mbwa, utazikwa siku inayofuata ktk kabuli la futi mbili au usizikwe kabisa. Usipomuona Alicia na wanawe, usiandamane!!

3. Ukimuona Bi Fourtuna Salehe na Bi Aweina Sinani na watoto wao katika maandamano andamana. Hii ni familia ya Maalim Seif ambayo inasemwa kuwa imepelekwa Oman mafichoni tayari. Wanasema watu wameuawa Zanzibar lkn hakuna jina la mtoto wa Maalim Seif wala wa mtoto wa Jussa hata moja. Usiwe mjinga, hukuzaliwa kuwa chambo, hukuzaliwa kwa ajili ya Urais wa Maalim au Lissu. Wakiwa Marais wewe haitokusaidia chochote. Usipomuona mtoto wa Maalim Seif, wake zake na familia yake jilalie zako nyumbani hauna cha kupoteza.

4. Ukimuona Anna Bwana, Wiza na Josina ktk maandamano yaliyoitishwa na wewe ungana nao, andamana kwa moyo mkunjufu kabisa. Hii ni familia ya Zitto Kabwe, akiwa peke yake muache aendelee na kazi yake. Zitto Kabwe ni Kiongozi wa Chama cha upinzani (KC), ni jicho la Dunia hawezi kupigwa risasi taratibu za kuzuia maandamano zinamtambua na kumlinda. Usipomuona mke wake, watoto na ndugu zake wengine achana na kazi hiyo haina faida itakupeleka kuzimu bure.

5. Ukimuona Askofu Bagonza na mkewe, na watoto wake wote ktk maandamano andamana. Akiwa peke yake muombee kwa Mungu, usijiunge nae. Ukimuona Lema na watoto wake, Sugu na mke wake na watoto zake, Msigwa na wadogo zake kutoka Iringa, Heche na mkewe na watoto wake andamana.
Ukiwaona wao peke yao usiandamane, Ubunge na Urais wao hauna maana yoyote kwako. Maisha yako ni ya kwako peke yako, pambana!!
#USIANDAMANE!!
 
Kwanini upinzani umeanguka vibaya:

1) Hakuna Mtanzania yeyote anayeweza kuchagua mbunge ambaye anashauri mashirika ya fedha na wadau wa maendeleo wasiipe fedha Tanzania kwa ajili ya ujenzi wa nchi yetu, hili liwe funzo watu wabishane kwa hoja lakini si kuchoma nyumba tunayoishi sote.

2) Hakuna Mtanzania anayeweza kuchagua mbunge ambaye hadi leo anaamini Corona ipo na akili zake ni kufanya lockdown, nasema Watanzania hawako tayari kwa hilo kabisa.

3) Hakuna Mtanzania anayeweza kukipigia kura chama kilichojipambanua wazi kwamba kitaweka rehani rasilimari za nchi yetu kama mafuta, madini, gesi na mbuga ili kuweza kukopa fedha nje kwa ajili ya kuleta maendeleo hapa nchini, watu wanaogopa kuweka rehani nyumba zao sembuse mali za nchi, hii ni sera mbovu sana kuwahi kutokea.

4) Hakuna Mtanzania ambaye anaweza kukubali kukipigia chama kinachopanga kubinafsisha miradi ya kimkakati kama Bwawa la Umeme, SGR inayoendelea kujengwa na kuwapa watu binafsi ambao ni wao wenyewe, tumeshatoka huko na hatutaki kurudi tena kwenye ujinga huo. Being there done that no turning back.

5) Hakuna Mtanzania ambaye anaweza kuchagua chama kinachotaka kuzidi kufukarisha maskini kwa kurasimisha madalali kama kangomba, chama cha ACT kiliifanya hii kuwa sera yao kuu kwenye uchaguzi huu, na wananchi wameweza kuwajibu vizuri.

