Kwaherini JF

Kwaherini JF

Dah pole sana Joanah, inahitaji ujasiri mkubwa mno kuandika ujumbe wa namna hii, so big respect kwako Joanah kwa kuwa muwazi hivi. Ni kweli binadamu wote safari yetu ni moja na hakuna anayeishi milele, lakini hii approach yako ya kukubali ukweli inaonyesha jinsi ulivyo mtu imara sana kiakili.

Hata hivyo, usiruhusu hofu icchukue maisha yako kwa sasa. Kila dakika unayopumua sasa hivi ni ya thamani kubwa sana. Cha msingi ni kupunguza stress na maumivu kadri inavyowezekana ili akili na mwili wako vipate utulivu. Tuko na wewe pamoja sana.
 
Mtu pekee mwenye kujua hatima yetu ni binadamu ni Mwenyezi Mungu pekee na wala sio hao madaktari though tunaheshimu sana taaluma yao

Mi nakuombea sana Dada yangu na naamini utaendelea kuishi kwa mapenzi ya Mungu na hata kama ukiondoka kama ilivyo kawaida kuwa kila nafsi itaonja umauti, bado utaendelea kuishi mioyoni mwetu

Mungu akutie nguvu kipindi hiki kigumu na akujaalie Siha njema InshaAllah

Pole sana Jojo
 
Mmmh bana... hii imenigusa sana aisee. Sijui niseme nini, lakini naskia uchungu sana.

Nimekukumbuka na jinsi ulivyokuwa unachangia kwenye JF, kila siku nimekuwa nikifuatilia posts zako.

Mungu akupokee kwa mikononi mwake mkuu, upumzike kwa amani. Familia yako na wote unaowapenda nao wapate nguvu ya kustahimili.

Kwaherini mdau, tutakukumbuka. 🕊️
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom