Mdogo wangu aliwahi kufanya checkup ya moyo kwenye hospitali fulani kubwa ya rufaa akaambiwa ana ugonjwa wa moyo na kupewa rufaa kwenda JKCI haraka asizidishe wiki mbili, kwamba tatizo lipo serious sana! Kutokana na msongo wa mawazo ndani ya siku chache wakati tukiandaa safari hiyo alikuwa tayari ana dalili kibao za ugonjwa huo!
Cha ajabu baada ya kufika JKCI alifanya vipimo 11 tofauti huku madaktari wakishangaa huko hospitali ya rufaa walipimaje hadi kubaini tatizo kubwa lisilokuwepo. Katika process za vipimo dogo alikuwa anaimarika kadri vipimo vinavyoendelea. Hadi vinakamilika zile dalili alizokuwa ame develop zilishatoweka kabisa anadunda zake. Hakupewa hata panadol za kumeza.
Nawe pia nenda hospitali kubwa zaidi upime, namini huumwi. Mungu akutangulie.