6) Wananchi wanapenda viongozi wenye hofu ya Mungu sio wale viongozi wanaobeza kumtegemea Mungu kama Tundu Lissu alivyokuwa anajidai kutumia science ya kuiga kuthibiti Corona huku akikejeri wito wa maombi uliotolewa na Mheshimiwa Rais Magufuli, akidai Mungu yuko busy hawezi dili na upuuzi huo. Bado aliacha kuvaa barakoa pamoja na matusi yake yote na kukusanya watu bila kujali taratibu za kujikinga na Corona.

7) Hakuna Mtanzania anayeweza kumchagua mbunge ambae anapinga na hana wazo la kuwajengea Wananchi Hospitali, Bandari, Meli, Barabara, Umeme, Maji, Kilimo, Shule bure, na mengine kama hayo, hakuna kabisa. Hivi wao wanaviita ni vitu na si maendeleo ya watu kwahiyo kwao havina maana wakati wananchi wanavitaka.

8) Wananchi wanapenda vitu vinavyowatatiza viongelewe na vipewe suluhu, sasa wapinzani wanapoongelea kuwapa wananchi uhuru, sera ngumu sana kueleweka kwasababu watu wako huru unawezaje kuwaahidi uhuru, uhuru upi wa kutukana matusi ama upi, kwahiyo hapa upinzani hawakuwa na agenda ya msingi na walipoteza muda mwingi kulihubiri hili kumbe ni tatizo lililopo vichwani mwao tu na wananchi wameshindwa kuwaelewa.

9) Kulikuwa kuna tofauti kubwa sana ya kuhubiri ilani, mgombea wa CCM alikuwa akifika sehemu anakuwa anayajua matatizo halisi ya eneo husika, kama ni maji, hospitali, uhitaji wa mji, mambo ya ardhi n.k na amekuwa akiyaongelea hayo matatizo halisi wakati Tundu Lissu ataanza kuongelea uhuru wakati wananchi wa eneo husika wanahitaji Hospital ama shule ama maji, ni ngumu kuchagulika ni ngumu sana. Tunawachagua wanaoyajua matatizo yetu halisi kabisa si matatizo yao kuyafanya ni ya kwetu.

10) Mimi kutomchagua Lissu, Mbowe, Sugu, Msigwa ama Lema hakunisumbui chochote kwa sababu kwanza hawana mahusiano mazuri na serikali, hawawezi kuongea na Rais kwa maana hiyo hawawezi lobby matatizo ya jimbo letu yatatuliwe, kwahiyo ntajisikia vizuri nikiwa na mbunge ambaye ana access na waziri husika na hata Rais inapobidi si mtu ambaye anapayuka na kubwabwaja bila mpango wowote, so napenda nipate mbunge mwenye mahusiano mazuri na viongozi wa serikali ili matatizo yetu yatatuliwe haraka.

Wenu katika ujenzi wa nchi.

Mwanakijiji Mpenda Nchi.
Dah...mie nadhani Hawa mbogamboga na tunguri zilitumika pia....kuna best wangu mmoja pingapinga sana...Ila alivyotoka kupiga kura akaniambia nimeona nimpe tu Jiwe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuanzia sasa kutakuwa na nyuzi nyingi kama huu ili kuwaondoa watu katika uhalisia wa mambo
Hawa wametumwa kubadili maongezi ili kuficha uharamia uliofanyika

CCM kushinda si tatizo, kinacholitia huzuni Taifa ni uharamia uliofanyika tena bila hata chembe ya akili.

Hoja iliyopo mbele ni jinsi ambavyo uchaguzi umegeuzwa kuwa uchafuzi na kulitia Taifa hasara

Kilichofanyika ni kutimiza kauli ya kufuta upinzani na imetekelezwa kwa kauli ya kupewa gari na mshahara halafu utangaze mpinzani. Tunajua , watanzania wanajua na Taifa lina huzuni, si matokeo bali uchafu uliofanyika

Chuki iliyojitokeza inatisha kuliko kishindo cha kushinda au kushindwa.
Maendeleo yanatoka wapi katika chuki, huzuni na mgawanyiko uliopo?

JokaKuu Mag3 tindo

Kula tano boss wangu.
 
Kumbukeni Mnyika alilia kujua karatasi za kupigia kura zimechapishiwa wapi na kudai wapewe kopi na hawa kupewa, dhumuni ni ili wakafeki na hizo feki walizozionyesha kwenye press yao hawawezi hata kupeleka police zikalinganishwe wanajua hilo
Ukweli uchaguzi huu wapinzani wamepigika kikwelikweli ndiyo maana wanahaha kwani ulikuwa wa wazi kiasi kwamba hata kura yako yaweza kufuatiliwa kujua ulimpigia nani hatumwagi ubuyu ila kama beberu ana dau basi twende kwenye mkeka
Wamshindwa vibaya kihistoria
 
Mleta mada unataka kutuambia kabisa nafsi yako haikuhukumu kwa haya uliyoandika hapa. Yaani hujui kwa nini hawakushinda wakati kila kitu kiko wazi. Mimi si mshabiki wa chama na haitatokea. Kwenye ukweli tuseme ukweli. Hata raisi aliyechaguliwa anasema msema ukweli ni mpenzi wa Mungu. Sasa ninakuuliza wewe ni mpenzi wa Mungu au wa shetani. Jibu unalo wewe kutoka kwenye nafsi yako. Tufike mahali tuache mihemko ya kisiasa tuwe wa kweli na tuseme ukweli. Yanayoendelea hapa kwetu tungekuwa wa kweli kila mtu angekuwa na amani. Unfrtunately amani imetoweka kwa wengi na chuki inaongezeka kwa wengi. Mungu tunakuomba ponya nchi yetu na uponye mioyo ya watu walioumizwa na haya matokeo ya uchaguzi.
 
Kwanini upinzani umeanguka vibaya:

1) Hakuna Mtanzania yeyote anayeweza kuchagua mbunge ambaye anashauri mashirika ya fedha na wadau wa maendeleo wasiipe fedha Tanzania kwa ajili ya ujenzi wa nchi yetu, hili liwe funzo watu wabishane kwa hoja lakini si kuchoma nyumba tunayoishi sote.

2) Hakuna Mtanzania anayeweza kuchagua mbunge ambaye hadi leo anaamini Corona ipo na akili zake ni kufanya lockdown, nasema Watanzania hawako tayari kwa hilo kabisa.

3) Hakuna Mtanzania anayeweza kukipigia kura chama kilichojipambanua wazi kwamba kitaweka rehani rasilimari za nchi yetu kama mafuta, madini, gesi na mbuga ili kuweza kukopa fedha nje kwa ajili ya kuleta maendeleo hapa nchini, watu wanaogopa kuweka rehani nyumba zao sembuse mali za nchi, hii ni sera mbovu sana kuwahi kutokea.

4) Hakuna Mtanzania ambaye anaweza kukubali kukipigia chama kinachopanga kubinafsisha miradi ya kimkakati kama Bwawa la Umeme, SGR inayoendelea kujengwa na kuwapa watu binafsi ambao ni wao wenyewe, tumeshatoka huko na hatutaki kurudi tena kwenye ujinga huo. Being there done that no turning back.

5) Hakuna Mtanzania ambaye anaweza kuchagua chama kinachotaka kuzidi kufukarisha maskini kwa kurasimisha madalali kama kangomba, chama cha ACT kiliifanya hii kuwa sera yao kuu kwenye uchaguzi huu, na wananchi wameweza kuwajibu vizuri.

