Sipendezwi na picha halisi ya twiga katika ndege za atcl

Buhaya Empire

Senior Member
Aug 3, 2016
116
299
Habari,

Bila kupoteza muda niseme tu kwamba binafsi kama mtanzania, nakerwa na kuchukizwa sana na picha halisi ya Twiga iliyopo katika mkia wa ndege katika kila ndege ya Shirika la ndege la Tanzania ATCL.

Sipendezwi na uamuzi huo wa kuweka picha halisi ya mnyama (Twiga) isiyokuwa na ubunifu wowote katika wakati huu ambapo dunia imebadilika sana katika matumizi ya nembo za kibiashara.

Kwanini hainipendezi?

1. Picha hiyo imeanza kutumika muda mrefu sana na pamoja na kwamba haina ubunifu wowote lakini nashangazwa ni kwanini shirika limeendelea kuing'ang'ania picha halisi ya mnyama wa mwituni pamoja na maendeleo yote ya kibiashara katika ulimwengu mpya.

2. Ndege za ATCL kuonekana zinatoka katika taifa "Primitive" ambalo halina ubunifu wa nembo za kibiashara na hivyo nchi nzima kutamburishwa kama shamba la wanyama pori.

3. Twiga huyo amechorwa akiwa amesimama kizembe kweli kweli, Hii kibiashara ni mbaya kwani humpa mteja hari ya kuamini kwamba shirika ni la watu wisiokuwa wachangamfu na wanyonge waliochoka kama Twiga huyo.
(Wabunifu wenzangu wa nembo za kibiashara watanielewa)

Maoni yangu.

Mchoro wa Twiga uwepo lakini uchorwe kama kielelezo tu (Illustration) cha Twiga na sio picha halisi ya mnyama husika, tena, ichorwe kwa ubunifu wa kuonesha kasi na uwajibikaji wa mnyama Twiga akiwa katika majukumu yake, ili basi kuendana na nembo za kibiashara za dunia ya kidigitali.

Mfano mzuri ni namna klabu ya mpira wa miguu ya Simba hapa nchini Ilivyoamua kuondoa picha halisi ya mnyama wa mwituni Simba na kuweka tu kielelezo cha mnyama huyo katika Nembo yao.
images.jpeg
 
Back
Top Bottom