Uchaguzi 2020 Kwanini Vyama vya Upinzani nchini Tanzania vimeanguka vibaya sana katika Uchaguzi Mkuu wa Rais, wabunge na madiwani

May 16, 2020
96
150
Kwanini upinzani umeanguka vibaya:

1) Hakuna Mtanzania yeyote anayeweza kuchagua mbunge ambaye anashauri mashirika ya fedha na wadau wa maendeleo wasiipe fedha Tanzania kwa ajili ya ujenzi wa nchi yetu, hili liwe funzo watu wabishane kwa hoja lakini si kuchoma nyumba tunayoishi sote.

2) Hakuna Mtanzania anayeweza kuchagua mbunge ambaye hadi leo anaamini Corona ipo na akili zake ni kufanya lockdown, nasema Watanzania hawako tayari kwa hilo kabisa.

3) Hakuna Mtanzania anayeweza kukipigia kura chama kilichojipambanua wazi kwamba kitaweka rehani rasilimari za nchi yetu kama mafuta, madini, gesi na mbuga ili kuweza kukopa fedha nje kwa ajili ya kuleta maendeleo hapa nchini, watu wanaogopa kuweka rehani nyumba zao sembuse mali za nchi, hii ni sera mbovu sana kuwahi kutokea.

4) Hakuna Mtanzania ambaye anaweza kukubali kukipigia chama kinachopanga kubinafsisha miradi ya kimkakati kama Bwawa la Umeme, SGR inayoendelea kujengwa na kuwapa watu binafsi ambao ni wao wenyewe, tumeshatoka huko na hatutaki kurudi tena kwenye ujinga huo. Being there done that no turning back.

5) Hakuna Mtanzania ambaye anaweza kuchagua chama kinachotaka kuzidi kufukarisha maskini kwa kurasimisha madalali kama kangomba, chama cha ACT kiliifanya hii kuwa sera yao kuu kwenye uchaguzi huu, na wananchi wameweza kuwajibu vizuri.

6) Wananchi wanapenda viongozi wenye hofu ya Mungu sio wale viongozi wanaobeza kumtegemea Mungu kama Tundu Lissu alivyokuwa anajidai kutumia science ya kuiga kuthibiti Corona huku akikejeri wito wa maombi uliotolewa na Mheshimiwa Rais Magufuli, akidai Mungu yuko busy hawezi dili na upuuzi huo. Bado aliacha kuvaa barakoa pamoja na matusi yake yote na kukusanya watu bila kujali taratibu za kujikinga na Corona.

7) Hakuna Mtanzania anayeweza kumchagua mbunge ambae anapinga na hana wazo la kuwajengea Wananchi Hospitali, Bandari, Meli, Barabara, Umeme, Maji, Kilimo, Shule bure, na mengine kama hayo, hakuna kabisa. Hivi wao wanaviita ni vitu na si maendeleo ya watu kwahiyo kwao havina maana wakati wananchi wanavitaka.

8) Wananchi wanapenda vitu vinavyowatatiza viongelewe na vipewe suluhu, sasa wapinzani wanapoongelea kuwapa wananchi uhuru, sera ngumu sana kueleweka kwasababu watu wako huru unawezaje kuwaahidi uhuru, uhuru upi wa kutukana matusi ama upi, kwahiyo hapa upinzani hawakuwa na agenda ya msingi na walipoteza muda mwingi kulihubiri hili kumbe ni tatizo lililopo vichwani mwao tu na wananchi wameshindwa kuwaelewa.

9) Kulikuwa kuna tofauti kubwa sana ya kuhubiri ilani, mgombea wa CCM alikuwa akifika sehemu anakuwa anayajua matatizo halisi ya eneo husika, kama ni maji, hospitali, uhitaji wa mji, mambo ya ardhi n.k na amekuwa akiyaongelea hayo matatizo halisi wakati Tundu Lissu ataanza kuongelea uhuru wakati wananchi wa eneo husika wanahitaji Hospital ama shule ama maji, ni ngumu kuchagulika ni ngumu sana. Tunawachagua wanaoyajua matatizo yetu halisi kabisa si matatizo yao kuyafanya ni ya kwetu.

