Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 74,891
- 155,891
Twiga ni mnyama legelege, mzuri anayevutia lakini hafaidiki na uzuri wake. Mrefu, anaona mbali na anaishia kuona tu.
Kwa kweli utambulisho wowote unaoamua ukutambulishe utabeba taswira na tabia yako.
Tanzania ni taifa ambalo ni legelege, haliko aggressive kwa lolote. Watu wake ni masikini, elimu duni lakini lina utajiri wa kutisha.
Tunamtumia twiga kujitambulisha, twiga yuko taratibu sana kwenye kujongea. Na sisi maendeleo yetu kwenye kila sekta ni ya taratibu sana. Usiwasikilize wanasiasa wanaosema tuko kwenye uchimi wa chini wa kati, jiangalie wewe binafsi.
Twiga na ukubwa na urefu wake hayumo hata kwenye the big five. Kwanini hatukutumia mnyama kama Simba, au ndege tai, au hata tembo?
Bora tungemtumia nyegere (honey badger) mnyama mbishi, mbabe, ambaye akiwa na jambo lake halali mpaka amelitimiza, mnyama asiyeogopa chochote duniani.
Kwa kumtumia twiga tumekuwa kama mwanamke mzuri asiyekuwa na akili, zinazoumia ni sehemu zake za siri. Sisi na uzuri wetu na utajiri wa rasilimali tulionao, hatutaki kujitaabisha kuzibadilisha rasilimali zetu kuwa pesa, tunataka pesa za mikopo na misada (hii ni sifa ya ma slay queen) wapige tu mizinga.
Twiga Anakula majani ya kwenye miti tu anaacha manyasi mengi ardhini kwasababu anaona uvivu kuinama. Twiga Ni sisi kabisa, tuna visingizio vingi sana vya kutufanya tusifanye kazi.
Ni aibu nchi haina hata mpango wa maendeleo wa miaka 20. Hiyo mipango ya miaka mitano mitano ni upi tumeufanikisha kwa asilimia mia moja?
Tunahitaji mabadiliko makubwa ya kimfumo, ifike mahala wanaoshindwa kutusogeza mbele tuwakatae kwa nguvu zote.
CCM na katiba ya mwaka 1977 vimeshindwa kuboresha hali za wananchi na kukuza uchumi, ni wakati sasa wote tuungane pamoja kuiweka CCM kando.
KAZI NDIO MSINGI WA MAENDELEO. NCHI MASIKINI HAIWEZI KUENDELEA KWA MSINGI WA FEDHA. NCHI MASIKINI HAIWEZI KUJITAWALA KAMA INATEGEMEA MSAADA KUTOKA NCHI ZA NJE- J. K. NYERERE
Hayo ni maneno ya Nyerere yaliandikwa kwenye Uwanja wa Mapinduzi, Uwanja wa Sokoine, kwa aibu ya kusutwa na dhamira CCM wameyafuta maneno hayo.