6) Wananchi wanapenda viongozi wenye hofu ya Mungu sio wale viongozi wanaobeza kumtegemea Mungu kama Tundu Lissu alivyokuwa anajidai kutumia science ya kuiga kuthibiti Corona huku akikejeri wito wa maombi uliotolewa na Mheshimiwa Rais Magufuli, akidai Mungu yuko busy hawezi dili na upuuzi huo. Bado aliacha kuvaa barakoa pamoja na matusi yake yote na kukusanya watu bila kujali taratibu za kujikinga na Corona.

7) Hakuna Mtanzania anayeweza kumchagua mbunge ambae anapinga na hana wazo la kuwajengea Wananchi Hospitali, Bandari, Meli, Barabara, Umeme, Maji, Kilimo, Shule bure, na mengine kama hayo, hakuna kabisa. Hivi wao wanaviita ni vitu na si maendeleo ya watu kwahiyo kwao havina maana wakati wananchi wanavitaka.

8) Wananchi wanapenda vitu vinavyowatatiza viongelewe na vipewe suluhu, sasa wapinzani wanapoongelea kuwapa wananchi uhuru, sera ngumu sana kueleweka kwasababu watu wako huru unawezaje kuwaahidi uhuru, uhuru upi wa kutukana matusi ama upi, kwahiyo hapa upinzani hawakuwa na agenda ya msingi na walipoteza muda mwingi kulihubiri hili kumbe ni tatizo lililopo vichwani mwao tu na wananchi wameshindwa kuwaelewa.

9) Kulikuwa kuna tofauti kubwa sana ya kuhubiri ilani, mgombea wa CCM alikuwa akifika sehemu anakuwa anayajua matatizo halisi ya eneo husika, kama ni maji, hospitali, uhitaji wa mji, mambo ya ardhi n.k na amekuwa akiyaongelea hayo matatizo halisi wakati Tundu Lissu ataanza kuongelea uhuru wakati wananchi wa eneo husika wanahitaji Hospital ama shule ama maji, ni ngumu kuchagulika ni ngumu sana. Tunawachagua wanaoyajua matatizo yetu halisi kabisa si matatizo yao kuyafanya ni ya kwetu.

10) Mimi kutomchagua Lissu, Mbowe, Sugu, Msigwa ama Lema hakunisumbui chochote kwa sababu kwanza hawana mahusiano mazuri na serikali, hawawezi kuongea na Rais kwa maana hiyo hawawezi lobby matatizo ya jimbo letu yatatuliwe, kwahiyo ntajisikia vizuri nikiwa na mbunge ambaye ana access na waziri husika na hata Rais inapobidi si mtu ambaye anapayuka na kubwabwaja bila mpango wowote, so napenda nipate mbunge mwenye mahusiano mazuri na viongozi wa serikali ili matatizo yetu yatatuliwe haraka.

Wenu katika ujenzi wa nchi.

Mwanakijiji Mpenda Nchi.

Kwanini upinzani umeanguka vibaya:

1) Hakuna Mtanzania yeyote anayeweza kuchagua mbunge ambaye anashauri mashirika ya fedha na wadau wa maendeleo wasiipe fedha Tanzania kwa ajili ya ujenzi wa nchi yetu, hili liwe funzo watu wabishane kwa hoja lakini si kuchoma nyumba tunayoishi sote.

2) Hakuna Mtanzania anayeweza kuchagua mbunge ambaye hadi leo anaamini Corona ipo na akili zake ni kufanya lockdown, nasema Watanzania hawako tayari kwa hilo kabisa.

3) Hakuna Mtanzania anayeweza kukipigia kura chama kilichojipambanua wazi kwamba kitaweka rehani rasilimari za nchi yetu kama mafuta, madini, gesi na mbuga ili kuweza kukopa fedha nje kwa ajili ya kuleta maendeleo hapa nchini, watu wanaogopa kuweka rehani nyumba zao sembuse mali za nchi, hii ni sera mbovu sana kuwahi kutokea.

