Kwanini Marekani ameshindwa kuimaliza Iran haraka?

Kwanini Marekani ameshindwa kuimaliza Iran haraka?

Bwana Armata, Marekani ya leo 2026 haina nguvu kama Marekani ya 1964.

Marekani ya mwaka 1964 was a formidable military behemoth lakini alishindwa Vietnam.

Anga lote la Vietnam lilikuwa limejaa ndege za Marekani huku chini wamejaa maelfu ya askari.

Marekani alilipua hivihivi na kufutilia vijiji vya watu ambapo mwishowe aliuawa watu milioni 4.

Alifanya yote lakini akashindwa....

Wanachoshindana sasa Marekani na Iran ni PAIN-ABSORPTION, ambapo kweli Iran katandikwa kelubu za kutosha na kutisha. Haya ambayo Marekani kafanya Iran, yangefanyika kwingine nchi ingekuwa ishaparanganyika. Mpaka sasa Iran katushangaza, serikali yote haipo lakini bado wanapigana vita. Sasa Marekani naye ameguswa, na Iran analenga kufanya kilekile alichofanya Vietnam (Kill many American Boys and send them home in body bags). Iran akiweza kuua hata Wamarekani 5000 tu, kelele zitatokea nyingi mno Marekani na Donald Trump na Pete Hegseth watashughulikiwa ipasavyo.

Ponapona ya Marekani ni kushinda hii vita, jambo ambalo haliwezi kufanyika kwa kuua majenerali. Mwaka 1934 kwenye Chinese-Civil War, Chiang-Kai Shek aliua maelfu ya wanajeshi wa Mao Zedong wakiwemo majenerali lakini yote hayo mwisho wake alichoka yeye, maana wakomunisti walikuwa wamejikataa, wakamshinda akakimbilia Taiwani mwaka 1949.

Likivuka hili wiki tu, wiki ijayo utatembea hapo Dar kwa mguu nakwambia. Mbaya zaidi hadi kule USA, Europe kutakuwa na hali mbaya maana Iran anashambulia Energy Infrastructure kuhakikisha kwamba Attack zake zinakuwa na The Multiplier Effect. Wamarekani wako mbali na Iran, lakini Iran has sent them A War Bill. Mfumuko wa bei utakaotokea Wamarekani watakuwa wa kwanza kuumia. Tena sanaaa.


Iran kaamua kama ni kushuka kiuchumi, Asishuke mwenyewe.

Kifo cha wengi harusi.

Anataka kila nchi ionje joto la jiwe.
 
Vita bado mbichi kusema Marekani ammeshindwa ni mapema Sana.

Kwa ninavyoona jinsi Amerika alivyopania. Sioni kama atashindwa. Atatumia Kila mbinu kubadilisha utawala hapo Iran.

Watu Aina ya Trump sio watu WA kukubali kushindwa
Kadri siku zinavyozidi kwenda ndivyo Iran anaanza kuwa wa baridi.
 
Hali itazidi kuwa mbaya for the coming days
US anaanza kuachilia vikwazo kwa Mrusi kisa mafuta
Waarabu lazima wamuinamie Muajemi

Vita hii ni ya kiuchumi na sio kidini
Pamoja na kuuwa viongozi 48 wa Iran lakini kosa kubwa kuuwa kiongozi Mkuu

Wachambuzi wa vita wanajua kabisa US ameishafeli pakubwa
Ila sio wachambuzi uchwara wa humu ambao wao wanaamini imani zao Badala ya uhalisia

Hawa wanaweza kubishana na wataalamu wa kivita wakidhani wanajua zaidi
 
Mkuu ulitegemea hakutakuwa na loss?
Wenzako wanaangalia faida ya baadae!

Hayo mabilioni unayosema wewe yamepotea, wenzako wameshajua watayarudiashaje.

Ni sawa na kule Venezuel US aliwekeza pesa nyingi jinsi ya kumkamata Maduro lakin baada ya kufanikiwa sasa hela zinarudi.
Adolf Hitler alipovamia USSR mwaka 1941 alidhani vita ingaisha wiki tatu tu, ikageuka miaka minne.

Benitho Mussolini alipovamia kisiwa cha Crete mwaka 1940 alidhani itakuwa wiki, kumbe miezi nane.

Lyndon Johnson alipeleka vikosi Vietnam mwaka 1965 wakitegemea itaisha mapema wakafika 1973.

Bill Clinton alipeleka vikosi Somalia mwaka 1993 akisema operesheni itakuwa ya saa moja, ikawa siku 1.

Siasa za dunia haziendeshwi kama MCHEZO WA UPATU, hii dunia ina mmliki wake halali na siyo USA.
 
WhatsApp Image 2026-03-06 at 1.34.17 PM.jpeg


Attach.png

Attach 2.png

Screenshot 2026-03-07 201931.png


Hadi jarida la WALIBERALI, The Economist linawakataa Donald Trump na Benjamin Netanyahu....
 
Mzee unaogopa kuwa na record mbaya kwa mafaili ya jamaa wa Msasani pale Mwai Kibaki?
Unaogopa kunyimwa ruhusa kujivinjari nchini kwao 😃
Mambo ya kugongewa muhuri kwenye mkoba au siyo?
'Titicomb', wewe ni mchokonozi.
Habari zote zimewekwa hapo; halafu wewe unakuja na vinadharia covu namna hii!

Kwa hali ilivyo sasa hivi duniani hakuna tena anayepapatikia kugongewa mhuri kwenda kokote. Tutabanana tu hapa hapa na hawa waovu mpaka waiachie nchi yetu iwe huru.
Hii ni nchi ya waTanzania, siyo wa Genge la watu waovu.

Naomba tafadhali usinikosee heshima tena, mkuu wangu 'Titi'.; kwa sababu mimi nakuheshimu kwa misimamo yako juu ya hatma ya taifa hili.
 
Kwa kuongezea kwa uchache ni kwamba, kama Iran ingepakana na US kama Russia na Ukraine, yamkini hadi sasa hali kwa Iran ingekuwa ni mbaya mbaya zaidi.
Sasa kwa nini na wewe usikumbuke kuwa Ukraine hapigani peke yake!

Hapana, simwondolei sifa ya wapiganaji wake; wameonyesha ujasiri na uwezo mkubwa sana; lakini bila ya 'sponsorship' anayopata kutoka kwa waliomchochea avimbe kichwa hali yake sasa hivi ingekuwa ni mbaya zaidi.
Sisemi kuwa angekuwa amesalimu amri moja kwa moja, lakini maeneo ya Donbas anayodai mRusi wakati huu yangekuwa yametwaliwa yote.
 
Muda huwa ni mwalimu mzuri sana.

Nakumbuka mabazazi na madunya wa humu ndani mnamo tarehe 24 February 2022 siku ambayo Urusi alivamia Ukraine walinitafuta na kunisimanga sana. Wengine walidiriki hadi kukashifu taaluma yangu. Walishangaa kwamba kwanini Urusi ameshindwa kuivamia Ukraine na kuimaliza kwa haraka ilhali anajiita taifa kubwa (Super-Power). Niliwaambia vijana wa humu ndani kwamba Urusi alifanya makosa kuvamia jirani yake na kuna mambo alikosea, lakini kusema kwamba NATO+EU wataiangusha ni jambo lisilowezekana. Mataifa makubwa huwa yanafanya makosa pia (Political Blunders)

Mpaka 2026, Urusi na Ukraine wanapigana, huku Ukraine wakiwa wameumizwa zaidi. Urusi anatumia fedha nyingi sana kwenye vita na usalama, jambo ambalo siku vita ikiisha litazua matatizo makubwa mno kwasababu watu wengi watakosa ajira ambazo wanazifanya sasa. Pia kuna mambo kadha wa kadha. Sasa huu ni utangulizi tu:

Naomba niwaulize ninyi vijana wa humu ndani, kwanini Marekani (The Only Global Super-Power) ameshindwa kulimaliza taifa la Iran ndani ya wiki kama alivyofanya Afghanistani au Venezuela ??? Fahamuni tu kwamba hivi vita hapigani Marekani peke yake bali anasaidiwa na Israeli na washirika wengine kama Australia ambao imejulikana hivi karibuni kwamba walisaidia kuzamisha manowari za Iran. Hapo kuna Saudi Arabia, Jordan, Qatar, Bahrain, UAE, Azerbaijan na Mgambo wa kikurdi (kurdish Militia).

Donald J Trump alisema ni siku nne tu baada ya Ayatollah kulambishwa mchanga basi, Iran ingekuwa kaputi. Ila sasa yametokea tofauti. Marekani kweli kawatandika Iran, lakini nao wamemtandika vibaya mno. Mara ya mwisho kambi za kijeshi za Marekani zimelipuliwa hivi ilikuwa ni mwaka 1941 kule Pearl Harbour ambapo Japan aliua zaidi ya wanajeshi 2000. Jambo la kushangaza kulikuwa na silaha za ulinzi za kisasa kabisa kwenye hizo kambi kama THAAD na PATRIOT ambazo zilikuwa na mfumo bora kabisa wa rada duniani ambao umelipuliwa.

Mahoteli ambayo walikuwa wanakaa MAJASUSI na WANAJESHI wa Marekani yamelipuliwa. Mpaka sasa maswali ni mawili tu: Aidha Iran alikuwa amejipanga sana AU kuna mtu anamsaidia maana siyo jambo rahisi kufanya haya ambayo Iran amekuwa akifanya hasa kwenye kufanya mashambulio ya ulengaji bila kukosea (Precision Attack) ambayo hutegemea kwa sehemu kubwa mifumo ya satellite. Israeli nako yamewakuta, sehemu muhimu za kiusalama zinalipuliwa. Utapinga, utanuna, utabisha na kuleta hasara ila hii ndiyo hali ilivyo.

SASA IRAN ANAPAMBANAJE: Mwaka 2018 nakumbuka kuna uzi wangu nilifurumushiwa matusi na mabazazi na madunya wa humu ndani, nilioandika kuhusu dhana ya ASYMETRIC WARFARE. Dhana hii inafanya kazi pale ambapo taifa dogo au kikundi kidogo kinapambana na taifa kubwa. Lengo siyo kutaka kupambana CONVENTIONAL WARFARE, ila ni kumsababishia maumivu makubwa yule aliye mkubwa kiasi cha kufanya akimbie. Mfano halisi, ni USSR vs Mujahedeen au USA vs Vietcong.

Iran hana AIRFORCE kama USA na ISRAEL. Iran hana NAVY kama USA na ISRAEL. Iran alichokiamua ni kutengeneza FORMIDABLE ROCKET AND DRONE FORCE, ambalo lina uwezo wa kisasa kabisa kushambulia taifa lolote lile hapa duniani. Jambo ambalo wengi hatulifahamu ni kwamba Iran mbali na udhaifu wao mwingi, walianza kupambana na Marekani tokea mwaka 1979, na wameshuhudia USA akishambulia wenzake kama Iraq, Afghanistan, Libya na Venezuela. Unadhani ni wajinga ???

MADHARA ENDAPO VITA HAITAISHA MAPEMA:

Mosi
, The Aura of American Invincibility has been shattered before the world. Zile propaganda za kusema hakuna wa kumgusa Marekani hazipo tena. Iran katuonesha kwamba Marekani na Israel wanagusika. Hebu sasa fikiria, endapo Uchina ataamua kuvamia Taiwani, nani anaamini kabisa kwamba kambi za Marekani zilizopo South-Korea, Philippines, Japan na Guam zitakuwa salama, kama tu kambi kubwa za Marekani barani Asia zimelipuliwa juzi na jana na Iran, taifa ambalo halina nguvu kama Uchina. Kiukweli, Marekani alizichanga karata vibaya na yanamtokea puani.

Pili, Urusi atapata nguvu kubwa kutokana na bei ya mafuta kupanda. Saudi Arabia, UAE, Oman, Qatar na Bahrain wanaogopa kupitisha mafuta Mfereji wa Hormuz, ambao kwa siku mapipa milioni 17 yanapita. Vita ikiendelea hivi na Iran akafanikiwa kufunga kabisa mfereji, basi mafuta ya Ulaya na Asia itabidi yapatikane Urusi ambako kuna vikwazo. Juzi Vladmir Putin kasema anafikiria kusitisha kabisa kuuza gesi Ulaya. Sasa USA na EU watabakiwa na maamuzi kama haya: Ondoa vikwazo ili tupate nishati kutoka Urusi. Bahati mbaya wakiondoa vikwazo Ukraine ndiyo kwaheri.

Tatu, Urusi atapenda kulipiza alichofanyiwa Ukraine. Hii ndiyo tabia kuu ya Urusi. Niguse-Ninuke. Marekani akitingwa kule Iran, basi lazima atapunguza kuangalia Ukraine. Sasa itabidi silaha zote zinazozalishwa zienda Persian Gulf (Ghuba ya Uajemi) siyo Ukraine. Urusi na Uchina wanaweza kuigeuza Iran, VIETNAM 2 endepo Marekani akiendelea hivi bila kuomba msamaha. Bahati mbaya sana kwa alichokifanya Donald Trump, Marekani ikirudi nyuma kama kipindi cha Twelve Days War mwaka 2024, basi ndiyo mwisho wa siasa za MAGA na Trump, na anaweza kufungwa kwasababu ameanzisha vita bila kibali cha Bunge.

