UTATA: Ni muda gani na wapi Rais anatumia Nembo ya Taifa, au Nembo ya Rais, kwenye mimbari?

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,271
Je Serikali imebadili nembo ya taifa kimyakimya bila kufuata utaratibu wa Kikatiba na kisheria? Rais wetu Samia anatumia hii nembo ya taifa gani katika nchi ya TANZANIA? Je, watu wanaelewa kweli hatari ya jambo hili? Nani katwaa Urais wa Rais Samia? Tunamtaka aliyetwaa Urais wa Samia aurejeshe haraka sana!

Kwa mujibu wa Sheria ya Nembo ya Taifa ya Mwaka 1971 na Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Mwaka 1977, Nembo ya Taifa hi hiyo inayoonekana kwenye picha ya Hayati Rais Magufuli, ambapo Sheria inasema Nembo ya Taifa itakuwa na Picha mbili za bibi na Bwana walioshika oembe za Ndovu huku wakiwa wamegeukiana mbele yao wakifunika alama ya Mwenge, Jembe na Nyundo.

Lakini hiki kinachoonekana katika hotuba nyingi za Rais Samia sio Nembo ya TANZANIA, ni nembo mpya ambayo haifahamiki ni ya taifa gani, inafanana kiasi na nembo ya Rais japo haina bendera ya Taifa pia rangi hazifanani, Tunahitaji ufafanuzi wa kina katika hili. Rais Samia ni Rais wa Tanzania, anatakiwa na Katiba ya Nchi na sheria zake kuzitii kwa kuzitumikia. Sharia ya Nembo ya Taifa inamtaka kutumia nembo halisi ya taifa, na sio nembo bandia. Ifahamike kuna "Nembo ya Rais" ambayo iko tofauti na nembo ya Taifa, hii inapatikana katika Bendera ya Rais, Hakuna sheria inayosema Rais atumie nembo ya Rais katika mimbari za Hotuba, Na kwakuwa hakuna Sheria hiyo inayomlazimisha, Basi ni wajibu tuheshimu sheria ya Nembo ya Taifa ya 1971. Hii ndio inatuongoza!

Utaratibu wa Kiprotokali tangu taifa lipate Uhuru, Rais anapohutubia kinachotakiwa kuwa mbele yake kwenye mimbari ni Nembo ya Taifa, na Pembeni yake (kulia na kushoto) inasimama Bendera yenye Nembo ya Rais.

Natoa changamoto kwa Wanasheria na Wakuu wa itifaki ya Rais, Je Matumizi ya "Nembo ya Rais" ni Takwa la Kisheria? Ni Wapi Rais atatumia Nembo ya Taifa kwenye mimbari, na Ni wapi atatumia Nembo ya Rais kwenye mimbari?" Kaka yangu Gerson Msigwa Msemaji Mkuu wa Serikali, Tunaomba ufafanuzi wa jambo hili zito. Rais wetu yuko wapi!

View attachment 2714333

images (36).jpeg
 
Bendera ya rais ina nembo ambayo haina bibi na bwana kwa hiyo unayoiona hapo kwenye podium ni nembo ya rais sio nembo ya taifa.

Nadhani ni maboresho wamefanya kwa sababu hapo mwanzo walikuwa wanatumia nembo ya taifa iliyochorwa kwenye podium baadaye wakaja na iliyochongwa kwa sasa naona wameboresha wakaweka nembo ya rais na tokea waanze kuitumia naona hajaiacha
 
Bendera ya rais ina nembo ambayo haina bibi na bwana kwa hiyo unayoiona hapo kwenye podium ni nembo ya rais sio nembo ya taifa.
Sasa hayo ni maboresho au mabadiliko...alieboresha ni Magufuli kutoka kitambaa hadi ya kuchongwa.

Samia amebadilisha hajaboresha.
 
Bendera ya rais ina nembo ambayo haina bibi na bwana kwa hiyo unayoiona hapo kwenye podium ni nembo ya rais sio nembo ya taifa.

Nadhani ni maboresho wamefanya kwa sababu hapo mwanzo walikuwa wanatumia nembo ya taifa iliyochorwa kwenye podium baadaye wakaja na iliyochongwa kwa sasa naona wameboresha wakaweka nembo ya rais na tokea waanze kuitumia naona hajaiacha
Unaona au una uhakika?

Kama 'unaona' basi bado hujamjibu mtoa mada kwa hoja bali umepuyanga tu.
 
Itakuwa vyema Ofisi ya Rais-Ikulu wakatunga sheria kama wanahitaji meza, kiti na podium ziwe na nembo ya Rais (presidential seal iliyopo kwenye bendera ya Rais) badala ya ngao ya Taifa.
 
Back
Top Bottom