Kwanini Marekani ameshindwa kuimaliza Iran haraka?

Kwanini Marekani ameshindwa kuimaliza Iran haraka?

Mkuu hapa hakuna kitu umechangia specifically kwenye hii mada. Reply yako tukiitoa tukaipachika kwenye mada ya kuuza nyanya, bado itaonekana inafaa. Sasa hii sio mada ya ujazo mdogo ulioleta hapa.
Bro point yangu iko hapa, taarfa zote za vita ya Urusi zilikuwa hewani. Niambie taarfa gani za USA ISRAEL, zipo hewani.

Wameamua kucheza chini ndo mana huoni chochote kilichoharibika kwao, propaganda ndo inaingia hapo. Iran kila siku anasema nani kafa au nani kaumizwa, hebu wewe nambie lini umesikia hata Trump akisema base zetu zimepigwa ?

Waarabu wale majirani walitoa taarfa za hatar na wakatoa taarfa IRAN kaharibu baadhi ya miundombinu ya kambi za kijeshi pale kwao ila kumsikia kaka mkubwa Trump never.

PROPAGANDA !!!!
 
Communism was never about race, but class struggle (Proletariat vs Bourgeoisie).

You make fallacious arguments when you claim that Communism brought racism.

Actually, it's Capitalism through its most perverse institutions like Slavery that brought racism.

Communism started in Europe, A White Man's Continent, how can you claim that it brought Anti-White racism ???
Mchaw lugha
 
too much information na pia confusing, lkn siyo kweli kwamba wazungu (Christians) wanawachukia waafrika na black people kwa ujumla hizo ni propaganda za communists + muslims ambazo zimefanywa dunia nzima walipo black people kuwatenganisha na Christianity na kuweza kuwafanya waafrika wachukie Christianity na Capitalism, kuwafanya waafrika waamini salvation yao iko kwa muslims na communists na ndiyo maana afrika na black people tumebakia wa mwisho duniani kwa maana tumedanganywa sana na communists na muslims, kwanza wazungu Christians wamesaida waafrika na black people klk yoyote yule duniani.

communists na muslims wana ugomvi na Christian capitalists world unaokwenda kwa zaidi ya miaka 1000 hivyo wanatafuta (communist + muslims) watu wa kuwadanganya to fight their battle, na ndiyo maana unaona wamewapata wajinga kama ramaphosa na ans wa ak wanapambana kutetea palestina, hivi sasa (afrika kusini) anakimbizana na israeli na akina netanyahu badala ya kuangalia uchumi wa afrika kusini na watu wake, ramaphosa yuko tayari kugombana na USA kiuchumi kutetea muslims palestina, anayepigana ugomvi kwa niaba ya muslims na communists vs Christian Capitalistis world siyo chinese au indonesian bali ni black man ramaphosa na anc wao ndio wanaishitaki israeli kwenye mahakama zote za kimataifa, swali ni kwamba why is it a blackman s problem? kwa nini siyo china, india au hata waarabu wenyewe wasihangaike na palestina na ugomvi wao wa gaza? kwa nini iwahusu afrika kusini? kwa nini uwe ugomvi wa black man? jibu ni rahisi wanatumiwa na commnists na muslims against Christianity.

hivyo siyo kweli kwamba Christian white people wanawachukia afrikans na black people hiyo ni communist na muslim propaganda, ila waafrika na black people dunia nzima wanatumiwa na communists to fight their battle against Christianity.

adui wa mwafrika na black people kwa ujumla ni communism na islam, siku tukija kuligundua hilo ndiyo siku tutaifungua minyororo ya utumwa na kujenga prosperity na kuheshimika duniani kama wengine wanavyoheshimika mf. chinese au hata indians ...
Christian, Capitilalist na USA!

Haya maneno matatu ndiyo yamekwepa au tuseme yana kinga ya uandishi wako mbovu.
 
Mkuu hapa hakuna kitu umechangia specifically kwenye hii mada. Reply yako tukiitoa tukaipachika kwenye mada ya kuuza nyanya, bado itaonekana inafaa. Sasa hii sio mada ya ujazo mdogo ulioleta hapa.
Bro, Trump kasema Iran ni taifa lenye nguvu kubwa sana. Leo kaacha propaganda ninaamini hata wewe utakubali ila ulikataa.

Bro hii dunia kuna namna inaendeshwa ni vile waAfrika tumekataa kutoka nje ya box lao. Na kasema kama wataachwa peke yao Israel anafutika.

Swali langu kwako, tufanye vile ulisema Iran wakubwa wote wamekufa ila ye hajaua, unahis kwanini hajauua na bado trump kasema wakiachwa wao Israel ataondoka duniani ?
 