4) Hakuna Mtanzania ambaye anaweza kukubali kukipigia chama kinachopanga kubinafsisha miradi ya kimkakati kama Bwawa la Umeme, SGR inayoendelea kujengwa na kuwapa watu binafsi ambao ni wao wenyewe, tumeshatoka huko na hatutaki kurudi tena kwenye ujinga huo. Being there done that no turning back.

5) Hakuna Mtanzania ambaye anaweza kuchagua chama kinachotaka kuzidi kufukarisha maskini kwa kurasimisha madalali kama kangomba, chama cha ACT kiliifanya hii kuwa sera yao kuu kwenye uchaguzi huu, na wananchi wameweza kuwajibu vizuri.

6) Wananchi wanapenda viongozi wenye hofu ya Mungu sio wale viongozi wanaobeza kumtegemea Mungu kama Tundu Lissu alivyokuwa anajidai kutumia science ya kuiga kuthibiti Corona huku akikejeri wito wa maombi uliotolewa na Mheshimiwa Rais Magufuli, akidai Mungu yuko busy hawezi dili na upuuzi huo. Bado aliacha kuvaa barakoa pamoja na matusi yake yote na kukusanya watu bila kujali taratibu za kujikinga na Corona.

7) Hakuna Mtanzania anayeweza kumchagua mbunge ambae anapinga na hana wazo la kuwajengea Wananchi Hospitali, Bandari, Meli, Barabara, Umeme, Maji, Kilimo, Shule bure, na mengine kama hayo, hakuna kabisa. Hivi wao wanaviita ni vitu na si maendeleo ya watu kwahiyo kwao havina maana wakati wananchi wanavitaka.

8) Wananchi wanapenda vitu vinavyowatatiza viongelewe na vipewe suluhu, sasa wapinzani wanapoongelea kuwapa wananchi uhuru, sera ngumu sana kueleweka kwasababu watu wako huru unawezaje kuwaahidi uhuru, uhuru upi wa kutukana matusi ama upi, kwahiyo hapa upinzani hawakuwa na agenda ya msingi na walipoteza muda mwingi kulihubiri hili kumbe ni tatizo lililopo vichwani mwao tu na wananchi wameshindwa kuwaelewa.

9) Kulikuwa kuna tofauti kubwa sana ya kuhubiri ilani, mgombea wa CCM alikuwa akifika sehemu anakuwa anayajua matatizo halisi ya eneo husika, kama ni maji, hospitali, uhitaji wa mji, mambo ya ardhi n.k na amekuwa akiyaongelea hayo matatizo halisi wakati Tundu Lissu ataanza kuongelea uhuru wakati wananchi wa eneo husika wanahitaji Hospital ama shule ama maji, ni ngumu kuchagulika ni ngumu sana. Tunawachagua wanaoyajua matatizo yetu halisi kabisa si matatizo yao kuyafanya ni ya kwetu.

10) Mimi kutomchagua Lissu, Mbowe, Sugu, Msigwa ama Lema hakunisumbui chochote kwa sababu kwanza hawana mahusiano mazuri na serikali, hawawezi kuongea na Rais kwa maana hiyo hawawezi lobby matatizo ya jimbo letu yatatuliwe, kwahiyo ntajisikia vizuri nikiwa na mbunge ambaye ana access na waziri husika na hata Rais inapobidi si mtu ambaye anapayuka na kubwabwaja bila mpango wowote, so napenda nipate mbunge mwenye mahusiano mazuri na viongozi wa serikali ili matatizo yetu yatatuliwe haraka.

Wenu katika ujenzi wa nchi.

Mwanakijiji Mpenda Nchi.
Upumbavu wako peleka kwa mumeo.
 
Yani chadema nawafananisha na harakati za pimbi. muda Sana hapa jukwani nilishasema majimbo yote yaliyowahi kushikwa na upinzani kwa miaka minji wananchi wake waliwashitukia jamaa si watu watu wazuri

Nakilichotokea Ni hili ambalo hata mla konyagi hamini,anatetemeka wapi ataendeleza makulaji
 
Back
Top Bottom