DELETED ACCOUNT
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 9,805
- 15,470
Kuwanyima maelfu ya Watanzania haki yao na fursa ya kuangalia mechi ya kihistoria katika uwanja wao kwa sababu za mvua ni kinyume cha juhudi zote za kuufanya mchezo wa mpira wa miguu uwafikie watu wengi zaidi.
Kuna timu nyingi, zingine zina mafanikio ambazo zinahangaika kutafuta mashabiki ila mpaka leo zinakosa. Timu ambazo zimeweza kupata rundo la mashabiki kindakindaki ambao wanakwenda viwanjani, wanasapoti timu zao kwa hali na mali na kuhamsha hamasa ya soka zinatakiwa kupongezwa na kutiwa moyo na siyo kukatishwa tamaa.
Kila mwaka timu za kusini mwa Africa zinakwenda ukanda wa kaskazini na zinachezeshwa usiku na katika baridi kali ambazo wachezaji na mashabiki wake hawajazoea ila hilo halijawahi kuonekana kama ni "mazingira mabaya yasiyo ya kimchezo". Inakuwaje mvua tu inaonekana inaharibu "sporting conditions" za wachezaji na mashabiki? Mbona mechi hazisitishwi pale mashabiki wa kiarabu wanapowasha moshi unaotanda uwanja mzima huko Morocco, Algeria na Misri katikati ya mchezo? Bado mazingira rafiki kwa wachezaji yanakuwa yamezingatiwa?
Tunajua serikali ya Tanzania ambao ndiyo wamiliki wa uwanja wa Benjamin Mkapa wanatakiwa kubeba lawama nyingi kutokana na hili la fainali ya pili kati ya Simba vs Berkane, lakini naamini haukufanyika uamuzi ulioangalia athari za muda mfupi na muda mrefu za kuwanyima fursa hii maelfu ya wapenzi na mashabiki wa Simba.
Ni wakati wa kuleta usawa katika mpira wa Africa na tuanze kwa kuhamisha makao ya vyama vyote vya mpira Africa kwenda Ethiopia ambapo ni umbali ulio karibu na sawa kutoka kila pembe ya Africa na pia ndipo yalipo makao makuu ya African Union. Kama FIFA ipi Uswizi ambapo yapo makao makuu ya taasisi nyingi za dunia, basi CAF na taasisi zake, nazo ziwepo mahali ambapo yapo makao makuu ya taasisi nyingine kuu za Africa.
Hata Simba ikibeba kombe huko Zanzibar, bado hili doa la kunyimwa kuiona timu yao kwa sababu nyepesi nyepesi halitaondoka katika mioyo ya wengi kwa miaka mingi.