Nne, mpaka sasa SECURITY DIPLOMACY ya Marekani imekufa. Ameingia makubaliano ya ulinzi na Saudi Arabia mwaka 1971, na mataifa kama UAE, Qatar na Bahrain kwamba wakitumia Dollar kuuza mafuta basi atawalinda. Bahati mbaya wanapigwa na Iran, wanaomba kuuziwa silaha na msaada wa kijeshi lakini bado hawajapata, kipaumbele chake ni Israel na kambi zake. Hii ndiyo vita kubwa ya kipropaganda ambayo Marekani hawezi kuishinda, endapo hatawalinda Saudi Arabia, UAE na Qatar dhidi ya Iran. Ujumbe utakuwa ni kwamba, kama Marekani ameshindwa kuwalinda UAE, Qatar na Saudi Arabia dhidi ya taifa dogo kama Iran, ataweza kweli kuwalinda Japan, South-Korea, Philippines na Australia dhidi ya taifa kubwa kama Uchina ???

Tano, THE COLLAPSE OF THE LAW OF NEUTRALITY. Katika sheria za kimataifa hasa wakati wa vita, The Law of Neutrality huyalinda mataifa ambayo hayapambani moja kwa moja, hata kama yanakuwa yanauza silaha kwa adui au kuwa na kambi za kijeshi ambazo hazitumiki kijeshi kushambulia adui. Kitendo cha Marekani kuvamia Iran bila sababu ni uvunjifu wa sheria za kimataifa. Hata Iran kuanza kuvamia Saudi-Arabia, UAE na Qatar ni uvunjifu wa sheria za kimataifa. Lakini Marekani hawezi kulalamika katika hili kwasababu yeye ndiye mvunjifu sugu wa sheria za kimataifa. Sheria za kimataifa ili zifuatwe na mataifa madogo, inategemea sana mataifa makubwa.

Hili lisipoangaliwa sana, tutaamka siku na kukuta Urusi kaanza kulipua Poland na Ujerumani kisa tu kuna kambi za jeshi za Marekani, hata kama hazitumiki kushambulia. Huku ndiko tunaelekea. Hivyo tukishafahamu haya, vitaifa masikini kama Tanzania vijiepushe na tabia za kupenda kujipendekeza kwa mataifa makubwa kama Uchina, Urusi na Marekani. Dunia inaelekea kubaya na kama tukitaka kuvuka itabidi kweli tusifungamane na upande wowote. Sasa wale wanopenda pesa za waarabu kisa ni wenzetu katika IMANI wakiendeleza tabia zao za kusajili manowari kule Zenji, wataliletea hili taifa matatizo makubwa mno. Tena kipindi hiki ukipigwa huna pakusemea maana kila mtu anapambana lwake.

==============================================================================

HALAFU KUNA MABAZAZI mengine yanasema INTERNATIONAL LAW IMEKUFA, haya nitayajibu baadaye.HAYANA AKILI

US alifelivibaya sana vita ya Afghan ambay ilidumu kwa miaka 10 toka 2011 -2021 na mpaka leo Taliban wako madarakani
 
Hii ni tofauti sana hauwezi linganisha, kule Urusi aliingia mazima mazima kwa kataifa jirani hapo, tena msafara haswa ila akaliwa za uso, lakini kwa hivi vita Iran, Marekani inapigana mbali sana na mpaka wake na inachezea angani tu hamna msafara wala nini na mpaka Sasa imeteka anga lote la Iran, imesambaratisha navy na air force yote ya Iran.
Viongozi wakuu wa Iran wamefyekwo, kilichosalia ni missile launchers ambazo zimefichwa maeneo mbali mbali na zinasakwa na kulipuliwa moja moja, zinasubiriwa zifyatue kisha zinasomwa na satellite na kupigwa.
Hivi ulivyo empy set AKA debe tupu AKA mbumbumbu AKA zuzu kiasi hiki.
Unapataje uthubutu wa kumquote Lumumba!?
Watu mnajiamini sana humu ndani!!!
 
