Kwanini Tanzania tuliamua kumtumia twiga mnyama legelege kwenye nembo ya taifa?

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,427
154,274
Twiga ni mnyama legelege, mzuri anayevutia lakini hafaidiki na uzuri wake. Mrefu, anaona mbali na anaishia kuona tu.

Kwa kweli utambulisho wowote unaoamua ukutambulishe utabeba taswira na tabia yako.

Tanzania ni taifa ambalo ni legelege, haliko aggressive kwa lolote. Watu wake ni masikini, elimu duni lakini lina utajiri wa kutisha.

Tunamtumia twiga kujitambulisha, twiga yuko taratibu sana kwenye kujongea. Na sisi maendeleo yetu kwenye kila sekta ni ya taratibu sana. Usiwasikilize wanasiasa wanaosema tuko kwenye uchimi wa chini wa kati, jiangalie wewe binafsi.

Twiga na ukubwa na urefu wake hayumo hata kwenye the big five. Kwanini hatukutumia mnyama kama Simba, au ndege tai, au hata tembo?

Bora tungemtumia nyegere (honey badger) mnyama mbishi, mbabe, ambaye akiwa na jambo lake halali mpaka amelitimiza, mnyama asiyeogopa chochote duniani.

1674356191310.png

Kwa kumtumia twiga tumekuwa kama mwanamke mzuri asiyekuwa na akili, zinazoumia ni sehemu zake za siri. Sisi na uzuri wetu na utajiri wa rasilimali tulionao, hatutaki kujitaabisha kuzibadilisha rasilimali zetu kuwa pesa, tunataka pesa za mikopo na misada (hii ni sifa ya ma slay queen) wapige tu mizinga.
Twiga Anakula majani ya kwenye miti tu anaacha manyasi mengi ardhini kwasababu anaona uvivu kuinama. Twiga Ni sisi kabisa, tuna visingizio vingi sana vya kutufanya tusifanye kazi.

Ni aibu nchi haina hata mpango wa maendeleo wa miaka 20. Hiyo mipango ya miaka mitano mitano ni upi tumeufanikisha kwa asilimia mia moja?

Tunahitaji mabadiliko makubwa ya kimfumo, ifike mahala wanaoshindwa kutusogeza mbele tuwakatae kwa nguvu zote.

CCM na katiba ya mwaka 1977 vimeshindwa kuboresha hali za wananchi na kukuza uchumi, ni wakati sasa wote tuungane pamoja kuiweka CCM kando.

KAZI NDIO MSINGI WA MAENDELEO. NCHI MASIKINI HAIWEZI KUENDELEA KWA MSINGI WA FEDHA. NCHI MASIKINI HAIWEZI KUJITAWALA KAMA INATEGEMEA MSAADA KUTOKA NCHI ZA NJE- J. K. NYERERE

Hayo ni maneno ya Nyerere yaliandikwa kwenye Uwanja wa Mapinduzi, Uwanja wa Sokoine, kwa aibu ya kusutwa na dhamira CCM wameyafuta maneno hayo.
 
Kutokana na sifa ya uzuri na kuona hata yasiyomuhusu, Twiga haleti morale ya ujasiri kwa vijana ila twiga analeta morale kwa wadangaji na machawa.
Inchi imejaa vijana wadangaji, machawa na wanao bet.
Ndio maana nchi imegeuka kuwa ya machawa, hawataki kufanya kazi wanataka tu kunyinya damu za wanaofanya kazi.
 
Naunga mkono tutumie nembo ya Honey badger,mwamba nasikia ni mbishi kweli,akishachukia hata simba hamsogelei,ila nasikia anajisaidia mahali pamoja tu,yuko tayari hata kutembea siku 10 akisafiri kwenda kujisaidia haja kubwa,hii inawakilisha uvumulivu wa hali ya juu sana,kwahiyo tukikomaa kama yeye lazima tufike kwenye uchumi wa kati...
 
Twende sawa mazee
 
Nabii GeorDavie wa Arusha amesema alama za Taifa zina maana kubwa sana kwa sababu zinaashiria aina ya WATU wa Taifa husika.

Misri alama yao Cobra, China ni Dragon, USA ni Eagle na Kenya ni Simba

Kwa mfano alama ya Tanzania ni Twiga Mnyama ambaye ni Mpole, siyo mchokozi na mwenye kuona mbali na hivyo ndivyo walivyo Watanzania wengi, amesema nabii GeorDavie.
 
Mimi nisijikite kisiasa; Kuna wanyama ni wa hivyo sana ila wanapewa sofa na thamani mpaka unabaki kujiuliza tu kwanini... Mfano twiga na ngamia utasikia warembo, wazuri mara mwendo wa kimiss n.k lakini ukifanikiwa kuwaona sasa!

Mimi hata kwenye jitimai nyama ya ngamia nilikuwa nakula huku nimekunja ndita yaani basi tu. Mkute mtu akisifia ngamia (hasa wale wapiga dufu na wamama wa mdadi) au mkute mtu wa siasa akichambua alama za taifa sasa atakavyompamba huyo twiga!
 
Aiseee
 
Similar Discussions

13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom