Hapa unalinganisha tembo na mbuzi kwenye uzito.
Russia imetimiza miaka minne tangu ianzishe mashambulizi dhidi ya Ukraine. Kwa kutumia vifaru, wanajeshi, helicopters, meli za kivita, bombers, fighter jets, submarines, missiles zikiwemo cruise, ballistic na hadi hypersonic, na silaha nyinginezo.
Marekani imeshambulia haina boots on ground, haina kifaru hata kimoja, inatumia missiles, ndege na meli sina hakika kama wametumia submarines mpaka sasa. Tofauti zao sasa:
1. Russia ina miaka minne (4), US haijatimiza mwezi.
2. Russia haijawahi miliki anga la Kiev, wala ndege yake kukatisha anga hilo walau mara moja katika miaka yote minne. US siku ya kwanza tu ndege zake zilifika Tehran na kila siku zinafika zinakotakiwa kufika popote ndani ya Iran. Ndoto kama hii kwa Russia haiwezekani.
3. Russia haijawahi muua mkuu wa majeshi, wala Rais, wala mkuu wa Air force, au wa Navy, au wa Army ya Ukraine. Upande wa Marekani hapa sitaji nitakukumbusha machungu.
4. Iran haijamuua General yeyote wa US, Ukraine imeua Russian Generals zaidi ya 15 kwenye mapigano.
5. Iran hajawahi shambulia mainland US. Wakati Ukraine anashambulia hadi ikulu ya Kremlin ya Urusi.
Hizo ni tofauti kubwa, mengine ni vita zina mambo yake. Ila aliyekutaarifu kuwa Marekani ameshindwa kummaliza Iran "kwa haraka" sijui ni nani.