Financial Times.jpg

Financial Times 2.png

Financial Times 3.png
 
Mkuu MALCOM LUMUMBA kwanza nikupe pole kwa maumivu ya kichwa unayopitia katika kipindi hiki cha vita. Nafikiri ulitegemea Iran iwe imelipua aircraft carrier ya Marekani huko Mediterania sea lakini mpaka sasa ni kipondo tu kinatembea. Kiuhalisia Iran inaona mambo ni magumu na baada ya wiki moja ya huu msako wananchi watajitoa mhanga kupambana na serikali ya kiimla ya Iran kwani mpaka sasa haina mkuu wa nchi na hata makamanda wakuu wa jeshi wameshakufa na kuna wasiwasi wa kuuawa kwa rais na wasaidizi wake wote. Kwa sasa Iran hata internet pia imezimwa siku ya sita leo na hili ni hatari kwa usalama wa taifa. Mkuu see you next
Niliahidi kukuita hapa baada wiki moja kama ulivyosema.

Haya wiki ishaisha Mkuu hebu tupe mrejesho wako.....
 
Niliahidi kukuita hapa baada wiki moja kama ulivyosema.

Haya wiki ishaisha Mkuu hebu tupe mrejesho wako.....
Mrejesho wa vita vimemkalia vibaya Iran, Iran kwa sasa analalamika kuwa hakuna taifa la kiislamu lililosimama na watu wa Iran. Sasa tujiulize Iran ina ndege za kivita? Iran ina makombora ya masafa marefu? Iran kiongozi wake mkuu yupo salama? Iran viongozi wake wanaouwa kuna mkakati wa kuwalinda waliobaki?

Mpaka sasa Iran inapambana na raia wake kuzuia kuzuka kwa maandamano kwa kuwatisha na kuwasingizia makosa ya ujasusi ili wasiende barabarani lakini mwisho wa hili ni kuwa Islamic republic is no more. Kuuawa kwa viongozi wa kiislamu hapo Iran kutasaidia kupunguza hali ya mvutano na huenda makundi ya kigaidi duniani yakapotea.
 
Muda huwa ni mwalimu mzuri sana.

Nakumbuka mabazazi na madunya wa humu ndani mnamo tarehe 24 February 2022 siku ambayo Urusi alivamia Ukraine walinitafuta na kunisimanga sana. Wengine walidiriki hadi kukashifu taaluma yangu. Walishangaa kwamba kwanini Urusi ameshindwa kuivamia Ukraine na kuimaliza kwa haraka ilhali anajiita taifa kubwa (Super-Power). Niliwaambia vijana wa humu ndani kwamba Urusi alifanya makosa kuvamia jirani yake na kuna mambo alikosea, lakini kusema kwamba NATO+EU wataiangusha ni jambo lisilowezekana. Mataifa makubwa huwa yanafanya makosa pia (Political Blunders)

Mpaka 2026, Urusi na Ukraine wanapigana, huku Ukraine wakiwa wameumizwa zaidi. Urusi anatumia fedha nyingi sana kwenye vita na usalama, jambo ambalo siku vita ikiisha litazua matatizo makubwa mno kwasababu watu wengi watakosa ajira ambazo wanazifanya sasa. Pia kuna mambo kadha wa kadha. Sasa huu ni utangulizi tu:

Naomba niwaulize ninyi vijana wa humu ndani, kwanini Marekani (The Only Global Super-Power) ameshindwa kulimaliza taifa la Iran ndani ya wiki kama alivyofanya Afghanistani au Venezuela ??? Fahamuni tu kwamba hivi vita hapigani Marekani peke yake bali anasaidiwa na Israeli na washirika wengine kama Australia ambao imejulikana hivi karibuni kwamba walisaidia kuzamisha manowari za Iran. Hapo kuna Saudi Arabia, Jordan, Qatar, Bahrain, UAE, Azerbaijan na Mgambo wa kikurdi (kurdish Militia).

Donald J Trump alisema ni siku nne tu baada ya Ayatollah kulambishwa mchanga basi, Iran ingekuwa kaputi. Ila sasa yametokea tofauti. Marekani kweli kawatandika Iran, lakini nao wamemtandika vibaya mno. Mara ya mwisho kambi za kijeshi za Marekani zimelipuliwa hivi ilikuwa ni mwaka 1941 kule Pearl Harbour ambapo Japan aliua zaidi ya wanajeshi 2000. Jambo la kushangaza kulikuwa na silaha za ulinzi za kisasa kabisa kwenye hizo kambi kama THAAD na PATRIOT ambazo zilikuwa na mfumo bora kabisa wa rada duniani ambao umelipuliwa.

Mahoteli ambayo walikuwa wanakaa MAJASUSI na WANAJESHI wa Marekani yamelipuliwa. Mpaka sasa maswali ni mawili tu: Aidha Iran alikuwa amejipanga sana AU kuna mtu anamsaidia maana siyo jambo rahisi kufanya haya ambayo Iran amekuwa akifanya hasa kwenye kufanya mashambulio ya ulengaji bila kukosea (Precision Attack) ambayo hutegemea kwa sehemu kubwa mifumo ya satellite. Israeli nako yamewakuta, sehemu muhimu za kiusalama zinalipuliwa. Utapinga, utanuna, utabisha na kuleta hasara ila hii ndiyo hali ilivyo.

SASA IRAN ANAPAMBANAJE: Mwaka 2018 nakumbuka kuna uzi wangu nilifurumushiwa matusi na mabazazi na madunya wa humu ndani, nilioandika kuhusu dhana ya ASYMETRIC WARFARE. Dhana hii inafanya kazi pale ambapo taifa dogo au kikundi kidogo kinapambana na taifa kubwa. Lengo siyo kutaka kupambana CONVENTIONAL WARFARE, ila ni kumsababishia maumivu makubwa yule aliye mkubwa kiasi cha kufanya akimbie. Mfano halisi, ni USSR vs Mujahedeen au USA vs Vietcong.

Iran hana AIRFORCE kama USA na ISRAEL. Iran hana NAVY kama USA na ISRAEL. Iran alichokiamua ni kutengeneza FORMIDABLE ROCKET AND DRONE FORCE, ambalo lina uwezo wa kisasa kabisa kushambulia taifa lolote lile hapa duniani. Jambo ambalo wengi hatulifahamu ni kwamba Iran mbali na udhaifu wao mwingi, walianza kupambana na Marekani tokea mwaka 1979, na wameshuhudia USA akishambulia wenzake kama Iraq, Afghanistan, Libya na Venezuela. Unadhani ni wajinga ???

MADHARA ENDAPO VITA HAITAISHA MAPEMA:

Mosi
, The Aura of American Invincibility has been shattered before the world. Zile propaganda za kusema hakuna wa kumgusa Marekani hazipo tena. Iran katuonesha kwamba Marekani na Israel wanagusika. Hebu sasa fikiria, endapo Uchina ataamua kuvamia Taiwani, nani anaamini kabisa kwamba kambi za Marekani zilizopo South-Korea, Philippines, Japan na Guam zitakuwa salama, kama tu kambi kubwa za Marekani barani Asia zimelipuliwa juzi na jana na Iran, taifa ambalo halina nguvu kama Uchina. Kiukweli, Marekani alizichanga karata vibaya na yanamtokea puani.

Pili, Urusi atapata nguvu kubwa kutokana na bei ya mafuta kupanda. Saudi Arabia, UAE, Oman, Qatar na Bahrain wanaogopa kupitisha mafuta Mfereji wa Hormuz, ambao kwa siku mapipa milioni 17 yanapita. Vita ikiendelea hivi na Iran akafanikiwa kufunga kabisa mfereji, basi mafuta ya Ulaya na Asia itabidi yapatikane Urusi ambako kuna vikwazo. Juzi Vladmir Putin kasema anafikiria kusitisha kabisa kuuza gesi Ulaya. Sasa USA na EU watabakiwa na maamuzi kama haya: Ondoa vikwazo ili tupate nishati kutoka Urusi. Bahati mbaya wakiondoa vikwazo Ukraine ndiyo kwaheri.

Tatu, Urusi atapenda kulipiza alichofanyiwa Ukraine. Hii ndiyo tabia kuu ya Urusi. Niguse-Ninuke. Marekani akitingwa kule Iran, basi lazima atapunguza kuangalia Ukraine. Sasa itabidi silaha zote zinazozalishwa zienda Persian Gulf (Ghuba ya Uajemi) siyo Ukraine. Urusi na Uchina wanaweza kuigeuza Iran, VIETNAM 2 endepo Marekani akiendelea hivi bila kuomba msamaha. Bahati mbaya sana kwa alichokifanya Donald Trump, Marekani ikirudi nyuma kama kipindi cha Twelve Days War mwaka 2024, basi ndiyo mwisho wa siasa za MAGA na Trump, na anaweza kufungwa kwasababu ameanzisha vita bila kibali cha Bunge.

Nne, mpaka sasa SECURITY DIPLOMACY ya Marekani imekufa. Ameingia makubaliano ya ulinzi na Saudi Arabia mwaka 1971, na mataifa kama UAE, Qatar na Bahrain kwamba wakitumia Dollar kuuza mafuta basi atawalinda. Bahati mbaya wanapigwa na Iran, wanaomba kuuziwa silaha na msaada wa kijeshi lakini bado hawajapata, kipaumbele chake ni Israel na kambi zake. Hii ndiyo vita kubwa ya kipropaganda ambayo Marekani hawezi kuishinda, endapo hatawalinda Saudi Arabia, UAE na Qatar dhidi ya Iran. Ujumbe utakuwa ni kwamba, kama Marekani ameshindwa kuwalinda UAE, Qatar na Saudi Arabia dhidi ya taifa dogo kama Iran, ataweza kweli kuwalinda Japan, South-Korea, Philippines na Australia dhidi ya taifa kubwa kama Uchina ???

Tano, THE COLLAPSE OF THE LAW OF NEUTRALITY. Katika sheria za kimataifa hasa wakati wa vita, The Law of Neutrality huyalinda mataifa ambayo hayapambani moja kwa moja, hata kama yanakuwa yanauza silaha kwa adui au kuwa na kambi za kijeshi ambazo hazitumiki kijeshi kushambulia adui. Kitendo cha Marekani kuvamia Iran bila sababu ni uvunjifu wa sheria za kimataifa. Hata Iran kuanza kuvamia Saudi-Arabia, UAE na Qatar ni uvunjifu wa sheria za kimataifa. Lakini Marekani hawezi kulalamika katika hili kwasababu yeye ndiye mvunjifu sugu wa sheria za kimataifa. Sheria za kimataifa ili zifuatwe na mataifa madogo, inategemea sana mataifa makubwa.

Hili lisipoangaliwa sana, tutaamka siku na kukuta Urusi kaanza kulipua Poland na Ujerumani kisa tu kuna kambi za jeshi za Marekani, hata kama hazitumiki kushambulia. Huku ndiko tunaelekea. Hivyo tukishafahamu haya, vitaifa masikini kama Tanzania vijiepushe na tabia za kupenda kujipendekeza kwa mataifa makubwa kama Uchina, Urusi na Marekani. Dunia inaelekea kubaya na kama tukitaka kuvuka itabidi kweli tusifungamane na upande wowote. Sasa wale wanopenda pesa za waarabu kisa ni wenzetu katika IMANI wakiendeleza tabia zao za kusajili manowari kule Zenji, wataliletea hili taifa matatizo makubwa mno. Tena kipindi hiki ukipigwa huna pakusemea maana kila mtu anapambana lwake.

==============================================================================

HALAFU KUNA MABAZAZI mengine yanasema INTERNATIONAL LAW IMEKUFA, haya nitayajibu baadaye.HAYANA AKILI

UMEFIRIWA UNATOKWA POVU KILA SEHEMU. BABAAAKE.... UMEPIGWA NA UKUNI HASWA HASWA. UPO HOI.
Screenshot_2026-03-17-20-56-07-548_com.twitter.android~2.jpg
Screenshot_2026-03-17-20-55-51-202_com.twitter.android~2.jpg
Screenshot_2026-03-17-20-56-11-865_com.twitter.android~2.jpg
Screenshot_2026-03-17-20-57-24-705_com.twitter.android~2.jpg
Screenshot_2026-03-17-20-34-28-120_com.android.chrome~2.jpg
Screenshot_2026-03-17-20-57-36-104_com.twitter.android~2.jpg
 
there is no need to insult each other ,just prepare yourself to pay more on oil,
Maybe those who think trump and zionist will help to give you cheap oil we don't care,
Hormuz is closed ,high price not on but even fertlizer ,aluminum,all products
You can support israel as you wish but remember after the war the comodity price will not be the same .
Dont insult just start to save no more cheap oil
 
Wenzako faida wataanza kuhesabu miaka 2 ijayo baada ya kufanikisha mision yao
Iran na maswahiba wake tayari wanahesabi faida Sasa,Leo hii,homusi,imefingwa,mafuta yamepanda bei,ulaya kelele nyingi, Kambi za USA gulf zote fyuu,vitegauchumi vya USA gulf vyote fyuu, Israel kama Gaza TU,Urusi anapiga Hela ndefu sana Sasa hivi,china anapata wese kirahisi TU,USA wanaendelea kupata hasara ya USD ambayo haijawahi kutoka toka Dunia iumbwe kutokana na gharama za vita ambayo alivyotegemea imekua sivyo.
Israel ilikua haijawahi kupigwa nyumbani kwake toka kuwa taifa 1945 kama kipigo hiki.
Uchumi umevurugika makamanda wakubwa wameuwawa,wataalamu weuwawa,n.k.
Kwa Iran ambayo Haina Cha kupoteza haya ni mafanikio makubwa mno
Na baada ya vita hii hakuna Tena nchi duniani itaipangia Iran namna ya kuishi.
 
Back
Top Bottom