You constantly shy away from speaking the truth. If you can not speak honesty due to your " Mahaba" it would be better to remain silent than to mislead people. As one of the Most prominent JF Speakers, Many may assume you hold the monopoly on Truth.
Once I felt a victim to your biased posts. back then I would slide into your profile and read your posts and I felt apprehensive about what the future holds for the world. due to your incessant take on Geopolitics.
Then, I have taken my time to study pattens and it appears that you prettily alarming opinionated emotional analyst.

In other hand.
adriz Remind your children that jumping into a conversation when adults are talking is a sign of being ill-mannered. Discourage this both in your home and elsewhere.
You're pathetic Scumbabag Dujeumsaeng
 
Ilitegemewa kwamba Iran lazima atajibu kwa nguvu tena alisema kabisa atakuwa anapiga kwenye kambi za USA zilizopo kwenye nchi za kiarabu na ilishatokea kwenye ile vita ya siku 12
Iran alijibu within hours baada ya kushambuliwa tena akifumua Radar kubwa ya Marekani middle east, akapiga kambi zote za Marekani middle east. Hakuna Taifa lililoshambulia kambi za Marekani zaidi ya Pearl Harbour miaka 85 iliyopita. Iran imeweza tena si kwa kubahatisha, ni kuilazimu USA kuomba hifuadhi Cyprus
Sasa Iran anakata moto kadri siku zinavyosogea! Awali alikuwa anarusha drones na makombora yapatayo 500 kila siku, leo anarusha chini ya 20 kwa siku.
Hapa ndipo inaonyesha hujui kinachoendelea, unahitaji msaada

Anga la Israel linalindwa na layers nyingi kuliko anga lolote duniani kwa mifumo hii, THAAD ya Marekani, PATRIOT ya Marekani, David Sling , Arrow na Iron dome. Iran ilihitaji kufumua mifumo hiyo kwanza.

Drones na makombora yalilenga ku deplete stock ya anti missile. Drone moja ina bei ya Dollar 25,000 wakati anti missile moja ina dola milioni moja. Iran ilichofanya ni ku flood the sky na kulazimisha Israel kutungua drone na makombora ya zamani kiasi cha kumaliza mfumo wa anga wa Israel

Baada ya hapo unaona Tel Aviv inapigwa kama Gaza. Kila kombora la Iran linatua eneo lolote la Israel.
Kwasasa Iran haihitaji kutumia makombora na drones nyingi kwasababu anga la Israel lipo wazi kama ilivyo middle east. Iran ilishambulia nchi zote zilizozuia makombora kutokana na somo la vita ya siku 12

Kwasasa kombora moja tu lina madhara kwasababu drones zimeufumua mfumo wa anga wa Israel.
Hakuna Taasisi yoyote ya ulinzi ya Israel iliyosimama.

Katika vita hii Israel yupo kama jina, wenye vita ni hawa; USA, UK, Australi, Netherland, Germany, France na EU ukiondoa Spain. Vita kati ya Israel na Iran ilikwisha, Iran ana deal na mkusanyiko wa Mataifa

Israel imepiga marufuku mashirika ya habari kupiga picha bila ruhusa.
Raia anayepiga picha anafungwa miaka 5.Unajua ni kwanini?
Kwa sababu lounchers na maghala ya siraha yanawindwa na Myahudi na kuyalipua kila siku.
Well, umeona teknolojia ya kuficha makombora ardhini?
Itafika hatua hututaona kombora hta moja ikitokea Iran ni suala muda tu
Iran haipigani vita kushinda inapigana ku survive. Iran inapigana na USA, EU na Washirika wao wa middle east
Juzi walionesha Khorramshir! wenyewe wanasema stock ya zamani imekwisha, wanaanza na mpya

Love or hate Iran, wapeni maua yao!
 
Leo hii ukimchukua Mwakinyo akapigana na Wema Sepetu, halafu Mwakinyo akamchapa kweli Wema Sepetu ngumi za kichwa, ila baadaye Wema Sepetu akafanikiwa kumpiga ngumi moja tu ya pua, na Mwakinyo damu zikaanza kutoka, wewe unadhani watu watazingatia ngumi za kichwa alizopigwa Wema Sepetu ??? A Bleeding Nose, is enough to enough to make Mwakinyo lose the entire fight...
Nimecheka kifala!
Weeeeh mzee una ubongo wa ajabu sana aisee!!!
Umewezaje kuja na huu mfano!?
 
Back
Top Bottom