10) Mimi kutomchagua Lissu, Mbowe, Sugu, Msigwa ama Lema hakunisumbui chochote kwa sababu kwanza hawana mahusiano mazuri na serikali, hawawezi kuongea na Rais kwa maana hiyo hawawezi lobby matatizo ya jimbo letu yatatuliwe, kwahiyo ntajisikia vizuri nikiwa na mbunge ambaye ana access na waziri husika na hata Rais inapobidi si mtu ambaye anapayuka na kubwabwaja bila mpango wowote, so napenda nipate mbunge mwenye mahusiano mazuri na viongozi wa serikali ili matatizo yetu yatatuliwe haraka.

Wenu katika ujenzi wa nchi.

Mwanakijiji Mpenda Nchi.
 

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
4,645
2,000
Nikulipe mshahara! Nikujazie mafuta ya gari! Halafu umtangaze mpinzani! Hii ndiyo siri ya mafanikio. Huku Neccm na policcm wakitimiza wajibu wao ipasavyo!

Vyombo vya habari na NGO's kupigwa mkwara mzito iwapo watawapa nafasi wapinzani kufanya siasa, nk.
 

dikteta2020

JF-Expert Member
Aug 14, 2018
585
1,000
Tanzania imeonekana kuwa ni nchi ya kipumbavu sana maana wameachiwa wajisimamie wenyewe uchaguzi lakini matokeo yake wameshindwa kabisa na hivyo inahitaji kusimamiwa zaidi hata ya ilivyokuwa awali kwakuwa haijaweza bado kujitawala.

Hatua kali sana zitakazochukuliwa dhidi ya Tanzania zitakuwa na mabadiliko makubwa. Na mimi naziunga mkono na nimeshaanza kuwachukulia hatua kali mashabiki wa Magufuli. Kucheka na mpumbavu ni upumbavu zaidi.
 

kindafu

JF-Expert Member
Nov 12, 2010
1,291
2,000
Kwanini upinzani umeanguka vibaya:

1) Hakuna Mtanzania yeyote anayeweza kuchagua mbunge ambaye anashauri mashirika ya fedha na wadau wa maendeleo wasiipe fedha Tanzania kwa ajili ya ujenzi wa nchi yetu, hili liwe funzo watu wabishane kwa hoja lakini si kuchoma nyumba tunayoishi sote.

Acha kujivika upofu! Watanzania hawaja wachagua, bali DOLA imewabeba kwa lazima na tena kwa ushamba mkubwa ambao kila mtu kaushtukia! Hata CCM wenyewe huko mitaani hawaamini kuambiwa wameshinda! Halafu tukiitwa SHITHOLE COUNTRY na wewe utakuwa wa kwanza kutoa povu! Aibu sana!
 
Jun 8, 2020
20
45
Kwanini upinzani umeanguka vibaya:

1) Hakuna Mtanzania yeyote anayeweza kuchagua mbunge ambaye anashauri mashirika ya fedha na wadau wa maendeleo wasiipe fedha Tanzania kwa ajili ya ujenzi wa nchi yetu, hili liwe funzo watu wabishane kwa hoja lakini si kuchoma nyumba tunayoishi sote.
Usijifu una mbio msifu na anayekukimbiza, na debate bila opponent ni ngonjera.
 

CHIBURABANU

JF-Expert Member
Sep 19, 2013
764
1,000
Kwanini upinzani umeanguka vibaya:

1) Hakuna Mtanzania yeyote anayeweza kuchagua mbunge ambaye anashauri mashirika ya fedha na wadau wa maendeleo wasiipe fedha Tanzania kwa ajili ya ujenzi wa nchi yetu, hili liwe funzo watu wabishane kwa hoja lakini si kuchoma nyumba tunayoishi sote...
Umesahau kuweka no yako ya simu halo chini boss.
Uteuzi unaanza Monday.
 

Graph Theory

JF-Expert Member
Jul 2, 2011
4,720
2,000
Screenshot_20201030-111116.png


Pia
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom